Hii ni Mahakama ya Wilaya ya Njombe Ambayo kwa sasa Pia Inatumika kama Mahakama Kuu Mkoa wa Njombe.
Mahakama Kuu ya Mkoa wa Njombe Hii Leo Imemuhukumu Kifungo cha Miaka Nane Jela Benard Ngailo Mwenye Umri wa Miaka 35 Baada ya Kumkuta na Kosa la Kumuuwa Bila Kukusudia Kaka Yake Ronward Ngailo
Akitoa Hukumu Hiyo Jaji M.S. Shangari Amesema Mahakama Imetoa Adhabu Hiyo Baada ya Kusikiliza Hoja za Pande Zote Mbili , na Kwamba Mahakama Imeridhika na Ushahidi Uliotolewa na Upande wa Mashtaka na Kuongeza Kuwa Adhabu Hiyo Imetolewa Kwa Mshtakiwa Ili Iwe Fundisho Kwa Watu Wengine Wenye Tabia Kama Hiyo.
Ukitoa Utetezi Upande wa Mshtakiwa Uliomba Kupunguziwa Adhabu Hiyo Kutokana na Mshtakiwa Ana Watoto Saba Wanaomtegemea na Amekaa Lumande Kwa Takribani Mwaka Mmoja.
Awali Akisoma Shtaka Hilo Mahakamani Hapo Wakili wa Serikali Francis Lojas Ameiambia Mahakama Kuwa Mshtakiwa Alitenda Kosa Hilo Aprili 20 Mwaka 2010 Majira ya Saa Tatu Usiku Katika Kijiji cha Igagala na Kuiomba Mahakama Itoe Adhabu Kali Kwa
Mshtakiwa.
Imedaiwa Mahakamani Hapo na Wakili wa Serikali Lojas Kuwa Siku ya Tukio Mshtakiwa Alimuuwa Ronward Ngailo Ambaye ni Kaka Yake Kwa Kumkata na Kitu Chenye Ncha Kali Sehemu za Kichwa na Mikono Pamoja na Kumtoboa Machao Kwa Bisibisi na Kisha Kutumbukiza Chaooni Kwa Kile Kilichodaiwa Kuwa ni Wivu wa Kimapenzi.
Wakati Huo Huo Mahakama Hiyo Imeshindwa Kutoa Hukumu ya Kesi ya Mauwaji Inayomkabili Sophia Mliulika Mkazi wa Mabengu Mkoa Njombe Kwa Kile Kinachodhaniwa Kuwa Mshtakiwa Ana Uwezekano wa Kuwa na Matatizo ya Akili.
Akitoa Hoja Hiyo Mahakamani Hapo Wakili wa Upande wa Utetezi Bwana Kingwe Ameiomba Mahakama Kabla ya Kutoa Hukumu Mshtakiwa Akafanyiwe Uchunguzi Kwani Alionekana Kuwa na Matatizo ya Akili, Hoja Ambayo Mahakama Hiyo Imelikubali.
Mshtakiwa Sophia Mliulika Anakabiliwa na Kesi ya Kumuuwa Mtoto Wake Kwa Makusudi.