Yuda James Mkazi wa Kibena Anayedaiwa Kupigwa na Kujeruhiwa Mkono na Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wakiongozwa na Erasto Ngole Jana.
Na Gabriel Kilamlya Njombe
Mkazi wa Kibena Yuda James Anadaiwa Kutekwa na Kupigwa na Watu Aliowataja Kuwa ni Wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Njombe na Kumsabashia Majeraha Katika Mkono Wake wa Kulia Wakimtuhumu Kuhusika na Kuchana Mabango ya Mgombea Urais Dokta John Pombe Magufuli.
Akizungumza na www.gabrielkilamlya.blogspot.com Bwana Yuda Amesema Kuwa Tukio Hilo Limemkuta Septemba 20 Mwaka Huu Akiwa Katika Mtaa wa Kibena Ambako Alijikuta Anaitwa na Mtu Aliyemfahamu Kwa Jina la Erasto Ngole na Kisha Kuingizwa Ndani ya Gari na Kupelekwa Katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Njombe Ambako Anadai Kupigwa na Kujeruhiwa Mkono Wake.
Amesema Kufuatia Tukio Hilo Alilazimika Kwenda Katika Kituo Cha Polisi Ambako Alipewa Fomu ya Matibabu PF3 na Kisha Kwenda Kutibiwa.
Mtandao Huu Umemtafuta Erasto Ngole Anayedaiwa Kufanya Tukio Hilo Ambaye Amekiri Kwenda Kumchukua Kibena na Kumpeleka Polisi na Sio CCM Kama Alivyosema Huku
Akikanusha Kuhusika Kumpiga na Kumjeruhi Mkono.
Amesema Sababu Iliyowafanya Kumfuata na Kumkamata ni Kutokana na Kuhusika Kuchana Mabango ya Chama Cha Mapinduzi CCM Ya Mgombea Urais Dokta Magufuli.
Jitihada za Kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Ili Kuthibitisha Tukio Hilo Zimegonga Mwamba Baada ya Kuelezwa Kuwa Kamanda Huyo Yupo Safarini.
Alatanga Nyagawa ni Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Njombe Ambaye Baada ya Kutafutwa Amelaani Vikali Kitendo Hicho na Kwamba Kinachotakiwa ni Kufanya Siasa za Kistaarabu na Sio Kugombana Kwa Sababu za Kuchana Mabango.
Hata Hivyo mtandao Huu Umefika Katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Njombe Ambapo Baada ya Kumkosa Katibu wa CCM Mkoa Bwana Hosea Mpagike Jitihada za Kumtafuta Kwa Njia ya Simu Zikafanikiwa Kupata Majibu Yakuwa Hana Taarifa Juu ya Tukio Hilo na Kushauri Atafutwe Mtuhumiwa Mwenyewe.