Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

MEMBE AWASILI NJOMBE KUOMBA WADHAMINI

$
0
0
Na Gabriel Kilamlya Njombe

Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa benard membe amesema endapo watanzania watampa ridhaa ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu ataimarisha mifumo ya masoko kwa ajili ya wakulima wa  Njombe.

Kauli hiyo  ameitoa leo Wakati akiwatafuta wadhamini katika mkoa wa njombe katika chama cha mapinduzi ccm ikiwa ni mwendelezo wa kuzunguka Mikoani akiwatafuta wadhamini hao.

Aidha membe amesema Tanzania haina sababu ya kupeleka bidhaa ambazo hazija chakatwa Nje ya nchi na kupewa tuzo kwa kufanya hivyo badala ya Kujenga Viwanda Vyetu Wenyewe.

Pamoaj na Mambo Mengine Amesema Endapo Watanzania Watampa Ridhaa ya Kuliongoza Taifa la
Tanzania Basi Suala la Ulinzi na Usalama wa Raia na Mali Zao Litapewa Kipaumbele Zaidi.

Amesema Atakachokifanya ni Kuimarisha Jeshi la Polisi Ikiwa ni Pamoja na Kuhakikisha Wageni Hawaingii Nchini Bila Utaratibu Maalumu.

Hata Hivyo Membe Baada ya Kupokea Majina ya Wadhamini Kutoka Katika Mikoa Ruvuma Mbeya na Njombe Ameelekea Mkoani Iringa Ambako Baada ya Hapo Leo Anaelekea Nchini Zanzibar Kabla ya Kwenda Bungeni Mjini Dodoma.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles