Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all 2276 articles
Browse latest View live

ASKOFU WA ANGLICAN DAYOSISI YA NJOMBE AFARIKI DUNIA

$
0
0
Pichani  ni Askofu John Simalenga wa Dayosisi ya Njombe Kanisa la Anglikan Amefariki Dunia Asubuhi ya Saa Kumi na Moja Novemba 24 Mwaka Huu na Mazishi Yanatarajiwa Kufanyika Novemba 28 Katika Kanisa Hilo.


Taarifa Toka Kwa Msaidizi wa Askofu Huyo Mchungaji Canon Mlelwa Amesema Kuwa Marehemu Simalenga Amefariki Dunia Baada ya Kuugua Kwa Kipindi Kifupi Kwa Ugonjwa wa Malari na Kisukari Alichogundulika Kuwa Nacho na Hivyo Hadi Kifo Chake Kinamkuta Alikutwa na Malari Mbili.

Aidha Mlelwa Amesema Kuwa Marehemu Askofu Simalenga Amekufa Akiwa na Miaka 60 Ambapo Alizaliwa Mwaka 1953 Katika Kijiji cha Milo Wilayani Ludewa na Uaskofu Alipata Julai 7 Mwaka 2007 Kisha Kuwa Askofu wa 7 Wa kanisa Hilo.

Katika Hatua Nyingine Askofu Simalenga Ameacha Watoto Wanne na Mjane Mmoja.

Taarifa zaidi Juu ya Msiba Huo Zitaendelea Kukujia Kupitia Mtandao Huu.

TANZANIA NA UN ZASAINI MKATABA WA UENYEJI WA KUJENGA TAASISI YA KUHIFADHI NYARAKA ZA MAHAKAMA YA ICTR

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb), (kulia) akibadilishana mikataba na Bw. Soares mara baada ya shughuli ya uwekaji saini kukamilika.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) kulia na Mwanasheria kutoka Umoja wa Mataifa, Bw.Serpa Soares wakiweka saini Mkataba ambapo Tanzania itakuwa Mwenyeji wa Taasisi mpya ya Umoja wa Mataifa itakayojengwa mjini Arusha kwa ajili ya kuhifadhi kumbukumbu na nyaraka za iliyokuwa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda. Uwekaji saini huo ulifanyika katika Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa jijini Dar es Salaam tarehe 26 Novemba, 2013.

Kutoka kushoto ni Balozi Dora Msechu, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. James Lugaganya, Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Bibi Naomi Zegezege, Kaimu Mkurugenzi wa
Kitengo cha Sheria na Bw. Benedict Msuya, Afisa Mambo ya Nje wakishuhudia uwekaji saini huo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa katika mazungumzo na Bw. Soares mara baada ya kukamilisha shughuli za uwekaji saini. katika mazungumzo hayo, Mhe. Waziri alilishukuru Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kuichagua Tanzania kuwa mwenyeji wa taasisi itakayohifadhi kumbukumbu na nyaraka za Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda.

Mazungumzo yakiendelea huku ujumbe wa Tanzania uliokaa upande wa kulia na ujumbe wa Umoja wa Mataifa ukifuatilia mazungumzo hayo.

Bw. Soares akisisitiza jambo huku Mhe. Membe akisikiliza kwa makini. wengine katika picha ni ujumbe wa Tanzania uliokaa upande wa kulia na ujumbe wa Umoja wa Mataifa uliokaa upande wa kushoto.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiagana na Bw. Soares mara baada ya shuguli ya uwekaji saini kukamilika 

Picha na Philip Kisaka

Article 1

$
0
0
 Mwenye Kofia ya CCM  Katikati Ni Bwana Hosea Mposola Ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Itulahumba Licha ya Kwamba Hawamtaki Kuongoza Kijiji Hicho.
 Baadhi ya Wananchi Walioonekana Kukerwa na Kitendo cha Uongozi wa Kata Hiyo Kuahirisha Mkutano Huo.
 Diwani wa Kata ya Mdandu Bi.Annaupendo Gombela Akizungumzia Hali ya Maendeleo Kwenye kijiji cha Itulahumba Leo na Kwamba Endapo Wananchi Wataendeleza Migogoro Watakuwa Nyuma Kimaendeleo.

 Hii ni Baadhi ya Picha Iliyoonesha Idadi ya Watu Licha ya Kwamba Camera ya Mtandao Huu Kuwakosa Baadhi ya Watu Waliokuwa Kwenye Engo Tata.
 Diwani wa Kata ya Mdandu Bi.Annaupendo Gombela Akizungumza Baada ya Kuahirishwa Kwa Mkutano Huo
Afisa Mtendaji wa Kata ya Mdandu Bwana Fute Akitolea Ufafanuzi wa Kisheria Juu ya Mikutano ya Hadhara Hususani Katika Suala la Idadi ya Mahudhurio.


Na   Gabriel  Kilamlya

Mpango wa Wananchi wa Kijiji cha Itulahumba Wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe Juu ya Kutaka Kumtoa Madarakani Mwenyekiti wa Kijiji Hicho Bwana Hosea Mposola Umegonga Mwamba Baada ya Uongozi wa Kata Uliopanga Kusuluhisha Mgogoro wa Wananchi hao na Serikali Yao Kuahirisha Mkutano Kwa Kile Kinachodaiwa ni Kuwepo Kwa Mahudhurio Hafifu ya Wananchi.

Hatua Hiyo  ya Kutaka Kumfukuza Madarakani Mwenyekiti Huyo Ilianza Tangu Mwezi wa Tisa Mwaka Huu Baada ya Wananchi Hao Kumtuhumu Mwenyekiti Huyo Kwa Mambo Mbalimbali Ikiwemo Kumhamisha Afisa Mtendaji Wao Kimyakimya na Kumleta Afisa Mtendaji Ambaye Wao

Hawamtaki.

Aidha Pamoja na Idadi Kubwa ya Wananchi Waliojitokeza Kushiriki Mkutano Huo Tofauti na Siku Nyingine Kwa Mujibu wa Maelezo ya Wananchi Hao,Uongozi wa Kata ya Mdandu Ukiongozwa na Diwani wa Kata Hiyo Bi.Annaupendo Gombela na Afisa Mtendaji wa Kata Hiyo Ulilazimika Kuahirisha Mkutano Huo Hadi Juma Tano ya Wiki Ijayo Ukidai Hauwezi Kusimamia Maamuzi Magumu ya Kumtoa Madarakani Mwenyekiti Bila Kufuata Sheria ya Kutokamilika Kwa Idadi ya Watu Waliohudhuria Mkutano Huo.

Kufuatia Hali Hiyo Wananchi Hao Wakaanza Kuzungumza Kuwa Kitendo cha Kuahirisha Mkutano Huo Ilihali Hakuna Shughuli Za Kimaendeleo Zinazofanyika ni Kuwakatisha Tamaa Kwani Hadi Sasa Kijiji Hicho Kimeonekana Kutokuwa na Uongozi Baada ya Mwenyekiti Huyo na Afisa Mtendaji wa Kijiji Kukataliwa Kufanya Kazi Kijijini Humo.

Pamoja na Mambo Mengine Wananchi Hao Wamesema Licha Ya Kuahirishwa Kwa Mkutano Huo Uliolenga Kumfukuza Mwenyekiti Huyo Lakini Bado Hawamtaki na Endapo Serikali Haitachukua Hatua za Haraka Kutatua Mgogoro Huo Basi Wametishia Kufanya Maandamano Makubwa Hadi Kwa Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe.

Hata Hivyo Kwa Upande Wake Mwenyekiti wa Kijiji Hicho Bwana Hosea Mposola Amesema Kuwa Tuhuma Wanazomtuhumu Hadi Sasa Hazina Ukweli Wowote Hivyo Hawezi Kuachia Madaraka Bila Maelezo Ya Kina.


Article 0

$
0
0

MWALI AMVUNJA KIDOLE MWANAFUNZI WAKE MBEYA. 

Jacline Staniely[9] akiwa nyumbani baada ya kutoka hospitali kutibiwa
Picha ya Xray ikionyesha Kidole cha kati kilichovunjika
Pf3 ya polisi

Wiki ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na watoto ikiwa imeanza kuadhimishwa duniani Novemba 25 mwaka huu bado vitendo hivyo vimezidi kushamiri Mkoani Mbeya ambapo mwanafunzi wa darasa la nne shule ya msingi Aiport Kata ya Iyela jijini Jacline Staniely[9] kuumizwa mkono wake wa kushoto.

Jacline akiongea kwa ridhaa ya mama yake amesema alipigwa kwa kutumia ubao na mwalimu wa shule hiyo Novemba 19 mwaka huu na mwalimu Kanyika kwa kosa la kuwa na nywele ndefu.
Mwanafunzi huyo amedai kuwa siku ya tukio alipigwa vibaya na kumsababishia maumivu makali ambapo siku hiyo mama yake alikuwa safarini Nairobi Kenya hivyo hakupata matibabu ambapo alilazimika kumwambia mwalimu jirani[Bibi]ambaye alimpeleka hospitali kutibiwa.
Hata hivyo Jackline amesema kuwa kutokana na maumivu makali alilazimika kufanya mtihani wa Taifa wa darasa la nne bila kupata matibabu ya kutosha.

Baada ya kurejea kutoka safari mama yake mzazi aitwae Rehema Adamson Ndeje[28] mkazi wa Block T jijini Mbeya amesema baada ya maumivu ya mwanae usiku ilimlazimu kwenda shuleni ili kujua kulikoni,ndipo alipoonana na mwalimu Kanyika baada ya kukutanishwa na Mwalimu mkuu.

Mama Jackine amesema hicho ni kipigo cha tatu kukubwa kwa mwanae kupigwa na mwalimu huyo ambapo alionesha makovu yaliyodaiwa yalitokana na vipigo vya mwalimu huyo miguuni akidai majeraha hayo yalidumu kwa miezi mitatu.

Hata hivyo Rehema aliamua kwenda Polisi Mwanjelwa kutoa taarifa za tukio na kila alipoitwa mwalimu huyo hakutokea ndipo jalada likapelekwa kituo kikuu cha kati ambapo mwalimu alikamatwa na mhanga kupewa PF 3 kwa ajili ya matibabu ambapo alipigwa picha na kuonekana moja ya kidole cha kati cha kushoto kuoneka kuathirika kutokana na kupigwa kwa kutumia ubao.

Mzazi huyo amesema hana ni mbaya na mwalimu Kanyika lakini kitendo cha kumwadhibu mwanae mara kwa mara ndicho kimemtia shaka hata kuamua kutoa taarifa Polisi ili sheria ichukue mkondo wake.
Mwandishi wa habari hii alipofika shuleni ili kujua mustakabali wa suala hili mwalimu alitoa nje mwandishi akidai yeye ana majukumu mengine lakini baada ya kufuatilia mkuu huyo alichukua gari lake aina ya RAV 4 na kwenda nyumbani kwa Mzazi wa mtoto na kwenda naye hospitali akiwa ameambatana na mmoja wa walimu wa shule hiyo ambaye ni jirani ambapo Jackline humwita Bibi.

Mwandishi alimtafuta mmoja wa wanaharakati wa kijinsia ambaye alikiri kupokea lalamiko hilo ingawa alijibu kwa mkato kuwa mtoto huyo kaumia kidogo tu na ni usanii mtoto huyo kufungwa POP na kwamba bado PF3 haijajazwa kitu hivyo hawezi kuzungumzia lolote.

Kumekuwa na malamiko mengi katika Dawati hilo kutokana na matukio kutochunguzwa kwa wakati hali inayotoa mwanya kwa vitendo hivyo kuibuka mara kwa mara na wahalifu kutoroka mkono wa sheria lakini baadhi kuwa na utendaji duni licha ya taarifa kutolewa kwa wakati.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya ameahidi kulifuatilia suala hilo na ikibainika mtuhumiwea atafikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma zinazomkabili.

Na Ezekiel Kamanga 
Mbeya yetu

Article 4

$
0
0

CHADEMA WATOA BARUA KWA WANACHAMA WAKE WATATU WALIOVULIWA UONGOZI 


Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimesema kimewaandikia barua aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Zitto Kabwe na Mjumbe wa kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo ambazo wanapaswa kujieleza kwa siku kumi na moja, kisha watapata fursa kujieleza mbele ya kamati kuu maalumu kwa nini wasifukuzwe kutoka Chamani.
Akizungumza katika makao makuu ya chama hicho, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, John Mnyika alisema barua hizo zipo tayari na wahusika watapatiwa wakati wowote kuanzia leo.
Mnyika alikuwa akitoa taarifa ya kikao cha Utekelezaji cha sekretarieti ya chama hicho iliyoketi baada ya mkutano wa kamati kuu iliyoketi tarehe 20 – 22 Novemba mwaka huu.
Ni katika Mkutano huo, Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho, Tundu Lissu alisema kuwa mkutano uliofanywa na Zitto na Dk 
Kitila mbele ya waandishi hawajazungumzia tuhuma zinazowakabili, badala yake walichofanya ni  kujitungia tuhuma ambazo kimsingi sizo zilizowavua nafasi zao.
Lissu alisema, Zitto na Dk Kitila hawakusimamishwa nyadhifa zao kwa masuala ya PAC, Uchaguzi wa mwaka 2010, wala kutoshiriki kwenye operesheni za chama au sababu nyingine, na walitaja  hizo sababu ili kupotosha tuhuma zinazowakabili kwa jamii: “walichokifanya kina Zitto na Kitilla ni "Diversion" (kubadili mwelekeo) wa  mashtaka yao yanatokana na waraka wa kihaini wa mabadiliko ambao ni kinyume na katiba, kanuni na maadili na itifaki ya Chama.  anawaambia waandishi, "wamevuliwa nafasi zao na kamati kuu kwa sababu ya waraka wenye nia ovu" alisema Lissu.
Aliongeza kuwa CHADEMA kina mwongozo wa uchaguzi uliopitishwa na kamati kuu, Zitto na Kitila wanaufahamu ingawa haijulikani ni kwa nini wao walienda kinyume na mambo yanayojadiliwa katika kamati kuuu
Aidha, Lissu alieleza kuwa Dk Kitilla anapotosha umma na wanachama kwa kauli yake kuwa Kamati Kuu haina mamlaka ya kumvua yeye nafasi yake ya Ujumbe wa Kamati Kuu maana amechaguliwa na Baraza Kuu. Alimtaka Kitila na Zitto waangalie vyema katiba ya Chama hasa majukumu ya Kamati Kuu, pale yanaporuhusu mwanachama yeyote kusimamishwa au kufutiwa uachama haraka kama Kamati Kuu itaona kuna umuhimu wa kufanya hivyo.
Kigaila alisema, Kamati kuu iliyoketi Novemba 20-22/2013 ilipitisha ratiba ya uchaguzi wa ndani ya chama kama ifuatavyo:-

  • 22/11/2013 - 14/12/2013 ni kukamilisha zoezi la usajili wa  wanachama, 15 Desemba hadi 15 Januari uchaguzi ngazi za vitongoji, 16 hadi 30 Januari 2014 Rufaa na ukaguzi, ambapo tarehe 01 hadi 15 Februari ni uchaguzi wa matawi.


  • CHADEMA pia ilisema 16 hadi 29 Februani ni kusikiliza rufaa na ukaguzi, ambapo uchaguzi wa majimbo utaanza rasmi 1 hadi 10 Aprili, huku uchaguzi ngazi ya Wilaya ukitarajiwa kufanyika 25 Aprili hadi Mei 5 mwaka 2014, na ngazi ya Mikoa ni 20 hadi 25 Mei.


  • Uchaguzi wa kanda unatarajiwa kufanyika Julai 9, na haada ya hapo Julai 23 hadi 30 utakuwa ndiyo muda wa uchaguzi ngazi ya Taifa, utakaoanza na Baraza la Wazee, Baraza la Vijana, Baraza la Wanawake kisha Uchaguzi wa ndani ya Chama.

MUME ADAIWA KUMUUWA MKEWE NJOMBE .

$
0
0
 Mwanamke Aliyeuawa Kwa Kukatwa Kichwani Njombe.
 Pichani ni Anjelika Mhenga Aliyeuawa na Mtu Anayesadikika Kuwa ni Mumewe Jana Majira ya Saa Tatu Asubuhi Mtaa wa Idundilanga Eneo la Ujamaa B Mjini Njombe.

Mtuhumiwa wa Mauaji ya Anjelika Mhenga Bwana Elia Mtweve Mkazi wa Kijiji cha Mkiu Wilayani Ludewa Aliyetoroka Baada ya Kudaiwa Kumuua Mke Wake Njombe.


Na  Gabriel  Kilamlya  Njombe

 Mtu Mmoja Mkazi wa Matembwe Wilayani Njombe Anjelika Mhenga Mwenye Umri wa Miaka 37 Amekutwa Amefariki Dunia Baada ya Kupigwa na Kitu Chenye Ncha Kali Sehemu za Kichwani na Mtu Anayesadikika Kuwa ni Mumewe Katika Eneo la Ujamaa "B" Mtaa wa Idundilanga Mjini Njombe.

Akizungumza na www.gabrielkilamlya.blogspot.com Kaka wa Marehemu Huyo Bwana Joseph Mhenga Amesema Kuwa Tukio la Mauaji ya Dada Yake Limetokea Jana Novemba 26 Mwaka Huu Majira ya Saa Tatu Asubuhi Baada ya Kupata Taarifa Kwa Njia ya Simu na Mdogo Wake Ambaye Alieleza Kuwa Naye Kapigiwa Simu na Shemeji Yake Kuwa Amegombana na Mkewe Hivyo Ameamua Kusafiri.

Aidha Bwana Mhenga Amesema Kuwa Shemeji Yake Huyo Anayedaiwa Kuhusika na

Mauaji Hayo Anafahamika Kwa Jina la Elia Mtweve Mwenye Umri wa Miaka 41 Mkazi wa Kijiji cha Mkiu Wilayani Ludewa Ambao Wote Kwa Pamoja Walikuwa Wakiishi Njobe Kama Mume na Mke.

Amesema Kuwa Hakuna Taarifa Zozote za Sababu za Kutokea Kwa Tukio Hilo Walizozipata Zaidi ya Taarifa za Ugomvi Waliokuwa Nao Licha Ya Kwamba Hata Ugomvi Huo Haifahamiki Ulitokana na Nani.

Kwa Upande Wake Balozi wa Eneo La Ujamaa 'B' Mtaa wa Idundilanga Bi.Catherine Nyatto Amesema Kuwa Baada ya Kupata Taarifa za Tukio Hilo Akafika na Kubaini Tukio Hilo Baada ya Kukuta Milango Yote Imefungwa Kwa Nje Ndipo Alipochukua Jukumu la Kuvunja Mlango Mmoja wa Nje na Kisha Kwenda Kutoa Taarifa Polisi.

Hata Hivyo Mwili wa Marehemu Anjelika Mhenga Umeruhusiwa Kuzikwa Leo Huko Matembwe Tarafa ya Lupembe Ambako Ndiko Nyumbani Kwao.

KILA MSIMU UNAKARAHA ZAKE

$
0
0
BARABARA YA LUPEMBE NJOMBE YAANZA KUWA KERO SASA.

 Msimu wa Kuharibika Kwa Miundombinu ya barabara Mkoani Njombe Ndio Huu.

Haya ni Magari Yaliyokwama Kutokana na Mvua Zilizoanza Kunyesha Siku Chache Zilizopita Hadi Sasa Katika Barabara ya Lupembe Huko Kidegembye.

Pamoja na Jitihada Kubwa za TANROAD Mkoa wa Njombe Katika Kushughulikia Suala la Miundombinu ya Barabara Lakini Hali ya Hewa Hususani Msimu wa Masika Huleta Adha Kubwa Katika Masuala ya Mawasiliano ya Barabara.

Mwandishi wa www.gabrielkilamlya.blogspot.com Bwana Prosper Mfugale Amefanikiwa Kunasa Matukio yanayoonekana Kwenye Picha Hizo Hapo Juu.

Article 1

$
0
0
SACCOS ZINAZO SINZIA KUFUTIWA USAJIRI NJOMBE.

Na Gabriel Kilamlya Njombe

Halmashauri ya Mji wa Njombe Imesema Itavifutia Usajili Vyama Vyote Vya Ushirika Vya Kuweka na Kukopa Ambavyo  Vimeshindwa Kujiendesha Kutokana na Uzembe wa Unaofanywa na Viongozi wa Bodi na Watendaji wa Vyama Hivyo.

Miongo Mwa Vyama Ambavyo Viko Katika Hatari ya Kufutiwa Usajili Wake ni Pamoja na Wahenga na Njoluma Saccos Ambavyo Vimeonekana Kupoteza Mwelekeo wa Malengo ya Vyama Vya Ushirika Ikiwemo Kukuza Uchumi wa Mwanachama Mmoja Mmoja na Taifa Kwa Ujumla Hali Inayopelekea Wanachama Wake Kusambaa.


Akizungumzia  Maendeleo ya Vyama Vya Ushirika Vya Kuweka na Kukopa , Afisa Ushirika Halmashauri ya Mji wa Njombe William Kinyaga Amesema Vyama Hivyo Vinaendelea Vizuri Licha ya Kuwepo Kwa Baadhi ya Changamoto Zinazovikabili Vyama Hivyo.

Bwana Kinyaga Amezitaja Baadhi za Changamoto Hizo Kuwa ni Pamoja na Masuala ya Kifedha Kutokana na Vyama Hivyo Kutegemea Zaidi Mikopo ya

Nje Badala ya Mikopo ya Ndani Hali Inayopelekea Kufilisika Kwa Mtaji wa Vyama Kutokana na Madeni Mengi na Makubwa Kutoka Nje.

Halmashauri ya Mji wa Njombe Ina Jumla ya Vyama 20 Vya Ushirika Vinavyojihusisha na Masuala ya Kuweka na Kukopo Huku Vyama Viwili  Vya Wahenga na Njoluma Saccos Vikionekana Kufa.


WAZIRI MKUU PINDA KUHUDHURIA MAZISHI YA ASKOFU SIMALENGA NJOMBE KESHO

$
0
0
 
Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda Kushiriki Mazishi ya Askofu Simalenga Kesho  Askofu John Simalenga Enzi za Uhai Wake.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Kesho Anatarajia Kushiriki Mazishi ya Aliyekuwa Askofu wa Kanisa la Anglikan Njombe 

Askofu John Simalenga Alifariki Dunia Majira ya Saa Kumi na Moja Asubuhi Novemba 24 Mwaka Huu Baada ya Kuugua Kwa Muda Mfupi Ugonjwa Malaria na Kisukari.

Marehemu Askofu Simalenga Amekufa Akiwa na Miaka 60 Ambapo Alizaliwa Mwaka 1953 Katika Kijiji cha Milo Wilayani Ludewa na Uaskofu Alipata Julai 7 Mwaka 2007 Kisha Kuwa Askofu wa 7 Wa kanisa Hilo.
Katika Hatua Nyingine Askofu Simalenga Ameacha Watoto Wanne na Mjane Mmoja.
Taarifa zaidi Juu ya Msiba Huo Zitaendelea Kukujia Kupitia Mtandao Huu.

Simanzi Zatanda Mazishi ya John Simalenga wa Anglican Njombe.

$
0
0

SPIKA WA BUNGE NA WAZIRI MKUU PINDA WAMZIKA ASKOFU SIMALENGA NJOMBE LEO.

 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muunghano wa Tanzania Mizengo Pinda Amewaongoza Viongozi wa Serikali , Dini Pamoja na Wananchi Katika Mazishi ya Aliyekuwa Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Njombe John Andrew Simalenga Yaliyofanyka Leo Katika Kanisa la Anglikana Mjini Njombe

Akizungumza Wakati wa Mazishi Waziri Mkuu Pinda Amesema Taifa Limepoteza Kiongozi Shupavu wa Dini Ambapo Amewaomba Waumini Pamoja na Familia ya Marehemu Kuwa na Uvumilivu na Mshikamano Katika Kipindi Hiki cha Majonzi.

Kwa Upande Wake Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi.Anna Makinda Amewapongeza Wananchi na Waumini Kwa Ushiruikiano Waliouonesha Huku Akielezea Jitihada Mbalimbali Zinazofanywa na Viongozi wa
Dini Katika Kusisitiza Suala la Kudumisha Amani ya Nchi.

Mapema Akiwakaribisha Viongozi Mbalimbali Kutoa Salaam Zao Askofu Mkuu wa Anglikana  Tanzania  Jacobo Chimeledya Amewashukuru Viongozi Pamoja na Wananchi Waliofika Kushiriki Katika  Mazishi Hayo  na  Kuwataka Waumini Kuendelea Kuonesha Umoja  na Mshikamano.

Askofu John Simalenga alifariki dunia akiwa nyumbani kwake mnamo November 24 mwaka huu na baada ya hapo mwili wa marehemu ulikwenda kuhifadhiwa katika hospitali ya Ilembula na Mazishi yamefanyika leo katika kanisa hilo diosisi ya kusini.



Article 0

$
0
0

MAELFU TUNDUMA WALIA NA MBOLEA YA MINJINGU MAZAO KWA VIONGOZI WA CCM TAIFA.

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutumia maelfu ya wananchi katika Uwanja wa Shule ya Msingi Mwaka, mjini Tunduma, wilayani Momba, jioni hii, Nov 28, 2013, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kuzungumza nao njia ya kuzitatua, katika mkoa wa Mbeya.
 Wananchi wakiwa wamembeba Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakati wa mkutano mkubwa wa hadhara uliohudhuria na maelfu ya wananchi katika uwanja wa shule ya msingi Mwaka mjini Tunduma wilayani Momba mkoani Mbeya, leo
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye 'akihutoa dozi' alipohutubia katika mkubwa wa hadhara uliohudhuria na maelfu ya wananchi katika uwanja wa shule ya msingi Mwaka mjini Tunduma wilayani Momba mkoani Mbeya, leo
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akitoa 'dozi' katika mkutano mkubwa wa hadhara uliohudhuria na maelfu ya wananchi katika uwanja wa shule ya msingi Mwaka mjini Tunduma wilayani Momba mkoani Mbeya, leo
 Dk. Asha-Rose Migiro akihutubia maelfu ya wananchi katika mkutano uliofanyika  Uanja wa shule ya  Mwaka, Tunduma,leo
Katibu wa NEC, Siasa na Uhisiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (katikati mwenye  miwani) akiselebuka na wananchi kwenye mkutano, Uwanja wa shule ya  Mwaka, Tunduma leo. 

kwa Hisani ya michuzi blog

Article 3

$
0
0




 Makamu Mwenyekiti wa Makambako Saccos Bwana Yohan Mangolai Akisoma Taarifa ya Chama Kwenye Mkutano Mkuu wa
Mwaka.

 Wanachama wakiendelea Kujadili Juu ya Simu Zao.
 Makamu Mwenyekiti Makambako SACCOS Akitoa Taarifa ya Mwaka ya SACCOS Hiyo.

Baadhi ya Wanachama wa Makambako SACCOS Wakizungumza Kwenye kikao cha mkutano mkuu wa Mwaka Mjini Makambako.

Katika Hali Isiyo ya Kawaida Wanachama wa Chama cha Ushirika Cha Makambako SACCOS Mkoani Njombe Wameutupia Lawama Uongozi wa SACCOS Hiyo Ikiwemo Bodi Kwa Kushindwa Kusimamia Vizuri Chama Hicho Baada ya Kuonekana Kikileta Mitafaruku Mikubwa Ndani ya Chama

Makambako SACCOS ni Miongoni Mwa SACCOS Mia Moja Zilizopo Kwa Mujibu wa Takwimu za Kipindi Cha Kuanzia Mwezi Mei Mwaka Huu Ambapo Chama Hicho Kimeoneka Kuwa na Kero Kubwa Katika Uendeshaji Wake Kutokana na Uongozi Wake Kushindwa Kuwajibika.

Miongoni Mwa Matatizo Makubwa Yaliyobainika Hapo Jana Kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka wa SACCOS Hiyo Ndani ya Chama Hicho Ni Pamoja na Chama Kuwa na Madeni Makubwa Kuliko Faida Hali Inayopelekea Wanachama Hao Kuutupia Lawama Uongozi wa Bodi Hiyo.

Hadi Sasa Chama Hicho Kimeonekana Kuwa na Mikopo Zaidi ya Shilingi Milioni Mia Tatu Kitu Ambacho Kimeonekana Kuwa Hakuna Usimamizi Thabiti Katika Utoaji wa Mikopo Hiyo.

Yohan Mangolai ni Makamu Mwenyekiti wa SACCOS Hiyo Ambaye Amesema Hali Inatokana na Wanachama Wengi Kuchukua Mikopo Mikubwa Kisha Kushindwa Kuirejesha Kwa Wakati.

Bwana Mangolai Amesema Kuwa Baadhi ya Changamoto Zilizopo Katika Chama Hicho ni Pamoja na Baadhi ya Wanachama Kukimbilia Mahakamani Kuzuia Maamuzi ya Chama Kinapotaka Kuuza Dhamana Zao Kisha Kuleta Matatizo Makubwa Katika Uendeshaji wa Chama Pamoja na Kupoteza Muda Mwingi Katika Ufuatiliaji wa Kesi Hizo.

Baadhi ya Wadau wa SACCOS Hiyo Wamesema Endapo Uongozi Huo Hautachukua Hatua za Makusudi Kujitathmini Katika Utendaji wao na Kufuatilia Madeni Hayo Basi Chama Hicho Kinaweza Kufa.
  .....................................................................................................................

Article 2

$
0
0

Wazazi waja Juu,Walimu Watishia Kuhama.


 Hii ni Taswira ya Shule ya Msingi Itulahumba
 Pichani ni Mwalimu Mkuu Anayetarajia Kustaafui Januari Mwakani Akiwa Katika Shule ya Msingi Itulahumba


 Baadhi ya Wazazi Waliokutana na Mtandao huu wa www.gabrielkilamlya.blogspot.co na Kisha kutoa Kero zao juu watoto wao Shuleni Hapo.

 Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Itulahumba Wilayani Wanging'ombe
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Itulahumba Bwana Ally Masawe Akitolea Ufafanuzi Juu ya Malalamiko ya Baadhi ya Wazazi Wakiwatuhumu Kuwatumikisha Watoto Wao.

Baadhi ya Wazazi wa Wanafunzi Katika Shule ya Msingi Itulahumba Mkoani Njombe Wamelalamikia Kitendo cha Walimu Kuwatumikisha Katika Kazi zao Pamoja na Kazi za Shule Hali Inayopelekea Kuibuka Kwa Chuki Miongoni Mwao na Walimu.

Wazazi Hao Wamesema Kuwa Watoto Wao Wamekuwa Wakifanya Kazi za Walimu na za Shule Kinyume na Taratibu Kwani Wakati Mwingine Wamekuwa Wakishinda Shambani Hadi Majira ya Saa Kumi na Mbili Jioni

Aidha Wamesema Kuwa Pamoja na Mambo Mengine Wamekuwa Wakiwatumia Watoto Hao Katika Shughuli zao za Nyumbani Kwa Kuwaambia Wawe Wanawachotea Maji,Kutafuta Kuni Pamoja na

Kupanda Mashamba Yao.


Wamesema kuwa Pindi wanapohoji Walimu Hao Hutishia Kuhama Shule Ili Wawaachie Watoto Wao.

 Ally Ahmed Masawe Ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Itulahumba Ambaye Amekiri Kuwa Wanafunzi Hao Huwasaidia Katika Shughuli za Kupanda,Kuchota Maji na Kuokota Kuni Lakini Kulima Wanalima Wenyewe Kwa Kuweka Vibarua Kutokana na Muda Mwingi Walimu Hao Kuutumia Kuwafundisha Watoto Hao.


Ameongeza Kuwa Hata Hivyo Kikao cha Wazazi Kiliridhia Wanafunzi Hao Wawe Wanawasaidia Katika Shughuli Ndogondogo.

Kituo Hiki Kilifika Shuleni Hapo na Kushuhudia Wanafunzi Wakiendelea Kupanda Shamba la Shule Wakati wa Masomo Kwa Kile Kilichoelezwa Kuwa Tayari Wameshamaliza SILABASI Hivyo Wanapanda Shamba Hilo Kama Maandalizi ya Kufunga Shule.

Na  Gabriel Kilamlya WANGING'OMBE.

Article 1

Article 0


Article 3

$
0
0

1331 WAHITIMU FANI MBALIMBALI KATIKA CHUO CHA SERIKALI ZA MITAA HOMBOLO DODOMA



 Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi (wa pili kulia ) mwenyekiti wa bodi ya chuo cha serikali za mitaa Hombolo Ndg. Ramadhani  Khalfan (kulia ) , meza kuu na halaiki yote iliohudhuria mahafali ya tano chuoni hapo wakiimba wimbo wa taifa tayari kuanza mahafali.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi kwa mamlaka aliyopewa akitunuku astashahada na stashahada kwa jumla ya wahitimu 1331 walihitimu fani za utawala,  usimamizi rasilimaliwatu, uhasibu na fedha na maendeleo ya jamii katika mamlaka ZA serikali za mitaa, katika chuo CHA serikali za mitaa hombolo jana,  Mkuu wa Mkoa alifanya kazi hiyo kwa niaba ya Waziri wa TAMISEMI.
 Baadhi ya wahitimu  wakipongezana kwa furaha baada ya kumalizika kwa mahafali ya tano ya chuo CHA serikali za mitaa Hombolo.

PICHA ya pamoja Mkuu wa Mkoa, bodi ya chuo, uongozi wa chuo, wanataaluma na wwfanyakazi wa chuo CHA serikali za mitaa hombolo mud mfupi baada ya kumalizika kwa mahafali ya tano chuoni hapo. 

Picha na Jeremiah Mwayoma, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma.A

Article 2

$
0
0

WAFANYABIASHARA NJOMBE NAO WAGOMEA MASHINE ZA EFD.


MENEJA WA TRA MKOA WA NJOMBE NA IRINGA BI ROSARIA MWENDA AKIWA NA MAAFISA TRA WENGINE WA MKOA WA NJOMBE NA IRINGA NA HAPA AKIJIBU MASWALI YA WAFANYABIASHARA KATIKA SEMINA ILIYOFANYIKA UKUMBI WA TURBO MJINI NJOMBE

WAFANYABIASHARA  WA NJOMBE MJINI  WAKIWA KATIKA UKUMBI WA TURBO WAKIMSIKILIZA MUWEZESHAJI WA TRA

Na Michael Ngilangwa Njombe.


Sakata la Wafanyabiashara la Kupinga Matumizi ya Mashine za Kodi Kielektroniki za  Kutolea Stakabadhi za EFD Limezidi Kushika Kasi Hapa Nchini Ambapo Hapo Jana Wafanyabiashara Mjini Njombe Wamepinga Matumizi ya Mashine Hizo Huku Wakitoa Mapendekezo Juu ya Mashine Hizo.

Miongoni Mwa Mapendekezo Waliyoyatoa Wafanyabiashara Hao ni Pamoja na Kuangalia  Upya Sheria Hiyo na Kuiomba Serikali Kulirudisha Bungeni Suala Hilo Ili Lijadiliwe Upya Huku Wakiishauri Serikali Kutoa Mashine Hizo Bure Kwa

Wafanyabiashara.

Akiongea Kwenye Semina Iliyoitishwa na TRA Mkoani Njombe Iliyolenga  Mfumo wa Matumizi ya Mashine za Kodi za EFD Katika Awamu ya Pili , Wafanyabiashara Hao Wameelezea Sababu za Kupinga Kutumia Mashine Hizo Kuwa ni Pamoja na Gharama Kubwa Ikilinganisha na Mitaji ya Wafanyabiashara Hao , Kukosa Baadhi ya Vifaa Ikiwemo Karatasi na Mafundi wa Kuzifanyia Matengenezo za Mashine Hizo Pindi Zinapoharibika.

Akijibu Baadhi ya Maswali na Hoja za Wafanyabaiasahara Hao Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA  Mkoa wa Njombe na Iringa Bi. Rosaria Mwenda Amesema Baadhi ya Hoja Zao Zitafikishwa Katika Sehemu Husika Hususan Suala la Mashine za EFD Ambalo Litarudishwa Bungeni Ili Lijadiliwe Upya na Kuangali Namna Gani Wafanyabiashara Hao Wataridhia.

Leo Tamambele ni Afisa Mtendaji wa TCCIA na Kiongozi  wa Wafanyabiashara  Mkoani Njombe Ambaye Ameahidi Kuwaita Viongozi Husika Kwa Lengo la Kujibu Kwa Kina Hoja na Maswali ya Wafanyabiashara Hao  Huku Akiitaka Serikali Kushirikiana na Wananchi na Wadau Wengine Katika Kutunga Sheria Ili Kuondoa Mkanganyiko Kati ya Serikali na Wananchi


Article 1

$
0
0

Maalim seif ahudhuria mahafali katika skuli ya Daarul Arqam iliyoko Kigamboni Dar es Salaam, ahani msiba wa Mhe Philip Mangula leo.

Baadhi ya wahitimu wa kidato cha nne katika skuli ya Daarul Arqam iliyoko Kigamboni Dar es Salaam.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika ya pamoja na uongozi wa skuli pamoja na baadhi ya wahitimu wa skuli ya Daarul Arqam iliyoko Kigamboni Dar es Salaam.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akitia saini kitabu cha maombolezi kufuatia kifo cha mtoto wa Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara)  Peter Philip Mangula.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akimpa pole Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara)  Bw. Philip Mangula, alipofika nyumbani kwake Ostabey Dar es Salaam, kufuatia kifo cha mtoto wake Peter Philip Mangula. (Picha na Salmin Said, OMKR)

Article 0

$
0
0

MGOGORO WA  ZIWA NYASA KATI YA TANZANIA NA MALAWI WAANZA KUFUMBULIWA.

ZiwaNyasaPhoto_730b3.jpg
Malawi na Tanzania zimewasilisha ushahidi na majibu ya maswali kuhusu umiliki wa maeneo kwenye Ziwa Nyasa, kwa jopo la wasuluhishi linaloongozwa na Rais mstaafu wa Msumbiji Joachim Chissano.

Wasuluhishi hao walizitaka Malawi na Tanzania kutoa majibu ya maswali manne muhimu, wakati wakiwasilisha ushahidi wao kuhusu umiliki wa ziwa hilo wenye mgogoro.

Mgogoro huo uliibuka baada ya Serikali ya Malawi bila kushauriana na Tanzania kutoa leseni kwa kampuni mbili za kigeni, kutafuta mafuta katika eneo la ziwa ambalo linamilikiwa na Tanzania.

Kwa mujibu wa gazeti la mtandaoni la Malawi la Nyasa Times, msemaji wa Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa wa Malawi, Quent Kalichero alithibitisha Jumatano wiki hii kwamba nchi hiyo imewasilisha majibu ya
maswali hayo na ushahidi uliohitajika.(P.T)
"Waziri wetu amewasilisha taarifa maalumu ya maandishi kwa wasuluhishi na kwa sasa yuko nchini Msumbiji, kwa ajili ya suala hilo," alisema Kalichero juzi.

Makabidhiano hayo yalifanyika mjini Maputo, Msumbiji ikiwa ni siku chache baada ya Rais Jakaya Kikwete kufanya mazungumzo na wasuluhishi, marais wa zamani wa Msumbiji, Joachim Chissano na wa Botswana, Festus Mogae jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya mkutano huo wa Jumatatu mjini Dar es Salaam, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Bernard Membe aliwaeleza wanahabari kwamba mazungumzo baina ya Rais Kikwete na wasuluhishi hao yalihusu zaidi ushahidi wa Tanzania katika suala la umiliki wa Ziwa Nyasa.

Pia alithibitisha kwamba Tanzania ilikuwa tayari kuwasilisha ushahidi wake kwa sekretarieti ya ofisi ya waliokuwa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (Sadc) inayoongozwa na Chissano, Jumatano iliyopita.

Baada ya mkutano huo wa Jumatatu, Membe alieleza kwamba nchi zote husika, yaani Tanzania na Malawi zinatakiwa kuheshimu maagizo na kuwasilisha ushahidi huo kwa wakati, na kuwaachia wasuluhishi kazi ya kupitia na kutekeleza wajibu wao wakiwa wamepewa muda unaofikia mwaka mmoja kupata suluhu.

Wasuluhishi hao wa Sadc, Chissano na Mogae waliwasili jijini Dar es Salaam Jumapili iliyopita kwa ajili ya mazungumzo kuhusu mgogoro huo, kama walivyofanya kwa Malawi Julai mwaka huu.

Julai mwaka huu, Rais Joyce Banda wa Malawi alinukuliwa akisema kuwa nchi yake haina nia ya kulegeza kamba katika mgogoro wa mpaka wa Ziwa Nyasa na Tanzania.

Alitoa msimamo huo baada ya kukutana na Chissano wa Msumbiji na Thabo Mbeki wa Afrika Kusini ambao ni wajumbe maalumu wa Jumuiya ya Sadc katika mgogoro huo.

Alisema kwamba madai ya Tanzania kuwa inamiliki sehemu ya Ziwa Nyasa, siyo ya kweli na kwamba mpaka uko ufukweni mwa ziwa hilo upande wa Tanzania.

Rais Banda alidai kuwa nchi yake inafuatilia kwa karibu upatanishi wa SADC na kwamba isiporidhishwa na uamuzi ya jumuiya hiyo italiwasilisha suala hilo Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ).

Kabla ya hatua hiyo ya Malawi, Aprili mwaka huu Serikali ya Tanzania iliitaka nchi hiyo kuacha kutapatapa na kuonya kuwa kamwe isithubutu kugusa eneo hilo la mpaka.

Akitoa kauli ya Serikali ya Tanzania Membe alisema: "Nadhani watasikia na kuelewa, Serikali ya Malawi iache kutapatapa, nchi zote ilikoenda kulalamika kuhusu mgogoro huu, Tanzania tumekuwa tukielezwa na hata hao wanaotueleza wanaishangaa sana Malawi." Kauli hiyo ya Serikali ilifuatia Rais Banda kusema kuwa mgogoro huo sasa utapelekwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), kwa madai kwamba juhudi za usuluhishi wa kidiplomasia zimeshindikana.

Hata hivyo, uamuzi huo wa Malawi ni kinyume na makubaliano baina ya nchi hizo mbili yaliyofanyika Novemba 7 mwaka jana, jijini Dar es Salaam ambapo zilikubaliana kwamba jopo hilo ndiyo sehemu ya mwisho ya makubaliano.

Katika maelezo yake, Rais Banda alisema nchi yake imejitoa katika mazungumzo ya usuluhishi kwa madai ya kuhujumiwa na katibu wa jopo hilo ambaye ni Mtanzania, John Tesha kwa maelezo kuwa anavujisha taarifa muhimu za Malawi kwa Tanzania kabla ya Tanzania haijawasilisha taarifa zake kwa jopo hilo. Alisema kuwa tangu kuibuka kwa mgogoro huo, Malawi imekwenda kulalamika katika nchi za Uingereza, Marekani, Umoja wa Afrika (AU) na katika Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (Sadc).

Hata hivyo, baadaye Julai mwaka huu, Serikali ya Malawi ilitangaza kuwa itaendelea na mazungumzo na Tanzania kuhusu mpaka huku ikieleza kuwa viongozi wa Tanzania hawaelewi mipaka ndiyo maana wanapigania kuwa wao ni sehemu ya ziwa.

Waziri wa Habari wa Malawi, Moses Kunkuyu aliliambia Shirika la Utangazaji la Malawi (MBC) kuwa viongozi wote wa Tanzania wanadhani wanamiliki Ziwa Malawi (Nyasa) lakini watakuja kubaini baadaye kuwa hawana hata tone la umiliki.
Chanzo:Mwananchi

Credit mjengwablog.

ZANZIBAR YAJAA MAJI

$
0
0
 KUFUATIA mvua kubwa iliyonyesha katika maeneo mbali mbali ya mji wa Zanzibar leo asubuhi Barabara nyingi zimejaa maji na kusababisha watumiaji kupata usumbufu kutokana na wasi wasi wa kuharibika kwa njia hizo pichani gari zikipita kwa tabu katika eneo la Mwanakwerekwe .(Picha na Haroub Hussein).
 Mabwawa kila pahala
 Hali ya mvua katika maeneo ya Jang'ombe Unguja leo.
 Maji kila kona

Biashara nyingi zimesimama
Viewing all 2276 articles
Browse latest View live