Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all 2276 articles
Browse latest View live

Article 1

$
0
0

  ZAWADI YA diamond  KWA MZEE GURUMO


Msanii mkongwe wa muziki wa dansi, Muhidin Gurumo akijaribu gari dogo alilokabidhiwa na mwanamuziki wa bongo fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond ‘ kutokana na kutambua mchango wake baada ya kustaafu kazi ya muziki.
Muhidin Gurumo akipokea funguo ya gari kutoka kwa Diamond
Gari alilozawadiwa mzee Gurumo.

JWTZ NA MONUSCO LAFANIKIWA KUITEKA NGOME KUU YA WAASI WA M23.

$
0
0

FIB Tanzania (special forces in Congo ambayo  ni  sehemu  ya  MONUSCO) imeichukua ngome kuu ya waasi wa M23 ya Kibati (Nyirangongo Territory - Goma, Eastern DRC).

Mizinga ya wapiganaji wetu ilirindima na kutembeza mabomu mfululizo huku askari wetu wa miguu wakipanda mlima ulio eneo hilo na kisha kuichukua ngome hiyo...




Habari  kwa  hisani  ya  wanabidii  na  JF

Article 5

$
0
0

KICHWA CHA MTU ALIYEFARIKI  KIKIWA NA MIKONO MIWILI YAKUTWA KATIKA OFISI YA MKUU WA POLISI NCHINI KENYA.


kenya-police-morgue_08ee5.jpg
JESHI la Polisi Kenya wapo katika uchunguza baada ya kichwa cha mtu aliyeuawa kiliwa kimewekwa nje ya afisi ya mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya polisi Johnston Kavuludi jijini Nairobi.
Kifurushi kimefungwa kwa karatasi ya plastiki, vilevile kilikuwa na mikono miwli ya binadamu iliyojaa damu. (P.T)
kando ya kifurishi hich
o kulikuwa na ilaani iliyoandiskwa ''Kavuludi wewe ndiye utakayefuata''.

Tangu uteuzi wake, kamishna huyo ameongoza harakati za kujaribu kuifanyia marekebisho idara ya polisi ambayo inadaiwa kuwa

fisadi zaidi Afrika Mashariki.

Kwa mujibu wa idara ya polisi, hakuna mshukiwa aliyekamatwa kauhusiana na tukio hilo na kuwa bado wangali wanachunguza mwili huo ulikuwa wa nani.

Katika miezi ya hivi karibuni kumekuwa na uhasama kati ya tume hiyo inayoongozwa na Kavuludi na ofisi ya mkuu wa polisi, huku zikilumbana kuhusu nani ana madaraka ya kuliendesha idara hiyo.


KWA Hisani ya Jumamtandablog.

Article 4

$
0
0

WANANCHI NJOMBE WAELEZA MAONI YAO KWENYE KATIBA.

 












WAKICHANGIA MAONI MBALIMBALI KWENYE RASIMU YA KATIBA MPYA WAKIWA KATIKA UKUMBI WA SHIRIKA LA COMPASSION

Article 3

$
0
0

WANANCHI NJOMBE WAELEZA MAONI YAO KWENYE KATIBA.

 












WAKICHANGIA MAONI MBALIMBALI KWENYE RASIMU YA KATIBA MPYA WAKIWA KATIKA UKUMBI WA SHIRIKA LA COMPASSION

WANANCHI NJOMBE WAELEZA MAONI YAO KWENYE KATIBA.

$
0
0

 












WAKICHANGIA MAONI MBALIMBALI KWENYE RASIMU YA KATIBA MPYA WAKIWA KATIKA UKUMBI WA SHIRIKA LA COMPASSION

WANANCHI NJOMBE WAELEZA MAONI YAO KWENYE KATIBA.

$
0
0

 












WAKICHANGIA MAONI MBALIMBALI KWENYE RASIMU YA KATIBA MPYA WAKIWA KATIKA UKUMBI WA SHIRIKA LA COMPASSION

FOOLISH AGE YA LULU MICHAEL YATUZWA NOTI KIBAO.

$
0
0

 
Wakati wa Uzinduzi wa Filamu ya Foolish Age ya Lulu
Michael
 
 
 
 
 
MSANII wa Filamu Bongo, Elizabeth Michael 'Lulu', usiku wa kuamkia leo amefanikisha zoezi la uzinduzi wa filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Foolish Age .
 Baada ya move hiyo kali ya dakika 120 iliyooesha ukali wa staa huyo kuoneshwa kwa dakika 20 tu na kubakisha zingine 100 kusubiri wateja kuziona majumbani kwao alipanda jukwaani kujitambulisha na kutoa shukrani kwa wamepenzi wa tasnia ya filamu nchini Tanzania kwa muitikio wao alipanda na kuimba wimbo huo wa Yahaya.

Akianzia kuimba kiitikio cha wimbo huo akiwa Back Stage, Lulu aliwashangaza watu pale alipomudu vyema wimbo huo kiasi cha mashabiki ‘Mapedeshee’ wakiongozwa na Pedeshee Rich Rich, kupanda jukwaani na kumtunza fedha kibao ambazo hakika zilimpagawisha msanii huyo na mwisho wa wimbo huo alisema mziki unalipa.
Tukio la uzinduzi huo lilifanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, na kuhudhuriwa na mastaa kibao wa tasnia mbalimbali hapa Bongo, wakiwemo; Judith Wambura 'Lady Jaydee', ambaye alitumbuiza sambamba na Barnaba na Amini.
 Wasanii mbalimbali walihudhuria show hiyo usiku huu pale Mlimani City


 Lulu akizungumza machache mara baada ya Move yake hiyo kuoneshwa kwa mashabiki na wapenzi wa filamu Tanzania ndani ya Ukumbi wa Mlimani City.


 Wadau walifuatilia burudani...
 Jide akikamua jukwaani...

 Mama na mwanao ni kama chanda na Pete... huyo ni Natasha (kulia) na Bintiye Monalisa.
 .... Walitunzana tu kivyao vyao...
 noti alizo tuzwa


 Rich Rich akimwaga noti

 Wadau wakifuatilia uzinduzi huo wa Filamu.
 Furaha ilitawala


 Mwogozaji wa Filamu za Kibongo, Leah Mwendamseke nae alikuwepo kuangalia kazi hiyo ya Lulu.
 Waongoza Shughuli hiyo watangazaji wa Redio na TV Double G na mwana dada kutoka Times FM walikuwepo.

UMEZISOMA HIZI?


Article 4

$
0
0

MBUNGE FILIKUNJOMBE AWAWEZESHA MADEREVA BODA BODA 

 

 Viongozi mbali  mbali wa  chuo cha  Veta wakiongozwa  na mkurugenzi  wa kanda ya  nyanda  za  juu Veronica Mbele (wa tatu  kushoto ) wakiwa na mbunge wa  jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe (wa nne kushoto) mara baada ya kuwatunuku vyeti na leseni  madereva  boda boda kata ya Mndindi Ludewa
 Madereva  boda  boda  kata ya Mndindi  Ludewa ambao  wamehitimu mafunzo ya udereva  yaliyoendeshwa na  Veta baada ya mbunge  wao Deo Filikunjombe  kuomba mafunzo hayo
 Mbunge  wa  jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe  akiwahamasisha  madereva  kuanzisha  umoja  wao ambapo  yeye  atakuwa mlezi  wao
 Wahitimu wa mafunzo ya  udereva  wa  boda  boda na magari  kata ya  Madope  wakiwa  katika mapokezi  ya kumpokea  mgeni  rasmi mbunge wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe


 Madereva  wakila  kiapo cha  utii baada ya  kuhitimu mafunzo yao yaliyoendeshwa na Veta

 Mbunge  wa  jimbo la Ludewa Deo  Filikunjombe katikati akiwa na OCD  Ludewa na RTO Njombe pamoja na washitimu wa mafunzo ya  udereva  boda boda na magari

 Mbunge  wa  jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe akimpongeza mwalimu mkuu  wa  shule ya msingi Luvuyo kata ya madope Bi Aprudensia Joseph Lugome  ambae amehitimu mafunzo ya muda  mfupi ya udereva  kupitia mpango  wa mbunge huyo  kuwasaidia madereva  hao  kupewa  mafunzo na VETA



Wananchi  wakiwa  wamejipanga  barabarani kumpokea mbunge wao Deo  Filikunjombe 

kwa hisani ya fg blogspot.com

Article 3

$
0
0

ZIARA YA VIONGOZI WA CCM MAKETE yabaini 

 


Katibu wa CCM wilaya ya Makete Miraji Mtaturu (kulia) akizungumza katika ziara ya kukagua maendeleo ya shule ya msingi Nkenja wilayani Makete, kushoto kwake ni mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Makete Francis Chaula(Picha zote na Edwin Moshi)
Viongozi wa CCm wilaya ya Makete wakikagua chumba cha darasa wanachosomea wanafunzi wa darasa la tatu na la nne kwa pamoja
 Katibu wa CCM wilaya ya makete Miraji Mtaturu, mwenyekiti Francis Chaula na diwani wa kata ya Kitulo Mbosa Tweve wakisikiliza maelezo kutoka kwa mkuu wa shule ya msingi Nkenja Hester Mahenge ofisini kwake
 Viongozi wa CCM wakikagua ujenzi wa madarasa unaodaiwa kusuasua, mwenyekiti wa CCM wilaya ya makete (katikati) akizungumzia ujenzi huo
 darasa wanalotumia wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili kusomea
 Turubai linalotumika kama bati kwenye jengo hilo
 Vyumba viwili vya madarasa ambavyo vinafaa kwa matumizi shuleni hapo

Article 2

$
0
0
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi  ya St.Benedict Mjini Njombe wakiwa kwenye Mahafali yao Agosti 31 mwaka Huu.


Jumla ya Wanafunzi 84 wanatarajia Kufanya Mitihani yao ya Kuhitimu Darasa la SabaKatika shule ya Msingi ya St.Benedict Iliyoko Ramadhani Mjini Njombe.

Na Prosper Mfugale Njombe.

Adha ya Maji Katika Mkoa wa Njombe Imetajwa Kuwa Kikwazo hadi kwenye Sekta ya Elimu Kutokana na Wanafunzi wengi Kutumia Muda Mwingi Kutafuta Maji Badala ya Masomo

Tatizo Hilo la huduma maji  Mkoani Hapa  Limeendelea  kuwa changa moto kubwa kwa shule nyingi   za msingi  na sekondari  hali inayo pelekea wanafunzi kutumia Muda Mwingi kutafuta maji katika maeneo Ya Mbali na  Mazingira ya shule    .

Hayo Yamebainishwa na Makamu Mkuu wa Shule ya Mtakatifu Benedict Bw Flaviani Mligo Iliyoko Ramadhani Mjini Njombe  wakati wa MaHafali ya 11 ya darasa la

saba Agosti 31 Mwaka Huu shuleni hapo ambapo makamu mkuu huyo amesema licha ya shule hiyo kuwa na mabomba lakini Wanalazimika kufuata maji mtoni na visima vya mitaani

Risala ya Wanafunzi Mbele  ya Mgeni rasmi Bwana Shejamabu Kutoka Kampuni ya Tanwatt Kibena Imeeleza  Kuwa Licha Adha ya Maji na Changamoto Mbalimbali wanazokabliana nazo Lakini watahakikisha wanafanya Vizuri Katika Mitihani yao ya Kuhitimu Darasa la Saba Inayotarajia Kufanyika September 10 na
 11 mwezi huu.

Kwa upande wao wazazi wa watoto wanaosoma katika shule hiyo wamewashukuru walimu kwa kuwalea na kuwafundisha huku wakiahidi kuendelea kuwasomesha mpaka elimu ya juu.

Jumla ya Wanafunzi 84 wa Darasa la Saba wanataraji Kufanya Mtihani huo Mwaka Huu Katika Shule Hiyo ya St.Benedict Ambapo Pamoja na Mambo Mengi Uongozi wa Shule Hiyo Umesema Big Results Now Katika Sekta ya Elimu Inahitajika Kuboreshwa Katika Shule zote Bila Kubagua.

NAIBU WAZIRI WA ELIMU ASISITIZA ELIMU KWA KILA MMOJA

$
0
0
Naibu waziri wa elimu na Mafunzo ya Ufundi Philip Mulugo akisikiliza jambo toka kwa Afisa Masoko wa Vodacom.
Maelekezo yakiendelea Kutolewa 
 

Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo, amewaasa wazazi,

walezi na jamii kwa ujumla kutumia teknolojia ya elimu masafa na mitandao kwa

kupata taarifa za uhakika za kitaluma na kimaendeleo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa maonesho ya Vodacom Elimu Expo 2013 juzi,

jijini Dar es Dalaam, Waziri Mulugo alisisitiza kuwa ushiriki wa wandau wote

kuendeleza sekta ya elimu inafungua fursa ya kupata na kutoa elimu bora kwa

kila mtanzania.

Maonesho ya Vodacom Elimu Expo 2013 ni ya kwanza Tanzania yaliodhaminiwa na

kampuni ya simu ya Vodacom kupitia huduma yake ya M-Pesa inayowezesha malipo

ya karo ya shule kwa urahisi zaidi.

Waziri Mulungo alisema: ““Hii ni fursa kubwa sana kwa wote wanaoshiriki

maonesho haya ususani wanafunzi, walimu na wazazi. Yanatoa nafasi kwa kila

mdau wa elimu kuchangia maendeleo ya elimu nchini. Na hasa ukizingatia kukuwa

kwa matumizi ya mtanda na simu za mkononi katika kila kaya, ni fursa kubwa

katika kubadilishana mawazo ya kujenga Tanzania yenye elimu bora na shindani

katika Nyanja za kimataifa.”

Alidokeza kuwa Serikali kupitia wizara ya elimu, ipo katika hatua za mwisho

za kutengeneza mkongo wa taifa utakao unganisha upatikanaji wa mtandao nchi

nzima kapitia program ijulikanayo kama ‘Tanzania Beyond Tomorrow’ kwa

kushirikiana na makampuni ya mawasiliano katika kuboresha elimu masafa

yaani”e-learning”.
“Naipongeza kampuni ya Vodacom kwa kuwa kampuni ya kwanza nchini kushirikiana

na Serikali kutekeleza mpango huu katika kuhakikisha kuwa sekta ya elimu

inaendelea na kuwa bora zaidi. Sasa ni rahisi kwetu wazazi kutumia njia bora,

tena ya uhakika naya kuhaminika ya M-Pesa kulipia watoto wetu karo ya shule,”

alisema Mulugo.

Naye Robert Mihalo, ambaye ni mwanafuzi wa shule ya green acres ya jijini

alipongeza wadhamini na waandaji wa maonyesho hayo akisema: “Nimeweza

kubandilishana mawazo na wanafunzi wa shule zingine. Zaidi ya yote, nimepata

mbinu mpya kwa kupanua wigo wa ushiriki wa wanafunzi katika kuleta elimu bora

Tanzania.”

Maonesho haya ni muhimu sana kwani yanawaelimisha wananchi kuhusiana na

Vodacom Elimu Expo 2013 ambayo itaaanza kutoa taarifa muhimu zinazohusu shule

mbalimbali ikiwa ni pamoja na gharama za ada na michango mingine katika shule

husika.Aidha itaendelea kutoa taarifa zinazohusu vyuo na taasisi za elimu ya

juu ikiwa pamoja na fani zitolewazo katika vyuo husika pamoja na gharama zake

kupitia simu za viganjani,tovuti na blogs za elimu.

Nae Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa,ambao ni

wadhamini wakuu wa maonesho hayo alionyesha matumaini yake kwa maonesho hayo

na kusema kampuni yake inaelewa umuhimu wa elimu kwa kila mtoto kwa hiyo

wanajisikia fahari kudhamini maonesho hayo kwani yanalenga kuboresha elimu ya

Tanzania.

Wadhamini wengine wa Maonesho hayo ni :- Clouds FM, DTV, Entertainment

Masters, Maxmalipo, Times FM, Primebiz Solutions Ltd na bima ya taifa ya

afya, NSSF, Azania Bank, FNB, Primebiz, NHIF, IPS, NMB, Global publishers,

DSTV, Clouds FM.
 
KWA hisani ya Michuzi blog

Article 0

$
0
0
MVIWATA NJOMBE WAASWA KWENDA NA WAKATI KATIKA KILIMO.
 Waandishi wa Habari Wakihojiana na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Nje ya Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe




 Wakulima Mbalimbali wakiwa kwenye Picha ya Pamoja na Mkuu wa Mkoa Wa Njombe.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Captain Mstaafu Asseri Msangi Akihojiwa na Vyombo vya Habari wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Mviwata Uliofanyika Katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe.

Merry Mwanyika na Prosper Mfugale NJOMBE

Wakulima Wadogowadogo Wa Njombe na Iringa Wametakiwa Kujikita Katika Ufugaji wa Nyuki na Kuku  Pamoja na Ulimaji wa Matunda  Ili kuweza  Kuongeza Kipato na Kukuza Soko la Biashara Katika Mikoa Hiyo.

Hayo Yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Capt.Mstaafu  Asseri Msangi  wakati wa  Mkutano wa Mwaka wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania Uliofanyika Agosti 30 mwaka Huu Katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe ambapo amewataka kuacha kulima kilimo cha mazoea kwa kuzingatia gharama za uzalishaji pindi wanapo uza mazao Kwa Mlengo wa  kupata faida

Aidha Captain Msangi amesema Kwa kuwa hali ya hewa ya Njombe inafaa kwa ufugaji na kilimo cha mazao mbalimbali ikiwemo Matunda kama nanasi na parachichi  hivyo  wakulima hao Hawana Budi Kusoma nyakati kwa Kuachana na

Kilimo cha Mazoea.

Pamoja na Mambo Mengine Amesema Kwa sasa Wakulima Hao Wanaweza Kuuza Mazao yao Hususani ya Matunda Nje ya Nchi Kufuatia Kujengwa kwa Uwanja wa Ndege wa Songwe Mkoani Mbeya.

Awali Akisoma Risala Mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mwenyekiti wa Mtandao wa vikundi vya wakulima Wadogao Wadogo MVIWATA Bwana   Venance Ngimbudzi Amesema Chama Hicho Kimefanikiwa Kutoa Elimu  Kwa Wanachama wa Mkoa wa Njombe na Iringa Ikwemo Kutoa Elimu ya Ujasiliamali na Ukimwi.

Pia Bwana Ngimbudzi Amesema Mtandao Huo Pia Unatarajia Kuongeza Wanachama na Wawezeshaji  Kutoka 64 Hadi 80 Ifikapo Mwaka 2015 na Kuendelea Kushirikiana Kufanya Kazi na Mitandao Mingine.

Kwa upande wao Wakulima Walio Hudhuria Katika Mkutano Huo Wamesema Wanakabiliwa na Changamoto Mbalimbali Ikiwemo Tatizo la bei za Mazao Kuwa Chini  Ikilinganishwa na Gharama za Uzalishaji Pamoja na Tatizo la Lumbesa Ambalo Linatajwa Kuwa Sugu Kwa Wakulima Wengi.
...........................................

Article 4

$
0
0

WANAHABARI WAFANYA MAANDAMANO YA AMANI YA KUMBUKUMBU YA MAREHEMU DAUD MWANGOSI IRINGA.

 Wanahabari  wa  vyombo  mbali mbali na  wadau  wa habari  mkoa  wa  Iringa  wakiwa katika  maandamano ya amani ya  kumuenzi  aliyekuwa mwenyekiti  wa klabu ya  waandishi  wa  habari  mkoa  wa Iringa (IPC) leo
 Maandamano  ya  wanahabari na  wadau  wa  habari yakipita  eneo la soko kuu la manispaa ya  Iringa
 katibu  wa IPC  Francis  Godwin  akiongoza  maandamano ya  wanahabari na  wadau huku akiwa  juu ya gari na picha ya marehemu Daudi Mwangosi
 Wanahabari  Iringa katika maandamano ya  kumuenzi  marehemu  Mwangosi  leo
 Maandamano ya  wanahabari  na  wadau  wa habari  mkoa wa Iringa ya  kumuenzi marehemu Daudi Mwangosi  yakipita  eneo ya  uhindini 


 Wananchi  wakishuhudia maandamano  hayo  leo





 katibu  mtendaji  wa IPC  Francis  Godwin akitoa taarifa ya  kuanza kwa maandamano ya kumuenzi marehemu Daudi Mwangosi leo
 Katibu  wa  IPC Francis  Godwin mwenye pama akikabidhi maandamano ya  mwenyekiti  wa IPC Frank Leonard na  wadau  wengine  eneo la Maktaba ya  mkoa wa Iringa


 Katibu  wa  IPC  FrancisGodwin kushoto akikabidhi picha ya marehdemu Daudi Mwangosi kwa  mwenyekiti  wa IPC  Frank Leonard kulia,wanaoshuhudia ni mzee  Fulgence  Malangalila  na Majid Mjengwa


 Mwenyekiti wa  IPC Frank Leonard  kushoto akikabidhi  picha ya  Mwangosi kwa mwasisi  wa IPC mzee Fulgence Malangalila








Viongozi  wa  IPC kutoka  kulia Francis Godwin katibu  na Frank Leonard  mwenyekiti na mwakilishi  wa wananchi 

MAANDAMANO ya  wanahabari  mkoa  wa  Iringa  kwa  ajili ya  kumbukumbu  ya  mwaka  mmoja  ya  kifo  cha  aliyekuwa  mwenyekiti  wa klabu ya  waandishi  wa habari  mkoa  wa  Iringa (IPC) na mwandishi  wa Chanel  Ten Marehemu  Daudi Mwangosi  yatikisa mji  wa  Iringa leo
Maandamano  hayo ambayo  yameanza majira ya saa 4 asubuhi  katika  viwanja   vya  bustani ya  Manispaa ya  Iringa yamepata  kuzungukakatika maeneo  mbali mbali ya  mji wa  Iringa kabla ya  kupokelewa na mwenyekiti  wa IPC  Frank Leonard katika  ukumbi wa maktaba ya  mkoa kwa mkutano wa  wadau  wa habari.

katika  maeneo  mbali mbali  ambayo maandamano  hayo yamepita  likiwemo  eneo la Uhindini , Mashine  tatu, Soko  kuu na stendi  kuu ya mabasi ya mikoani  wananchi  walilazimika  kusitisha  shughuli  zao kushuhudia maandamano  hayo ambayo yaliongozwa na  askari  wa  usalama barabarani .

Akizungumza  baada ya kupokea  maandamano  hayo ,mwenyekiti wa IPC Bw  Leonard  alisema  kuwa  lengo la maandamano  hayo ni  kumkumbuka  Mwangosi pamoja na  kutazama  changamoto  mbali mbali ambazo  wanahabari  wamekuwa  wakikabiliana.

Alisema  kuwa hakuna  mtanzania  asiyetambua  mchango  wa  Mwangosi  katika uhai  wake  na  kuwa kutokana na mchango  wake  umoja  wa  vilabu  vya  waandishi  wa habari Tanzania (UTPC) umeanzisha  tuzo maalum kwa wanahabari itakayopewa  jina la Daudi Mwangosi  na mshindi  atapewa kiasi cha  Tsh milioni 10.
Alisema  tuzo  hiyo  itakuwa  ikitolewa  kila mwaka  na UTPC na ili mwanahabari  aweze  kushinda  tuzo hiyo ,lazima apitie katika misuko  suko katika  kazi  hiyo ,pia  wale  watakaopigania  maslahi yao  na  fisa  nyingine  nyingi.
 
Hivyo  aliwataka  wanahabari  wanachama  wa Vilabu  vya  wanahabari  na  wale  wasio  wanachama  ambao  wanafanya kazi  Tanzania  kujitokeza   kuchangamkia tuzo  hiyo.

Mbali   hilo  aliwataka  wanahabari  kuendelea  kuzingatia  maadili  yao  ya kazi hiyo  ili  kuongeza imani kwa  watanzania  .

Alisema  kuwa iwapo  wanahabari  watafanya  watazingatia  maadili  ya  uandishi  Taifa  linaweza  kupiga  hatua  katika maendeleo.

Wakati  huo  huo IPC  imetoa  mikopo  ya  zaidi ya  Tsh 500,000 kwa  wanachama  wake  ili kuwawezesha  kuboresha  zaidi  shughuli  zao kwa  kununua  vifaa vya kazi

Marehemu   Mwangosi  aliuwawa  na  polisi septemba  2 mwaka 2012  katika kijiji  cha  Nyololo  wilaya ya  Mufindi   wakati  wa  ufunguzi  wa  tawi la  Chadema kijiji  cha Nyololo.
MWSHO
 
kwa hisani ya Francisgodwinblog

Article 3

$
0
0
Afisa Elimu ya Msingi Halmashauri ya Mji wa Njombe Bwana Shegeli Shengelo.

Halmashauri ya Mji wa Njombe Imeanzisha Vituo vya Walimu Kujisomea na Kujikumbusha Masuala ya Kielimu Kwa Kila Kata Katika Shule za Msingi Katika Kutekeleza Sera ya Elimu Kupitia Big Results Now

Hatua Hiyo Imekuja Kufuatia Walimu Wengi Kushindwa Kuendana na Wakati na Mabadiliko ya Mitaala na Hivyo Wanafunzi Kushindwa Kupata Elimu Stahiki.

Akizungumza na www.gabrielkilamlya.blogspot.com Afisa Elimu wa Shule za Msingi Katika Halmashauri ya Mji wa Njombe Bwana Shegeli Shengelo Amesemu Kuwa Kuwekwa kwa Vituo Hivyo Kutasaidia Kuongeza Ujuzi na Mbinu za Kiufundishaji watoto kwani Imebainika Kuwa Baadhi ya Walimu wengi walishindwa Kufanya Vizuri Kwenye Mtihani Aliowatungia Hivi Karibuni.

Aidha Amesema Kuwa Kwa Sasa Kila Afisa Elimu Anatembelea Shule Mbalimbali Badala ya Kushinda Ofisini na Hivyo Kufanya Hivyo Kunasaidia Kupunguza Utoro kwa

Walimu Ambao wamekuwa wakishindwa Kufundisha Darasa.

Pamoja na Mambo Mengine Amesema Kuwa Kwa sasa wameweka Utaratibu wa Kuwawekea Semina Mbalimbali walimu hao Pindi wanapopata Fedha Ili Kuwapa Fursa Walimu ya Kupanuka Kimawazo na Kifikra.  

Article 2

$
0
0

 WAASI WA M23 WALIVYO MUUWA ASKARI WA JWTZ.


JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limeleezea namna mwanajeshi wake, Meja Khatibu Shaaban Mshindo, alivyouawa baada ya kuangukiwa na bomu, wakati akiwa katika jukumu la ulinzi wa amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
 
Pamoja na hayo, Watanzania wametakiwa kuimarisha mshikamano na kuachana na makundi yenye nia ya kuleta mgawanyiko, hasa katika kipindi hiki kigumu ambacho Tanzania imepoteza askari wake waliopewa dhamana ya kitaifa ya ulinzi wa amani katika nchi zenye migogoro Afrika.
 
Akitoa salamu za rambirambi wakati askari huyo wa kikosi cha Mizinga namba 83 KJ kilichopo Kibaha akiagwa rasmi kijeshi Dar es Salaam jana, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamnyange, alisema askari huyo pamoja na askari watano wa Tanzania, waliangukiwa na bomu hilo na kujeruhiwa vibaya.
 
“Waliangukiwa na bomu Agosti 28, mwaka huu huko Goma DRC eneo walilokuwa wakifanyia kazi… Meja Mshindo aliumia vibaya na kukutwa na mauti njiani akipelekwa hospitalini,” alisema Jenerali Mwamunyange.
 
Alisema katika tukio hilo, askari wengine watano wa Tanzania walijeruhiwa vibaya na wanaendelea vizuri na matibabu nchini humo na hali zao zinaendelea vizuri.
 
Akimzungumzia Meja Mshindo, Jenerali Mwamunyange alisema katika uhai wake alikuwa mchapakazi, muaminifu, hodari na mtiifu na kifo chake kimetokea wakati jeshi linamhitaji.
 
“Kifo chake kimeacha pengo ndani ya JWTZ na itachukua muda mrefu kuziba pengo hili.” Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, alisema kifo cha askari huyo ni msiba wa kitaifa na kumtaja Meja Mshindo kuwa shujaa aliyekutwa na mauti wakati akitekeleza kazi aliyotumwa na nchi yake.
 
Alisema kifo hicho pamoja na vifo vya askari wengine saba wa JWTZ vilivyotokea Darfur mwaka huu, ni chachu kwa Tanzania kuendeleza jitihada za kusaidia nchi zenye migogoro na kuhamasisha amani Afrika.
 
“Serikali inapata matumaini namna Watanzania walivyosimama pamoja na kuunga mkono jeshi letu katika kipindi hiki kigumu. Ingekuwa nchi nyingine, haya yaliyotokea yangeleta mgawanyiko mkubwa miongoni mwa raia, lakini kwa hapa kwetu hali imekuwa tofauti,” alisema Membe.
 
Aliwataka wachache wenye mawazo ya kutumia matukio hayo kuwagawa Watanzania, waache mara moja nia yao hiyo, kwa kuwa moja ya kazi ambayo Tanzania inayo, ni pamoja na nia yake ya kuhamasisha na kutangaza amani Afrika na dunia kwa ujumla.
 
“Jamani wajibu wetu ni kuhakikisha haya maeneo yenye migogoro yanakuwa na amani, kule DRC hali ni mbaya, watu wanakufa kila kukicha na akinamama na watoto wanabakwa na kudhalilishwa, sasa sisi kama taifa ni vyema kujitokeza na kusaidia wenzetu,” alisisitiza.
 
Meja mshindo, alizikwa jana nyumbani kwao Fujoni Zanzibar na ameacha mke mmoja, Hawa Mnimbo na watoto watatu ambao ni Shaaban, Abuu na Samir Mshindo.
 
KWA Hisani ya Mpekuziblog

Article 1

$
0
0

MADAKTARI, MANESI WADAIWA KUFANYA VITENDO VYA KINYAMA kwa Wagonjwa Dar.

 
HOSPITALI ya Mbagala Zakhem, jijini Dar es Salaam, inakabiliwa na kashfa nzito, baada ya madaktari na wauguzi wake kudaiwa kuwafanyia vitendo vya kinyama wagonjwa, ikiwamo kumfukuza mama mjamzito mwenye uchungu usiku wa manane na mtoto mchanga kunyweshwa maji ya dripu.
Tuhuma hizo zimetolewa hivi karibuni na watu waliokumbwa na matukio hayo wakati walipofuata tiba hospitalini hapo.


Madai ya watu hao yalitolewa mbele ya Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndugulile, wakati alipokutana na wananchi wa Mbagala Kichemchem kujua kero zinazowakabili.


Hata hivyo, madai hayo yalionyesha kumpa wakati mgumu mganga mkuu wa Hospitali hiyo, Julius Nyakazilibe, ambapo ilibidi aokolewe na mbunge huyo kufuatia wananchi hao kupinga utetezi wake.


Mwananchi wa kwanza kuituhumu Hospitali hiyo yenye hadhi ya

Wilaya, alikuwa Omar Lipweremwike (50), ambaye alidai mke wake alifukuzwa usiku akiwa katika hali ya mwisho ya kujifungua na muuguzi mmoja kwa kile alichoelezwa muda huo hawezi kuzalisha mtu.

"Mama mjamzito akiwa katika hatua ya mwisho ya kujifungua hawezi kusubiri, lakini yule muuguzi alituambia tuondoke na turudi pale asubuhi ndipo atakuwa tayari kumuhudimia," alisema Lipweremwike.


Hata hivyo, alidai baada ya kuona hali hiyo, ilimbidi kumuwahisha kituo cha Afya cha Roundtable na alifanikiwa kujifungua salama muda mchache.


"Jambo hili ni baya sana tena linawanyanyasa wanawake kwa ujumla, haiwezekani Hospitali kubwa ikawa na wafanyakazi wazembe huku vituo vya afya vikisifika kwa huduma bora," aliongeza kusema.


Naye Ester Makunda. (25) alisema mtoto wake mchanga, Mariam Mohamed alinusurika kupoteza maisha baada ya wauguzi kukataa kumuwekea dripu ya maji kwa njia ya kawaida, badala yake walimlazimisha mama yake kumnywesha maji hayo kwa kutumia chupa ya maji safi.


Alisema tukio hilo lilitokea Agosti 15, mwaka huu, baada ya mtoto wake kuugua ugonjwa wa kuharisha.


Makunda alisema alipofika hapo alifuata taratibu zote ikiwamo kumuona daktari na mtoto kufanyiwa vipimo, baada ya majibu kutoka ilionekana ameishiwa maji, hivyo ilihitajika kuongezewa.


"Kitu cha kushangaza nilipofika wodini ili mtoto awekewe maji, wale wauguzi wakaanza kushindana wenyewe na baadaye walikataa wakanilazimisha nikanunue chupa ya maji ili niweke yale maji ya dripu ili nimnyweshe mwanangu, kwa kweli nilikataa," alisema Makunda.

 

Kama hiyo haitoshi, Makunda, alisema hata yeye mwenyewe wakati aliporudi kwa mara ya pili kupata matibabu kutokana na afya yake kutokuwa nzuri, aliambiwa maini yake yameharibika jambo ambalo si la kweli.


Alisema alibaini kitu hicho baada ya daktari aliyemuona siku hiyo kumshauri kumtafuta daktari bingwa wa maini wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, lakini baada ya kumtafuta daktari mwingine kwa ajili ya kuomba msaada zaidi alimueleza mtu aliyemuona awali hakuwa na utaalamu kwa sababu majibu ya vipimo vyake vinaonyesha yupo safi.


Tuhuma hizo zilimfanya Dk. Ndugulile kumuinua Mganga Mkuu wa hospitali hiyo kujibu, huku akimuambia afanye uchunguzi wa kina kubaini wafanyakazi wanaofanya vitendo visivyofaa kwa wagonjwa.


Wakati akijibu, Nyakazilibe aliwataka wananchi kumpigia simu haraka endapo watapata manyanyaso wakati wanapokwenda kupata huduma.


Alisisitiza ofisi yake ipo wazi muda wote kupokea malalamiko ya wananchi na kuyafanyia kazi.


Hata hivyo, aliwakasirisha wananchi hao na kuanza kupiga kelele za kumtaka akae chini, baada ya kuwaambia wananchi hao waache kutoa tuhuma kwenye mikutano ya viongozi kwani wanaweza kumuona yeye na kutatua kwa wakati.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Article 0

$
0
0
RASIMU YA KATIBA NJOMBE YAWATAKA WATANZANIA KUWA NA MAZOEA YA KUJISOMEA
Afisa Habari wa Mkoa wa Njombe Bwana Christopher Philimon Ambaye Alikuwa Mratibu wa Mchakato wa Rasimu ya Katiba Mpya Mkoa Akizungumza na Mtandao Huu. Leo Ofisini Kwake.

Na Gabriel Kilamlya Njombe.
 
Pamoja na Kumalizika Salama Mchakato wa Utoaji Maoni ya Rasimu ya Katiba Mpya Agosti 31 Mwaka Huu Nchini Kote Wananchi Mkoani Njombe Wametakiwa Kujijengea Mazoea ya Kujisomea Ili kuendana na Wakati .

Akizungumza na www.gabrielkilamlya.blogspot.com Leo Afisa Habari wa Mkoa wa Njombe Bwana Christopher Philimon Amesema Kuwa Wananchi wengi wamekuwa Hawana Mazoea ya Kujisomea Hali Iliyopelekea Wananchi wengi Kushindwa Kupata Fursa ya Kutoa Maoni yao ya Rasimu ya Katiba Kwa Kushindwa Kusoma Rasimu.

Article 2

$
0
0
Mahakama ya Wilaya ya Njombe Jana  Imemuhukumu Kifungo cha Mwaka Mmoja Jela Izack Kahogo Mkazi wa Kambarage Mjini  Njombe  Baada ya Kumkuta na Kosa la Wizi Katika Nyumba ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Kaptein Mstaafu Aseri Msangi.

Akisoma Hukumu Hiyo Hakimu wa Mahakama Hiyo John Kapokolo Amesema Mahakama   Imetoa Adhabu Hiyo Kwa Mshtakiwa Chini ya Kifungu cha Sheria Namba 258 Kifungu Kidogo cha Sheria Namba 256 Sura ya 16 Kilichofanyiwa Marekebisho Mwaka 2002,Pamoja na Kuridhishwa na Ushahidi Uliotolewa na Upande wa Mashtaka.

Ameongeza Kuwa Mahakama Imetoa Adhabu Hiyo  Kwa Kuzingatia Utetezi na Ombi la Mshtakiwa ya Kuomba Apunguziwe Adhabu Kwani Amekaa Mahabusu Kwa Takribani Mwaka Mmoja.

Awali Akisoma Hati ya Mashtaka Mwendesha Mashtaka  Selapian Matiku Ameiambia Mahakama Kuwa Mshtakiwa Alitenda Kosa Hilo  selaphiani Agosti 26 Mwaka Jana  na Kwamba Alifikishwa Mahakani  29 Agosti Mwaka 2012.  

Imedaiwa Mahakamani Hapo na Mwendesha Mashataka Kuwa Siku ya Tukio Mshtakiwa Alifika Nyumbani Kwa Mkuu wa

Mkoa wa Njombe na Kuiba Kompyuta Ndogo  LAPTOP Aina ya Lanovo na Simu Tatu Zenye Thamani ya Shilingi Milioni Moja na Laki Mbili.

Wakati Huo Huo Mahakama Hiyo Imemuhukumu Kifungo cha Miezi Sita Jela Ama Kulipa Faini ya Shilingi Elfu  30 Winfirida Wilomo Mkazi wa Kifanya Wilaya ya Wanging'ombe Baada ya Kumkuta na Hatia ya Kujifungua na Kumtupa Mtoto Mchanga wa Siku Moja Chooni na Kusababisha Kifo cha Kichanga Huyo.

Akitoa Hukumu Hiyo Hakimu wa Mahakama Hiyo John Kapokolo Amesema Mahakama Imetoa Adhabu Hiyo Chini ya Kifungu cha Sheri Namba 218 Kifungu cha 35 cha Kanuni ya Adhabu , Sura ya 16 Kilichofanyiwa Marekebisho Mwaka 2002.

Hakimu Kapokolo Ameongeza Kuwa Mahakama Hiyo Imetoa Adhabu Hiyo Kwa Kuzingatia Utetezi na Maombi ya Mshtakiwa Kuwa Alikuwa na Mtoto Mdogo Mwenye Umri wa Mwaka Mmoja.

Awali Akisoma Hati ya Mashtaka Mwendesha Mashtaka Selapian Matiku Ameiambia Mahakama Kuwa Mshtakiwa Alitenda Kosa Hilo Agosti 19 Mwaka Huu Majira ya Saa Sita Usiku na Kwamba Alikamatwa Agosti 23 Mwaka 2013 na Kuongeza Kuwa Mshatakiwa Amefikishwa Hii Leo Kwa Mara ya Kwanza na Kusomewa Hukumu Baada ya Kukiri Kutenda Kosa Hilo.

Akitoa Utetezi Wake Mahakamani Hapo Mshtakiwa Ameiambia Mahakama Kuwa Alifanya Hiavyo Kutokana na Kichanga Hicho Kutoonesha Dalili za Kuwa Hai na Kwamba Alikuwa na Mtoto Mdogo wa Mwaka Mmoja.

Article 1

$
0
0

 SARE ZA JWTZ ZAKAMATWA ZIKIWA NA MWANAMKE.



JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limemkamata Saida Mohamed (30), mkazi wa Mwasonga Kigamboni, akiwa na sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ). 

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleimani Kova, alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa Agosti 31, mwaka huu, katika eneo la Mwasonga, Kigamboni.

Alisema Saida alikamatwa na suruali saba, mashati saba ya kombati, kofia 10, shati mbili nyepesi, fulana mbili na kofia moja aina ya bareti, vyote vikiwa mali ya JWTZ.

Alisema mtuhumiwa huyo, alikuwa na begi moja la kuwekea nguo za jeshi, cheo kimoja cha Koplo na mikanda miwili ya

kijeshi.

Alisema uchunguzi unaendelea juu ya mwanamke huyo ili kubaini sababu za kumiliki sare za jeshi, kabla ya kufikishwa mahakamani.

Katika tukio jingine, polisi wamemkamata Husein Mkondoa (25), mkazi wa Gongolamboto Mzambarauni, akiwa anaendesha pikipiki huku akiwa amevaa nguo za kiraia na kofia ngumu ya kijani yenye nembo ya Polisi.

Alisema polisi walimtilia mashaka na kumkamata mtuhumiwa na anaendelea kuhojiwa.

“Naomba kutoa onyo kwa watu wote wenye silaha na sare za jeshi wazisalimishe kwa polisi au ofisi yoyote ya Serikali, msako wa kuwakamata wahalifu utakuwa endelevu na tutaingia nyumba hadi nyumba kuwatafuta wahalifu.

“Sambamba na operesheni hii, licha ya kubadilisha uongozi katika kituo cha Polisi Ubungo, tumeamua kutupia macho vitendo vya utapeli katika eneo la Ubungo Bus Terminal, ambalo watu wengi wanajifanya askari.

“Licha ya hilo, tumeunda kikosi cha kutumia video kamera na kamera za picha mnato ili kubaini na kuchukua hatua na nyendo mbalimbali ili kujenga ushahidi wa wahalifu hao wasiepuke mkono wa sheria,” alisema Kova.

Wakati huo huo, Jeshi la Polisi linawashikilia watuhumiwa wawili kwa kuchonga hati mbalimbali zinazotaka kufanana na za Serikali.

Kamishina Kova, aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Shadrack Samwel (27) mkazi wa Mbagala Sabasaba na Mwangi Samwel (38) mkazi wa Kimara Baruti.

Alisema watu hao, hawana ofisi maalumu hivyo hufanya shughuli hiyo sehemu yoyote na ofisi zao kuu ni mkoba pamoja na gari ambalo wanatembelea, lenye namba za usajili T 397 ADX aina ya Crester.

“Watuhumiwa hawa, tuliwakuta na mihuri 27 ambayo ni ya Serikali na taasisi binafsi, mihuri ya mawakili wa kujitegemea na wa serikalini, mhuri wa Jeshi pamoja na mhuri wa Serikali za mitaa.

“Pia tumewakamata na nakala mbalimbali za SUMATRA, ikiwemo karatasi za kukagulia magari, pleti namba za magari pamoja na nakala mbalimbali za ofisi hiyo,” alisema.

Katika hatua nyingine, polisi wanawashikilia watu watano, akiwamo Enea Dawsoni, ambaye ni mfanyakazi katika Kapuni ya Ndege ya Fast Jet, kwa jaribio la kutaka kupora fedha kiasi cha Sh 60,000,000 katika Kampuni hiyo.

Alisema watuhumiwa hao walinaswa katika Mtaa wa Samora na iligundulika walikuwa wana mawasiliano ya simu.

“Baada ya kuwakamata watu hawa, Polisi walielekea katika ofisi hizo na baada ya kufika walichukua simu ya watuhumiwa hao na kuona ujumbe mfupi wa maneno, ulioeleza kuwa fedha zipo karibu na chooni.

“Polisi walichukua simu ya wahalifu na walipopiga simu hiyo iliyokuwa na mawasiliano na majambazi hao, simu iliita kwa sauti kubwa ndani ya maungo ya mmoja kati ya watumishi wa Fast Jet.

“Mtumishi Enea Dawson alikuwa ameficha simu hiyo sehemu za siri katika nguo zake ambapo aliumbuka na kugundulika kuwa alikuwa na uhusiano wa karibu na majambazi hao,” alisema Kova.


kwa hisani ya mpekuziblog.
Viewing all 2276 articles
Browse latest View live