Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

DOLA MILIONI 16.4 TOKA OPEC KUNUFAISHA KAYA MASIKINI NJOMBE NA ARUSHA

$
0
0
 Kaimu mkuu wa Mkoa wa Njombe ambaye ni mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba akielezea hali halisi ya utekelezaji wa  shughuli za TASAF katika mkoa wa Njombe .
 Meneja wa miundombinu mhandisi Elisifa kinasha akielezea madhumuni ya mkutano wa TASAF awamu ya tatu.
 Meneja wa fedha Bw.Godwinne Mkisi akitoa mada juu ya uratibu wa kutuma fedha.
 Afisa wa uratibu toka TASAF bw.Quintus Kassese  akiwasilsha mada juu ya mpango wa kunusuru kaya masikini
 Katibu mkuu ofisi ya Rais Ikulu Peter Ilomo akizindua mkutano wa kazi juu ya utekelezaji wa miradi ya kupunguza umasikini ya OPEC awamu ya tatu Mjini Njombe leo.
 Baadhi ya washiriki wa mkutano wa kazi wakisikiliza na kunukuu hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo toka kwa katibu mkuu ofisi ya Rais Ikulu bw. Peter  Ilomo (Hayupo pichani).
  Mkurugenzi mtendaji wa TASAF akitoa maelezo ya utangulizi juu ya miradi ya kupunguza umasikini ya OPEC awamu ya tatu.
 Baadhi ya washiriki wa mkutano wa kazi wakisikiliza na kunukuu hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo toka kwa katibu mkuu ofisi ya Rais Ikulu bw.Peter Ilomo (Hayupo pichani).
 Mtendaji Toka TASAF Beatrice Mbyallu akiwa na Baadhi ya Watendaji wa TASAF  wakifuatilia kwa makini michango ya washiriki
 Baadhi ya Watendaji wa TASAF  wakiandaa mahitaji katika mkutano huo.
 Katibu mkuu ofisi ya Rais Ikulu Peter Ilomo (katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na watendaji toka TASAF Wakiwemo wenyeviti wa Halmashauri na Wakurugenzi watendaji
Katibu mkuu ofisi ya Rais Ikulu Peter Ilomo (katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa mkutano wa kazi kutoka Halmashauri za mkoa wa Njombe.








nNa Gabriel Kilamlya Njombe

Wakazi katika Halmashauri 13 za Mikoa ya Njombe na Arusha Wanaanza Kunufaika na Mradi wa 

Kupunguza Umaskini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF utakaogharimu kiasi cha dola za 

kimarekani milioni kumi na sita nukta nne kwa ufadhili wa OPEC awamu ya tatu.

Kaul Hiyo imetolewa Leo na Katibu Mkuu ofisi ya rais Ikulu bwana Peter Ilomo Wakati akizindua 

rasmi utekelezaji wa mpango huo wa OPEC awamu ya tatu mjini Njombe na kuhudhuriwa na Wakuu wa 

wilaya, wenyeviti wa halmashauri, wakurugenzi watendaji, wakuu wa Idara na watendaji wa TASAF 

ambao watapata fursa ya kujengewa uwezo juu ya
utekelezaji wa mpango huo kwa muda wa siku mbili.

Kaya zitakazonufaika na miradi hiyo ni zile zilizobainishwa na kuandikishwa kwenye Mpango wa 

Kunusuru Kaya Maskini katika Halmashauri zote za mkoa wa Njombe na Arusha. 

Ilomo amesema  kuwa mradi huo utatekelezwa kwa muda wa miaka mitatu pekee hivyo unapaswa 

utekelezwe kwa kasi na umakini mkubwa ili kuhakikisha fedha hizo zinatumika kwa malengo 

yaliyokusudiwa.


Pamoja na mambo mengine,mkurugenzi mtendaji wa TASAF bw.Ladislaus Mwamanga pia ametumia fursa 

hiyo kuwaonya watendaji watakaofanya kazi ya kuzibaini kaya masikini hususani katika maeneo 

ambayo hayajafikiwa kuacha kuwaweka watu ambao watakuwa hawana sifa kwa kuwa tu ni ndugu,rafiki 

au jamaa zao jambo ambalo halitofumbiwa macho hata kidogo.


Bw. Mwamanga amezitaja baadhi ya changamoto ambazo zinachangia kuwepo kwa malalamiko miongoni 

mwa wananchi kuwa ni pamoja na kuchelewa kuanza kwa mradi huo hususani kwa kaya ambazo 

zimeshafikiwa.

Miongoni mwa mambo yatakayofanyika katika miradi hiyo ni pamoja  na kutoa ajira za muda mfupi 

kwa walengwa,kuanzisha miradi endelevu ya ujasiliamal Pamoja na miradi ya elimu ya afya katika 

jamii  ambayo itatoa fursa ya kujiongezea kipato kwa wanufaika hao.

Hata hivyo jumla ya wakazi milioni 3.1 watanufaika  na miradi hiyo mara baada ya kutambuliwa 

kupitia mradi huo wa Awamu ya tatu katika mikoa hiyo miwili.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles