Wadau wa amani wakiwa jukwaa kuu wakiwa wanafuatilia matukio mbali mbali ya maadhimisho ya kuutakia amani mkoa wa Arusha baada ya kukumbwa na matukio mbali mbali yaliotokea baada ya uchaguzi mkuu na mabomu kwenye kanisa la Joseph mfanyakazi olasit na Soweto mkutano ulioandaliwa na msajili wa vyama vya siasa na vyama vya siasa mkoani hapa na kufanyika kwenye uwanja wa kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid jijini hapa
Mchungaji Christopher Mwakasege akiombea amani ya mkoa wa Arusha kwenye siku hiyo ya kusahau tofauti na matukio yaliotokea kwenye mkoa huu wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 kwenye uwanja wa sheikh Amri Kaluta Abeid
Juu na chini wanaonekana viongozi mbali mbali wa serikali, vyama vya siasa na dini mkoani Arusha Pamoja na mgeni Rasmi Jaji Francis Mutungi Msajili wa Vyama vya siasa wakiwa kwenye maombi yaliokuwa yakiombwa na mwalimu na mchungaji Christopher Mwakasege kwenye uwanja wa sheikh Amri Kaluta Abeid.
Picha zote na Mahmoud Ahmad wa Globu ya Jamii, Arusha)