Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all 2276 articles
Browse latest View live

MWALIMU AFUNGWA MIAKA 30 KWA KUMBAKA MWANAFUNZI WAKE

$
0
0
MAHAKAMA ya Wilaya ya Ludewa katika Mkoa wa Njombe imemhukumu kwenda jela miaka thelathini na kuchapwa viboko 30 matakoni mwalimu Romanus Msango wa shule ya msingi Ingwachanya na mkazi wa Lupembe wilayani Njombe kwa kosa la kubaka mwanafunzi wa miaka 14 na kumuumiza vibaya katika sehemu za mwili wake.

Akisoma hukumu hakimu mkazi mfawidhi katika mahakama ya wilaya ya Ludewa Fredrick Lukuna alisema mahakama imeridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na kwamba hakuna shaka lolote katika kuthitisha mshtakiwa kutenda kosa hilo linaloangukia katika kifungu namba 1309(1) na 31(1) kaanuni ya adhabu zuzu ya mwaka 2002.
Pamoja na kuwa mshtakiwa ni mkosaji wa kwanza na kwa kuzingatia taaluma ya mshtakiwa na makosa haya kushamili katika jamii ya wana Ludewa, matendo haya yakiachwa yanaweza kuleta athari kwa watoto na wananwake ikiwemo magonjwa ya kuambukizwa. Natoa amri utakwenda jela miaka 30 na viboko thelethini.””” aliamuru Lukuna

Awali ilidaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashtaka mratibu wa polisi Edison Kasekwa(SP) kuwa mshtakiwa Romanus Msango alitenda ukatili huo wa kinyama Augost 20 mwaka jana katika kijiji cha Masimbwe kata ya Mlangali ambapo kabla ya kutenda kosa hilo alimshambulia mhanga na kisha kubaka na kumlawiti na kumsababishia maumivu makali mwilini.

hakuna makosa ya awali kwa mshtakiwa hata hivyo serikali ilimpa dhamana kubwa ya kulea watoto ambao ni nguvukazi ya Taifa la kesho lakini amewageuka na kutenda kitendo kinyume na maadili ya kazi yake na kuidharirisha taaluma pamoja na serikali naomba mahakama itoe adhabu kali ili liwe fundisho kwa walimu wenye tabia kama hii’’’’’ alihitimisha Kasekwa

Kasekwa aliongeza kuwa mshtakiwa alikusudia kutenda makosa hayo kwa sababu alimfuata mwanafunzi huyo shambani alikokuwa akivuna mahindi na wenzake ambao walikimbia kwenda kijiji kutoa taarifa baada ya mwalimu kumkamata mwenzao na kumpeleka kichakani.

Wakati huohuo watu wawili Bahati Mtega na Flowin Mtweve wakazi wa Milo wamehukumiwa kifungo cha maisha na kuchapwa viboko 12 kila mmoja kwa kosa la kumbaka kwa pamoja mtungo au (gang rape) Ester Mchiro makosa yanayoangukia katika kifungu cha 131(A).

Watuhumiwa hao walimbaka Bi. Ester Mchiro ambaye ni mke wa mtu hali ambayo ilisababisha mama huyo kupiga kelele na kuomba msaada ndipo raia wema walipokusanyika na kumkamata moja wa wabakaji hao na kumshikisha adabu kabla ya kumpeleka kituo cha Polisi Lugarawa ambapo mtuhumiwa mmoja alitimua mbio.



SERIKALI YACHELEWA MALIPO KWA WAKULIMA NJOMBE

$
0
0
 
Bi.Rose Mbuya  msimamizi wa NFRA kituo cha Ludewa mjini akiwa kazini
 Bi.Rose Mbuya akiendelea na majukumu ya kila siku
            Baadhi ya mahindi ambayo yameshanunuliwa

Wakulima wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe wameanza kutoa malalamiko kutokana na kutolipwa fedha zao kwa wakati kutoka kwa wakala wa hifadhi ya chakula Taifa(Nation Food Reseve Agents)kwani mategemeo yao ni kuuza mahindi na kupata fedha kwa wakati ili waweze kuwalipia watoto wao michango ya shule.

Akitoa malalamiko hayo mmoja mmoja wa wakulima wilayani hapa Bw.Mathayo Mwinuka alisema kuwa kumekuwa na ucheleweshaji mkubwa wa malipo tofauti na awali ambapo ilikuwa haidizi muda wa wiki moja baada ya kupima mahindi na kupewa fundi wakulima kulipwa fedha zao.

Bw.Mwinuka alilalamikia hilo kutokana na mamlaka hiyo inayonunua mahindi wilayani Ludewa na wilaya nyingine nchini kukaa na fedha za wakulima wa mahindi wilayani humo zaidi ya wiki tatu hivi sasa bila ya kuwalipa wakulima hao ambao hutegemea fedha hiyo katika kulipia ada watoto wao na matumizi ya kila siku.

“Inashangaza kuona tunauza mahindi ili tuweze kutatua matatizo yetu haraka lakini tunacheleweshewa malipo yetu mpaka watoto wetu wanafukuzwa mashuleni na kuzuiliwa kufanya mitihani kutokana na kukosa ada,kwani awali tulikuwa tukiuza mahindi na kupata fedha kwa wakati hivyo tunaomba Serikali kuliangalia hilo sisi si wakulima wa kahawa ambao huchukua fedha kwa msimu”,alisema Bw.Mwinuka.

Alisema mpaka sasa ni wananchi wengi ambao wameuza mahindi yao katika mamlaka hiyo hawajapata fedha lakini wako wengine waliowauzia walanguzi tayari wameshalipwa fedha zao kwa wakati hali inayowakatisha tamaa wakulima wengine kupeleka mahindi katika mamlaka hiyo wakihofia kucheleweshewa fedha zao.

Aidha Msimamizi wa manunuzi wa mamlaka ya NFRA katika kituo cha Ludewa mjini Bi.Rose Mbuya aliwataka wakulima hao wasiwe nawasiwasi kuhusiana na malipo ya mazao yao kwani kulikuwa na matatizo kidogo katika ofisi ya kanda Makambako lakini tatizo hilo limesha tatulika na hivi punde malipo hayo yatafanyika.

Bi.Mbuya alisema mpaka sasa mahindi yaliyonunuliwa ni zaidi ya tani 64501 na bado mahindi yanaendelea kununuliwa hivyo wakulima wanashauliwa kuendelea kupeleka mahindi yao ili yapimwe mapema bila kujali fedha za awali bado hazijalipwa kama wanavyolalamika.

Alisema kuwa wamepokea malalamiko mengi yakiwemo ya kutotenda haki katika upimaji na wengine kukataa kukatwa kiasi kilo moja na nusu kwaajili ya uchafu wa mahindi wanayoyaleta,hizo zote ni changamoto tu lakini malipo yao yatafanyika hivi karibuni.

“ni kweli wakulima hawajalipwa kwa muda mrefu na tunakili tumewaharibia malengo yao lakini wasihofu walipo yatafanyika ila kitu cha msingi ni kwamba wasikatishwe tamaa na hali hii iliyotokea sasa,kulikuwa na matatizo kidogo katika kituo cha Makambako ila hali imeshatengamaa nawashauri waendelee kuleta mahindi yao malipo yatafanyika”,alisema Bi.Mbuya.

Bi.Mbuya alisema wanakumbana na changamoto nyingi katika manunuzi ya mahindi ikiwemo ya wakulima kuleta mahindi machafu yenye fumbi na kugomea wanapopewa utaratibu wa kufanya kutokana na hali hiyo imekuwa vigumu kuwaelimisha wakulima hao kutokana na wao kuona hawatendewi haki.

Mwisho.
habari hii ni kwa udhamini wa Lukotiko bucher.

Ni wauzaji wa nyama ya Ng'ombe wa kienyeji wanapatikana wilayani Ludewa.
ufikapo wilayani Ludewa wanapatikana sokoni katika jengo la soko la Samaki.

kwa nyama bora kwaajili ya harusi,sherehe na matatizo mbalimbali onana na Lukotiko bucher.

Pia wananunua ng'ombe wa kienyeji pahala popote wilayani Ludewa.

kwa mawasiliano zaidi piga simu namba 0765878297/0764096248/0765796655 na 0755194056.
kutana na Lukotiko Bucher kwa nyama bora.

Article 1

$
0
0

MGOMO WA MADEREVA DALADALA WA POSTA IRINGA NA IPAMBA watatuliwa.

 

daladala  pekee  ya Ipamba  Posta  inayoendelea kufanya kazi
Mbunge wa  jimbo la Iringa mjini akiongozana na madereva hao
Mbunge  wa jimbo la Iringa mjini akiingia ofisi za Sumatra  kuhoji madai ya madereva waliogoma kama yana ukweli  wowote
wawakilishi wa madereva hao wakiingia ofisi za Sumatra
Mbunge  wa  jimbo la Iringa  mjini mchungaji Peter Msigwa (kulia) akifanya majadiliano na ofisa wa Sumatra mkoa wa Iringa Bw Rahim Kondo (wa  pili kulia) mbele ya wawakilishi wa madereva kushoto juu  ya malalamiko yao ya kudai kunyanyasika ,japo hadi sasa madai  hayo yameonyesha  kuwa si kweli kwa hisani ya fg blog.

Article 0

$
0
0

BODI MPYA YA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA MBEYA YAZINDULIWA 

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akimkabidhi sanduku lenye vitendea kazi makamu mwenyekiti wa bodi hiyo Msambichaka
 Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akizindua bodi mpya ya Mamlaka ya maji Jiji la Mbeya
Mwenyekiti mpya wa bodi ya maji na usafi wa mazingira Jaji Atuganile Ngwala akishukuru kwa kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa bodi hiyo
Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Simon Shauri, akitoa taarifa ya Mamlaha hiyo mbele ya mgeni rasmi, Mkuu wa mkoa wa Mbeya A
 Mmoja wa wajumbe wa bodi ya maji iliyomaliza muda wake Aloyce Mwitagila akitoa shukrani kwa niaba ya mwenyekiti wa zamani Mwakatundu

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akimkabidhi sanduku lenye vitendea kazi Mwenyekiti wa bodi hiyo Jaji Atuganile Ngwala

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akimkabidhi sanduku lenye vitendea kazi mmoja wa wajumbe wa bodi mpya ya maji Katibu tawala wa mkoa wa Mbeya Mariam Mtunguja.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro wa pili kutoka kushoto, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi mpya ya Mamlaka ya Maji na usafi wa mazingira Jiji la Mbeya.


Na Mbeya yetu

Article 24

$
0
0
CCM WILYA YA NJOMBE YATAKA KUENDELEZWA KWA MIRADI KATA YA MATOLA.7 2aac9
Na  Steven  Ngole Njombe

 Chama cha Mapinduzi Wilayani Njombe Kimewataka Wananchi wa Kata ya Matola Kuiendeleza Miradi ya Maendeleo Inayotekelezwa Katika Kata Hiyo Kwa Lengo la Kusogeza na Kuboresha Huduma za Kijamii.

Agizo Hilo Limetolewa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Njombe Adam Msigwa Wakati wa Ziara ya Siku Moja Iliyolenga Kutembelea na Kukagua Miradi ya Maendeleo Inayotekelezwa  Katika Kata Hiyo , Ikiwa ni Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu ya Mwaka 2010/2015.

Aidha Mwenyekiti Huyo Aliyeambatana na Viongozi Wengi wa CCM Wilaya   Kwenye Ziara Hiyo Wametembelea na Kukagua Ujenzi wa Vyumba Vya Madarasa, Mabweni , Nyumba za Walimu, Zahanati, Pamoja na Vyoo Vya

Miradi Ambayo Inagharimu Zaidi ya Shilingi Milioni 297  Hadi Kukamilika Kwake.

Akiongea na Wananchi wa Kata ya Matola  Katibu Mwenezi wa CCM  Wilaya ya Njombe Hitra Msola Amewataka Wananchi wa Kata Hiyo Kuwapuuza Watu Wanao Eneza Udini na Ukabila Kwani Husababisha Migogoro Katika Jamii.

Katika Hatua Nyingine Bwana Msigwa Amempongeza Diwani wa  Kata Hiyo Edwini Mwanzinga Pamoja na Wananchi  Wake Kwa Ushirikiano Waliyouonesha Katika Kusimamia Miradi ya Maendeleo na Kuhakikisha Wanasogeza Huduma za Kijamii.

Article 23

$
0
0

TISA WAKAMATWA TUKIO LA KUVAMIWA NA KUSHAMBULIWA MJUMBE WA TUME YA KATIBA, DK SENGONDO MVUNGI

PIX 4
PIX 1
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio la kuvamiwa na kushambuliwa Dk Sengondo Mvungi, Mjumbe wa Tume ya Katiba. Waziri Nchimbi alisema upepelezi wa tukio hilo umefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 80 ambapo tayari watuhumiwa tisa wamekamatwa wakiwa na mapanga na simu moja ya mkononi, watuhumiwa hao walitajwa majina yao katika mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Hata hivyo, Waziri Nchimbi aliwaomba wananchi na waandishi wa habari wawe na subira wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi kwa ajili ya kuwakamata watuhumiwa wengine. Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Kulia ni Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova. 
 PIX 3Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova akiwaonyesha waandishi wa habari mapanga waliyoyakamata wakati wa msako mkali wa kuwasaka watuhumiwa waliomvamia na kumshambulia Dk Sengondo Mvungi Mjumbe wa Tume ya Katiba. Katika msako huo watuhumiwa tisa walikamatwa wakiwa na mapanga na simu moja ya mkononi. Katikati (waliokaa meza kuu) ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi. Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Hata hivyo, Waziri Nchimbi aliwaomba wananchi na waandishi wa habari wawe na subira wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi kwa ajili ya kuwakamata watuhumiwa wengine. Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo.

Sehemu ya waandishi habari waliohudhuria mkutano wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi alipokuwa anazungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari vya nchini na nje ya nchi kuhusiana na tukio la kuvamiwa na kushambuliwa Dk Sengondo Mvungi, Mjumbe wa Tume ya Katiba. Waziri Nchimbi alisema upepelezi wa tukio hilo umefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 80 ambapo tayari watuhumiwa tisa wamekamatwa wakiwa na mapanga na simu moja ya mkononi, watuhumiwa hao walitajwa majina yao katika mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. Hata hivyo, Waziri Nchimbi aliwaomba wananchi na waandishi wa habari wawe na subira wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi kwa ajili ya kuwakamata watuhumiwa wengine. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Article 22

$
0
0
WANANCHI  WA KIJOMBE NJOMBE WAKUBALI KUJENGA CHUMBA CHA UZAZI.
 Hapa ni kijiji cha Isoliwaya Wanging'ombe na njia inayoonekana inaelekea kata ya Kijombe hadi mpakani mwa Wilaya ya Wanging'ombe na Mbarali Mbeya.
Hapa Kuna Ofisi ya Kata ya Kijombe.
 Diwani wa kata ya Kijombe Wilaya ya Wanging'ombe Mkoani Njombe bwana Nashon Kilamlya Akizungumza na www.gabrielkilamlya.blogspot.com juu ya ujenzi wa Chumba cha Zahanati Hiyo.

Na  Gabriel  Kilamlya Wanging'ombe

Kina Mama Wajawazito Katika Kijiji cha Kijombe Huendea Wakaondokana Adha ya Kulazwa Wodi Moja na Wagonjwa Wengine Pindi Wanapofika Katika Zahanati ya Kijiji Hicho Kwa Lengo la Kujifungua, Baada ya Uongozi wa Kata ya Kijombe Wilayani Wanging'ombe Kuanza Ujenzi wa Chuma Kwa Ajili ya ya Wodi ya Kina Mama Wajawazito.

Wakiongea Kwenye Baraza la Maendeleo ya Kata ya Kijombe (KAMAKA) Wilayani Wanging'ombe Wamekubaliana Kuanza Ujenzi wa Chumba Kwa Ajili ya  Huduma ya Uzazi Kwa Kinamama Wajawazito Katika Zahanati ya Kijiji cha Kijombe

Wajumbe Hao Wamefikia Makubaliano Hayo Kwenye Kikao Hicho Kutokana na  Adha Wanayoipata Kina Mama Wajawazito Wakati Wanapofika Katika Zahanati Hiyo Kwa Lengo la Kujifungua Kwani Hulazimika Kuchanganywa Katika Chumba Kimoja na Wagonjwa Wengine.

Akiongea na www.gabrielkilamlya.blogspot.com Mwenyekiti wa Baraza Hilo Nashon Kilamlya Ambaye Pia ni Diwani wa Kata Hiyo Amesema Chumba Hicho Kitajengwa Kwa Nguvu za Wananchi na Wadau Wengi wa Maendeleo Ambapo Wananchi Wanatakiwa Kuchangia Kiasi cha Shilingi Elfu Saba Mia Tano.

Mwemyekiti Huyo Amesema Fedha Nyingine Zitatumika Kwa Ajili ya Ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Kijombe Pamoja na Majengo ya Shule ya Sekondari Kijombe , Ambapo Takribani Shilingi Laki Tisa Zinatarajia Kutumika Katika Ujenzi  wa Chumba Hicho  cha Mama Wajawazito Huki Kikitarajiwa Kukamilika Mwishoni Mwa Mwaka Huu.

Article 21

$
0
0
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe ACP Fulgency Ngonyani Amethibitisha Kutokea Kwa Matukio Hayo.

Na  Gabriel  Kilamlya Njombe

Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limethibitisha Kutokea kwa Matukio Matatu Tofauti Likiwemo la Mkazi wa Mtaa wa Kibena Kukutwa Akiwa Amefariki Dunia  Chumbani Kwake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe ACP Fulgency Ngonyani Amesema Kuwa Tukio la Kwanza Limetokea Novemba 10 Mwaka Huu Majira ya Saa 11:40 Asubuhi Huko Katika Maeneo ya Kibena Shuleni Kata ya Ramadhani Wilaya ya Njombe Ambapo Mkazi Mmoja Selena Mwinuka Mwenye Umri wa Miaka 49 Alikutwa Chumbani Kwake Akiwa Amefariki Dunia.


Amesema Kuwa Mwili Wake Ulikutwa Katika Chumba Cha Uani Akiwa Amefariki Dunia na Mwili Wake Ukiwa Kitandani na Hauna Majeraha Wala Alama Yoyote Huku Chanzo Cha Tukio Hilo Kikiendelea Kuchunguzwa na Mwili Wake Umepelekwa Katika Hospitali ya Mji Njombe Kibena Kwa Uchunguzi Zaidi.


Katika Tukio la Pili Kamanda Ngonyani Amesema Kuwa Mtu Mmoja Aliyefahamika Kwa Jina la Ruphinus Mlelwa Mkazi wa Mtaa wa Kambarage Mjini Njombe Aligundulia Kuibiwa Kwa

Pikipiki Yake na Mtu/Watu Wasiojulikana Yenye Thamani ya Shilingi Milioni 1,750,000

Tukio Hilo Limetokea Novemba 10 Mwaka Huu Majira ya Saa 4:00 Usiku Huko Katika Mtaa wa Kambalage Ambapo Pikipiki Yenye Namba za Usajiri T 797 CMB Aina ya HOUJOE Iliyokuwa Imehifadhiwa Sebuleni katika nyumba yake baada ya wezi kuvunja mlango na kuingia ndani na Kwamba Mtuhumiwa anatafutwa na Jeshi la polisi.

Pamoja na Hayo  Kamanda Ngonyani Amesema Kuwa Tukio la Mwisho Limetokea Katika Barabara Kuu ya Mbeya-Makambako Ambapo Gari Lenye Namba za Usajili ACV.4199 Toyota Corolla Mali ya Seventy Seventy Five Car Hire Investment Ya Ndola Zambia Ikiendeshwa na William Kaunda Mkazi wa Zambia Mwenye Umri wa Miaka 32 Ilimgonga Mpanda Baiskeli na Kumsababishia Kifo Chake Papo Hapo.

Kamanda Ngonyani Amesema Tukio Hilo Limetokea Novemba 10 Mwaka Huu Majira ya Saa 04:30 Usiku Huko Katika Kijiji cha Igando Tarafa ya Wanging'ombe Ambapo Gari Hilo Lilimgonga Fanuel Mhanzi Mwenye Umri wa Miaka 14 Aliyekuwa Akisoma Kidato Cha Kwanza Katika Shule ya Sekondari Luduga.

Hata Hivyo Amesema Kuwa Marehemu Alikuwa Akivuka Barabara Kwenda Kuchota Maji Akiwa Amebeba Madumu Matupu Katika Baiskeli Ndipo Tukio Hilo Lililopo Mkuta na Kumsababishia Kifo Chake Papo Hapo.

Amesema Kuwa Chanzo Cha Ajali Hiyo Bado Kinachunguzwa na Mtuhumi Amekamatwa Kwa Mahojiano Zaidi.

Article 20

$
0
0

MSANII WA TAARAB NYAWANA FUNDIKIRA AFARIKI DUNIA.

 
Marehemu Nyawana Fundikira enzi za uhai wake.
Msanii wa taarab nchini anayejulikana kwa jina la Nyawana Fundikira aliyetamba na wimbo wa 'Nipo Kamili Nimejipanga', amefariki dunia mchana huu kwa ugonjwa wa malaria.Nyawana amefariki akiwa kwake maeneo ya Mwananyamala B na mwili wake sasa umepelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala, Dar.Marehemu Nyawana alizaliwa mwaka 1977 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kupata elimu yake katika shule mbalimbali kuanzia Msingi, Sekondari na elimu ya juu.Shule ya Msingi Zanaki ndipo alipopata elimu yake mwaka 1983 na kuhitimu mwaka 1989, wakati ile ya Sekondari alisoma Masjid Quba mwaka 1992 na kumalizia Al Haramain.Baada ya hapo alisomea Uhadhiri kabla ya kumaliza na kusomea masomo ya Uandishi wa Habari na Utangazaji, ambapo pia alishiriki shindano la urembo na kunyakua taji la Miss Tabora, mwaka 1996.Mbali na sanaa ya uimbaji, pia Nyawana ni mwandishi na mtangazaji, aliyefanya vyema mno, hasa kwa kutangaza vipindi vya taarabu, katika redio kadhaa, ikiwamo ile ya Voice of Tabora.Baadhi ya nyimbo alizorekodi marehemu nitpamoja na 'Nipo Kamili Nimejipanga' na 'Umesharoga Wangapi', nyimbo ambazo zilitangaza na kuonyesha kipaji chake halisi.Baadhi ya makundi ya taarab aliyowahi kufanya nayo kazi marehemu ni, Kings Modern Taarab na  Tanzania Moto Modern Taarab, maarufu kama T-Moto.Mungu ailaze mahali pema peponi! AMEN

RAIS KIKWETE AZINDUA MGODI WA DHAHABU GEITA.

$
0
0

 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi mgodi unaomilikiwa na kampuni ya Nsagali uliopo Ushirombo wilayani Bukombe, Mkoa wa Geita jana.Kushoto ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mh.Masele,Wa pili kushoto ni mmoja wa wamiliki wa mgodi huo Bwana Emmanuel Silanga, Wanne kulia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mh.Profesa Kalikoyela Kahigi na kulia mwisho ni Mkuu wa Mkoa mpya wa Geita Mhe. Said Magalula.
Mmoja wa Wamiliki wa Mgodi wa Ngasali Bwana Emmanuel Silanga kulia akimwonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete uchenjuaji wa dhahabu unaofanyika katika mgodi huo
uliopo Ushirombo,Wilayani Bukombe, mkoa wa Geita. Picha na Freddy Maro

Kwa Hisani ya Michuziblog.

BREAKING NEWZZZZZZZ

$
0
0

DOKTA SENGONDO MVUNGI AMEFARIKI DUNIA AFRIKA KUSINI.
Sengondo Mvungi 1 

 Aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Marekebisho ya Katiba Mpya na Kiongozi wa NCCR-

Mageuzi Dokta Sengondo Mvungi Jana Amefariki Dunia Nchini Afrika Ya Kusini

Alikokuwa Amelazwa Baada ya Kuvamiwa na  Kujeruhiwa Vibaya Na Watu Wasio

Julikana.

Marehemu Dokta Sengondo Mvungi Alilazimika Kupelekwa Nchini Afrika Ya Kusini Kwa

Matibabu Zaidi Kufuatia Majeraha Makubwa Aliyoyapata Baada ya Kuvamiwa AKiwa

Nyumbani Kwake Jijini Dar es Salaam


Taarifa ya Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Ilieleza Kuwa Watu Tisa Wamekatwa Kuhusika na Tukio Hilo.

Article 17

$
0
0

MWILI WA DKT. SENGONDO MVUNGI KUWASILI  IJUMAA  NOVEMBA 15 2013, KIKWETE ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO.

 Rais Jakaya Kikwete akitia saini kitabu cha maombelezo ya kifo cha Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi nyumbani kwake Kibamba jijini Dar es Salaam.

  Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba wakifurahia jambo na Waziri wa Katiba na Sheria Mathias Chikawe (kushoto), Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani na Mjumbe wa Tume Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim (kulia) walipokutana nyumbani kwa marehemu Dkt. Sengondo Mvungi Kibamba jijini Dar es Salaam.
(Picha na Tume ya Katiba)
  Rais Jakaya Kikwete (katikati) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba (kushoto) nyumbani kwa marehemu Dkt. Sengondo Mvungi walipokwenda kuipa pole familia. Kulia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia na Mjumbe wa Tume Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim.

 Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Richard Lyimo akimpa pole mke wa marehemu Dkt. Sengondo Mvungi, Bi. Anna Mvungi wakati Wajumbe wa Tume walipokwenda kumpa pole.
  Rais Jakaya Kikwete akimpa pole mke wa marehemu Dkt. Sengondo Mvungi, Bi. Anna Mvungi alipokwenda kumpa pole nyumbani kwake Kibamba jijini Dar es Salaam.
 wenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba wakifurahia jambo na Waziri wa Katiba na Sheria Mathias Chikawe (kushoto), Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani na Mjumbe wa Tume Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim (kulia) walipokutana nyumbani kwa marehemu Dkt. Sengondo Mvungi Kibamba jijini Dar es Salaam.
(Picha na Tume ya Katiba)
.............................................................................................................................
Tume ya Mabadiliko ya Katiba inawafahamisha wananchi kuwa taratibu za kuusafirisha mwili wa Mjumbe wake, Dkt. Sengondo Mvungi aliyefariki nchini Afrika Kusini zimekamilika na mwili wake unatarajia kuwasili nchini siku ya Ijumaa, Novemba 15, 2013.


Baada ya kuwasili, mwili huo utahifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo iliyopo jijini Dar es Salaam.


Aidha, siku ya Jumamosi, Novemba 16, 2013 kutafanyika Ibada ya mazishi katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam kuanzia saa 4:00 asubuhi. Baada ya misa, marehemu ataagwa katika Viwanja vya Karimjee kuanzia saa 6:30 mchana siku hiyohiyo ya Jumamosi, Novemba 16, 2013.


Aidha, Marehemu Dkt. Mvungi anatarajiwa kusafirishwa siku ya Jumapili, Novemba 17, 2013 kwenda Kisangara Juu, Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu, Novemba 18, 2013.


Dkt. Mvungi alifariki jana (Jumanne, Novemba 12, 2013) katika Hospitali ya Millpark jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini alikopelekwa kwa ajili ya uchunguzi na matibabu zaidi akitokea Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI) aliokuwa amelazwa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake Kibamba, wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam na watu waliomjeruhi vibaya kichwani usiku wa kuamkia siku ya Jumapili, Novemba 3, 2013.


Wakati huohuo, Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakiongozwa na Mwenyekiti wake Jaji Joseph Warioba leo (Jumatano, Novemba 13, 2013) wameungana na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kufika nyumbani kwa marehemu Dkt. Mvungi eneo la Kibamba jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa pole kwa familia, ndugu na jamaa wa marehemu Dkt. Mvungi.

Mwisho.

Imetolewa na:
Ndg. Assaa A. Rashid,
Katibu,
Tume ya Mabadiliko ya Katiba,
Dar es Salaam
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahaman Kinana amesikitishwa na taarifa ya kifo Cha Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dr Sengondo Mvungi kilichotokea Jana katika Hospitali ya Millpark nchini Afrika ya Kusini.

Kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi, Katibu Mkuu anawapa pole wanafamilia, Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba na Uongozi wa Chama Cha NCCR-Mageuzi. Hakika Taifa limepoteza Mtaalamu wa Sheria, Kiongozi Mzalendo na hodari katika kipindi ambacho mawazo yake yanahitajika kwa kiasi kikubwa kuliendeleza Taifa hili.
Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi.
Imetolewa na:
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
ITIKADI NA UENEZI
13/11/2013

Article 16

$
0
0
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe ACP Fulgency Ngonyani

Watu Wawili Wamefariki Dunia Mkoani Njombe Katika Matukio Mawili Tofauti Likiwemo la Mwanafunzi wa Shule ya Secondary Uwemba Aliefariki Dunia Baada ya Kuzama Katika Mto Hagafilo Wakati Akijaribu Kuvuka Kuelekea Ng'ambo ya Pili ya Mto Huo.

Aidha Katika Tukio la Pili Mkazi Mmoja wa Kijiji Cha Nyumbanitu Amefariki Dunia Baada ya Kugongwa na Gari Aina ya Toyota Mark Two Yenye Namba za Usajili T AGZ 404.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe ACP Fulgency Ngonyani Imesema Kuwa Katika Tukio la Kwanza Mnamo Nov 11 Mwaka Huu Majira ya Saa Moja Asubuhi Katika Mto Hagafilo Aulelius Mligo Mwanafunzi wa Kidato Cha Nne Shule ya Secondary Uwemba Alifariki Dunia Wakati Akijaribu Kuvuka Mto Huo.

Amesema Katika Tukio la Pili Mtoto Malaki Nyika Mwenye Umri wa Miaka Mitano Alifariki Dunia Baada ya Kugongwa na Gari na Kwa Mujibu wa Uchunguzi wa Daktari Unaonesha Kuwa Marehemu Alifariki Kutokana na

Majeraha Alioyapata Sehemu za Kichwani.

Wakati Huo Huo Watu Wasiofahamika Wamevamia na Kuvunja Zizi na Kuiba Ng'ombe Wapatao Kumi na Mmoja Wote Wakiwa ni Majike Wenye Thamani ya Shillingi Millioni Nne na Laki Mbili Mali ya Bw Peragia Mlowe.

Tukio Hilo Limetokea Nov 10 Mwaka Huu Majira ya Saa Mbili na Nusu Usiku Katika Kijiji Cha Uliwa na Kwa Mujibu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe Hadi Sasa Hakuna Mtu Anaeshikiliwa Kutokana na Tukio Hilo Huku Juhudi za Kuwatafuta Wahusika Zikiendelea Kufanywa na Jeshi la Polisi.

RC NJOMBE AAGIZA KUVUNJWA KWA MAKUNDI KWA MADIWANI WILAYA YA WANGING'OMBE .

$
0
0
.Ni wakati wa Kikao cha kwanza cha baraza la madiwani Katika Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe.
 

 Mkuu wa Mkoa wa Njombe Captain Mstaafu Asseri Msangi Akiwasili Kwenye Kikao Cha Kwanza cha Baraza la Madiwani  Katika Ukumbi wa Primium Power Point Uliopo Kwenye Makao Makuu ya Wilaya ya Wanging'ombe Igwachanya.

 Baadhi ya Madiwani wa Kata Mbalimbali za Wilaya ya Wanging'ombe Wakiwa Kwenye Kikao cha Kwanza Cha Baraza la Madiwani Leo.,Wamekosa Yunifomu Kutokana na Kwamba Kikao Hicho ni Cha Kwanza.

 Pichani ni Mkurugenzi wa Halmashauri Mpya ya Wilaya ya Wanging'ombe Bi.Lucy Msofe.
 Mkuu wa Mkoa wa Njombe Captain Mstaafu Asseri Msangi Akiagiza Kuvunja Makundi Kwa Madiwani Katika Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe.
 Naibu Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Jimbo la Njombe Magharibi Mhandisi Gerson Lwenge Akikemea Tabia ya Madiwani Kutoa  Nje Siri za Makubaliano Yanayofikiwa Kwenye Vikao na Kuleta Mkanganyiko kwa Jamii.
 Mkuu wa Wilaya ya Makete Bi.Josephine Matiro Aliyemkaimu Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Esterina Kilasi Akizungumza Kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani Wilayani Wanging'ombe Leo.
 Baadhi ya Wakuu wa Idara na Wataalamu Katika Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe Ambao Kwa Asilimia 99.9 Wamekaimu Vyeo Hivyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe Bwana Antony Emmanuel Mahwata Akifunga Kikao cha Kwanza cha Baraza la Madiwani  Leo Huko Igwachanya.

Na   Gabriel  Kilamlya Wanging'ombe.

Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Captain Mstaafu Asseri Msangi Amewaagiza Madiwani wa Kata za Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe Kuvunja Makundi Yaliyokuwepo Baina Yao Yaliyotokana na Uchaguzi wa Wenyeviti na Kamati Mbalimbali Katika Halmashauri Hiyo.

Agizo Hilo Amelitoa Leo Kwenye Kikao Cha Kwanza Cha Baraza la Madiwani Katika Halmashauri Hiyo  Kufuatia Kuwepo Kwa Makundi Yanayoweza Kuwagawa Wananchi Katika Shughuli za Kimaendeleo Ilihali Wote ni Madiwani wa

Wilaya Moja.

Pamoja na Mambo Mengine Captain Mstaafu Msangi Ameitaka Halmashauri Ya Wilaya ya Wanging'ombe Kuweka Bajeti ya Kilimo Cha Zao la Karanga Kutokana na Zao Hilo Kustawi Vizuri Wilayani Humo na Hivyo Zao Hilo Liwe Tegemeo Kama zao La Kuinua Uchumi Kwa Wananchi wa Wilaya Hiyo.

Wakizungumza na www.gabrielkilamlya.blogspot.com Mara Baada ya Kikao Hicho Baadhi ya Madiwani Hao Wameiomba Serikali Kuwaongezea Magari Katika Halmashauri Hiyo Ambayo ni  Mpya Ili Kuharakisha Huduma Kwa Wananchi.

Hata Hivyo Wamesema Kuwa Wataalamu Katika Halmashauri Hiyo Wamekuwa Wakishindwa Kufanya Kazi Zao Kwa Wakati Kutokana na Uhaba Mkubwa Wa Vyombo Vya Usafiri Kwenye Halmashauri Hiyo.

Mhandisi Gerson Lwenge ni Mbunge wa Jimbo la Njombe Magharibi na Naibu Waziri wa Ujenzi Ambaye Amelaani Tabia ya Baadhi ya Viongozi Wakiwemo Madiwani Kutoa Siri za Makubaliano Ya Vikao na Kuyafikisha Kwa Wananchi.

Kwa Mara Ya Kwanza Halmashauri Ya Wilaya ya Wanging'ombe Imefanya Kikao cha Kwanza Cha Baraza la Madiwani,Halmashauri Iliyoonekana Kuwa na Changamoto Nyingi Kutokana na Upya Wake.
...........................................................................................................................

Article 14

$
0
0
VIJANA WA TAMBALANG'OMBE HUKO MALANGALI WAJITOA KIMAENDELEO.


 HAWA NDIYO VIJANA  WACHAPA KAZI LAKINI WAMESEMA WANAKOSA MITAJI YA  KUENDESHEA MIRADI YAO.

 KAZI HII LAKINI INAKWENDA SAMBAMBA NA UHARIBIFU WA MAZINGIRA PINDI WANAPOTAFUTA KUNI ZA KUCHOMEA

 VIJANA WA MALANGALI WAKIWA KATIKA KIJIJI CHA TAMBALANG'OMBE WILAYANI MUFINDI WAKIWAJIBIKA AKIWEMO ABDUL KIDUMULE NA CHRISTOPHA CHONYA KATIKA KAZI YA UCHOMAJI WA TANURI ZA MATOFARI
 MZEE ALFRED MKAKALA AKIWASINDIKIZA NA KUWAELEKEZA NAMNA YA UPANGAJI WA KUNI KWAAJILI YA UCHOMAJI  WA TOFARI KWENYE TANURI ZA TOFARI HIYO HUKU WAKISHUSHIA KINYWAJI CHA ASILI KIJULIKANACHO KAMA UGIMBI YAANI POMBE YA KYENYEJI YA MACHICHA
VIJANA HAWA PIA NI WAFUGAJI MAARUFU WA MIFUGO AINA YA NG'OMBE NA MBWA KWAAJI YA KUWINDIA WANYAMA POLI WAKIWEMO NDEZI NA PANYA AMBAO NI WAHARIBIFU WAKUU WA MAZAO YA MAHINDI MSIMU WA KILIMO.

kwa Hisani ya Michael Ngilangwa blog.

Article 13

$
0
0
HAYA MAISHA TUUUUUUUUUUUU!!!!!!!!!!

Article 12

$
0
0
 
Meneja wa TANESCO Wilaya ya Njombe Mhandisi Emanuel  Kachewa Amesema Tatizo Hilo Limetokana na Upungufu wa Vifaa Unaolikabili Shirika Hilo

 Hii ni Listi ya Majina ya Wateja Waliolipia Huduma Hiyo Lakini Bado Hawajapata Kwa Zaidi ya Miezi Saba Sasa.

Na  Prosper  Mfugale Njombe

Zaidi ya Wateja Mia Sita wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Wilayani Njombe Wameulalamikia Uongozi wa Shirika Hilo Kwa Kushindwa Kuwaunganishia Huduma ya Umeme Kwa Zaidi ya Miezi Sita Licha ya Kukamilisha Taratibu Zote Ikiwemo Malipo ya Huduma Hiyo.

Aidha Wateja Hao Wamelalamikia Kitendo Cha Shirika Hilo Kukiuka Mkataba wa Huduma Kwa Mteja Ambao Kwa Mujibu wa Wateja Hao Walitakiwa Kuunganishiwa Huduma Hiyo Ndani ya

Siku Thelathini Baada ya Kukamilisha Malipo na Kujaza Mkataba.

Wakizungumza na mwandishi wa mtandao huu Baadhi ya Wateja Hao Wamesema Licha ya Kufika Mara Kadhaa Katika Ofisi za Shirika Hilo Kwaajili ya Kufuatilia,Bado Kumekuwa Hakuna Majibu ya Uhakika Jambo Linalosababisha Kushindwa Kupata Huduma Hiyo Hadi Sasa.

Akizungumzia Hali Hiyo Meneja wa TANESCO Wilaya ya Njombe Mhandisi Emanuel  Kachewa Amesema Tatizo Hilo Limetokana na Upungufu wa Vifaa Unaolikabili Shirika Hilo Kwasasa na Kusema Hali Hiyo Imeendelea Kujitokeza Katika Mikoa Mbalimbali Nchini.

Kutokana na Hali Hiyo Bw Kachewa Amewataka Wateja Hao Kuendelea Wavumilivu Katika Kipindi Hiki Ambapo Shirika Hilo Linaendelea Kulitafutia Ufumbuzi Tatizo Hilo na Kuongeza Kuwa Tayari Shirika Hilo

Limezungumza na Wateja Hao na Kuwafahamisha Tatizo Lililopo Kwasasa.

Article 11

$
0
0

MENO YA TEMBO YAKAMATWA TENA ZANZIBAR.

Meno ya Tembo

Kwa mara nyingine katika kipindi kisichozidi wiki mbili, polisi nchini Tanzania wamenasa shehena kubwa ya meno ya tembo yakiwa yamefichwa katika kontena, bandarini Zanzibar.

Watu wawili wamekamatwa wakihusishwa na meno hayo.
Kwa mujibu wa Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, meno hayo yalikuwa yamehifadhiwa katika kontena la futi arobaini yakiwa yamechanganywa katika mifuko iliyohifadhi makombe ya konokono wa baharini, tayari kwa kusafirishwa nje.

Kamishna Mussa amesema, kwa sasa kiasi hicho cha meno ya tembo bado hakijafahamika kutokana na
kuendelea kwa kazi ya kupakua kutoka kontena hilo.

Hivi karibuni raia watatu wa China walikamatwa nchini Tanzania kwa kukutwa na meno 706 ya tembo, sawa na tembo 353 waliouawa katika hifadhi mbalimbali nchini humo.

Kukamatwa kwa meno haya ya tembo, kumekuja wakati tayari serikali imetangaza kusitisha Operesheni Tokomeza Ujangili, ambayo ililenga kunusuru wanyama walio hatarini kutoweka kutokana na kuuawa katika hifadhi za taifa nchini Tanzania. 

Wanyama wanaolengwa zaidi na majangili kutokana na meno yao na pembe ni tembo na faru.

Matukio ya kukamatwa kwa meno ya tembo kutoka Afrika Mashariki yamekuwa yakiripotiwa kila mara. Oktoba, 20, 2012, tani nne za meno ya tembo yenye thamani ya dola milioni 3.4 za Kimarekani yalikamatwa Hong Kong, yakidaiwa kusafirishwa kutoka Kenya na Tanzania.

Pia Agosti 16 mwaka huu polisi wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, walimkamata raia wa Vietnam akiwa na meno ya tembo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 18 sawa na dola zaidi ya elfu 11, yakisafirishwa kwenda nje.

 Chanzo BBC SWAHILI.

Article 10

$
0
0
 Hili Ndilo eneo makabidhiano Yalipofanyika.
 Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Njombe Kibena Dokta Patrick Msigwa Akielezea Hali ya Hospitali Hiyo Wakati Wakati wakipokea Vifaa Hivyo.

 Baadhi ya Watumishi wa Hospitali ya Kibena Wakati wa Kupokea Msaada Huo leo.
 Hivi ni Baadhi ya Vifaa vilivyotolewa Yakiwemo Magodoro,Vitanda,na Mashuka.

 Meneja Wa NMB Tawi la Njombe Bwana Hemed Risasi Akitoa Taarifa ya vifaa Vilivyotolewa na Benki Hiyo Leo Katika Hospitali ya Kibena.

Na  Gabriel  Kilamlya Njombe.

Benki ya NMB Tawi la Njombe Hii Leo Imekabidhi Msaada wa Vifaa Vyenye Thamani  ya Shilingi Milioni Kumi Katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji Njombe Kibena Ambayo Kwa Sasa Inatumika Kama Hospitali ya Mkoa wa Njombe Kwa Muda Tangu Mwezi Agosti Mwaka Huu.

Akikabidhi Msaada Huo Kwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Keptein Mstaafu Asseri Msangi , Meneja wa NMB Tawi la Njombe  Bwana Hemed Risasi Amesema Kuwa Vifaa Hivyo Vimetolewa Kufuatia Ombi la Mkuu wa Mkoa Wakati wa Ziara ya Rais Kikwete Mkoani Hapa Ambaye Alitumia Fursa Hiyo Kuwaomba Wadau Mbalimbali wa Afya Kujitokeza Kusaidia Sekta Mbalimbali Mkoani Njombe.

Akiongea Mara ya Baada ya  Kupokea Msaada Huo Kwa niaba ya Uongozi wa Hospitali Hiyo Mkuu wa Mkoa wa Njombe Keptein Mstaafu Asseri Msangi   Amepongeza Jitihada za
Benki Hiyo Kutambua Adha Wanayoipata Wagonjwa Katika Hospitali Hiyo Huku Akiwataka Watumishi wa Hospitali Hiyo ya Halmashauri ya Mji wa Njombe Kuhakikisha Wanavitumia Kwa Uangalifu na Kuvitunza.

Dokta Patric Msigwa ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Kibena Katika Halmashauri ya Mji wa Njombe Ambaye Amesema Vifaa Hivyo Vitasaidia Kupunguza Uhaba Mkubwa wa Vitanda na Mashuka Katika Hospitali Hiyo na Ambapo  Amewaomba Wadau Mbalimbali  Kujitokeza Kuendelea Kusaidia Hospitali Hiyo.

Hata Hivyo Hatua ya Utoaji wa Misaada Hiyo Ni  Muendelezo wa Makampuni na Taasisi Mbalimbali Mkoani Njombe Kama Mchango Wake Ikiwa Hivi Karibuni Kampuni ya TANWAT Kibena Ilitoa Misaada ya Vitu Mbalimbali Kwa Wazee Pamoja na Kutoa Huduma za Afya Bure.
.................................................................................


Article 9

$
0
0

WALIOMUUA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA RUNGWE WAHUKUMIWA KUNYONGWA hadi kufa.

 


Aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Marehemu  John Mwankenja, enzi za uhai wake
Kushoto Hakimu Mwakalinga ambaye ni mshtakiwa wa kwanza kuhukumiwa kunyongwa
Baadhi ya wananchi wakiwa nje ya mahakama wakisubiria matokeo ya
hukumu


WATUHUMIWA wawili kati ya wanne  wa kesi ya mauaji dhidi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, John Mwankenja, wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia katika Mahakama kuu kanda ya Mbeya.

Hukumu hiyo ilitolewa katika Mahakama kuu kanda ya Mbeya iliyokuwa ikiendesha vikao vyake katika Mahakama ya Wilaya ya Rungwe chini ya Jaji Samweli Karua, baada ya kuahirishwa kutolewa kwa hukumu hiyo kwa zaidi ya
mara tatu na kuzua hali ya sintofahamu kwa ndugu wa washtakiwa na wafuatiliaji wa kesi hiyo.

Awali kabla ya kusoma kwa hukumu hiyo Mwendesha mashtaka wa Serikali., Archiles Mulisa, aliwataja watuhumiwa wote wanne kuwa ni Hakimu Mwakalinga, Daudi Mwasipasa, Obote Mwanyingili na Kelvin Myovela wanaokabiliwa na tuhuma za kumuua kwa maksudi aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe John Mwankenja.



Alisema watuhumiwa hao wenye kesi namba 131/2012 walitenda kosa hilo Mei 19, 2011 katika kijiji cha Mpandapanda, Kata ya Kiwira Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.


Mulisa aliyekuwa akisaidiwa na Wakili wa Serikali Lugano Mwakilasa kwa upande wa mashtaka huku  Watuhumiwa wakitetewa na Mawakili wawili ambao ni Victor Mkumbe na Simon Mwakolo.

Mulisa alidai mahakamani hapo kuwa kesi inayowakabili  watuhumiwa hao walilitenda Mei 19,2011 kwa kumuua kwa maksudi John Mwankenja kinyume na kifungu cha 196 sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Akisoma hukumu hiyo Jaji Karua ambaye alianza majira ya saa 14:37 mchana na kukamilisha saa 15:37 alisema katika kesi hiyo upande wa mashtaka na utetezi haubishaniwi kuhusu kifo cha marehemu.

Aliongeza kuwa pande hizo mbili pia hazibishaniwi kuhusu ripoti za kitaalamu na dhamira za mauaji hayo bali kinachobishaniwa ni uhusika wa watuhumiwa hao dhidi ya mauaji hayo.

Alisema katika kutetea hoja zao upande wa mashtaka ulileta mashahidi 11 ambao wote kwa pamoja  wakiongozwa na shahidi namba moja waliwatuhumu washtakiwa kuhusika na tukio hilo.

Shahidi huyo namba moja Weston Jacob(17) mkazi wa Kiwira Mwanafunzi kidato cha Tatu katika shule ya Sekondari Kipoke ambaye pia ni Mjomba wa marehemu ambaye aliiambia mahakama kuwa siku ya tukio akiwa nyumbani akijisomea majira ya 2: 30 usiku ambapo marehemu alifika nyumbani na kupiga honi ya gari akitaka afunguliwe mlango.


Mbali na ushahidi huo Jaji Karua alisema pamoja na ushauri wa wazee wa baraza la mahakama ambao pia wanawatuhumu washtakiwa hao kuhusika na tukio hilo nae anakubaliana nao lakini siyo kwa watuhumiwa wote.

Kutokana na ushahidi huo alisema Mshtakiwa namba moja na namba mbili ambao ni Hakimu Mwakalinga na Daudi Mwasipasa wanatiwa hatiani kuhusika moja kwa moja na mauaji kutokana na ukiri wao kwa mlinzi wa amani, Mchukua maelezo na  vipimo vya vinasaba.

Alisema Mshtakiwa namba tatu Obote Mwanyingili yeye anatiwa hatiani kutokana na kosa la kumhifadhi mtuhumiwa namba moja baada ya kutoka kufanya mauaji hivyo yeye hausiki moja kwa moja na kosa hilo.

Jaji karua alisema kwa upande wa mshtakiwa namba nne Kelvin Myovela anatiwa hatiani kutokana na kuhifadhi silaha iliyotumika nkatika mauaji hayo ingawa hakusika na kitendo hicho moja kwa moja.

Aliongeza kuwa kutokana na kifungu cha sheria cha mwenendo wa makosa ya jinai kifungu namba 300 na 217 washtakiwa namba tatu na namba nne wanatiwa hatiani na mahakama.

Mwendesha mashtaka wa Serikali Archiles Mulisa, aliiambia mahakama hiyo kwamba itoe adhabu kali kutokana na kitendo alichofanyiwa marehemu na iwe fundisho kwa watu wengine.

Kwa upande wa utetezi ambao siku ya hukumu uliwakilishwa na Wakili Merick Luvinga alisema mahakama iwanee huruma washtakiwa kwa kuwa wote umri wao ni mdogo wanaweza kujifunza na kurudi kuungana na jamii pia ni kosa lao la kwanza hivyo wasipewe adhabu kali.

Kutokana na utetezi huo, Jaji Karua alisema kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo kuthibitisha kuhusika pasipo shaka kwa washtakiwa namba moja na namba mbili hivyo adhabu yao ni kunyongwa hadi kufa.

Aliongeza kuwa Mshtakiwa namba tatu Obote Mwanyingili anayehusika kumhifadhi mtuhumiwa wa kwanza ataenda jela miaka saba kwa kosa hilo sambamba na mshtakiwa namba nne  Kelvin Myovela aliyehifadhi silaha iliyotumika kwenye mauaji.

Alisema kutokana kosa hilo mtuhumiwa huyo atatumikia kifungo jela miaka saba ingawa pia tayari alikuwa amehukumiwa kifungo jela cha miaka 20 kwa kosa la kukutwa na silaha kinyume cha sheria.

Wakati huohuo

MAHAKAMA kuu kanda ya Mbeya imemhukumu kwenda jela miaka 35 mtuhumiwa wa mauaji dhidi ya watoto huku mwingine akiachiwa huru baada ya kukutwa bila hatia.

Hukumu hiyo ilitolewa jana na Jaji wa Mahakama kuu kanda ya Mbeya Samweli Karua mbele ya mwendesha mashtaka wa serikali Archiles Mulisa katika vikao vilivyofanyika katika Mahakama ya wilaya ya Rungwe.

Awali mwendesha mashtaka wa serikali Archiles Mulisa aliiambia mahakama kuwa washtakiwa Baraka Mwandibwa na Zuberi Lwila walifikishwa mahakamani hapo wa kosa la kumlawiti na kumuua mtoto Esta James(5) Novemba 21, 2010.

Alisema kosa hilo ni kinyume cha sheria kifungu cha 196 (16) kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002, ambalo walilifanya katika kijiji cha Bulyaga Wilayani Rungwe baada ya kumteka mtoto huyo.

Akisoma hukumu hiyo Jaji Karua alisema Mshtakiwa namba moja anatiwa hatiani kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo ambao ulitoka kwa shahidi namba moja ambaye ni mtoto aliyejulikana kwa jina la Marietha.

Alisema mtoto huyo ambaye alisema siku ya tukio alikuwa akicheza na marehemu ambapo mtuhumiwa alifika na kumpa pipi aina ya Ivory marehemu kisha kuondoka naye ambapo shahidi huyo aliwerza kumtambua mtuhumiwa katika gwaride la utambuzi.

Mbali na hilo alisema ushahidi mwingine ni ushaidi wa Vinasaba ambao unawahusisha moja kwa moja watuhumiwa wote wawili ikiwa ni pamoja na ushaidi wa kimazingira unaomhusisha mtuhumiwa wa kwanza.

Alisema kutokana na ushahidi huo Mtuhumiwa wa kwanza anahusika moja kwa moja na mahakama inamtia hatiani ingwa kwa mujibu wa ushahidi hakuua kwa makusudi kutokana na kutokuwa na vifaa vya mauaji kama visu panga na silaha zingine.

Alisema katika mwili wa marehemu ulikutwa ukiwa unadamu na mbegu za kiume sehemu zake za siri na hakuwa amejeruhiwa nsehemu yoyote, hivyo mahakama iliona mtuhumiwa hakuua kwa kukusudia bali ilikuwa ni bahati mbaya.

Hata hivyo upande wa Mshtaka uliomba mahakama itoe adhabu kubwa na kali dhidi ya washtakiwa kutokana na mazingira aliyofanyiwa mtoto huyo ili iwe fundisho kwa wanaume wengine wenye tabia za kuwalaghai watoto wadogo.

Akitoa hukumu hiyo Jaji karua alisema anakubaliana na ushauri wa upande wa mashtaka kwamba tukio hilo ni kubwa na mstakiwa wa kwanza Baraka Mwandibwa ataenda jela kwa miaka 35 huku mshtakiwa wa pili Zuberi Lwila akiachiwa huru baada ya kutokuwa na ushahidi wa kuhusika katika tukio hilo.

Picha na Ezekiel Kamanga

Mbeya yetu
Viewing all 2276 articles
Browse latest View live