Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

KITUO KIKUU CHA UMEME KIWANDA CHA KARATASI MGOLOLO CHALIPUKO , MUFINDI ,NJOMBE NA MBEYA GIZANI

$
0
0
Transformer ya kiwanda cha karatasi mgololo yalipuka na kuwaka moto leo
Magari  yakiwa  eneo la  Kiwanda  hicho 
Moto  ukiendelea  kuwaka katika  eneo hilo la kiwanda cha karatasi mgogolo
Wananchi  wakitazama  moto  huo
MOTO  mkubwa  umeteketeza   kituo  kikubwa  cha  umeme  eneo la  Kiwanda  cha karatasi Mgololo  wilayani Mufindi mkoani  Iringa    leo na  kupelekea   wilaya  nzima ya  Mufindi ,makambako na  mkoa  wa Mbeya  kuwa gizani .

Baadhi ya  mashuhuda  waliozungumza na mtandao  wa www.matukiodaima.co.tz   wamedai kuwa  moto  huo  ambao  ulianza  kuwaka  majira ya saa 4.5 asubuhi  chanzo chake  kinadaiwa ni  hitirafu ya   mitambo hiyo ya   kusambaza  umeme .

Salum  Omary  ambae ni mmoja kati ya mashuhuda  alisema  kuwa  eneo  hilo  ndilo  lenye Transformer  kubwa  linalosambaza  umeme  katika  kiwanda  cha karatasi Mgololo ,wilaya  nzima  ya Mufindi , hadi  mkoani Mbeya.

Alisema  kutokana na mlipuko mkubwa  uliotokea  eneo hilo la Transformer  hiyo  kubwa  wafanyakazi  walilazimika   kutimua  mbio  kutoka nje ya  kiwanda   hicho  huku  kiwanda  kikizimwa  ili  kuepusha  madhara  zaidi  kutokea .

Hata    hivyo  alisema  tatizo hilo la  umeme  si rahisi  kurejea  leo ama  kesho  kwani  madhara ni makubwa  zaidi   na kuwa  upo uwezekano wa wananchi wa wilaya ya Mufindi na mkoa wa Mbeya  kuendelea  kuwa  gizani.

" Toka  eneo  lilipokuwa  Transforme hilo na  kilipo  kiwanda ni  kama  umbali wa  Km moja   hivi   hivyo  iwapo  jitihada za haraka  zisingefanyika  huenda  madhara  yangejitokeza kwa  kiwanda  hicho cha karatasi mgololo"

Meneja  wa  Tanesco  mkoa wa Iringa  hakuweza kupatikana  kuendelea madhara  zaidi  yaliyojitokeza katika  moto  huo.

Kwa  upande wake mkuu wa wilaya ya  Mufindi Evarista Kalalu amethibitisha   kutokea kwa  moto  huo na kuwa  hakuna madhara  kwa  binadamu  wala  kiwanda  hicho  cha karatasi na  kuwa  moto  huo  umezimwa na  gari la  zimamoto  la misitu ya  Sao hill .

Mkuu  huyo  wa  wilaya  alisema kuwa  kwa  sasa  wilaya ya Mufindi  hadi mkoa wa Mbeya  upo  gizani  kutokana na  tatizo hilo  kubwa la umeme .
 
Kwa hisani ya fg blog




Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles