Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

WALIMU WA SKULI MBALI MBALI ZA WILAYA WAPATIWA MAFUNZO YA MICHEZO NA KAMATI YA OLIMPIKI TANZANIA (TOC) MJINI ZANZIBAR

$
0
0


ol1Mkufunzi wa Mafunzo ya Walimu wa Michezo wa Skuli yaliyoandaliwa na   Kamati ya  Olimpiki Tanzania  (TOC) Suleiman Mahmoudu Jabiri  akitowa maelezo kwa washiriki  katika siku ya mwisho ya mafunzo hayo yaliyoanza  tarehe 01 mwenzi huu.
ol2Mkurugenzi wa Idara ya Elimu mbadala na Watu wazima Mashavu  Fak akifunga mafunzo ya walimu wa michezo wa Skuli katika  Skuli ya Elimu Mbadala Rahaaleo Mjini Zanzibar.
ol3Mkurugenzi wa Idara ya Elimu mbadala na Watu wazima Mashavu  Faki  akiwakabidhi vyeti washiriki  wa mafunzo  yaliyoandaliwa na Kamati ya  TOC  katika Ukumbi wa Elimu Mbadala Rahaleo Mjini Zanzibar.
……………………………………………………………………………………………………………..
Na Rahma Khamis Maelezo Zanzibar 
Idara ya ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imeshauriwa kuwaandalia michezo nje ya nchi walimu wa michezo wa skuli kwa lengo la kujipatia taaluma zaidi na kukukuza mechezo nchini ,

Hayo yameelezwa huko Rahaleo katika Ukumbi wa Elimu Mbadala na Watu wazima na Mkurugenzi Idaraya hiyo Zanzibar Mashavu Faki  wakati akifunga mafunzo yalioandaliwa na  Kamati ya Olimpiki Tanzania  (TOC) yaliyofunguliwa tarehe 1 mwezi huu.

Amesema iwapo walimu wa michezo watapatiwa mafunzo zaidi nje ya nchi wataweza kuwasomesha wanafunzi wao wa
skuli na kuinua sekta  ya michezo Zanzibar.

Mkurugenzi Mashavu amesema katika mwaka 2013 kulifanywa utafiti wa kimchezo na kuonekana kuwa nchi zinazoimarisha michezo maskulini ndizo zinazofanya  vizuri zaidi katika masomo yao.

Aidha amesema michezo huimarisha afya, kujenga  upendo, udugu na uzalendo katika jamii hivyo hakuna budi kuendelezwa  kwa manufaa ya wanamichezo wenyewe na Taifa kwa jumla.

Sambmba na hayo Mkurugenzi huyo amewashauri waalimu waliopata mafunzo hayo kwa kushirikiana na Idara husika  kuandaa mafunzo kila baada ya miezi mitatu.

Nae mkufunzi wa mafunzo hayo Suleiman Mahamoud Jabir amewataka washiriki wa mafunzo hayo kujenga moyo wa kujitolea kwani katika kufundisha mara nyingi hujitokeza matatizo mengi.

Kwa upande wao waalimu waliopata mafuzo hayo Mussa Abdulrab na Arafa Talib Omar wamesema   wamejifunza mambo mengi wasioyajua na kuahidi kuwa watayafanyia kazi.
Mafunzo hayo ya siku tano ya walimu wa michezo wa skuli mbali mbali za  Zanzibar yameandaliwa na Kamati  Tanzania.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles