Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

TANESCO NJOMBE WATAKIWA KUJIFUNZA TANWATT JUU YA NGUZO ZA UMEME ZINAZOZALISHWA

$
0
0
NJOMBE

Shirika la Umeme nchini Tanzania TANESCO Mkoa wa Njombe limetakiwa kwenda kujifunza namna kampuni ya Miwati ya Tanwatt iliyopo kibena Mjini Njombe inavyozalisha nguzo za Umeme badala ya Kuagiza  Nje ya Nchi.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu  Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Mussa Uledi wakati akiwa katika Ziara ya kutembelea kiwanda hicho kujifunza namna kinavyozalisha bidhaa bora licha ya kutofahamika sana Nchini Tanzania.

Katibu Mkuu  Uledi ameonekana kufurahishwa na utendaji kazi wa kampuni hiyo na kwamba imekuwa ikizalisha Nguzo za umeme nyingi, kufua umeme pamoja na kuzalisha malighafi za kutengenezea samani zinazotafutwa na Nchi za Afrika  mashariki na kati.

Akizungumzia hali ya kiwanda hicho meneja misitu wa Tanwatt Antery Kiwale amesema kuwa pamoja na ubora wa malighafi wanazozalisha na uwezo Mkubwa wa kiwanda Lakini wamekuwa wakikosa Tenda za kusambaza Nguzo za umeme kwa kile kinachoelezwa Tanesco  Kupitia bodi ya tenda imekuwa ikiangalia vigezo vidogovidogo amnavyo havina maslahi kwa taifa.

Aidha Kiwale amesema bado wanaendelea kuboresha huduma za kiwanda hicho ili kiendelee kukubalika zaidi kwani Nchi Jirani ya Kenya imekuwa ikifika kununua Bidhaa zinazozalishwa kiwandani hapo wakati watanzania wamekuwa wakishindwa
kunufaika Nazo.

Kwa Upande wake Afisa Utawala na Fedha katika Kampuni Hiyo Edmund Munubi Amesema Mbali na Uzalishaji huo Lakini kimetoa Ajira ya Watu 1500 hadi 3000 kutegemeana na Msimu kitu ambacho kinaongeza pato la Taifa na mtu mmoja Mmoja.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles