Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

MWENYEKITI Mpya WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE VALENTINO HONGORI LEO AMEFUNGA MKUTANO WA BARAZA LA KWANZA LA MADIWANI LILILOFANYIKA SIKU MBILI

$
0
0
 
 HUYU NDIYE MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA NJOMBE VALENTINO HONGORI AKIHUTUBIA MADIWANI NA WATUMISHI WA HALMASHAURI
 
 MBUNGE WA JIMBO LA LUPEMBE  JORAM HONGORI AKITOA NASAHA MBELE YA MADIWANI HAO






 PICHA YA PAMOJA YA MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA



Na Michael NgilangwaNJOMBE

Madiwani Wa Halmashauri Ya Wilaya Ya Njombe  Wamemuagiza Mkurugenzi Wa Halmashauri Hiyo

Kuhakikisha Watumishi Wote Wanaishi Kwenye Vituo Vyao Vya Kazi  Wakiwemo Waratibu Elimu Na

Watendaji Wa Kata Na Kwamba Kwa Wasiyofanya Hivyo  Wanatakiwa Kushushwa Wadhifa Wao  Na

Kwenda Kufundisha Shuleni Kwa Waratibu Hao.

Wakizungumza Kwenye Mkutano Huo Wa Baraza La Madiwani  Wa Halmashauri Ya Wilaya Ya

Njombe Madiwani Hao Wamesema  Shughuli Za Utekelezaji Wa Miradi Ya Vijiji  Na Kata Kutokana Na

 Watumishi Kuishi Mbali Na Vituo Vyao Vya Kazi Ambapo Wamesema Idadi Kubwa Ipo Kwa

Watendaji Wa Vijiji,Waratibu Elimu Na Watendaji Wa Kata.

Wamesema Kuwa Halmashauri Hiyo Imeshindwa Kufikia Lengo  Ambalo Ilijiwekea La Kukusanya

Mapato  Huku Majukumu Mengine Ya  Ukamilishaji Wa Miradi Nayo Yakidaiwa Kushindwa

Kukamilika  Pamoja Na Uharifu Kutokea Katika Maeneo Ya Vijiji Kutokana Na Walinzi Wa Amani

Kuwa Hawapo Maeneo Yao Ya Kazi.

Akizungumza Kwenye  Hitimisho La Baraza La Madiwani  Mwenyekiti  Wa Halmashauri Ya Wilaya Ya

Njombe  Valentino Hongori  Amesema  Watendaji Na Waratibu Wanaoishi Mabili Na Mahala Pa Kazi

Mkurugenzi Anapaswa Kuchukua Hatua Za Kinidhamu  Dhidi Yao Ikiwemo Kushushwa Vyeo Vyao

Kwa Watakao Kaidi  Agizo Hilo.

Mkurugenzi Wa Halmashauri Ya Wilaya Ya Njombe Paul Malala Amesema Kuwa  Tatizo Hilo Ambalo

Limelalamikiwa Na Madiwani  Atakwenda Kufuatilia Na Majibu Atayatoa Kuanzia Mwezi Januari  Na

Ameahidi Kuanza Kufuatilia Kwa Afisa Elimu Ili Kuhakikisha Waratibu Na Watendaji Wote Wanakaa

Kwenye Vituo Vyao Vya Kazi Na Atakayekiuka Hatua Kali Zitachukuliwa  Dhidi Yao.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles