NG'OMBE 6 pamoja na punda watatu waumeuwawa katika mgogoro wa ardhi kwenye kijiji cha Isimani kaya ya Kihorogota wilaya ya Iringa vijijini baada ya kuwekewa sumu ya kuua panywa katika pumba katika shamba hilo lenye mgogoro .
Wakizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.co.tz baadhi ya wafugaji ambao mifugo yao imeuwawa kwa sumu hiyo walisema kuwa tukio hilo limetokea juzi majira ya asubuhi baada ya mmoja kati ya watu waliopo katika mgogoro huo wa ardhi kudaiwa kuweka sumu hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake Geofrey Sanga alisema siku moja kati ya tukio hilo mmoja kati watoto wa mwenye shamba hilo alionekana majira ya jioni katika eneo hilo ambalo hata hivyo limekuwa halilimwi kwa muda mrefu .
Hata hivyo siku ya pili yake kama kawaida alipita eneo hilo na mifugo yake kuelekea shamba na baada ya kufika eneo hilo mifugo hiyo ilikula pumba hiyo ambayo iliwekwa sumu na hivyo kupelekea kufa.
Alisema kuwa sumu hiyo ilikuwa imewekwa katika pumba ambayo ilimwagwa katika mae neo mbali mbali ya shamba hilo .
Sanga alisema kuwa kwa upande wake ni pumba watatu na ng'ombe mmoja ndio waliokufa kwa sumu hiyo wakati mwenzake Chesco Mdendemi jumla ya ng'ombe wake watatu walikufa huku NIco Kahongole sumu hiyo iliua ng'ombe wake wawili
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo diwani wa kata ya Kihorogota alisema kuwa kuwa hadi sasa tayari kuna mtuhumiwa mmoja amekamatwa huku msako wa kuwasaka wengine waliohusika na uwekaji wa sumu hiyo unaendelea kufanywa na wananchi kwa kushirikiana na jeshi la polisi .
Alisema katika eneo hilo la Isimani kumekuwa na kero kubwa ya panya na serikali iliwapa dawa ya kuua panya kutoka Morogoro ila dawa iliyotumika kuua mifugo hiyo si ile ambayo walipewa na serikali .
Alisema kuwa eneo hilo limekuwa na mgogoro kwa muda mrefu baada ya familia kutaka wananchi wanaoishi eneo hilo kuhama kwa madai kuwa eneo la hekari 300 katika kijiji hicho ni mali yao jambo ambalo tayari mahakama iliwapa ushindi wananchi hao kuendelea kuwepo eneo hilo. |