Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all 2276 articles
Browse latest View live

Article 13

$
0
0
Jumla ya Shilingi Bilioni 13.647  Ambazo ni Bajeti ya Barabara Mkoa wa Njombe Kwa Mwaka wa Fedha wa 2013/2014 Zimetajwa Kuanza Kutumika Katika Kuboresha Miundombinu ya Barabara Katika Maeneo Mbalimbali Mkoani Hapa.

Pamoja na Fedha Hizo Kushindwa Kufika Zote Kwa Wakati Lakini Hadi Sasa Fedha za Kuwalipa Wakandarasi Wanaomaliza Kazi Zao Zinaendelea Kutolewa Kutokana na Sekta ya Miundombinu ya Barabara Kupewa Kipaumbele Kikubwa Hapa Nchini.

Meneja wa Tanroad Mkoa wa Njombe Mhandisi Yusuph Mazana Amesema Kuwa Fedha Hizo ni Zile za Barabara Zenye Urefu wa Kilomita 1123.42 Katika Maeneo Yote ya Barabara za Mkoa Ambazo Baadhi ya Zabuni Bado Hazijakamilika.

Mhandisi Mazana Amesema Kati ya Fedha Hizo Shilingi Bilioni 3.150 Zinatoka Kwenye Mfuko wa Matengezo wa Barabara na Kiasi cha Shilingi Bilioni 10.497 Zinatoka Kwenye Mfuko wa Barabara Kuu.

Katika Hatua Nyingine Ameeleza Kuwa Jumla ya Kilomita 719.44  za Barabara ni za Mkoa na Kilomita 403.98 ni Barabara Kuu Ambazo Zinaendelea Kulimwa Katika Kipindi Chote cha Mwaka wa Fedha.

Hata Hivyo Amewataka Wakandarasi Hao Kuhakikisha Wanakamilisha Kazi Zao Kwa Kiwango Kilicho Pangwa na Kwa  Mujibu wa Mikataba Yao Ili Kuendana na Kasi ya Maendeleo Katika Mkoa wa Njombe.


RUFANI YA BABU SEYA NA MWANAE YAGONGA MWAMBA

$
0
0

Nguza Viking a.k.a Babu Seya (kulia) na wanawe watatu wakiwa kizimbani

Mwanamuziki Nguza Vikingi, ambaye anatumikia kifungo cha maisha baada ya kukutwa na hatia ya kulawiti na kubaka watoto 10, amedai kuwa hukumu kesi hiyo dhidi yake ilikuwa ni kisasi cha mpenzi wake aliyemuapia kulipiza kisasi, baada ya kuachana naye.

Hayo yalijulikana leo katika Mahakama ya Rufaa Tanzania, wakati mahakama hiyo ilipokuwa ikisikiliza rufani ya mwanamuziki huyo na watoto wake, waliopinga kuwa wakipinga hukumu hiyo ya kifungo cha maisha, iliyotolewa na Mahakama ya HAKIMU Mkazi Kisutu.

Mbali na hilo imedaiwa kuwa Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Addy Lyamuya alitoa hukumu kwa mwanamziki huyo pamoja na watoto wake kwa kutumia mawazo yake binafsi.

Katika rufani hiyo, Nguza (babu Seya) pamoja na watoto wake - Papi Ngunza, Nguza Mbangu na Francis Nguza - wameiomba mahakama hiyo, kupitia mwenendo mzima wa ushahidi uliopelekea wao kutiwa hatiani na kusababisha kuhukumiwa kifungo hicho.

Wakili Mabere Marando ambaye anawatetea washitakiwa hao, aliwasilisha hoja hizo mbele ya Jopo la Majaji watatu lililokuwa likiongozwa na Nathalia Kimaro pamoja na wenzake ambao ni Jaji Mbarouk Salim Mbarouk na

Jaji Salum Massati.

Marando alidai kuwa Babu Seya alikuwa na mpenzi wake aliyemtaja kwa jina la Farida ambaye mara baada ya kuachana alimuambia kuwa atamkomesha ambapo alidai kuwa kunauwezekano kesi hiyo ikawa ni kisasi cha mwanamke huyo ambaye alitoa vitisho hivyo.

Aliendelea kudai kuwa kunauwezekano wa Farida kuwafundisha watoto hao wanaodaiwa kubakwa, kusema uongo Mahakamani ili kuweza kumfunga Babu Sey na wanawe kama kisasi alichodai kumlipia.

Awali Marando alidai Mahakamani hapo kuwa upande wa utetezi unaondoa sababu za kutaka rufani hizo ambazo ni sababu ya 1,2,3,5,6,7,8,11,14 na 15 ambapo alidai kuwa katika rufani hiyo wataanza na sababu namba tisa kutokana na misingi ya kisheria.

Alidai kuwa sababu hiyo inaeleza maelezo ya anayeitwa Mahakamani kwa ajili ya kutoa ushahidi ambapo alidai kuwa mujibu wa sheria za motto kutoa ushahidi Hakimu ananatakiwa kumuhoji kabla ya kutoa ushahidi wake ili aweze kuona kama motto anauelewa gani juu ya kiapo cha ushahidi.

Marando alidai kuwa katika rufani ya awali katika Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam, nchini ya Jaji Thomas Mihayo alisema kuwa utaratibu uliokuwa umetumiwa na hakimu aliyekuwa ametoa hukumu hiyo ilikuwa na makosa kutokana na watoto ambao walitoa ushahidi kutohojiwa kabla ya kutoa ushahidi wao.

Alidai kuwa mahojiano ya awali na mtoto anayetoa ushahidi ni ili kupata maamuzi na kujua kama mtoto anajua maana ya kiapo ambapo mahojiano hayo baina ya hakimu na mtoto yanatakiwa kuhojiwa.

“Kwa kutozingatia mambo hayo ushahidi ambao utakuwa umetolewa na mtoto huyo utakuwa batili na hauna maana yoyote,” alidai Marando.

Aliongeza kuwa muelekeo wa Jaji Mihayo aliyesikiliza rufani hiyo kwa mara ya kwanza haukuwa mzuri kutokana na sheria mbalimbali alizozitumia kugongana ambapo alidai kuwa kutokana na hali hiyo Jaji huyo alifanya kosa kisheria.

Wakili huyo alidai kuwa mashahidi 10 kati ya tisa wa upande wa Jamuhuri ambao walitoa ushahidi wao hawakuapishwa wala kuangalia uwezo wao kama wanaelewa maana ya kiapo.

Pia alidai kuwa katika rufani iliyosikilizwa na Jaji Mihayo alisema kuwa hakimu aliyetoa hukumu hiyo kwakuangalia ushahidi wa pande mbili ambapo alidai kuwa Jaji huyo alikosea kwakua ushahidi wa utetezi haukuangaliwa vyema.

“ Katika nyaraka rejea zilizotumiwa na hakimu aliongeza mawazo yake binafsi kutokana na kupingana na maelezo ya mashahidi, katika ukurasa wa 532 mstari wa saba katika hukumu hii, hakimu anapingana na shahidi aliyejitambulisha kwa jina la Lubaba ambaye mama yake ni Mzaramo na baba yake Mkongo.

“Lakini katika maelezo ya hakimu anaonyesha kijana huyo ni Mzaramo wakati si kweli, hiyo yote inaonyesha jinsi gani hakimu alivyokuwa akiweka mawazo yake binafsi,” alidai Marando.

Marando alidai kuwa kwa muda wa miaka 30 ambayo amefanya kazi ya uwakili hajawahi kuona hukumu ya namna hiyo ambayo hukumu inatolewa kwa kufuata mawazo ya hakimu badala ya ushahidi wa pande mbili.

Aliendelea kudai kuwa hakuna ushahidi ambao ulionesha mshitakiwa wa pili alibaka au kulawiti kabla au baada ya kufanya safari zake za kimuziki katika mikoa ya Mwanza na Arusha ambapo alisema kuwa hakimu aliweza kuweka mawazo yake binafsi ili kuwezesha mshitakiwa huyo kuwa na hatia ya kumfunga gerezani.

“Mbali na hayo mshitakiw ahuyo wa pili alidai kuwa kati ya Agosti na Septemba alikuwa akirekodi albamu yake na mwanamuziki Lady Jee dee , lakini badala ya hakimu kuandika maelezo hayo na matokeo yake aliandika ‘So what?’,” alidai wakili huyo.


Alidai kuwa hakimu huyo hakuandika maelezo ya mashahidi wa upande wa utetezi na badala yake aliandika idadi ya mashahidi ambao walifika kutoa ushahidi wa upande wa utetezi ambapo wakili huyo alihoji hali hiyo iliyofanywa na hakimu huyo.


Wakili huyo alidai kuwa kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa na watoto ambao wanadaiwakufanywa vitendo vya ubakaji na kulawitia walitaja baadhi ya watu ambao hawakuweza kuitwa na upande wa mashitaka kufika Mahakamani kwa ajili ya kutoa ushahidi wao.

Alidai kuwa watoto hao walimtaja Mangi ambaye anauza duka ambalo lipo karibu na nyumbani kwa Babu Seya ambaye anadaiwa kuona watoto hao wakati wakiingia na kuchukuliwa na mshitakiwa huyo wa kwanza na pia anadaiwa kusikia wakati watoto hao wakilia wakati wakifanyiwa vitendo hivyo.

Pia mbali na Mangi pia ilidai kuwa watoto hao walimtaja dada na bibi ambao walikuwa wakikutwa katika nyumba hiyo ambapo Marando alihoji kutokuitwa kwa watu hao kufika kutoa ushahidi ili kuweza kuthibitisha madai hayo.

“Kitu cha kushangaza zaidi ni madai ambayo yalitolewa kuwa watoto hao walifanyiwa vitendo hivyo tarehe 11 Oktoba wakati siku hiyo ilikuwa ni Jumamosi na pia mshitakiwa wa kwanza alikuwa amekamatwa na katika maelezo ya watoto hao inadaiwa kuwa walikuwa wakifanyiwa vitendo hivyo wakati wakitoka shule.

“Je siku hiyo ya jumamosi mbona haikutajwa wakati maelezi yanadai kuwa walifanyiwa siku za katikati ya wiki, Jamuhuri ingeweza kufanya uchunguzi ili kuweza kubaini mtu ambaye aliweza kuwabaka watoto hao na si kama jinsi inavyodaiwa,” alidai.

Alidai kuwa baadhi ya shahidi mtoto alishindwa kumtambua Babu Seya na mwingine alikanusha kubakwa na mshitakiwa wa 3 na 4 ambapo alidai kuwa hakimu aliandika kuwa kutokana na watoto hao kujuana alihisi kuwa ni lazima watoto hao walibakwa licha ya watoto hao kutothibitisha.

Aliongeza kuwa katika kielelezo kilichotolewa na Hospitali ya Mwananyamala kilidai kuwa mtoto mmoja aliambukiza Kisonono ambapo washitakiwa hao kupitia mawakili wao waliomba kwenda kuwapima washitakiwa hao ili kuweza kuona ni mshitakiwa yupi aliyekuwa amemuambukiza ugonjwa huo wa zinaa.

Alidai kuwa licha ya ombi hilo upande wa Jamuhuri ulikataa kuwapeleka washitakiwa hospitali kwa ajili ya kuweza kuwapima ugonjwa huo ambapo alidai kuwa mtoto mwingine katika maelezo yake alidai kuwa alilazimishwa na Babu Seya kumkamua vipele vilivyokuwa katika sehemu zake za siri vilivyokuwa vikitoa usaha na maji.

Hata hivyo wakili huyo alidai kuwa upande wa Jamuhuri haukuwa tayari kuwafikisha watuhumiwa hao katika kituo cha afya ili kuweza kuthibitisha madai hayo yaliyokuwa yamedaiwa.

“Mshitakiwa wa nne ambaye alikuwa ni mwanafunzi naye pia anadaiw akushiriki katika vitendo hivyo lakini upande wa Jamuhuri haukuwahi kumuita Mkuu wa shule ya sekondari ya Mbezi ambayo alikuwa anasoma ili kuweza kuthibitisha kama mwanafunzi wake alikuwa hafiki shule.

“Lakini mambo yote hayo hayakuweza kufanywa wakati kila mmoja anaelewa kuwa muda ambao anatoka mwanafunzi huyo watoto hao wanakuwa tayari hawapo lakini hazikuweza kufanyika jitihada mbalimbali,” alidai.

Alidai kuwa katika jarada la kesi hiyo, mashitaka mawili yalikuwa yakiingiliana ambapo shitaka moja lilidai kuwa watoto hao walifanyiwa vitendo hivyo Oktoba ambapo shitaka jingine lilidai kuwa watoto hao walifanyiwa vitendo vinvyo kwanzia April hadi Oktoba.

Alidai kuwa katika maelezo ya mashahidi hakuna shahidi aliyedai kuwa alifanyiwa vitendo hivyo kati ya Aprili hadi Julai na kwamba kwa kipindi hicho ambacho kimetajwa mshitakiwa wa 2 na 3 walikuwa wakishinda katika kambi yao ya mazoezi ya FM Academy.

Naye wakili wa upande wa Jamuhuri uliokuwa ukiongozwa na Justuce Mlokozi alikili watoto hao kutorekodiwa na pia kutofanyiwa kiapo ambapo alidai kuwa Mahakama iliegemea ushahidi wa Jamuhuri na kwamba hata kama kulikuwa na makosa madogomadogo yanaweza kutibika chini ya sheria namba 388 ya mwenendo wa mashahidi.

Mlokozi alidai kuwa waliamua kuwaleta watoto katika ushahidi huo kutokana na wao ndio walikuwa walengwa zaidi na wakati wakifanyiwa kitendo hicho hakuna watu wengine waliokuwa wakiona.

Aliendelea kudai kuwa kuhusu kutofautiana kwa miezi katika jarada la kesi hiyo alidai kuwa hakukuw ana tarehe maalum ambayo watoto hao wlaifanyiwa vitendo hivyo na kwamba walikuwa wakifanyiwa kwa nyakati tofauti.

Aliongeza kuwa kuhusu kusafiri kwa mshitakiwa wa 2 alidai kuwa hiyo si hoja kuwa hajatenda kosa ambapo alidai kuwa anaweza kuwafanyia kipindi ambacho anakuwa hapa jijini Dar es Salaam na kudai kuwa kuhusu Farida haiwezekani kuwafundisha watoto wote kusema uongo kama inavyodaiwa na utetezi.

Akihairisha kesi hiyo Jaji Kimaro, alisema kuwa Mahakama itatoa tarehe ya hukumu ya rufani hiyo baada ya kusoma maelezo yote yaliyotolewa na pande hizo mbili ikiwa ni pamoja na nyaraka rejea zilizotolewa.

Wakati kesi hiyo ikisikilizwa umati mkubwa watu ulimiminika Mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza rufani hiyo ambapo watu walijaa katika chumba cha Mahakama na katika naeneo ya Mahakama hiyo.

Mara baada ya kuhairishwa kwa kesi hiyo Marando alionekana kuwa mfalme na mkombozi kutokana na maelezo ambayo aliweza kuyatoa jambo ambalo liliwafanya mashabiki wa wanamziki hao kumita Simba wa Yuda Simba wa Yuda huku wakimpigia makofi.

Licha ya hayo wakati rufani hiyo ikiendelea hali isiyo ya kawaida watu walijikuta wakipiga makofi wakati ndani ya chumba hicho kilichokuwa kikitumiwa wakati wa kusikiliza rufani hiyo.

Babu seya na watoto wake watatu walihukumiwa kifungo cha maisha mwaka 2004, baada ya Mahakama kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa Jamuhuri dhidi ya kesi ya kudhalilisha kijinsia watoto wa kike.

Kesi hiyo iliyovuma kwa wakati huo ambayo ilikuwa ikisikilizwa na kutolewa hukumu na Hakimu Mkazi Addy Lyamuya ambaye amestaafu hivi karibuni. 


kwa hisani ya michuziblog

Article 11

$
0
0
NANI ANAFAA KUWA RAIS KWA AWAMU IJAYO?Urais Tanzania 2015.jpg

MAPACHA WATATU KUADHIMISHA SIKU YA KUZALIWA LE0.

$
0
0
Meneja wa bendi ya Mapacha Watatu, Khamis Dakota akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maadhimisho yao ya miaka minne tokea bendi yao imeanzishwa. Pembeni yake wanamuziki wajasiriamali, Khalid Chuma ‘Chokoraa’ na Joseph Michael Mponezya ‘Jose Mara’.
Waandishi wa habari wakifuatilia Mkutano huo ndani ya kiota cha Etasi (zamani Business Park) uliopo Victoria jijini Dar.

-BENDI ya Mapacha Watatu inayoongozwa na wanamuziki wajasiriamali, Khalid Chuma ‘Chokoraa’ na Joseph Michael Mponezya ‘Jose Mara’ leo Ijumaa Nov 22 katika ukumbi wa letasi (zamani Bussines Park) uliopo Victoria jijini Dar inatarajia kuzindua albam yake ya pili waliyoipa jina la Yarabi Nafsi.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari meneja wa bendi hiyo Khamis Dakota alisema kuwa baada ya miaka mine yenye changamoto nyingi wameamua kusherehekea pamoja na wanamuziki wakongwe kutoka bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’.

Bendi ya Mapacha Watatu ina albamu mbili ambazo ni Shika Ushikacho na Yarabi nafsi.

Dakota akizitaja nyimbo zilizomo katika albamu yao ya pili Yarabi Nafsi ni pamoja na Yarabi Nafsi uliobeba jina la albamu, Ujasiriamali, Naonewa, Chanzo Wanaume, Sumu Ya Mapenzi Remix, Usia wa Babu, Mpenzi Nenda na Wivu.

Naye Khalid Chuma Chokoraa alisema kwamba anawaalika mashabiki wa bendi hiyo waje kwa wingi leo kwani kutakuwa na burudani ya aina yake ambapo wakishuka FM Academia wakiingia Mapacha Watatu kazi itakuwa bubwa.

Akizuungumzia safari ya muziki ya bendi hiyo Meneja Dakota amesema kwamba wamepitia misukosuko mingi, kiingilio ni sh. 10,000.

kwa hisani ya Michuziblog

Goodmorning Njombe?????

P-SQUARE WATUA BONGO TAYARI KWA SHOW KESHO LEADERS CLUB

$
0
0

 Mwanamuziki wa kundi la P - Square, Paul Okoye akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarake Nyerere, Tayari kwa ajili ya kutoa burudani kwa Watanzania, Msanii huyo aliambatana na Pacha wake Peter Okoye ambao kwa pamoja wanaunda kundi la P- Square. Wasanii hao wameambatana na wenzao 13 ambao watatoa burudani jumamosi ya tarehe 23 Novemba. Tamasha hilo limeandaliwa na East African Radio na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
 Wanamuziki wa kundi la P- Square Peter na Paul Okoye wakisalimiana na Mtangazaji wa kiruo cha Televisheni cha EATV, mapema baada ya kuwasili katika Uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Nyerer e jijini Dar es Salaam. Wasanii hao wameambatana na wasanii wengine 13 kutoka katika bendi yao. Tamasha hilo limeandaliwa naEast African Radio na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
 Mwanamuziki wa kundi la P- Square Peter Okoye akizungumza na waandishi wa habari, mapema baada ya kuwasili katika Uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Nyerer e jijini Dar es Salaam. Wasanii hao wameambatana na wasanii wengine 13 kutoka katika bendi yao.  Pamoja nao katika picha ni pacha wa msanii  huyo Paul Okoye ambao kwa pamoja wanaunda kundi la P - Square Tamasha hilo limeandaliwa na EATV na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu akizungumza na wasanii Peter na Paul Okoye punde baada ya kuwasili katika Uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Nyerer e jijini Dar es Salaam. Wasanii hao wameambatana na wasanii wengine 13 kutoka nchini Nigeria.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu  na Afisa Udhamini na Matukio wa kampuni hiyo  Ibrahim Kaude, wakiongozana na wasanii Peter na Paul Okoye punde baada ya kuwasili katika Uwanja wa kimataifa wa Mwalimu Nyerer e jijini Dar es Salaam. Wasanii hao wameambatana na wasanii wengine 13 kutoka nchini Nigeria.

PSQUARE KUFANYA SHOW KWENYE JUKWAA HILI KESHO

BREAKING NEWZZZZ.

$
0
0

ZITTO NA KITILA MKUMBO WAVULIWA VYEO VYOTE NDANI YA CHADEMA.

 
Kikao cha Kamati Kuu ndiyo kimeisha muda huu, na taarifa zilizopo ni kwamba kambi ya PM7 imevunjwa rasmi baada ya viongozi wake kuvuliwa vyeo vyote walivyo navyo ndani ya chama.

Waliovuliwa vyeo ni Zitto Kabwe, ambaye amevuliwa nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa chama pamoja na nafasi ya Naibu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni. Dr. Kitila Mkumbo yeye amevuliwa nafasi ya mjumbe wa kamati kuu.

 
Kamati Kuu imewaandikia barua Zitto na Kitila, wajieleze ndani ya siku 14 kwanini wasifukuzwe uanachama.



WATUHUMIWA 10 WA MAUAJI YA DK. MVUNGI WAPANDISHWA KIZIMBANI LEO

$
0
0




 Watu 10 wanaotuhumiwa na mauaji ya Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Marehemu Dkt. Edmund Sengondo Mvungi (pichani) , leo walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, wakikabiliwa na shitaka moja la mauaji ya mwanasheria huyo mkongwe.
 

Saa 2:30 asubuhi washtakiwa hao wakiwa chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi walifikishwa katika viunga vya mahakama hiyo kwa ajili ya kusomewa mashitaka yao.

Washtakiwa hao ni,  wafanyabiashara Chibago Magozi maarufu kama Chiligati (32), mkazi wa Vingunguti, John Mayunga ama Ngosha (56), mkazi wa Kiwalani na Juma Kangungu (29), mkazi wa Vingunguti.

Wengine ni mlinzi wa Dk. Mvungi, Longishu Losingo (29), mkazi wa Kariakoo Msimbazi, dereva Masunga Msukuma (40), mkazi wa  Kitunda,Paulo Mdonondo (30), mkazi wa Tabata Darajani na Mianda Mlewa ama White (40), mkazi wa Vingunguti Shule ya Tapa.

Wengine ni, Zacharia Msese (33), mkazi wa Buguruni Ghana kwa Hawa Masudi, Msigwa Matonya (30), mkazi wa Vingunguti Machinjioni na Ahmad Kitabu (30), mkazi wa Kinondoni Mwananyamala.

Walisomewa mashitaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mhe. Sundi Fimbo. Wakili wa Serikali Aida Kisumo alidai kuwa washtakiwa hao wanakabiliwa na shitaka la mauaji ya makusudi.

Wakili Kisumo alidai kuwa Novemba 3, mwaka huu, eneo la Msakuzi Kiswegere, wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, washtakiwa kwa pamoja na kwa makusudi  walimuua Dk. Mvungi. 


Hata hivyo, Hakimu Sundi alisema kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka kisheria kusikiliza kesi za mauaji, hivyo  washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote hadi pale upepelzi wa kesi yao utakapokamilika,  na kesi hiyo kuhamishiwa Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam. 

Upande wa Jamhuri ulidai  kuwa upelelezi haujakamilika hivyo waliomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya kutajwa kesi hiyo. Hakimu Sundi alisema kesi hiyo itatajwa Desemba 5, mwaka huu, aliamuru washtakiwa wapelekwe mahabusu.

kwa hisani ya michuziblog

Article 4

$
0
0

Edward LOWASSA  ACHANGIA MAENDELEO YA ELIMU KATA YA KIGAMBONI JIJINI DAR 

 Umati wa Wakazi wa Mji wa Kigamboni,jijini Dar es Salaam wakiongoza Msafara wa Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli Mh. Edward Lowassa wakati alipokuwa akiwasili kwenye uwanja wa Swala,Tuamoyo Kigamboni,jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya hafla hupi ya kukabidhi madawati kwa shule mbali mbali za Msingi katika kata hiyo ya Kigamboni.Hafla hiyo iliandaliwa na Diwani wa Kata ya Kigamboni,Mh. Dotto Msawa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli Mh. Edward Lowassa akipata maelezo kutoka kwa wakinamama wajasiliamali wa Kikundi cha Vikoba Kata ya Kigamboni.Kushoto ni Mwenyeji wake ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kigamboni,Mh. Dotto Msawa.Mh. Lowassa ameahidi kukisaidia kikundi hicho sh. Mil 10 kwa ajili ya maendeleo ya kikundi hicho.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwasalimia wakazi wa Kata ya Kigamboni kwa kuwapungia mkono,wakati alipokuwa akiwasili kwenye Uwanja wa Swala,Tuamoyo Kigamboni,jijini Dar es Salaam.
Mh. Lowassa na Mwenyeji wake Diwani wa Kata ya Kigamboni,Mh. Dotto Msawa wakiangalia burudani mbali mbali zilizokuwa zikitolewa Uwanjani hapo.
Burudani mbali mbali.
Mh. Lowassa akipena mikono na Kinamama wa Kigamboni.
Diwani wa Kata ya Vijibweni,Mh. Suleiman Mathew nae alipata wasaa wa kutoa neno lake mbele ya mgeni rasmi.
Mratibu wa Elimu Kata ya Kigamboni na Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi,Raha leo,Mwl. Asha Ferouz akisoma lisala mbele ya mgeni rasmi.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokea lisala ya Maendeleo ya Elimu kata ya Kigamboni kutoka kwa Mratibu wa Elimu Kata ya Kigamboni na Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi,Raha leo,Mwl. Asha Ferouz.
Diwani wa Kata ya Kigamboni,Mh. Dotto Msawa akizungumza na Wananchi wake wa Kigamboni waliokuwa wamefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Swala,Tuamoyo Kigamboni,jijini Dar es Salaam leo.
Kinamama wa Kigamboni.
Diwani wa Kata ya Kigamboni,Mh. Dotto Msawa (katikati mwenye kipaza sauti) akiwatambulisha baadhi ya watendaji wake.
Diwani wa Kata ya Kigamboni,Mh. Dotto Msawa akizungumza na Wananchi wake wa Kigamboni waliokuwa wamefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Swala,Tuamoyo Kigamboni,jijini Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli Mh. Edward Lowassa akiwahutubia wakazi wa Kigamboni.
wakielekea kukata utepe.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na baadhi ya wanafunzi wa shule mbali mbali za msingi katika Kata ya Kigamboni jijini Dar es Salaam,wakati wa kuwakabidhi madawati 100,yaliyotolewa na Diwani wa Kata hiyo,Mh. Dotto Msawa.Wakati huo huo pia Mh. Lowassa ameahidi kuwaongezea wanafunzi hao idadi ya madawati mengine 100.
Baadhi ya wanafunzi wa shule mbali mbali za msingi katika Kata ya Kigamboni jijini Dar es Salaam wakiwa wameketi kwenye madawati hayo mara baada ya kukabidhiwa.
Mh. Lowassa akiagana na wana Kigamboni.
 
kwa hisani ya michuziblog

Article 3

$
0
0

RAIS DOKTA KIKWETE  AHITIMISHA ZIARA NCHINI POLAND NA KUREJEA NCHINI.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe Fatma Fereji wakati akiondoka hoteli ya Bristol jijini Warsaw, Poland, leo Novemba 22, 2013 tayari kwa safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi nchini Poland ambako alihudhuria Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabia nchi akiwakilisha viongozi wa Bara la Afrika
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Waziri wa Nchi katika Makamu wa Rais Dkt Tereiya Huvisa wakati akiondoka hoteli ya Bristol jijini Warsaw, Poland, leo Novemba 22, 2013 tayari kwa safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi nchini Poland ambako alihudhuria Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabia nchi akiwakilisha viongozi wa
Bara la Afrika

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na Katibu Mkuu  katika Ofisi ya Makamu wa  Rais  Mhe Sazi Salula  wakati akiondoka hoteli ya Bristol jijini Warsaw, Poland, leo Novemba 22, 2013 tayari kwa safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi nchini Poland ambako alihudhuria Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabia nchi akiwakilisha viongozi wa Bara la Afrika
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono Mwandishi wa Uhuru na Mzalendo Bw. Ramadhani Mkoma wakati akaiaga na kuondoka hoteli ya Bristol jijini Warsaw, Poland, leo Novemba 22, 2013 tayari kwa safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi nchini Poland ambako alihudhuria Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabia nchi akiwakilisha viongozi wa Bara la Afrika. Kushoto ni mwandishi wa ITV Bw. Emmanuel Buhohela, akifuatiwa na Naibu Mkurugenzi wa Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Richard Muyungi na Msaidizi wa Waziri Huvisa
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt Terezya Huvisa na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe Fatma Fereji wakati akiondoka hoteli ya Bristol jijini Warsaw, Poland, leo Novemba 22, 2013 tayari kwa safari ya kurejea nyumbani baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi nchini Poland ambako alihudhuria Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabia nchi akiwakilisha viongozi wa Bara la Afrika.Picha Zote na IKULU

CHADEMA HALI TETE

$
0
0

MAKAMU MWENYEKITI BARA CHADEMA AJIUZULU.Kushoto ni Waziri Mkuu wa TANZANIA mIZENGO pINDA Akiwa na Said Arfi Aliyejiuzulu Umakamu Mwenyekiti Bara CHADEMA.

Jopo La Chadema Lililowavua Uongozi Zitto KABWE na Dr.Kitila Mkumbo.

Taarifa Rasmi ya Dr.Arfi juu ya Kujiuzulu Kwake.

Napenda kuwasilisha kwako taarifa ya kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara kuanzia Leo Ijumaa 22 Novemba 2013 kwa kuchoshwa na Unafiki unaoendelea ndani ya Chama. Napenda ifahamike pia kwangu maslahi ya Wapiga kura, Wakaazi na wananchi wa Mpanda Mjini na Wilaya ya Mpanda ni muhimu katika kuwatumikia, hivyo basi sipo tayari kuchaguliwa marafiki.

Kwa kipindi kirefu zimekuwepo shutma dhidi yangu na kutiliwa mashaka mahusiano yangu na Mhe Pinda Waziri Mkuu pamoja na

kulijadili katika vikao kadha Mpanda na Dar es Salaam bado yapo mashaka kwa nini alipita bila kupingwa hayo yalikua maamuzi ya Wanampanda kwenu imekua ni tatizo lakin hamsemi kwa nini Majimbo mengine 16 nchini yalipita bila kupingwa mlikua wapi na nani alaaumiwe huu ni Unafiki  wa kupindukia.

Aidha mmechukizwa sana kwa nini nilihoji kauli ya Muasisi wa Chama Mhe Mtei kutuchagulia viongozi naomba ifahamike wazi kwamba huu ni mtazamo wangu na utabakia hivyo siku zote kwa chama cha demokrasia kutoruhusu uongozi wa kiimla kwa kukidhi matakwa ya Waasisi ambao huvigeuza vyama kuwa Mali binafsi

Kwa kusema ukweli na kusimamia ukweli daima itabakia kuwa lengo langu katika maisha yangu siku zote hata kama itanigharimu maisha yangu

Nawasilisha.

Said A Arfi (mb)

Article 1

$
0
0

Ismail Aden Rage KUTOA TAMKO LAKE LEO SIMBA BAADA YA KUREJEA BONGO.

.Akerwa Zitto Kabwe kuvuliwa Uongozi. rage

DSC_0023Mwenyekiti wa klabu ya Simba Ismail Aden Rage amewasili Dar es salaam Tanzania leo akitokea Sudan ambapo alipokelewa na baadhi ya Wanachama wa Simba kwenye Uwanja wa ndege wa mwalimu JK.Nyerere.
Waandishi wengi walikua na maswali mengi kuhusu yeye kusimamishwa kuwa Mwenyekiti wa Simba lakini akayapangua kwa kusema kesho mchana ndio atazungumza na Waandishi kuhusu kila kitu ila sentensi moja iliyonyakwa na millardayo.com ni ‘taarifa za kusimamishwa Uwenyekiti sijazipata ndio kwanza nakusikia wewe, ninachojua mimi bado ni Mwenyekiti wa Club ya Simba’
‘Nimefurahi kwa mapokezi mazuri ambayo yameonyesha imani ya Wanachama kwangu mimi, mimi kama Mwenyekiti nitatoa tamko langu rasmi kesho mchana makao makuu ya Club ya Simba, sasa hivi siwezi manake rafiki yangu mpenzi Zitto kabwe ameondolewa kwenye Unaibu katibu mkuu na mimi sijafurahia kwa hiyo siko kwenye mood ya kuongea’ – Aden Rage
Alipoulizwa kama ana taarifa za kocha mpya Simba na pia kikao hicho atakifanyiaje Makao Makuu wakati ameondolewa kwenye Uwenyekiti, Rage kasema swala la kocha atalizungumza kesho ila hilo la kufanyia mkutano na Waandishi wa habari makao makuu ya Simba, waandishi wasiwe na wasiwasi kwani yeye ndio Mwenyekiti.
rageKuhusu kikao kilichofanyika na kumuondoa kwenye nafasi ya Uwenyekiti, Ismail Aden Rage amesema kikao kilichofanyika sio halali manake ukisoma katiba ya Simba, FIFA na CUF katika aya zote hakuna aya inayosema kamati ya utendaji ina mamlaka ya kumsimamisha Rais au Mwenyekiti.
DSC_0005            Baadhi ya Wanachama wa Simba wakicheza wakati wa mapokezi.

Article 0

$
0
0
WATUHUMIWA 10 WA MAUAJI YA DR.SENGONDO MVUNGI HAWA HAPA.

Article 4

$
0
0

ZITTO NA DR.MKUMBO WAMEANZA YAO NA WANAHABARI SASA.

ZK_692ab.png
Ndugu zangu,
Kuna habari kubwa leo; mkutano wa Zitto na Dr. Kitila Mkumbo na Watangazaji wa habari.

Wengine sisi ni wadadisi na wachambuzi wa habari.

Endelea Kufuatilia mtandao huu kwa kitakachojiri.

Article 3

$
0
0

PAMOJA NA KUSIMAMISHWA  UENYEKITI RAGE AAGIZWA KUITISHA MKUTANO SIMBA NDANI YA SIKU 14.


Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage ameagizwa kuitisha Mkutano Mkuu wa Dharura wa klabu ndani ya siku 14 kuanzia sasa.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa agizo hilo baada ya kubaini kuwa mgogoro katika klabu baada ya kupokea barua mbili; moja kutoka Kamati ya Utendaji ikielezea kumsimamisha uongozi Rage, na nyingine kutoka kwa Mwenyekiti huyo ikielezea kutotambua kusimamishwa huko.

Uamuzi wa TFF umefanywa kwa kuzingatia Ibara ya 1(6) ya Katiba ya Simba inayosema: “Simba Sports Club ni mwanachama wa TFF, itaheshimu Katiba, kanuni, maagizo na uamuzi wa TFF na
FIFA, na kuhakikisha kuwa zinaheshimiwa na wanachama wake.”

TFF itatuma wawakilishi wake katika mkutano huo, na kumuagiza Mwenyekiti wa Simba kuhakikisha wanachama wote wenye hoja wanapata fursa ya kusikilizwa.

Article 2

$
0
0
 Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Mkoa wa Njombe TCCIA  Bwana  Oraph Mhema Akifungua Kikao Hicho Leo Mchana.
 Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Mkoa wa Njombe Bwana Menardy MlyukaAkizungumza Kwenye Kikao Hicho Leo.
 Baadhi ya Wafanyabiashara Mkoani Njombe Wakiwa Kwenye Kikao Chao Leo.



Na Gabriel Kilamlya Njombe

Wafanyabiashara wa Biadhaa Mbalimbali Mkoani Njombe Wametishia Kugomea Utaratibu wa Matumizi ya Mashine Mpya za Risiti za EFD Endapo Serikali Haitowapunguzia Kodi ya Asilimia 18% Pamoja na Kuangalia Uwezekano wa Kupunguza Gaharama za Ununuzi wa Mashine Hizo.

Kauli hiyo Wameitoa Leo Kwenye Kikao cha Wafanyabiashara Hao Kilichoitishwa na Chama cha Wafanyabiashara Mkoa wa Njombe Tanzania Chamber of Commerce TCCIA Kilicholenga Kujadili namna ya Kukutana na Serikali Kupitia Mamlaka ya Mapato TRA Katika Kupata Ufafanuzi Juu ya Mashine Hizo.

Baadhi ya Wafanyabiashara Hao Ambao Tayari

Wanaendelea Kuzitumia Mashine Hizo Wamesema Kuwa Matumizi ya Mashine Hizo Yamekuwa Yakiwaletea Shida Kubwa Kutokana na Usumbufu Wake Kwani Zimekuwa Zikiharibika Mara kwa Mara na Hata Mafundi wa Kuzitengeneza Hawapatikani.

Akifungua Kikao Hicho Kilichofanyika Katika Ukumbi wa Turbo Mjini Njombe  Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Mkoa wa Njombe TCCIA  Bwana  Oraph Mhema  Amewataka Wafanyabiashara hao Kuimarisha Umoja wao Ili Kurahisisha Uwasilishaji Hoja Zao Serikalini Kwa Nia ya Kukuza Uchumi wa Taifa na Wafanyabiashara Wenyewe Tofauti na Ilivyo sasa.

Kwa Upande Wake Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Mkoa wa Njombe Bwana Menardy Mlyuka Amesema Kwa Kuwa Serikali Mkoani Njombe Imepanga Kukutana nao Novemba 27 Mwaka Huu Kuzungumzia Suala Hilo Ni Lazima Kama Wafanyabiashara Wakajitokeza Kwa Wingi Ili Kufahamu Dhima ya Serikali Kwa Wafanyabiashara Katika Kilio chao Juu ya Mashine Hizo.

Hivi Karibuni Wafanyabiashara wa Mikoa ya Dodoma,Mbeya na Dar es Salaam Waligomea Kununua Mashine Hizo Kutokana na Gharama Kubwa Ya Shilingi Laki Nane Pamoja na Makato Mbalimbali Yanayotokana na Biashara zao Hali Inayopelekea Kufilisika Mtaji Ilihali Wanakopa Benki na Kwenye Taasisi Nyingine.
.

Article 1

$
0
0

ZITTO KABWE ASEMA CHADEMA NDICHO KILICHOMLEA HIVYO HAWEZI KUHAMA.

 

1. Utangulizi 

Katika kikao chake cha siku mbili kilichofanyika tarehe 20 - 22 Novemba 2013, Kamati Kuu ya CHADEMA, pamoja na mambo mengine, iliazimia kunivua nafasi zangu zote za uongozi ndani ya chama. Kwa mujibu wa taarifa ya chama iliyotolewa katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Ijumaa tarehe 22 Novemba 2013, ilielezwa kwamba sababu za kuvuliwa uongozi mimi na Dk Kitila Mkumbo ni uhaini na hujuma kwa chama kutokana na waraka unaojulikana kama mkakati wa uchaguzi 2013. Ukweli ni kwamba waraka uliotajwa si sababu ya mimi kuvuliwa nafasi zangu za uongozi kama ilivyojadiliwa katika Kikao cha Kamati Kuu . Sababu za kufukuzwa kwangu kama zilizojadiliwa katika kikao cha Kamati Kuu ni tuhuma lukuki ambazo si mara yangu ya kwanza kuzisikia zikijadiliwa ndani na nje ya vikao vya chama. 
 
Hitimisho la tuhuma hizi ni kwamba mimi nimekuwa nikikisaliti chama kwa kutumika na CCM na Usalama wa Taifa. Nitazianisha tuhuma hizi na kuzijibu kama ambavyo nimekuwa nikizijibu katika vikao mbalimbali vyama.

Ninatambua kwamba chama changu kinapita katika wakati mgumu sana sasa hivi. Nataka nitamke mapema sana kwamba mimi Zitto Zuberi Kabwe sitokuwa chanzo cha CHADEMA kuvunjika. Hiki ndicho chama kilichonilea na kunifikisha hivi nilivyo. Ningependa chama hiki mtoto wangu atakapokuwa mtu mzima na atakapoamua kujiunga na siasa aingie CHADEMA. Bado nina imani kubwa na chama changu na ninaamini ndicho kinachostahili kuendesha nchi jana, leo na kesho.

2. Kuhusu tuhuma mbalimbali zinazo elekezwa kwangu


Zipo tuhuma nyingi ambazo zimekuwa zikirudiwarudiwa katika vikao vya chama na nje ya vikao na baadhi ya viongozi wenzangu. Tuhuma hizi zinalenga kuonyesha kwamba mimi ni mbinafsi na kwamba ninapokea rushwa ili kukihujumu chama changu. Nitazianisha tuhuma kwa kifupi na kuzijibu kama ambavyo nimekuwa nikizijibu katika vikao mbalimbali vya chama. 



i) Tuhuma kwamba sikushiriki kumpigia kampeni mgombea wetu wa urais katika uchaguzi wa mwaka 2010. Ningependa kueleza yafuatayo kuhusu jambo hili: 
  • Mimi nilikuwa mgombea wa ubunge katika Jimbo la Kaskazini huko Kigoma.
  • Pamoja na kuwa mgombea wa ubunge, nilifanya kampeni katika majimbo mengine 16 katika mikoa mbalimbali, ikiwemo Dar es Salaam, Mtwara, Pwani, Shinyanga, Mara na Rukwa. 
  •  
  • Hakuna kiongozi yeyote wa juu aliyefanya kampeni katika majimbo mengi kama mimi, ukiacha mgombea urais.
  •  
  • Kote nilipopita nilimpigia kampeni wagombea wetu wa udiwani, ubunge na Rais.
  •  
  • Katika Mkoa wa Kigoma nilizunguka na mgombea urais katika kata zote za Kigoma Kaskazini na majimbo yote manane ya Mkoa wa Kigoma.

ii) Tuhuma kwamba katika Mkoa wa Kigoma nilishindwa kuwapigia kampeni wagombea wetu kiasi kwamba peke yangu ndiye niliyeshinda katika uchaguzi huo. Ukweli ni kwamba niliwapigia sana kampeni wagombea wetu, na hivyo ndivyo wapiga kura wa Kigoma walivyoamua. 


iii) Tuhuma kwamba nilishiriki kuwashawishi wagombea wetu katika baadhi ya majimbo kujitoa katika uchaguzi wa mwaka 2010 ili kuwapisha wagombea wa CCM wapite bila kupingwa kwa njia ya rushwa. Majimbo yanayotajwa ni pamoja na Sumbawanga, Musoma Vijijini na Singida Mjini. Kama nilivyokwisha kueleza katika vikao mbalimbali vya chama jambo hili si la kweli na hakuna popote ambapo watoa tuhuma hizi wamewahi kutoa ushahidi kwamba nilifanya jambo hili. Nipo tayari kwa uchunguzi ndani ya chama na watoa tuhuma waje na ushahidi bayana wa jambo hili. Si afya kwa chama kuendelea kurudiarudia tuhuma hizi kila mara tangu mwaka 2010 bila uchunguzi wowote kufanyika na jambo hili lifikie mwisho. 

iv) Tuhuma kwamba nimekuwa sishiriki katika operesheni mbalimbali za chama: Ukweli ni kwamba nimeshiriki sana katika operesheni mbalimbali za chama ndani na nje ya nchi. Kwa mfano, mwaka 2011 tulikuwa na operesheni kubwa katika mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na nilikwenda katika mikoa yote tuliyotembelea. Mwaka 2012 baada ya hoja ya mkonge bungeni nilifanya ziara Mkoa wa Tanga. Mwaka 2012 kulikuwa na operesheni kubwa moja katika mikoa ya kusini ya Mtwara na Lindi. Operesheni hii sikushiriki kwa sababu nilikuwa nchini Marekani kufungua matawi kwa mwaliko wa Watanzania wanaoishi huko. 


v) Tuhuma kwamba nimekidhalilisha chama kwa tamko la PAC kwamba Hesabu za Vyama hazijakaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG): Katika jambo hili ninatuhumiwa kwamba mimi kama Naibu Katibu nilipaswa kuwasiliana kwanza na viongozi wa chama 'kuwatonya' ili wajiandae. Kwamba kutokuwatonya kumekidhalilisha chama na kukiweka kundi moja na CCM na nastahili kuadhibiwa vikali kwa kuwa katika taarifa yangu nilikuwa na nia mbaya na chama chetu. Maelezo yangu niliyoyatoa na ambayo ningependa kuyakariri hapa kuhusu jambo hili ni kama ifuatavyo: 

  • Utawala bora hautaki mimi kutumia nafasi yangu ya uenyekiti wa PAC kulinda chama changu na kuonea vyama vingine. Kufanya hivyo ni kuendeleza tabia zile zile ambazo tunazipinga na ambazo tunapigania kuzibadilisha
  •  
  • Napenda kusisitiza kwamba hakuna chama ambacho kimewahi kukaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG). Natambua kwamba mahesabu ya chama changu yamekuwa yakikaguliwa na wakaguzi wa nje kwa utaratibu tuliojiwekea. Lakini matakwa ya kisheria ni kwamba mahesabu ya vyama vya siasa hayajakaguliwa na CAG, na hili ni kosa la kisheria, bila kujali kosa hili ni la nani.

vi) Tuhuma kwamba mimi ni mnafiki katika kukataa kwangu kuchukua Posho za Vikao 

Mtakumbuka kwamba mimi nilikataa kuchukua posho tangu mwaka 2011 kama ishara ya kuonyesha kwa vitendo msimamo wa chama chetu wa kupinga posho za kukaa na matumizi mengine yasiyofaa katika fedha za umma kama ilivyoanishwa kwenye Ilani yetu ya mwaka 2010-2015. Mtakumbuka kwamba hivi karibuni Mheshimiwa Lema amenishutumu kwamba kukataa kwangu kuchukua posho ni unafiki kwa sababu ninapokea posho kubwa zaidi katika mashirika ya umma ambapo mimi ni mwenyekiti wa kamati husika. Ninapenda kueleza yafuatayo kuhusu jambo hili:


  • Sipokei posho yeyote ya vikao (sitting allowance) ndani na nje ya Bunge tangu mwaka 2011. Hii ni pamoja na vikao vyote katika Kamati za Bunge ninavyohudhuria. Mtu yeyote mwenye ushahidi vinginevyo auweke hadharani.
  • Swala la kukataa posho (sitting allowance) ni swala la kiilani katika chama chetu, na kwangu ni swala la kimisingi zaidi. Katika Wilaya yangu vifo vya kina mama wajawazito ni 1900 kati ya wanawake 100,000 wenye ujauzito. Vifo hivi vinatokana na ukosefu wa huduma kwa sababu ya bajeti finyu. Ndiyo maana nilifurahi sana kwa chama chetu kuliweka swala la kupunguza matumizi ya Serikali katika Ilani, na kuondoa posho za wabunge, ambao tayari wanapokea mishahara mikubwa, kungesaidia sana kupatikana fedha ambazo zingeokoa vifo vingi vya kina mama.
  • Jambo hili si suala la ugomvi baina yangu na Mheshimiwa Lema. Ni suala la msingi katika chama chetu.

3. Usambazaji wa Ripoti ya Siri kuhusu Zitto Kabwe 

Hivi karibuni kulisambazwa waraka unaoitwa ripoti ya siri kuhusu mimi ukibeba lundo la tuhuma kwamba nimehongwa fedha nyingi ili kukihujumu chama changu. Waraka huu ulidaiwa kuwa umechomolewa kutoka makao makuu ya CHADEMA. Jambo hili pia lilijadiliwa katika kikao cha juzi kwa kifupi, na majibu ya viongozi wa chama ilikuwa ni kwamba waraka huu haukuandaliwa wala kusambazwa na makao makuu. Katika mchango wangu nililalamikia mambo matatu yafuatayo:



  1. Kwamba baadhi ya waliokuwa wanasambaza waraka ule walikuwa ni viongozi wa chama chetu. Bahati mbaya hadi leo hakuna hata mmoja ambaye amekwishachukuliwa hatua za kinidhamu. Ninaamini kwamba kuna siku watu hao watachukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu za chama chetu.
  2. Kwa kuwa chama kimekana rasmi kuhusika na waraka huu, nitaendelea na taratibu za kisheria ili kuhakikisha kwamba wote waliohusika kutengeneza hekaya ile wanachukuliwa hatua stahiki za kisheria.

4. Hitimisho

Ninatambua kwamba kuna watu walitegemea leo ningejibu mapigo na ningewazodoa watu kwa majina kama ilivyo kawaida katika siasa za Tanzania. Natambua pia kwamba, kama ilivyo kawaida wakati wa migogoro katika vyama vya siasa hapa Tanzania, kuna watu walitegemea leo ningetangaza 'maamuzi magumu'. Natambua kwamba wapo ambao wangependa kupata nafasi ya kuendelea kutumia suala hili katika harakati zao za kudhoofisha mapambano ya demokrasia na uthabiti wa siasa za ushindani nchini mwetu. Napenda wanachama wa CHADEMA na wapenda demokrasia na siasa safi wote nchini watambue kwamba mimi bado ni mwanachama mwaminifu wa chama hiki na nitakuwa wa mwisho kutoka kwenye chama hiki kwa hiari yangu. Nitafuata taratibu zote ndani ya chama katika kuhitimisha jambo hili.


Naomba wanachama waelewe kwamba mimi kama binadamu ninaumia ninapopigwa. Tuhuma ninazorushiwa ni kubwa na zinanikwaza. Tuache siasa za uzushi ili tujenge chama chetu na nchi yetu, ili hatimaye tuwakomboe Watanzania wenye matarajio na imani kubwa kwa chama chetu.



Kama mwanasiasa kijana niliyekaa katika siasa kwa muda sasa yapo mengi mazuri nimeyafanya. Lakini kuna maeneo nilipojikwaa na yapo makosa niliyofanya kisiasa katika maisha yangu ya siasa.


Kinachoendelea ndani ya chama chetu ni mapambano ya kukuza demokrasia. Ni mapambano baina ya wapenda demokrasia dhidi ya wahafidhina, waumini wa uwajibikaji dhidi ya wabadhirifu na wapenda siasa safi dhidi ya watukuzao siasa majitaka. Hii ni changamoto kubwa ndani ya chama chetu inayohitaji uongozi shupavu kuikabili. Nitasimama daima upande wa demokrasia. Kama alivyopata kunena mmoja ya wanasiasa maarufu, 'kiwango cha juu kabisa cha uzalendo katika nchi ni kukubali kutofautiana kimawazo', na ninatamani huu ndio uwe utamaduni wa chama chetu.(tembelea Mwananchi Blogu)


Kabwe Zuberi Zitto, Mb

Dar es Salaam.

Article 0

$
0
0
 

 Refa Huyo Anayeonekana Anaitwa Bwana Mashaka Lulambo Ndiye Aliyeanza Kupigwa Uwanjani Humo Leo.



Baadhi ya Askari Polisi Waliovalia Mavazi ya kawaida Wamenaswa Wakileta Vurugu Katika Uwanja wa Sabasaba Mjini Njombe Baada ya Timu yao Kufungwa na Timu ya Njombe Mji Leo.

Baadhi ya Watu Wameweza Kupigwa na Kujeruhiwa na Askari hao Akiwemo Refa Pamoja na Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Radio Uplands Fm Bwana Michael Ngilangwa na Kuvunjiwa Vifaa Vyake Vya Kazi Ikiwemo Kamera Aliyokuwa Akipigia Picha na Kinasa sauti na Simu yake Ya Mkononi.

Article 4

$
0
0

SERIKALI ZA MITAA ZISHIRIKIANE NA SEKTA BINAFSI - WAZIRI MKUU,PINDA


WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema anatamani kuona Serikali za Mitaa hapa nchini zinasimamia maendeleo kuanzia ngazi ya chini kwa kushirikiana na sekta binafsi ikiwa ni njia ya kuharakisha maendeleo kwa wananchi.

Ametoa kauli hiyo huo leo mchana (Jumatatu, Novemba 25, 2013) wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano wa ushirikiano baina ya Mamlaka za Serikali za Mitaa za China na Tanzania ulioanza leo jijini Dar es Salaam.

Ni muhimu tukaanzisha ushirikiano huu kwenye ngazi ya Serikali za Mitaa kwa sababu usimamizi wake unakuwa karibu zaidi na wananchi kuliko ilivyo hivi sasa”, alisema.
 

Kuhusu ujio wa magavana, mameya na wafanyabiashara wapatao 71 kutoka majimbo manne ya Shandong, Liaoning, Shaanxi na Jilin, Waziri Mkuu alisema ujio wao
umekuja wakati muafaka kwani unasaidia kujenga mahusiano ya karibu zaidi na wananchi kwenye ngazi ya chini kuliko inavyokuwa kuna mahusiano kwenye ngazi ya Kitaifa peke yake.

KWA Hisani ya Michuziblog.
Viewing all 2276 articles
Browse latest View live