Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all 2276 articles
Browse latest View live

Article 0

$
0
0
WANAWAKE WAONGOZA KWA MAGONJWA YA ZINAA MKOANI NJOMBE.
 Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe Bwana Richard  Ngwale Akizungumza Wakati wa Maadhimisho ya sIKU ya Ukimwi Katika Kijiji Cha Itambo Kata Ya Mdandu.


 Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Bi.Esterina Kilasi Akiwahutubia Wananchi wa Kijiji cha Itambo Katika Maadhimisho ya Ukimwi Akiwa Mgeni Rasmi.

 Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Shaibu Masasi Akizungumza Kwa Niaba ya Mwenyekiti wa Halmashauri Hiyo.
 Mgeni Rasmi Katika Maadhimisho ya Ukimwi Bi.Esterina Kilasi Ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Akienda Kukagua Sehemu ya Kupima Virusi vya Ukimwi.
 

Na  Gabriel  Kilamlya
 
Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Bi.Esterina Kilasi Amelaani Vikali Tabia ya Unyanyapaa n a Ukatili Unaofanywa Kwa Watoto na Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Katika Jamii.

Bi.Kilasi Amesema Kuwa Katika Wilaya ya Wanging'ombe Kumekuwa na Matukio ya Ukatili Ukiwemo Ubakaji na Kuwanyanyapaa Watu Wenye Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi Hali Inayowakatisha Tamaa ya Kuishi Watu Wenye na Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi.

Akizungumza Wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani Yaliyofanyika Katika Kijiji cha Itambo Wilayani Wanging'ombe Kwa Halmashauri za Njombe,Makambako na Wanging'ombe Yenyewe Bi.Kilasi Amesema Katika Kuadhimisha Siku ya Ukimwi ni Lazima Jamii Ikubali Kuachana na Vitendo vya Kurithi Wajane na Wagane,Kufanya Tohara Kwa Wanaume Pamoja na Kujitokeza Kuendelea Kupima Virusi Vya Ukimwi Mara Kwa Mara.

Akisoma Taarifa ya Ukimwi Katika Halmashauri ya
Njombe,Wanging'ombe na Mji Makambako Mratibu wa Ukimwi wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Bwana Godwin Mtui Amesema Kuwa  Mwingiliano Mkubwa wa Watu Katika Masuala ya Kibiashara,Elimu Ndogo Juu ya Ukimwi na Mila Potofu Zimezidi Kuonekana Sababu Kubwa Zinazopelekea Ongezeko la Maambukizi ya
 Ukimwi.

Aidha Amesema Kuwa Kadri Siku Zinavyokwenda Serikali Imeendelea Kukabiliana na Changamoto Hizo Ikiwemo Kuwasaidia Watumishi na Watoto Wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi.


Taarifa ya Watu Waliogunduliwa na Magonjwa ya Zinaa Imebainika Kuwa Watu 11,906 Walitibiwa Magonjwa ya Zinaa na Kati ya Hao Wanawake ni 8918 Wanaume ni 3998. 

Pamoja na Mambo Mengine Serikali Imesema Kuwa Itaendelea Kuboresha Huduma ya Dawa za Kufubaza Makali ya Virusi Vya Ukimwi Ili Waathirika hao Waendelea Kutumia Dawa Kila Siku.

Kauli Mbiu ya Siku ya Ukimwi Duniani Kwa Mwaka 2013 ni Maambukizi Mapya-Sifuri,Vifo Vitokanavyo na Ukimwi-Sifuri,Unyanyapaa -Sifuri. 



Article 0

$
0
0

KITUO CHA CHILDREN SUPPORT TANZANIA MBEYA  CHA ADHIMISHA SIKU YA WALEMAVU DUNIANI.

Mgeni rasmi toka benki ya NMB akikata utepe kuzindua uwanja wa michezo wa kituo hicho
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho Noela Msuya amesema katika maadhimisho ya Ulemavu duniani watanzania wanapaswa kutowatenga watoto wenye ulemavu kwa kuwa hakuna eneo wala kijiji kilichotengwa kwa ajili ya watu wenye ulemavu bali tunatakiwa kuishi nao pamoja.
Mwalimu Mkuu wa Kituo hicho, Omoding James amesema kituo kilianza kupokea watoto tangu mwaka 2009 baada ya kusajiliwa kikiwa na watoto 13 lakini hadi sasa kuna watoto zaidi ya 200.
Mtoto Maxel mlemavu wa mikono na miguu nae akiwa katika vazi rasmi la mahafali ya kumaliza Darasa la awali kuingia darasa la kwanza
Kituo cha kulelea na kufundishia watoto cha Children Support Tanzania kilichopo Block T Jijini Mbeya kimeungana na Ulimwengu mzima katika kuadhimisha siku ya Ulemavu Duniani inayoadhimishwa kila tarehe 3 Disemba kwa kuzindua uwanja wa mazoezi na mahafali ya Chekechea.
Aidha kituo hicho kimetumia siku hiyo kwa kusheherekea mahafali ya watoto 15 ambao wanavuka hatua kutoka Chekechea tayari kwa kujiunga na Darasa la Kwanza mwakani baada ya kupata sifa za kujua kusoma na kuandika.
Katika Sherehe hizo zilizofanyika katika Viwanja vya kituo hicho zilizohudhuriwa na wazazi wa wanafunzi wanaosoma hapo pia umezinduliwa uwanja wa mazoezi unaofahamika kwa jina la CST Fun Village ambao utakuwa na michezo mbali mbali ya watoto.
Akizungumza katika Sherehe hizo Mwalimu Mkuu wa Kituo hicho, Omoding James amesema kituo kilianza kupikea watoto tangu mwaka 2009 baada ya kusajiliwa kikiwa na watoto 13 lakini hadi sasa kuna watoto zaidi ya 200.
Amesema kituo hicho kinapokea watoto wenye ulemavu wa akili, Viungo,viziwi, wanaoishi katika mazingira magumu na watoto wa kawaida ambapo wanafundishwa elimu maalumu ya darasani, ufundi, mziki na michezo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo hicho Noela Msuya amesema katika maadhimisho ya Ulemavu duniani watanzania wanapaswa kutowatenga watoto wenye ulemavu kwa kuwa hakuna eneo wala kijiji kilichotengwa kwa ajili ya watu wenye ulemavu bali tunatakiwa kuishi nao pamoja.
Amesema kauli mbiu ya Siku ya walemavu Duniani inasema, “Vunja vizuizi, fungua milango kwa jamii jumuishi kwa maendeleo kwa wote”ambayo inapaswa kuenziwa kwa kuwajengea mazingira ya kuwapenda walemavu na kuwashirikisha katika shughuli za kiuchumi.

Na Mbeya yetu

RAIS KIKWETE AMTEUA DR.ASHA ROSE MIGIRO KUWA MBUNGE WA HESHIMA

$
0
0
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone:255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425



PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dr. Asha-Rose Migirokuwa Mbunge.

Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar Es Salaam leo, Jumanne, Desemba 3, 2013, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Dr. Florens Turuka inasema kuwa uteuzi huo umeanza jana, Desemba 2, 2013.

Dr. Asha-Rose Migiro ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa katika Chama cha Mapinduzi.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

3 Desemba, 2013

Article 1

$
0
0
KINANA NA MSAFARA WAKE KUWASILI MKOANI NJOMBE DISEMBA 5 JIONI.
 
  
Katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Bwana Hosea Mpagike Akizungumzia Ratiba ya Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdurlahman Kinana na Msafara Wake Mkoani Njombe.
 
Na  Gabrie  Kilamlya Njombe
 
 Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Abdurlahman Kinana Anatarijia Kuwasili Mkoani Njombe Kesho Jioni Kwa Ziara ya Kikazi ya Siku Mbili Ikiwa ni Muendelezo wa Ziara Yake ya Kutembelea Kukagua Miradi Mbalimbali ya Maendeleo.

Ujio wa Katibu Mkuu wa Chama Hicho Bwana Kinana Umelenga Kukagua Shughuli Mbalimbali Zinazofanywa na Vijana Katika Maeneo Mbalimbali Pamoja na Chama cha Mapinduzi CCM Ikiwa ni Pamoja na Kuhakikisha Serikali Inatekeleza Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010/2015 Kama Inavyosema.

Akizungumzia Juu ya Ziara ya Kiongozi Huyo wa Kitaifa,Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Njombe Bwana Hosea Mpagike Amesema Kuwa Bwana Kinana Pia Ataongozana na Viongozi Mbalimbali wa Chama Akiwemo Mbunge Mteule Dokta Asha Rose Migoro Pamoja na Katibu Mwenezi wa CCM Taifa Ndugu Nape Mnauye.

Bwana Mpagike Amesema Kuwa Kinana Ataanzia Ziara Yake Wilayani Makete Katika Mkoa wa Njombe Ambapo Disemba 6 Mwaka Huu Atakuwa Wilayani Humo Katika Vijiji Mbalimba na Kukagua Shughuli Mbalimbali za Vijana Kisha Kuwasili Mjini Njombe Majira ya Saku Jioni Siku Hiyo.

Akiwa Mjini Njombe Katibu Mkuu Kinana Atazindua Mradi wa Kitega Uchumi wa CCM na Kufanya Mkutano wa Hadhara Katika Uwanja wa Roman Catholic Karibu na Benki ya CRDB Hapo Disemba 7 Mwaka Huu.

Katika Kipindi Hiki Chama cha Mapinduzi CCM Taifa Kupitia Katibu Wake Mkuu Kimeendelea Kufanya Zaiara Katika Mikoa Mbalimbali Ambapo Hadi Sasa Msafara Huo Utawasili Mkoani Njombe Ukitokea Jijini Mbeya.

RAIS KIKWETE AFANYA UTEUZI WA KAMISHNA WA UHAMIAJI ZANZIBAR.

Article 2

$
0
0

WANANCHI  WA KIJIJI CHA ITULAHUMBA WAAHIRISHA SHUGHULI ZAO KWA AJILI YA KUMNG'OA MWENYEKI WA KIJIJI CHAO.
 AFISA TAARAFA YA MDANDU BENSON WANDERAGE AKIWA KWENYE MKUTANO WA HADHA AMBAO ULIKUSUDIA KUWAKATAA VIONGOZI WA KIJIJI AMBAO NI MWENYEKITI NA MTENDAJI ALIYEHAMISHIWA KIJIJINI HAPO



 DIWANI WA KATA YA MDANDU BI ANNA UPENDO GOMBELA AKIONGEA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA ITULAHUMBA KUHUSIANA NA MGOGORO WA KUWAONDOA VIONGOZI HAO






 WAJUMBE NA VIONGOZI WA SERIKALI YA KATA NA KIJIJI CHA ITULAHUMBA


 AFISA MTENDAJI WA KATA YA MDANDU BWANA  TIMOTH FUTE AKIZUNGUMZA NA WANANCHI JUU YA NAMNA ALIVYOHAMISHWA MTENDAJI HUYO TOKA KIJIJI CHA ITAMBO KWENDA KIJIJI CHA ITULAHUMBA HUKU ALIKWISHA KUTUHUMIWA NA WANANCHI KWA UBADHILIFU WA MALI ZA KIJIJI
 MIONGONI MWA WANANCHI WA KIJIJI CHA ITULAHUMBA WAKIHOJI JUU YA KUPELEKEWA MTENDAJI HUYO




 WANANCHI WAKIWASIKILIZA VIONGOZI WA KATA NA TAARAFA YA MDANDU WILAYANI WANGING'OMBE
 HII NI OFISI YA KIJIJI CHA ITULAHUMBA



 HUyU NI MWENYEKITI ALIYEKAIMISHWA BWANA SHAIBU MAHEGELE  BAADA YA WANANCHI KUMFUKUZA MWENYEKITI WA ZAMANI BWANA HOSEA MPOSOLA

HUYU NI MWENYEKITI WA KIJIJI BWANA HOSEA MPOSOLA ALIYEFUKUZWA NA WANANCHI WA KIJIJI CHA ITULAHUMBA WAKISEMA HAWANA IMANI NAE

  Na  Michael Ngilangwa
 
Hatimae sakata la wananchi wa kijiji cha Itulahumba la kuwakataa viongozi

limeingia sura mpya baada ya wananchi hao kumufukuza mwenyekiti wao na

kumuchagua mwenyekiti wa muda huku wakimuomba mkurugenzi kumuondoa afisa

mtendaji ambae amepelekwa hivi karibuni kusimamia maendeleo ya kijiji hicho.

Wakiongea mbele ya viongozi wa kata na taarafa ya Mdandu wananchi hao

wameelezea sababu za kumkataa mwenyekiti wa  kijiji hicho bwana Hosea Mposola

kwa kuruhusu afisa mtendaji aliyekuwepo bwana Method Mligo kuhamia kijiji cha

Itambo  bila kusoma hesabu za mapato na matumizi,kuruhusu afisa mtendaji mpya

kuhamia katika kijiji hicho pasipo wananchi kufahamishwa uwepo wake jambo

lililopelekea wananchi kutokuwa na imani na mwenyekiti huyo.

Kuhusu afisa mtendaji aliehamishiwa katika kijiji hicho akitokea kijiji cha Itambo

 bwana Batista Msemwa wananchi hao wamesema kuwa hawamuhitaji

mtendaji huyo kutokana na wananchi wa kijiji cha Itambo kumkataa kutokana na kutuhumiwa kuhusika na   ubadhilifu wa mali za kijiji cha Itambo na kwamba serikali  imekuwa na tabia ya kuwahamishia vijiji vingine watumishi wanaotuhumiwa na ubadhilifu wa mali za wananchi ili waendelee na ufujaji wa mali za wananchi.

Akizungumza kwenye mkutano  wa hadhara afisa taarafa ya Mdandu bwana Benson

Wanderage amesema kufuatia kuteuliwa kwa mwenyekiti wa muda wananchi

wanatakiwa kuonesha ushirikiano katika kutekeleza miradi ya kijiji hicho huku

akisema kuwa serikali ya kata itakwenda kumuagiza afisa mtendaji aliyehamishwa

arudi kijijini hapo ili asome  taarifa ya hesabu za mapato za matumizi.

Diwani wa kata ya Mdandu bi Anna Upendo Gombela amesema  amewapongeza wananchi kwa  mahudhurio ya wananchi hao na kwamba  lengo la kuwakutanisha wananchi hao ni kutatua mgogoro uliokuwepo baina ya viongozi na wananchi  wa kutokuwa na imani na uongozi wa kijiji  akiwemo mwenyekiti huku akisema wajumbe wa  serikali ya kijiji wameridhia kufanya uteuzi wa mwenyekiti wa muda ambae anakubalika na wananchi wote.

Afisa mtendaji wa kata ya Mdandu bwana Timoth Fute amesema kuwa ofisi ya halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe tayari imechukua  hatua za kumuandikia barua yakwenda kusoma hesabu za mapato na matumizi ya kijiji cha Itulahumba   mtendaji huyo pindi atakapo pona kwani kwa sasa amelazwa katika hospitali ya Kibena ambapo ameahidi kumsimamia ili kuhakikisha anakwenda kusoma taarifa za mapato na matumizi ya kijiji hicho ndipo  aweze kahama.

Article 1

$
0
0
Dr.Slaa Akutana na Makubwa Kahama
Katibu mkuu  wa  Chadema  Dr  Wilbroad Slaa akiwahutubia  wananchi  wa Kahama mara  baada ya  kuwasili mjini hapo kwa  ziara  yake  ya  kichama jana
Dr Slaa akisalimiana na  wananchi waliofika  kumpokea mjini Kahama  jana. leo Desemba 5, atakuwa Wilaya ya Kakonko, Jimbo la Buyungu na Desemba 6, atakuwa Jimbo la Muhambwe.

KINANA AHITMISHA ZIARA YAKE MKOANI Mbeya,NJOMBE LEO.

$
0
0

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wakazi wa Mbeya mjini, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana jioni katika Uwanja wa Rwanda Nzovwe, wilaya ya Mbeya mjini, ikiwa ni mkutano wa kuhitimisha ziara yake katika mkoa huo, ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua.

Katibu NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akihutubia maelfu ya wananchi wa Mbeya, katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana jioni katika Uwanja wa Rwanda Nzovwe, wilaya ya Mbeya mjini, ikiwa ni mkutano wa kuhitimisha ziara yake katika mkoa huo, ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua.
Leo Jioni Msafara Huo Utawasili Mkoani Njombe Kwa Ziara ya Siku Mbili.


Article 5

$
0
0

KAMPUNI KUBWA YA KOREA KUWEKEZA NISHATI YA UMEME TANZANIA.


Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Afrika na Mashariki ya Kati katika Wizara ya  Mambo ya Nje ya Korea Kusini, Bw. Moon Duk-ho walipokutana kwa mazungumzo Jijini Soul, Kore Kusini hivi karibuni. Balozi Mbelwa yupo nchini Korea Kusini kwa ziara ya kikazi.

Balozi Mbelwa (kulia) akimsikiliza Bw. Moon Duk-ho wakati wa mazungumzo yao. Pembeni kwa Balozi Mbelwa ni Bw. Francis Mosongo, Afisa katika Ubalozi wa Tanzania nchini Japan.

Picha ya pamoja kati ya Balozi Mbelwa (wa tatu kutoka kulia) na Bw. Moon Duk-ho (wa tatu kutoka kushoto) pamoja na Wajumbe waliofutana nao.

Kampuni ya Daewoo ya nchini Korea Kusini, imetangaza kuwekeza katika mradi wa kufua umeme kwa kutumia maji, Mkoani Iringa. Taarifa ya uwekezaji huo ilitolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Afrika na Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea ya Kusini, Bwana Moon Duk-ho, wakati alipofanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Asia na Australasia wa Wizara ya

Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki, jijini Seoul, Jumatatu 3 Desemba, 2013.

Akifafanua kuhusu mradi huo wa umeme unaojulikana kama (Iringa Hydro-Power Project), Bwana Moon Duk-ho alisema kuwa tayari Kampuni ya Daewoo kwa kushirikiana na Taasisi ya Serikali ya Korea ya Kusimamia Rasilimali Maji, wamekwisha anza kazi ya upembuzi yakinifu na kwamba utekelezaji wa mradi huo utaanza mara tu kazi hiyo itakapamalizika mwanzoni mwa mwaka 2014.

Mradi huo utaokagharimu mamilioni ya Dola za Kimarekani unatarajiwa kuwanufanisha zaidi ya wakazi 2000 kutoka vijiji mbalimbali mkoani Iringa na mikoa ya jirani ya Njombe, Songea na Mbeya.

Upatikanaji wa nishati ya umeme ni moja ya changamoto kubwa kabisa inayoikabili Tanzania, kwani kati ya Watanzania kumi, ni wawili tu ndio wanaopata nishati hii muhimu.

Sambamba na uwekezaji huo, Serikali   ya Korea imedhamiria kuanzisha ushirikiano na Tanzania katika masuala ya nishati ambapo mwakani mwezi Februari 2014, Timu ya Wataalam wa Nishati kutoka Korea watatembelea Tanzania kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Wataalam wa Wizara ya Nishati na Madini.

Akitoa salamu za shukrani, kwa niaba ya serikali ya Tanzania, Balozi Mbelwa Kairuki alisema,“mradi huu wa Daewoo unakuja wakati muafaka ambapo Serikali ya Tanzania chini ya dira ya Taifa (Vision 2025) imedhamiria kuongeza huduma ya upatikanaji wa nishati ya umeme kwa Watanzania kutoka asilimia 18.4 hadi 30 kwa ngazi ya taifa, na kutoka asilimia 6.5 hadi 15  kwa maeneo ya vijijini, ifikapo mwaka 2025.”

Aidha Balozi Kairuki, alitumia fursa hiyo pia kukaribisha wawekezaji zaidi kutoka Korea Kusini kuwekeza kwenye Sekta ya Viwanda na Utalii ili kutengeneza fursa za ajira.

Korea  Kusini ni miongoni mwa nchi marafiki wa karibu wa Tanzania na kwa zaidi ya miongo minne, Serikali za Tanzania na Korea Kusini zimeshirikiana na kusaidiana kwenye masuala mbalimbali ya kiuchumi na kijamii. Ujio wa kampuni kubwa kama ya Daewoo unaonesha mahusiano mazuri yaliyopo kati ya nchi hizi mbili.

Mbali na ushiriikiano katika kuendeleza sekta ya nishati, Serikali ya Korea ya Kusini pia imeahidi kuendelea kuisaidia Tanzania kupitia mradi wa kuanzisha vijiji vya mfano vitakavyowezeshwa kwa kupatiwa teknolojia za kilimo na miundombinu ya maji, umeme na barabara.  Tayari Korea imeanzisha vijiji vya aina hiyo huko Pangawe, Morogoro na Zanzibar.

Aidha, Korea Kusini, imeahidi kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali ya Tanzania katika kukuza elimu ya juu kwa kuongeza fursa za masomo kwa Watanzania hususan kwenye sekta ya gesi na mafuta.


kwa hisani ya michuziblog

Article 4

$
0
0
NELSON MANDELA[MZEE MADIBA]AFARIKI DUNIA
 
Nelson Mandela  


Mandela amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwenye mapafu kwa muda mrefu, alilazwa na baadaye kuruhusiwa kutoka hospitali ambapo mauti yamemkuta akiwa nyumbani kwake mjini Pretoria.

RAIS wa kwanza wa Afrika Kusini na mpinga siasa za ubaguzi wa rangi, Nelson Mandela amefariki nchini humo akiwa na umri wa miaka 95. Taarifa za kifo chake zimetangazwa na rais wa nchi hiyo, Jacob Zuma ambaye amesema Mandela amefariki majira ya saa 2.50 usiku wa Alhamisi kwa saa za Afrika Kusini.
Mandela amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwenye mapafu kwa
muda mrefu, alilazwa na baadaye kuruhusiwa kutoka hospitali ambapo mauti yamemkuta akiwa nyumbani kwake mjini Pretoria.

Tayari viongozi mbalimbali duaniani wameshaanza kutuma salamu za rambirambi kwa familia na taifa la Afrika Kusini.

Viongozi hao ni pamoja na Rais Barack Obama wa Marekani na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki-Moon.

WAKAZI NANE WA MKOANI DODOMA WAKABIDHIWA BODABODA ZAO KUTOKA VODACOM.

$
0
0

Kaimu Meneja Masoko wa Vodacom-Tanzania Kanda ya Kati, Heladius Kisiwani (Kulia), akimkabidhi kofia ngumu, mmoja kati ya washindi wanane wa promosheni inayoendeshwa na kampuni hiyo ya simu"Timka na Bodaboda", Asha Yohana, mkazi wa Dodoma, katika hafla ya kukabidhi pikipiki "Bodaboda" kwa washindi wanane wa mkoani humo.
Kaimu Meneja Masoko wa Vodacom Kanda ya Kati, Heladius Kisiwani (Kulia), akizungumza wakati wa hafla ya kuwakabidhi zawadi za pikipiki, washindi wanane wa promosheni ya "Timka na Bodaboda" inayoendeshwa na kampuni hiyo ya simu. Hafla hiyo ilifanyika jana mjini Dodoma.
Kaimu Meneja Masoko wa Vodacom Kanda ya Kati, Heladius Kisiwani (Wapili kulia), akiwa ameshikana mikono na washindi wa promosheni ya "Timka na Bodaboda" mara baada ya kuwakabidhi pikipiki wakazi wanane wa
mkoani Dodoma.
Washindi wanane wa promosheni ya "Timka na Boda boda", mkoani Dodoma, wakiwa kwenye pikipiki zao "Bodaboda" mara baada ya kukabidhiwa na Kaimu Meneja Masoko wa Vodacom-Tanzania Kanda ya Kati, Heladius Kisiwani

Article 2

$
0
0

MAKAMU WA RAIS AKABIDHI TUZO ZA MUAJIRI BORA WA MWAKA 2013.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo ya Muajiri Bora wa mwaka 2013, Meneja Rasilimali Watu wa Benki ya NMB, Rashid Nassoro, wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo hizo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempisky jijini Dar es Salaam, jana usiku.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo ya Muajiri Bora wa mwaka 2013, Meneja wa Sera wa CCBRT, Frederick Msigala, wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo hizo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempisky jijini Dar es Salaam, jana usiku.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo ya jumla ya Muajiri Bora wa mwaka 2013, Meneja Uhusiano wa Nje wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, Salum Mwalimu wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo hizo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempisky jijini Dar es Salaam, jana usiku.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo ya Muajiri Bora wa mwaka 2013, Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel, Francis Ndenje, wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo hizo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempisky jijini Dar es Salaam, jana usiku.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo za Muajiri bora wa mwaka 2013, iliyofanyika kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinsky, jijini Dar es Salaam, jana usiku.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa makampuni na mashirika baada ya kukabidhi tuzo hizo.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya wageni waalikwa baada ya kuwasili katika ukumbi huo kwa ajili ya kukabidhi tuzo hizo. 
 
kwa hisani ya michuziblog

SERIKALI WILAYANI NJOMBE IMELAANI WAATHIRIKA WA VVU KUTELEKEZA DAWA ZA ARV's .

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba

Wananchi Wanaoishi na Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi Wilayani Njombe Wameshauriwa  Kuendelea Kutumia Daza za Kupunguza Makali ya Ukimwi ARV's na Kuacha Tabia ya Kwende Kwa Waganga wa Tiba za Asili Kwa Madai Kuwa Dawa Hizo Zinauwezo wa Kutibu Ukimwi.

Rai Hiyo Imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi. Sara Dumba Ikiwa
ni Takribani Siku Tano Tangu Kuadhimishwa Kwa Siku ya Ukimwi Duniani
, na Kusema Kuwa Baadhi ya Wagonjwa wa Ukimwi Wameacha Kutumia Dawa za Kufubaza Makali ya Ugonjwa Huo Hali Inayopelekea Kukwamisha Jitihada za Serikali za Kupambana na Janga la Ukimwi Nchini.

Bi. Dumba Amesema Wagonjwa Wengi wa Ukimwi Wamekuwa Wakijihusisha na Masuala ya Kimila na Kukatisha Matumizi ya Dawa za Kufubaza Makali ya Virusi Vya Ukimwi, Ambapo Amelani Mila Hizo na Kusema Kuwa Mila na Desturi Zilizopitwa na Wakati Zinatakiwa Kupigwa Vita

Simulizi Za Mzee Madiba:

$
0
0

  Siku Mandela Alipofika Nyumbani Kwa Nyerere Msasani..!

mandelaa_a5117.jpg
Na Maggid Mjengwa,
 
Mandela alikuwa njiani kuelekea Addis Ababa kwenye mkutano ambao ANCC walialikwa rasmi. Ni mkutano wa PAFMESCA ambao ungeshirikisha nchi na viongozi wengi wa nchi za Afrika zilizokuwa huru wakati huo. Ilikuwa ni fursa kwa Mandela kufungua milango ya mawasiliano na viongozi mbali mbali kwa manufaa ya ANC na mapambano yao ya ukombozi kutoka ubaguzi wa rangi.

Mandeka aliingia Tanganyika kwa mara ya kwanza kwa kupitia Mbeya. Na tuone kwanza ni jinsi gani Mandela alivyoitafakari nchi yake ya kwanza ya Kiafrika aliyoiona tangu azaliwe. Ikumbukwe,
kwenye safari yake ya Tanganyika, Mandela aliongozana na Bw. Joe Matthews, Mzungu mwanaharakati wa kupinga ubaguzi na mwanachama wa ANC.
Mandela alishangazwa sana na aliyoyaona pale Mbeya, na hususan pale kwenye hoteli waliyofikia. Na hapa Mbeya inaingia katika historia kuwa ni mji wa kwanza wa nchi huru ya Kiafrika uliopatwa kutembelewa na shujaa wa Afrika, Nelson Mandela.
Na kuna Mtanzania anayeingia pia kwenye historia, ni Bw. John Mwakangale, huyu ni
Mtanzania wa kwanza, akiwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na kiongozi wa TANU , ambaye ndiye aliyempokea na kuongea rasmi na Nelson Mandela alipofika Mbeya.(P.T)
Na pale hotelini Mbeya Mandela alishangazwa kuona kuwa hakukuwa na ubaguzi wa rangi kama ilivyo kwao Afrika Kusini. Mandela alibaini mara moja, kuwa amefika katika nchi inayotawaliwa na Waafrika weusi. Kwamba mzungu hakuwa mtu wa kuogopewa. Na hilo linathibitishwa pale bwana mmoja Mtanganyika mweusi, alipoona Mandela na mwenzake wanashangaa shangaa, ndipo Mtanganyika yule alipokwenda sehemu ya mapokezi ya hoteli na kumwuliza mhusika, dada wa Kizungu;
" Madam, did Mr Mwakangale inquire after these two gentlemen" Aliuliza huku akiwaonyesha Mandela na Joe Matthews. Anasimulia Mandela.
Bwana yule Mtanganyika alimwuliza dada yule mhusika kwa vile alimwona Mwakangale akifika hapo kuwaulizia wageni wake hao.
" I am sorry, sir,'– Samahani bwana, alisema dada yule na kisha akaendelea kusema;
" He did, but I forgot to tell them"- kwamba ni kweli Mwakangale amewaulizia, lakini nilisahau kuwaambia. Alisema dada yule mhudumu wa kizungu.
Bwana yule Mtanganyika akamalizia kwa kumwambia mhudumu;
" Please, be careful, madam"- Kwamba , tafadhali dada, uwe mwangalifu.
Ndipo hapo kwa maneno yake, Mandela anasimulia juu ya tukio hilo;
" I then truly realized that, I was in a country ruled by Africans"- Kwamba ndipo kwa ukweli alipobaini, kuwa yuko kwenye nchi inayotawaliwa na Waafrika.
Na Mandela alijiona, kwa mara ya kwanza maishani mwake, kuwa yuko huru, mbali ya kwamba nyumbani kwao Afrika Kusini ni mtu anayesakwa kwa udi na uvumba na watawala.
Hatimaye safari ya kutoka Mbeya kwenda Dar es Salaam ikawadia. Mandela akawasili Dar es Salaam siku ya pili yake.
Alipofika Dar es Salaam, Mandela akakutana na Julius Nyerere nyumbani kwake Msasani. Ndio, ni Julius Nyerere, Rais kijana kwenye nchi ambayo ilikuwa na mwaka mmoja tu tangu ipate uhuru. Mandela alishangaa kuona Rais anakaa kwenye nyumba isiyo ya kifahari. Alishangaa pia kumwona Rais anayeendesha mwenyewe gari yake. Mandela anasema;
" I recall that he drove himself in a simple car, a little Austin"- Nakumbuka aliendesha mwenyewe gari ndogo ya kawaida aina ya Austin. ( Nelson Mandela, Long Walk To Freedom, pg. 345- 346)
Naam, ni yepi mengine yalimshangaza Mandela juu ya Nyerere alipokutana naye pale Msasani? Na je, waliongea nini?


Article 5

$
0
0

MZEE NELSON MANDELA KUZIKWA JUMA PILI DISEMBA 15,2013.

Rais Jacob Zuma ametangaza muda mfupi uliopita kwamba mazishi ya Nelson Mandela yatafanyika siku ya Jumapili, Desemba 15 kijijini kwake Qunu, katika jimbo la Eastern Cape.

Rais Zuma pia ametangaza siku 10 za maombolezo kitaifa na bendera zitapeperushwa nusu mlingoti katika muda wote huo.  Na ameitangaza siku ya Jumapili ya Desemba 8, 2013 kuwa siku maalumu ya kitaifa ya maombolezo na kumkumbuka Madiba nchi nzima.

 Tayari msisimko wa mazishi hayo yanayotarajiwa kuwa ya kihistoria umekamata dunia nzima, ambapo tayari Rais Obama wa Marekani, ms
taafu Bill Clinto na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ni baadhi tu ya viongozi ambao wamethibitisha kushiriki. 

 Sala ya mazishi imepangwa kufanyika katika uwanja wa Taifa wa  FNB  Desemba 10, 2013  jijini Johanesburg.

Mwili wake utawekwa jengo la serikali liitwalo Union Buildings kuanzia  Desemba 11 hadi 13,   kwa kupewa heshima za mwisho, kabla ya kupelekwa kijijini Qunu kwa mazishi

 Uwanja wa Taifa wa michezo wa Johannesburg ambako sala rasmi ya Kitaifa ya mazishi itafanyika  siku ya Jumapili ya
Desemba 10, 2013
Jengo la Union Buildinga ambapo mwili wake utawekwa kwa ajili ya kupewa heshima za mwisho kuanzia Desemba 11 hadi 13, 2013
Ulinzi mkali katika nyumba ya familia ya Madiba kijijini kwake Qunu ambako atapumzishwa katika nyumba yake ya milele Desemba 15, 2013.

JANUARY MAKAMBA AWASILI WASHINGTON, DC

$
0
0
Naibu Waziri wa mawasiliano, Sayansi na Teknologia, Mhe. January Makamba akiwa na mkewe Ramona Makamba wakipokewa na Afisa Ubalozi Mindi Kasiga(wapili toka kushoka) na mwenyekiti wa Vijimambo Baraka Daudi mara tu walipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia. Mhe. Makamba amekuja maalum kama mgeni rasmi kwenye sherehe ya Uhuru wa Tanzania itakayofanyika Jumamosi Desemba 7, 2013 Laurel, Maryland nchini Marekani.
 Mhe. January Makamba na mkewe Ramona wakibadilishana mawili matatu na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mindi Kasiga.
 Kutoka kushoto ni Afisa Ubalozi Abbas Missana,
Afisa Ubalozi Mindi Kasiga, Ramona Makamba na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknologia, Mhe. January Makamba.

DR.ASHA ROSE MIGIRO AJUTIA ZIARA YA KINANA MKOANI NJOMBE;

$
0
0

 Gari aliyokuwa amepanda Katibu wa NEC,Siasa na mahusiano ya Kimataifa,Dkt Asharose Migiro ikiwa imepoteza muelekeo,kufuatia eneo hilo kukumbwa na utelezi mkubwa kutokana na mvua iliyokuwa imenyesha.Dkt.Migiro alikuwa kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana walipokuwa wakitokea Wilayani Makete kuelekea Wilaya mpya ya Wanging'ombe,mkoani Njombe mapema leo ambapo hata hivyo walifika salama na kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii.
 Juhudi ya kulinasua gari hilo zikiendelea kufanyika.
Pichani Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa sambamba na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na wadau wengine wakitoka kutoa msaada wakati gari ya Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa iliponasa kwenye tope.
 Katibu wa NEC,Siasa na Mahusiano ya Kimataifa,Dkt.Asharose Migiro akiwa amesimama kando kando ya barabara akisubiri gari yake iliyokuwa kwenye msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana,iondolewa mara baada ya kunasa kwenye tope,kufuatia eneo hilo kuharibika kutokana na mvua kunyesha na kusababisha utelezi mkubwa eneo hilo.
 Juhudi za kulinasua gari hilo zikiendeleA
 Eneo linavyoonekana

KWA HISANI YA michuziblog

Article 2

$
0
0
VIJANA WAPONGEZA UJIO WA KINANA NA MSAFARA WAKE MKOANI NJOMBE


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana  watatu kushoto, akiungana na Vijana wa CCM kula kiapo cha uanachama, baada ya kuwakabidhi kadi za Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) vijana 40, katika mkutano uliofanyika kwenye kiituo cha Mafunzo ya zana za kilimo kwa wakulima katika Kijiji cha Usuka, Kata ya Isuka Wilayani Wanging'ombe mkoa mpya wa Njombe leo mchana. Kushoto ni Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Mbunge mteule, Dk. Asha-Rose Migiro.
Vijana waliopatiwa kati za CCM na Katibu Mkuu wa CCM,  katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kituo cha Mafunzo ya zana za kilimo kwa wakulima katika Kijiji cha Usuka, Kata ya Isuka Wilayani Wanging'ombe katika mkoa mpya wa Njombe.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi ya UVCCM, kijana Geawa Wibiki, wakati wa mkuytno wa hadhara uliofanyika kwenye Kituo cha Mafunzo ya zana za kilimo kwa wakulima katika Kijiji cha Usuka, Kata ya Isuka Wilayani Wanging'ombe katika mkoa mpya wa Njombe. Kushoto ni Dk. Asha-Rose Migiro na watatu kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe, Deo Sanga.
 Vijana wakimshangilia Kinana katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kituo cha Mafunzo ya zana za kilimo kwa wakulima katika Kijiji cha Usuka, Kata ya Isuka Wilayani Wanging'ombe katika mkoa mpya wa Njombe.
 Kinana, Napa na Dk. Asha-Rose wakiwasalimia wananchi walipowasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kituo cha Mafunzo ya zana za kilimo kwa wakulima katika Kijiji cha Usuka, Kata ya Isuka Wilayani Wanging'ombe katika mkoa mpya wa Njombe.
 
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa KImataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akisalimiana na Mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Esterina  Kilasi, katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kituo cha Mafunzo ya zana za kilimo kwa wakulima katika Kijiji cha Usuka, Kata ya usuka Wilayani humo katika mkoa mpya wa Njombe.
 Kinana akifurahia ngoma zilizokuwa zikitumbuizwa na kinamama wa Wanging'ombe, alipowasili katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kituo cha Mafunzo ya zana za kilimo kwa wakulima katika Kijiji cha Usuka, Kata ya Isuka Wilayani Wanging'ombe katika mkoa mpya wa Njombe.
 Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa KImataifa, Dk. Asha-Rose Migiro akijaribu Power Tiller, katika  Kituo cha Mafunzo ya zana za kilimo kwa wakulima katika Kijiji cha Usuka, Kata ya Isuka Wilayani Wanging'ombe katika mkoa mpya wa Njombe.
 HEEEE JAMANI, ZA SIKU NYINGI... Mtangazaji wa zamani Sarah Dumba ambaye sasa ni Mkuu wa wilaya ya Njombe, akimsalimia kwa bashasha Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asjha-Rose Migiro alipowasili katika mkoa huo leo
Umarti wa wananchi ukipokea msafara wa Kinana kuingia mkoa wa Njombe
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Itukadi na Uenezi, Nape Nnauye wakiwa mbele ya Jengo la Mradi wa CCM, mkoa wa Njombe, baada ya Kinana kuzindua jengo hilo leo

Article 1

$
0
0

MAKAMU WA RAIS Dr.Gharib Bilal Awa Mgeni Rasmi Kwenye Mahafali ya  KWANZA CHUO KIKUU BAGAMOYO.

Maka
mu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye mahafali ya kwanza ya chuo kikuu cha Bagamoyo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam leo Disemba 7-2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi maalum kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo Petired Bishop Elinasa Sendoro wakati wa mahafali ya kwanza ya Chuo hicho yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam leo Disemba 7-2013.
Sehemu ya wahitimu wa ngazi mbalimbali wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo hicho yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam leo Disemba 7-2013.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, katikati akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa ngazi mbalimbali wa Chuo Kikuu cha Bagamoyo wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo hicho yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam leo Disemba 7-2013.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata keki ya mahafali ya kwanza ya chuo kikuu cha Bagamoyo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es salaam leo Disemba 7-2013, kulia Mkuu wa Chuo hicho Petired Bishop Elinasa Sendoro, kushoto Makamu Mkuu wa Chuo
Prof. Costa Ricky Mahalu.Picha na OMR


KWA Hisani ya michuziblog

Article 0

$
0
0
 Mkufunzi wa Mafunzo ya Wadau wa nishati ya umeme wa Maji ya Maporomoko Dokta Reonald Lweyemamu Akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba Aliyekuwa Mgeni Rasmi Katika Ufunguzi wa Mafunzo Hayo Leo Mjini Njombe.
 Wadau wa Nishati ya Umeme wa Maporomoko ya Maji Vijiji Kupitia Mradi wa REA Wakimsikiliza Mgeni Wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo Hayo.


 Wadau wa Nishati ya Umeme wa Maporomoko ya maji Wakiwa Kwenye Picha ya Pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Baada ya Ufunguzi wa Mafunzo Hayo Leo Katika Ukumbi wa Nazareth Center Mjini Njombe.

Wadau Kutoka Mikoa Mbalimbali ya Tanzania Wanaoendelea na Mafunzo Juu ya Uendelezaji wa Vyanzo vya Maporomoko ya Maji Kwa ajili ya Kufua Nishati ya Umeme Mkoani Njombe.

Na  Gabriel  Kilamlya Njombe.

Serikali Imeagiza Kutekelezwa Kwa Vitendo Mafunzo Mbalimbali Yanayotolewa Katika Maeneo Mbalimbali Kwa Wajasiliamali Ili Kuendana na Dhima ya Serikali Katika Kuwakwamua Wananchi Kiuchumi.

Agizo Hilo Limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba Kwa Wadau Mbalimbali Kutoka Katika Mikoa Mbalimbali Hapa Nchini Ukiwemo Mkoa wa Njomb,Wadau  Wanaopata Mafunzo Juu ya Uzalishaji wa Nishati ya Umeme Kupitia Maporomoko ya Maji

Akifungua Mafunzo Hayo ya Wiki Mbili Yanayofanyika Katika Ukumbi wa Nazareth Center Mjini Njombee Bi.Dumba Amesema Kuwa Haina Maana Endepo Serikali Inatoa Mafunzo Hayo Kupitia Wakala wa Nishati ya Umeme Vijijini REA Halafu Yakashindwa Kutumika Kwa Vitendo Ili Kutoa Huduma Kwa

Jamii.

Akizungumzia Lengo la Mafunzo Hayo Yanayoendelea Hadi Disemba 17 Mwaka Huu Mkufunzi wa Mafunzo Hayo Kupitia Wakala wa Nishati Vijijini REA Dokta Reonald Lweyemamu Amesema Kuwa Yamelenga Kuendeleza Miradi ya Maporomoko ya Maji Kwa ajili ya Kufua Nishati ya Umeme Iliyoanzishwa na Wadau Mbalimbali Katika Vijiji Mbalimbali Hapa Nchini Ukiwemo Mkoa wa Njombe.
 

Hope Mjema na Charity Nyava ni Miongoni Mwa Wadau wa Miradi ya Nishati ya Umeme wa Maji ya Maporomoko Hapa Nchini Ambao Kwa Niaba ya Wadau Wengine Wamesema Kuwa Wamekuwa Wakikumbana na Changamoto Mbalimbali Ikiwemo Jamii Kuendelea Kuharibu Mazingira Kwa Kuchoma Moto Misitu Kitu Kinachopelekea Kupungua Kwa Maji Kwenye Vyanzo Vyake Kisha Kulazimika Kujikita na Utoaji Elimu Juu ya Utunzaji wa Mazingira Katika Jamii.


Katika hatua nyingine wamesema kuwa endapo Miradi Hiyo Itakamilika kama walivyopanga basi Jamii Itanufaika na Nishati ya Umeme Kwa Bei ya Chini Kutokana na Mchango Wao.

Mafunzo Hayo Yaliyoandaliwa na Wakala wa Nishati Vijijini REA Yameanza Tangu Disemba Sita Mwaka Huu na Kuzinduliwa Rasmi Disemba 8 Yanatarajiwa Kuhitimishwa Disemba 17 Ikiwa Mkoa wa Njombe Ukionekana Kuwa na Vyanzo Vingi Vya Maporomoko ya Maji ya Kufua Umeme Kuliko Mikoa Mingine Yote Hapa Nchini.
............................................................................................................................
Viewing all 2276 articles
Browse latest View live