Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

WASANII 21 KATI 50 WAANZA MAISHA YA KIJIJINI RASMI

$
0
0
1
Katibu wa SHIWATA, Selemani Pembe (Kushoto) akisaidiana na wasanii kuingia vyombo kwenye gari la mizigo ya wasanii waliohamia kijiji cha Mwanzega, Mkuranga
(Picha na Mpiga Picha Wetu)
2
Baadhi ya wasanii wakielekea kulima eneo la makazi waliyofikia katika kijiji cha wasanii Mwanzega, Mkuranga jana kwa ajili ya maandalizi ya kuanza maisha mapya ya kijijini.
3
Gari aina ya pick Up likiwa limesheheni magodoro, majembe, ndoo, na mabegi ya nguo za wasanii wakiondoka jijini Dar es Salaam jana kwenda kuanza maisha mapya kijiji cha wasanii Mwanzega Mkuranga.
4
Mmoja wa wasaniii Bibi Mrangi akisafisha vyombo na wenzake wakiandaa vitafunio vya chai katika kijiji cha Mwanzega Mkuranga jana.
…………………………………………………………………………………………
Na Peter Mwenda
WASANIII 21 kati ya 50 walioamua kwenda kuanza maisha mapya katika kijiji cha Wasanii Mwanzega, Mkuranga wamehamia.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA), Cassim Taaalib akiongoza msafara huo jana alisema kundi la kwanza la wasanii limehamia na jingine litafuata baada ya mwezi mmoja.
Alisema wasanii hao ambao watakuwa na jukumu la kufanya mazoezi ya kuigiza filamu na tamthilia pia watakuwa wanapata mafunzo ya kilimo cha bustani na kufanya mazoezi ya michezo mbalimbali ya soka, netiboli, basketi na michezo mingine.
Mwenyekiti Taalib alisema wasanii hao watakuwa wanapata masomo ya darasani ya kilimo kwanza na tayari SHIWATA imeandaa wataalamu kwa ajili ya
kutoa mafunzo hayo.
Wakiwa kambini hapo wasanii hao walisema hawaamini kama SHIWATA inaweza kutumia gharama kubwa kuwaandalia makazi mapya kwa ajili ya kutafuta maisha yao ya baadaye kupitia kilimo na kutumia vipaji vyao kukuza sanaa.
Mmoja wa wasanii hao, Yolanda Mussa alisema SHIWATA imeonesha njia ya kukomboa wasanii wake kwa njia ya kujitegemea hivyo anaiomba Serikali nayo iunge mkono na kuwapa nguvu taasisi hiyo ili kukiimarisha kijiji hicho ambacho baadaye kitakuwa chenye thamani kubwa kwa watanzania.
Kundi jingine la wasanii 30 wanatarajiwa kuandoka mwezi ujao baada ya kumaliza mafunzo yao ya sanaa na kilimo kwanza.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles