Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

SIKU YA AMANI DUNIANI-NJOMBE: VYOMBO VYA HAKI VYATAKIWA KUTENDA HAKI

$
0
0

Bwana Kyelula[Nyepe wa Nyepe]

Baadhi ya  Wakazi wa Njombe Ambao wamezungumza na www.gabrielkilamlya.blogspot.com juu ya Siku ya Amani Duniani.

Na Gabriel Kilamlya Njombe

Wakati Tanzania Ikiungana na Mataifa Mengine Dunia Kuadhimisha Siku ya Amani Hii Leo,Wananchi Mkoani Njombe Wamekuwa na Maoni Tofauti Juu ya Amani Katika Taifa la Tanzania.

Wakizungumza Kwa Nyakati Tofauti Baadhi ya Wananchi Hao Wakiwemo Wanasiasa Wamesema Kuwa Tanzania Imekuwa Haina Amani Bali Imekuwa na Kuvumiliana Katika Mambo Mbalimbali Yanayotendeka Katika Maeneo Mbalimbali.

Wamesema Kuwa Vyombo Vyenye Wajibu wa Kutenda Haki Vimekuwa Havitendi Haki Jambo Linaloondoa Maana Halisi ya Siku ya Amani Duniani.

Wengine Wamesema Kuwa Kutokana na Mazingira Wanayoishi Hawajakutana na Matukio Yoyote ya Uvunjifu wa Amani Hivyo Wanaamini Amani Ipo ya 
Kutosha Nchini Tanzania.

Stella Vuzo ni Afisa Habari wa Umoja wa Mataifa Ambaye Amesema Kuwa Tafiti Zinaonesha Kuwa Vita na Vurugu Mbalimbali Zinazojitokeza Zinatokana na Kutopatikana Kwa Haki Baina ya Watawala na Watawaliwa.



Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles