Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all 2276 articles
Browse latest View live

Article 2

$
0
0

JENGO LA UHAMIAJI MKOA WA MBEYA LAZINDULIWA.

Jengo la Uhamiaji Mbeya


KATIKA kuhakikisha Wimbi la Uhamiaji Haramu linakomeshwa Mkoani Mbeya, Serikali imeagiza viongozi wa Serikali za Vijiji kusimamia uhalali wa Wakazi wanaoishi katika maeneo yao kisheria.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, wakati wa Hafla ya uzinduzi wa Jengo la Ofisi za Uhamiaji Mkoa wa Mbeya lililokuwa likifanyiwa ukarabati kufuatia uchakavu wa Ofisi ziliokuwepo awali.
Kandoro alisema Mkoa wa Mbeya umejipanga kuhakikisha Wimbi la Uhamiaji Haramu linakuwa Historia kwa kuwabana Viongozi wa Serikali za vijiji ambao watabainika kuishi na Wahamiaji haramu katika maeneo yao kinyume na utaratibu kwa kuwachukulia hatua za kisheria.
Mbali na hilo Kandoro alipongeza kuwa Serikali ya Mkoa imepanga na kupitisha agizo kuwa Mtu yeyote atakayebainika kuwasafirisha Wahamiaji Haramu atakamatwa pamoja na Gari lake na kuamriwa kuwarudisha alikowatoa chini ya uangalizi wa Maofisa Uhamiaji ikiwa ni pamoja na kutaifisha Chombo chake ili kupunguza msongamano wa watu magerezani.
“ Mnajua tunawahamiaji wengi sana magerezaji na wanatumia gharama kubwa za serikali kuwatunzia na kuwarudisha, hivyo tumeamua kuwa atakayekamatwa akiwasafirisha ama kuwahifadhi nyumbani kwake atalazimika kuwarudisha alikowatoa na nyumba au Gari vitataifishwa na kuwa mali ya Serikali” alisema Kandoro.
Alisema mbinu hiyo inaweza kusaidia kuondoa kabisa wahamiaji haramu wanaopita kwa wingi Mkoani Mbeya kwa ajili ya kwenda nchi jirani za Kusini mwa Afrika ambako wanaamini kuwa kunamaisha mazuri kuliko nchi za Kaskazini Mwa Tanzania.
Kwa upande wake Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mbeya, William Bambanganya, alisema wimbi la uhamiaji haramu bado ni changamoto katika Jeshi hilo kutokana na ukosefu wa vitendea kazi vinavyoweza kusaidia kuendeshea misako ya Wahamiaji na kuziba mianya na njia za panya wanazotumia kuvukia.
Alisema vitendea kazi vinavyotakiwa sana ni pamoja na Magari ya kufanyia Doria katika Maeneo yote ya Mipaka ambayo ndiko njia kuu za Wahamiaji ziliko na kuongeza kuwa pamoja na Wananchi kukosa ushirikiano na elimu juu ya madhara ya kuwaruhusu Wahamiaji haramu katika majumba yao bila kuwajua tabia zao.
Alisema kwa kipindi cha Mwezi wa Saba jumla ya Wahamiaji 106 walikamatwa ambao wengi wao ni raia wa Nchi jirani ya Ethiopia ambao bado wako Gerezani wakisubiri taratibu za kuwarudisha makwao.
Aidha akitoa taarifa za ukarabati wa Ofisi hizo, Afisa huyo alisema wameamua kukarabati ili kutekeleza agizo la Serikali la kuhakikisha Ofisi na Makazi ya Watumishi wa Serikali yanaboreshwa ili kuleta ufanisi wa utendaji wa kazi.
Alisema katika mpango huo jumla ya Shilingi Milioni 472,997000 zimetumika kukarabati jingo la Ofisi za Uhamiaji Mkoa wa Mbeya na Nyumba mbili za kuishi Watumishi katika kituo cha Tunduma Wilayani Momba.
Aliongeza kuwa awali Ofisi hizo zilikosa mvuta wa viongozi kutembelea kutokana na uchakavu wa Majengo na Thamani za ndani pamoja na eneo la kuegesha magari ambalo halikuwepo awali lakini limetengenezwa katika ukarabani huu.
 
source Mbeya yetu.

 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, akikata utepe  uzinduzi wa Jengo la Ofisi za Uhamiaji Mkoa wa Mbeya lililokuwa likifanyiwa ukarabati kufuatia uchakavu wa Ofisi ziliokuwepo awali.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, akipanda mti kwenye jengo hilo la Uhamiaji
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, akihutubia mara baada ya uzinduzi wa jengo la uhamiaji
Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mbeya, William Bambanganya, akisoma taarifa kwa mgeni rasmi
Kaimu kamishana wa Uhamiaji Tanzania vicky Lembeli akimkaribisha mkuu wa mkoa Mbeya
Viongozi mbali mbali walialikwa katika uzinduzi huo

Kwaya toka Njombe ikitumbuiza 
Kamishna wa sheria toka makao makuu akimshukuru mgeni rasmi
Picha ya pamoja

WEZI WA JARIBIO LA KUIBA TRANSFOMA NJOMBE WAKAMATWA

$
0
0
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe Fulgency Ngonyani akiongea na mtandao huu ofisini 

Na Prosper Mfugale Njombe


Jeshi la polisi mkoani Njombe linawashikilia watu watatu kwa kuhusika na matukio mawili Tofauti likiwemo la kutaka kuiba Transformer mali ya kampuni ya Tanesko katika kituo cha makambako Njombe

Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la polisi kwa vyombo vya habari ina sema kuwa tukio la kwanza limetokea Augost 20 mwaka huu majira ya saa nne katika kijiji cha Ilunda ambapo
jeshi la polisi linawashikilia Imrani Sulemani miaka 40  na Beatus Urasa miaka 40 wakazi wa dar es laam kwa tuhuma za wizi wa tranfoma

Taarifa hiyo imesema kuwa jeshi la polisi lilipata taarifa ktoka kwa msamaria mwema na kisha kuweka mtego katika eneo la
transfoma hiyo mpaka lilipofanikiw kuwa tia mbaroni wakatti watuhumiwa wakati wakijiandaa kuiba na baaba ya kupekuliwa walikutwa na spana katika eneo la tukio

Na katika tukio jingine jeshi la polisi linamshikilia Wainfrida wilomo mkazi wa kijiji cha kifanya mwenye umri wa miaka 20 kwa tuhuma za kumtumbukiza kwenye choo mtoto wa kiume mwenye umri wa miezi saba baada ya kujifungua  nyumbani kwake

Jeshi la polisi linaendelea kumshikilia mtuhumiwa na kiini cha tukio hilo kinaendelea kuchunguzwa

Article 0

$
0
0

SERENGETI FIESTA 2013 TABORA UWANJA WA AL-HASSAN MWINYI.

Abdul Kiba,msanii wa muziki wa bongofleva akiimba mbele ya umati mkubwa wa wakazi wa mji wa Tabora waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu.Tamasha hilo linaandaliwa na kampuni bingwa ya Burudani hapa nchini,Prime Time Promotions Ltd kwa kushirikiana na Clouds FM,na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake murua kabisa cha Serengeti Premium Lager.
 Sehemu ya  umati wa mji wa Tabora waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Neylee akiimba kwa hisia mbele ya wakazi wa mji wa Tabora waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu.Tamasha hilo linaandaliwa na kampuni bingwa ya Burudani hapa nchini,Prime Time Promotions Ltd kwa kushirikiana na Clouds FM,na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake murua kabisa cha Serengeti Premium Lager.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Linah pichani kati akiwa na madensa wake wakitumbuiza jukwaani usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu. 
 Sehemu ya  umati wa mji wa Tabora waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu.
 Anaitwa Amin,mmoja wa wasanii mahiri akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu kwenye u kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu. Tamasha hilo linaandaliwa na kampuni bingwa ya Burudani hapa nchini,Prime Time Promotions Ltd kwa kushirikiana na Clouds FM,na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake murua kabisa cha Serengeti Premium Lager.
 Wenyewe mashabiki waki wanamuita Baba Levo na yeye kabaki Levo kwenye gemu ya muziki wa bongofleva,ndiye pichani Baba Levo akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani Tabora.

 Ni shwangwe tu usiku huu kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani Tabora.

 Wanamuita Mzee wa Masauti,Christian Bella akiwaimbisha mashabiki wake wa muziki wa dansi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta,liinalofanyika usiku huu kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi.
 Sehemu ya umati wa wakazi wa mji wa Tabora waliojitokeza usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 wakiwa wamewasha tochi za simu zao wakiashiria kushoo love ya pamoja

Msanii wa muziki wa bongofleva,Rachael akicheza jukwaani na mmoja wa madensa wake,huku mashabiki wake wakipiga mayowe ya shangwa kuonesha kukunwa vilivyo na msanii huyo.

 Sehemu ya  umati wa mji wa Tabora waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,linalofanyika kwenye uwanja wa Al-Hassan Mwinyi mkoani  humu.Tamasha hilo linaandaliwa na kampuni bingwa ya Burudani hapa nchini,Prime Time Promotions Ltd kwa kushirikiana na Clouds FM,na kudhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake murua kabisa cha Serengeti Premium Lager.Picha Kwa Hisani ya Michuzijr Blog

Article 11

$
0
0

MTOTO WA MIAKA 8 AOLEWA NA MWANAUME WA MIAKA 38.


Mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Samson (38), mkazi wa Kijiji cha Mindukeni, Tarafa ya Tarawanda katika Wilaya ya Bagamoyo, Pwani amefanya maajabu ya milenia baada ya kudaiwa kuoa mtoto mwenye umri wa miaka nane .

Habari za kiuchunguzi zilisema kuwa mwanaume huyo ambaye tayari alishaoa mke wa kwanza, alidaiwa kumtorosha mtoto huyo nyumbani kwao, Iringa.


Ilidaiwa kuwa Samson alifanya tukio hilo kwa kushirikiana na mjomba wa mtoto huyo, wakati akichunga mbuzi mkoani Iringa.

Habari zilieleza kuwa baada ya Samson kumtorosha mtoto huyo kijijini kwao alimpeleka kijijini Mindukeni, Pwani na kumuweka kinyumba akiwa ni mke wake wa pili.


Ilidaiwa kwa kuwa mtoto huyo analingana na watoto wake kwa mke wa kwanza, alimweka chumba kimoja na wanaye.

Kabla ya ishu kubumburuka, Samson alikuwa akiishi na mtoto huyo akiwa ni mke mdogo huku akimtumia kufanya kazi mbalimbali kama kuchunga mbuzi, kuchota maji kisimani na kusaidia kubeba au kulea watoto wa mke mkubwa.
 
Kwa mujibu wa mtoto huyo, hadi sasa hajui alifikaje kijijini hapo na wala hatambui jinsi ya kurudi kwao kwani walimuiba tu.

Alisema baada ya kufikishwa kijijini hapo, alikuwa akilala chumba cha watoto na mwanaume huyo akitaka kumuingilia anaingia chumbani humo na kufanya naye mapenzi kisha kurudi kwa mke mkubwa.
 

“Nilikuwa naumia wakati akiniingilia, alikuwa anakuja chumba tunacholala na watoto wake wengine, ananichukua pembeni na kufanya mapenzi, akimaliza anarudi kwa mke mkubwa,” alisema mtoto huyo na kuongeza:
 

“Kusema kweli mwanzoni nilikuwa nasikia maumivu makali hadi nilipokuja kuona ni kitu cha kawaida.”

Mtoto huyo alisema kuwa kila kulipokucha alikuwa anaona aibu kwani wale watoto wengine wanalingana naye hivyo alikuwa akiumia kufanyiwa kitendo kama hicho cha ukatili na mtu ambaye ni sawa na baba yake.


Aliendelea kusema kuwa aliumia kupelekwa katika kijiji hicho na kuishi na mwanaume huyo na tayari ameshakaa miaka minne kama mke wake, akimuingilia mara kwa mara na kumsababishia maumivu. 


“Nimeishi naye muda mrefu kama miaka minne, natamani kurudi kwetu nikasome,” alisema mtoto huyo.


Kwa upande wake mtangazaji wa Kipindi cha Wanawake Live cha EATV, Joyce Kiria alifika katika kijiji hicho na baadaye alikwenda katika Kituo cha Polisi Bagamoyo kisha kuchukua askari usiku wa manane ambapo Samson alitiwa mbaroni na hadi sasa yupo mahabusu huku mtoto huyo akisubiri kuanza shule.

Habari hii ni ya kusikitisha kwa sababu huu ni zaidi ya ukatili kwa watoto wadogo, ili kujua na kuona mengi zaidi yaliyotokea kupitia runingani, usikose kuangalia Kipindi cha Wanawake Live cha EATV.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio la kuolewa kwa mtoto huyo, serikali ya Rais Jakaya Kikwete kupitia Jeshi la Polisi chini ya IGP Said Mwema wanatakiwa kuchukua hatua kali dhidi ya watu wanaofanya ukatili katika jamii hasa kwa watoto wasio na hatia. 


kwa hisani ya Mpekuziblog.

Article 10

$
0
0
WAKAZI WA ISANGA MBEYA WAINGILIWA NA MAGUFULI.
 
Baadhi ya  ya wakazi wa Isanga Mbeya wakiwa hawaamini kinachotokea










Zoezi la Bomoa Bomoa Limehamia Jijini Mbeya Huku wananchi wakiwa Hawa amini Kinachotokea.












kwa hisani ya Mbeyayetublog

MGOGORO WA MADINI ULIWA NJOMBE WATATULIWA.

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba.

Na Michael Ngilangwa Njombe.

Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi Sara Dumba Amewataka Wachimbaji Wadogo wa Madini Wilayani Njombe Kuzingatia Taratibu za Kuomba Leseni Kwa Wakati Kabla ya Kuanza Shughuli za Uchimbaji Ili Kuhepusha Migogoro Inayotokana na Wachimbaji Wengi Kutozingatia Taratibu Zilizopo Katika Uchimbaji wa Madini.

Aidha Mkuu Huyo wa Wilaya Pia Amewataka Maafisa wa Madini Kuwasaidia Waombaji wa Leseni Kwa Uadilifu na Kwa Kuzingatia Maadili ya Utumishi wa Umma Jambo Ambalo Linapaswa Kutekelezwa na Maafisa Hao Ili Kupunguza Migogoro Hiyo.

Akisoma Taarifa ya Mgogoro wa Uchimbaji Madini Katika

Kijiji Cha Uliwa Wilayani Njombe,Mbele ya Makamishna wa Madini Kanda ya Nyanda za Juu Kusini,Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba Amesema Kwa sasa Mgogoro Huo Tayari Umeshapatiwa Ufumbuzi Baada ya Pande Zote Kukutanishwa na Kufikia Muafaka Kuhusu Uchimbaji wa Madini Katika Kijiji Hicho.

Amesema Serikali Itaendelea Kusikiliza Kero za Wananchi na Kuhakikisha Inazipatia Ufumbuzi Kadiri Inavyowezekana Huku Akitoa Angalizo Kwa Viongozi wa Vyama Vya Siasa Kuwaeleza Ukweli Wananchi Kuhusu Mambo Yanayojitokeza Katika Maeneo Yao.

Kwa Upande wake Kamishna Msaidizi wa Utoaji wa  lesseni za Madini Kanda ya Kusini John Nayopa Amewataka Watafiti na Waombaji wa Lesseni za Uchimbaji wa Madini Mkoani Njombe Kuhakikisha Wanazingatia Taratibu Zilizopo Ili Kuhepuka Migogoro ya Mara Kwa Mara.
............................................................................................................................

Article 8

$
0
0

DADA YAKE FREEMAN MBOWE AIKIMBIA CHADEMA NA KUJIUNGA CCM.

Picture: Grace Mbowe, Hassan MtengaKatibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro, Hassan Mtenga kushoto akimkabidhi yadi ya CCM, Grace Mbowe, baada ya kutoka CHADEMA kwa kile alichodai hakuna jambo jipya.

 Grace amesema amehama kutokana na kuwepo propaganda zisizotekelezeka. Hata hivyo, amesisitiza kwamba kuwepo kwake katika Chadema, siyo kwa sababu ya familia.

Alikabidhi kadi hiyo jana kwenye ofisi za CCM Wilaya ya Hai. Alisema itikadi za kisiasa, zisihusishe masuala ya kifamilia, kwani upendo wao uko pale pale.


DADA wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Grace Mbowe, amejiunga na Chama Cha Mapinduzi ( CCM) akitokea Chadema, kwa kile alichodai haoni jambo jipya katika chama hicho.

Grace amesema amehama kutokana na kuwepo propaganda zisizotekelezeka. Hata hivyo, amesisitiza kwamba kuwepo kwake katika Chadema, siyo kwa sababu ya familia.

Alikabidhi kadi hiyo jana kwenye ofisi za CCM Wilaya ya Hai. Alisema itikadi za kisiasa, zisihusishe masuala ya kifamilia, kwani upendo wao uko pale pale.

Alisema kilichomfanya kujiunga na chama hicho ni utashi wake. Alidai CHADEMA wanafanya propaganda za
kuwadanganya wananchi.

Alisema itikadi za chama, haziwezi kuingilia masuala ya kifamilia, hivyo kwake siyo ajabu kuondoka CHADEMA, kwani kila mtu ana utashi wake wa kisiasa.

“Nimeamua kwa hiari yangu mwenyewe bila kushawishiwa na mtu, ndio maana nimetoka Dar es Salaam kuja Hai kwa ajili ya kurejesha kadi ya CHADEMA na kujiunga na CCM, suala la itikadi lisihusishe masuala ya kifamilia kwani upendo wetu upo palepale,”alisema Mbowe.

Alisema, “kuwapo kwangu CHADEMA siyo kwa sababu ya familia, hivyo hakuna wa kunizuia, natoka kwa utashi wangu, na tutaendelea kuheshimiana na mdogo wangu Freeman Mbowe katika masuala ya kifamilia.”

“Freeman Mbowe ni mdogo wangu wa kuzaliwa kabisa, hakunishawishi kuingia CHADEMA, hivyo sioni haja ya kuendelea kubaki huku wakati sioni jambo jipya, mimi tangu naifahamu CCM iko vile vile, bali propaganda za upinzani ndizo zinawalaghai wananchi,” alisema.

 
Aliviasa vyama vya siasa, kuwa sasa umefika wakati wa kuacha malumbano na maandamano ya itikadi, yasiyokuwa na faida yoyote, badala yake huu ni muda wa kujenga nchi kwa ushirikiano.

Awali, akipokea kadi ya CHADEMA, Katibu wa CCM Wilaya ya Hai, Hassan Mtenga alisema alichokifanya Grace ni uamuzi wa busara, baada ya kutazama Chadema ilipo na inapokwenda.

Alisema wimbi la wanachama wa Chadema kurudisha kadi na kujiunga na CCM, limekuwa kubwa wilayani Hai. Alisema tangu Januari hadi sasa amepokea wanachama 530.

Mtenga aliwataka wananchi kutambua kwamba Jimbo la Hai, siyo kitovu cha upinzani bali CHADEMA ni chama kilichotoa upinzani kwa CCM katika uchaguzi mkuu wa 2010. Alisema hali hiyo, ilitokana na makundi ya CCM.

Alisema kwa sasa watu asitarajie tena suala hilo kutokea. --- via HabariLeo

Article 7

$
0
0

MAKATIBU WA CCM WA WILAYA WALIOTEULIWA hawa hapa.




 UTEUZI
Kikao cha Halmashauri Kuu pia kimeridhia, uteuzi wa Makatibu wateule wapya wa Jumuiya za CCM, za Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Jumuia ya Wazazi na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).

Katika uteuzi huo mapendekezo hayo yaliyofanywa na Kamati Kuu ya CCM na kuridhiwa na NEC, kwa upande wa UVCCM ameteuliwa aliyekuwa Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, Sixtus Mapunda na kwa upande wa Jumuia ya Wazazi ni Mjumbe wa NEC kutoka Pemba, Seif Shabani Mohamed, huku kwa upande wa UWT akiachwa Katibu Mkuu wa sasa, Amina Makilagi.

Mapunda atachukua nafasi iliyokuwa imneshikiwa na Martine Shigela ambaye ameongoza UVCCM kwa miaka mitano sasa, na Seif Shabani Mohammed kutoka Pemba akichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Hamis Suleiman Dadi ambaye pia amekuwa katika wadhifa kwa miaka mitano sasa.

Pia, NEC imeridhia mapendekezo  ya Kamati Kuu kwa ajili ya kuziba nafasi Makatibu wa CCM wa mikoa mitatu ya Morogoro, Kaskazini Pemba na Geita ambayo kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa imekuwa wazi kwa muda mrefu sasa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo.

Kufuatia mapendekezo hayo ya Kamati Kuu, ambayo yameridhiwa na NEC, walioteuliwa na mikoa yao ikiwa kwenye mabano ni Msaidizi Kitengo cha  Uchaguzi, CCM Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Romuli Rojas John (Morogoro), aliyekuwa Katibu Katibu wa wilaya ya Mkinga, Kassim Mabrouk Mbarak (Kaskazini Pemba) na aliyekuwa Katibu wa CCM Igunga, Mary Maziku (Geita).

Kuhusu sakata la madiwani wa Bukoba mjini, CCM imesema suala hilo, linaendelea kushughulikiwa ambapo baada ya kikao hicho cha NEC, Kamati kuu iliendelea kukutana na viongozi wa wilaya ya Bukoba, Mwenyekiti wa CCM na Katibu wa wilaya hiyo.

Mapema kabla ya kikao cha NEC, Kamati Kuu ilikutana na Mbunge wa Bukoba mjini Khamis Kagasheki na Meya wa Manispaa ya Bukoba mjini na kuwahoji, wakati jana Kamati Kuu ilikutana na  Mwenyekiti na Katibu wa CCM mkoa wa Kagera.

Taarifa Rasmi ya CCM ya majina ya Makatibu wa Wilaya walioteuliwa na NEC
 
Ndugu Ashura Amanzi
Ndugu Rukia Saidi Mkindu
Ndugu Elias J. Mpanda
Ndugu Jonathan M. Mabihya
Ndugu Mulla Othman Zuberi
Ndugu Jumanne Kapinga
Ndugu Ali Haji Makame
Ndugu Jacob G. Makune
Ndugu Juma A. Mpeli
Ndugu Hawa Nanganjau
Ndugu Abdulrahman Shake
Ndugu Subira Mohamed Ameir
Ndugu Abdallah Shaban Kazwika
Ndugu Juma Bakari Nachembe
Ndugu Josephat Ndulango
Ndugu Rajab Uhonde
Ndugu Abeid Maila
Ndugu Mohamed Lawa
Ndugu Mariam Sangito Kaaya
Ndugu Bakar Lwasa Mfaume
Ndugu Julius Peter
Ndugu Jumanne Kitundu Mginga
Ndugu Mathias Nyombi
Ndugu Mohamed Hassan Moyo

Article 6

$
0
0

JK AMUAPISHA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA JAJI FRANCIS MUTUNGI .



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mzee James Mapalala baada ya kumuapisha Msajili wa Vyama vya Siasa mpya Jaji Francis Mutungi (kushoto) Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii




Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Msajili wa Vyama vya Siasa Mstaafu Jaji Francis Mutungi (kushoto) na Msajili wa Vyama vya
Siasa Mstaafu Mhe John Tendwa katika picha ya kumbukumbu baada ya kumuapisha Jaji Mutungi Ikulu jijini Dar es salaam leo



Kwa hisani ya Michuziblog

SAKATA LA TRAFIKI FEKI LAFIKISHWA MAHAKAMANI.

$
0
0

 

 
JAMES Hussein, mkazi wa Kimara, Dar alikuwa na wakati mgumu wa kukwepa kamera zilizotua Mahakama ya Wilaya Ilala, jijini Dar juzi baada ya kufikishwa kwa kosa la kujifanya trafiki.

Tukio hilo lilijiri mahakamani hapo Agosti 22, mwaka huu ambapo mshitakiwa alikana mashitaka mbele ya Hakimu Mfawidhi, Joyce Minde.


Trafiki feki huyo alitumia muda mwingi kujificha sura ili kamera zisimchukue lakini alichemsha kwani kila alipojifunua kidogo alikuta kamera ziko mbele yake.

Hali hiyo ilimfanya mshitakiwa huyo aamue kujiachia kwa kutoa kofia aina ya kapelo kichwani na picha za kumwaga kupatikana.

Akisoma mashitaka hayo, Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Nassoro Katuga alisema mnamo Agosti 14, 2013, huko Tabata Kinyerezi Mnara wa Voda, Dar, mtuhumiwa alikutwa amevaa nguo za askari wa usalama barabarani akijifanya ni mwajiriwa wa jeshi la polisi jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Hata hivyo, mshitakiwa alipelekwa rumande Segerea, hadi Septemba 5, 2013 baada ya kukosa wadhamini wawili kwa shilingi milioni kumi na nne.

SERIKALI WILAYANI NJOMBE KUPAMBANA NA WAHARIBIFU WA VYANZO VYA MAJI SASA.

$
0
0

Haya ni Badhi ya  maeneo yanayo Limwa na wananchi wa Mtaa wa Maheve Karibu na Vyanzo vya Maji Mjini Njombe.
 
Na Prosper Mfugale Njombe

Serikali Wilayani Njombe Imesema Itaendelea Kuwachukulia Hatua za Kisheria Wananchi Ambao Wanaendelea na Shughuli za Kilimo Kwenye Maeneo ya Vyanzo Vya Maji na  Kusababisha Uharibifu wa Mazingira.

Kauli Hiyo ya Serikali Imekuja Kufuatia Malalamiko ya Baadhi ya Wananchi na Wadau Kudai Kuwa Sheria ya Utunzaji wa Vyanzo Vya Maji Inayokataa Kuendesha Shughuli za Kiuchumi Ikiwemo Kilimo Kwa Umbali Mita Sitini Kutoka Chanzo cha Maji Kuwa Inapelekea Wananchi Hao Kukosa Mavuno ya Uhakika.

Akiongea na Kituo Hiki Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sara Dumba Amesema Zinahitajika Jitihada Zaidi Katika Utunzaji wa Mazingira Hasa Vyanzo Vya Maji Ili Kukabiliana na Tatizo la Ukame Linaloanza Kujitokeza Kufatia Wananchi Wengi Kuendesha Shughuli za Kiuchumi Kando ya Vyanzo Vya

Maji Pamoja na  Kupanda Miti Ambayo Si Rafika na Vyanzo Hivyo.

Kwa Upande Wao Baadhi ya Wananchi na Wadau Hao Wamesema Uharibifu wa Mazingira Pamoja na Vyanzo Mbalimbali Vya Maji  Inasababishwa na  Baadhi ya Watu na Makampuni Yanayopanda Miti Ambayo Si Rafiki na Vyanzo Vya Maji.

Licha ya Kuwa Wilaya ya Njombe ni Miongoni Mwa Wilaya Zenye Vyanzo Vingi Vya Maji na Mvua za Kutosha Lakini Wilaya Hiyo Inakabiliwa na Tatizo la Upatikanaji wa Maji ya Uhakika Kwa Muda Mrefu .

UTATA WA MASHAMBA KWA WAKULIMA WANGAMA WILAYANI WANGING'OMBE WASULUHISHWA.

$
0
0
Maeneo ya Kujenga Makao Makuu wanging'ombe yaanza Kupimwa.
Na Gabriel Kilamlya Wanging'ombe

Zoezi la Ugawaji Mashamba ya Wakulima waliokubali Kupisha Eneo la Kujenga Ofisi za Makao Makuu ya Wilaya ya Wanging'ombe Limetajwa Kuendelea Vizuri kwa Wananchi wa Igwachanya baada ya Zoezi Hilo Kukamilika Kwa wananchi wa Kijiji cha Chalowe.

Akizungumza na Kituo hiki Kaimu Mwenyekiti wa Kijiji cha Igwachanya Bwana Petro Ndone Amesema Kuwa Jumla ya Ekari 12 zinaendelea Kutolewa katika Maeneo Mbalimbali ya Vitongoji vya Kijiji cha Igwachanya  kwa wananchi sita Ambao ni Miongoni mwa Wakulima waliokuwa wakilima Katika Eneo la Ujenzi wa Makao Makuu ya Wilaya ya Wanging'ombe.

Mwenyikiti Ndone Amesema Kuwa Wananchi watatu walipewa Mashamba hayo Jana Katika Kitongoji cha Makungu na Leo zoezi hilo linaendelea Kukamilishwa kwa Wananchi watatu Waliosalia Katika

Kitongoji cha Igombatavangu .

Katika Hatua Nyingine Amesema Kuwa Kukamilika kwa Zoezi hilo bila Tatizo kutapelekea zoezi la Ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Wilaya Hiyo Kwenda Vizuri kwani Hadi sasa Upimaji wa Maeneo unaendelea Vizuri.

Yob Sahara ni Miongoni mwa wananchi wanaoendelea Kupatiwa Maeneo hayo ambaye Amepongeza hatua ya Serikali Kuwagawia Mashamba hayo hata Kama yanapatika mbali na Maeneo waliyokuwa wakiyalima.

Hata Hivyo Wananchi Hao wamesema kuwa Kitendo cha Serikali Kukubali Kuwaonesha Maeneo Mengine Kumewafanya kuacha Malalamiko waliyokuwa nayo hapo Awali hali iliyopelekea Kuyafikisha kwa Mbunge wao.

KATIKA HILI,UKIPANDA HUMO TUSILAUMIANE.

$
0
0
 
Kama ndege nazo husukumwa usalama utakuwaje???

Article 1

$
0
0
ACP Fulgency Ngonyan Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Amethibitisha Kutokea kwa Matukio Hayo.

Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Linawashikilia Watu Wawili Maria Kilasi na Charles Mbata Wakazi wa Wilaya ya Njombe Kwa Tuhuma Tofauti ,Ambapo Maria Kilasi Anatuhumiwa Kutupa Mtoto Mchanga Ndani ya Shimo na Kisha Kumfukia na Kusababisha Kifo cha Mtoto Huyo.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe ACP Fulgence Ngonyani Amesema Tukio Hilo Limetokea Agosti 26 Mwaka Huu Majira ya Saa Tano Asubuhi Katika Eneo la Mashujaa Mjini Makambako Baada ya Mbwa Kufukua Mwili wa Mtoto Huyo.

ACP Ngonyani Amesema Mnamo Agosti 23 Mwaka Huu Mtuhumiwa Alijifungua Mtoto wa Kiume na Siku ya Agosti 26 Mwaka Huu Alimfukia Ndani ya Shimo na  Kwamba Upelelezi Dhidi ya Tukio Hilo Linaendelea , Mtuhumiwa Atafikishwa Mahakamani Pindi Upelelezi Huo

Utakapokamilika. 

Katika Tukio Lingine Jeshi Jeshi Hilo Linamshikilia Charles Mbata Kwa Tuhuma za Kuchoma Moto Mali Mablimabli Ikiwemo Shamba la Miti Zaidi ya Hekari 50 Pamoja na Ng'ombe Watatu Zenye Thamani ya Shilingi Milioni 20 na Laki Tano Mali ya Bwana Kaini Nyigu.

Aidha Jeshi Hilo Pia Linawatafuwa Watuhumiwa Wengine Wanaotuhumiwa Kuhusika na Wizi wa Ng'ombe Watano  Wenye Thamani ya Shilingi Milioni Nne Mali ya Inocent Ngole Mkazi wa Mtaa wa Maheve.

Article 0

$
0
0
 

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi  wa CCM, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uamuzi wa kamati kuu wa kubatilisha kufukuzwa kwa madiwani wa Bukoba nje ya ukumbi wa NEC.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
 Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa imejadili na kutolea maamuzi pamoja na mambo mengine suala la Madiwani wanane waliotangazwa kufukuzwa uanachama na Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera.


Katika maamuzi yake, Kamati Kuu imebatilisha uamuzi uliofanywa na Halmashauri Kuu CCM ya Mkoa wa Kagera Agosti 13, 2013 wa kuwafukuza uanachama Madiwani hao. Hivyo Madiwani hao wanane ni wanachama halali wa CCM.


Kamati Kuu imetoa uamuzi huo, baada ya kubaini kuwa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera haikuzingatia Katiba ya CCM ya 1977 Toleo la 2012 Ibara ya

93 (15). Ibara hiyo inasomeka kuwa moja ya kazi ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa ni:-
“Kumwachisha au kumfukuza uongozi kiongozi yeyote ambaye uteuzi wake wa mwisho unafanywa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa, isipokuwa kwa suala la kumvua uanachama au uongozi Diwani lisifanyike hadi Kamati Kuu imearifiwa na kutoa maelekezo”.


Aidha, Kamati Kuu imewaonya Madiwani wa CCM wa Manispaa ya Bukoba, Mbunge wa Bukoba Mjini na Meya kwa kusababisha kukosekana kwa utulivu, mshikamano na amani katika Manispaa na Chama.


Kamati Kuu pia imeitaka Serikali kumwagiza mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali(CAG) kufanya ukaguzi maalum wa haraka wa mambo yanayolalamikiwa dhidi ya Meya ili ukweli ujulikane na matokeo ya uchunguzi huo yawasilishwe kwenye baraza la madiwani ili hatua stahiki zichukuliwe kwa mujibu wa sheria na taratibu zinazoongoza Serikali za Mitaa.


Wakati tuhuma hizo dhidi ya Meya zikichunguzwa; Kamati Kuu inawataka Madiwani wa CCM  kurejesha utulivu kwenye Manispaa na Chama kwa ujumla ili kufanikisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuwaletea maendeleo wananchi wa Bukoba.

Imetolewa na:-


Nape Moses Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM
ITIKADI NA UENEZI
27/08/2013

Article 4

$
0
0

MWIGULU NCHEMBA ATAKA MBOWE NA DR. SLAA WAKAMATWE KWA MAUAJI YA RAIA.

 MBUNGE wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba (CCM), amechafua hali ya hewa bungeni kwa kuitaka Serikali kuwachukuliwa hatua viongozi wa juu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Mbunge huyo alisema mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe pamoja na Katibu Mkuu wake, Dk. Wilbroad Slaa, wanapaswa kuchukuliwa hatua kwa madai ya kusababisha mauaji ya raia.

Mwigulu, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bara, alisema katika kipindi cha miaka miwili tangu nchi ilipotoka kwenye uchaguzi, viongozi hao wamekuwa wakihamasisha maandamano na kusababisha umwagaji wa damu za Watanzania.

“Mheshimiwa Naibu Spika, katika kipindi cha miaka miwili tangu nchi yetu ilipomaliza Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Mbowe na Dk. Slaa wamekuwa wakitoa kauli za wazi na hata kusababisha mauaji ya watu bila hatia.

“Kutokana na hali hii, sijui Serikali inafanya nini katika kuwachukulia hatua, kwani viongozi hawa wamekuwa wakitafuta umaarufu wa kisiasa kwa kuchochea chuki na mauaji dhidi ya raia.

“Kwa hali hiyo, tangu kipindi hicho hadi leo hii wanasubiri nini badala ya kwenda kuwaweka jela, kwani huko ndiko wanatakiwa kuwa,” alisema.

Mwigulu, alisema kukosekana kwa maadili kwa baadhi ya viongozi wa siasa, ambao wamekuwa wakitumia majukwaa na kuhubiri umwagaji damu ni hatari kwa taifa.

Alisema viongozi hao wamekuwa wakitumia majukwaa hayo na kusababisha vifo vya wananchi, huku akitaja vurugu zilizotokea katika mikoa ya Morogoro, Iringa, Arusha na Singida.

Akijibu swali hilo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika, alisema Serikali inafanya kazi kwa mujibu wa sheria, ikiwa ni pamoja na kukusanya ushahidi na kwamba mahakama ndicho chombo chenye uamuzi wa mwisho dhidi ya adhabu kwa raia au kiongozi yeyote wa kisiasa.

Kauli hiyo ya Mwigulu ilionekana kuchafua hali ya hewa ndani ya Bunge, ambapo Mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje (Chadema), alisimama na kuomba mwongozo wa Spika, huku akimtaka Mwigulu kuthibitisha kauli yake, vinginevyo aombe radhi.

Wenje alisema hoja ya Mwigulu imekosa mashiko na ina lengo la kuwadhalilisha viongozi wa Chadema, huku akisahau kuwa baada ya uchaguzi wa Arumeru Mashariki, aliyekuwa Mwenyetiki wa Chadema tawi la Usa River, Omari Mbwambo, aliuawa na watu anaodaiwa kuwa ni wafuasi wa CCM.

Awali katika swali la msingi, Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango (CCM), alitaka kujua Serikali inachukua hatua gani kwa wanasiasa wanaokiuka maadili na kusababisha uvunjifu wa amani.

“Wanataaluma kama vile madaktari, wahandisi, wahasibu na hata wakandarasi pindi wanapokiuka maadili ya kazi zao huchukuliwa hatua kwa kufutiwa leseni zao.

“Vile vile viongozi wa kisiasa wanayo maadili yanayowaongoza, kwanini pale wanapokiuka maadili ya kazi zao hawachukuliwi hatua kama ilivyo katika makundi hayo? (taaluma),” alisema Kilango.


-Mtanzania

Article 3

$
0
0
 Halmashauri ya Mji Njombe kwa Kushirikiana na Wananchi wameanza Kujenga Daraja lililoleta Mvutano Mkubwa.


 Kukosekana kwa Bajeti Halmashauri Kumepelekea Kujenga Daraja Hilo kwa Magogo Ujenzi unaopingwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe.


Wananchi wa Mitaa ya Kihesa na National Housingi Wameamua Kufanya Ukarabati wa Daraja Linaloiunganisha Mitaa Hiyo na Mji wa Njombe.

Wananchi Hao Wamefikia Hatua Hiyo Kufuatia Daraja Hilo Kuwa Bovu na Kuhatarisha Maisha ya Wakazi wa Mitaa Hiyo Wanaotumia Daraja Hilo Licha ya Uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Kuahidi Kulijenga Bila Mafanikio.

Akizungumza na Kituo Hiki Mwenyekiti wa Mtaa wa Kihesa Bi. Mary Mng'ong'o Amesema Daraja Hilo ni la Muda Wakati Taratibu za Ujenzi wa Daraja la Kudumu Zikiendelea na

Pindi Fedha Kwa Ajili ya Ujenzi Huo Zitakapopatikana.

Kwa Upande Wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Edwin Mwanzinga Amewataka Wananchi Kushiriki Kaika Shughuli za Maendeleo Ikiwemo Ujenzi wa Madaraja na Si Kutegemea Msaada Kutoka Serikalini.

Ukarabati wa Daraja Hilo Umekuja Ikiwa ni Siku Chache Tangu Halmashauri ya Mji wa  Njombe Kuahidi Kuwa Ifikapo Agosi 21 Mwaka Huu Litakuwa Limejengwa Ahadi Ambayo Haikuweza Kukamilika.


Article 2

$
0
0

GARI LA RC IRINGA YAGONGWA ,MWENYEWE ANUSURIKA

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dokta Christine Ishengoma Anusurika kwenye Ajari Mkoani Iringa.
MKUU WA MKOA WA IRINGA MHE DKT. CHRISTINE ISHENGOMA (MB.ANUSURIKA AJALI BAADA YA GARI LAKE KUGONGWA NA DALADALA YENYE NAMBA ZA  USAJILI T 163 CBE. PAMOJA NAE ALIKUWA NA KAIMU KATIBU WAKE DENNIS GONDWE NA DEREVA WAKEHAMID UGULUMU,katika hajali  hiyo hakuna madhara yoyote kwa binadamu
kwa hisani ya francisgodwinblog

Article 1

$
0
0

TRAFIKI FEKI MAZITO TENA ADAIWA KUWA ALIKUWA MFUNGWA.

MAZITO tena yameibuka kuhusu yule trafiki feki James Hussein, mkazi wa Kimara Matangini, jijini Dar es Salaam ambaye yuko  Gereza la Segerea, Dar akikabiliwa na kesi ya kujifanya askari wa usalama barabarani
.                          Trafiki feki James Hussein akiwa kwenye gari baada ya kunaswa.
Habari za ndani kutoka Gereza la Isanga, Dodoma zinadai kuwa, trafiki huyo ana mambo mengi ya kushangaza ambayo Watanzania wengi hawayajui.
JINA HALISI
Mtoa habari wetu alisema kuwa, James Hussein si jina halisi la trafiki feki huyo. Alisema jina lake halisi ni Ali Kinanda

 .                           Mtuhumiwa huyo akiwa na watuhumiwa wenzake.
“Yule jamaa anaitwa Ali Kinanda, sisi kumwona kwenye picha gazetini akijiita James Hussein tulishangaa sana,” kilisema chanzo chetu.
YADAIWA ALIKUWA ASKARI MAGEREZA
Chanzo kikazidi kudai kwamba, kuanzia mwaka 1984 jamaa huyo alikuwa ni askari magereza katika Gereza la Butimba, Mwanza hadi mwaka 1987 alipoacha.

                                                   Akiwa mikononi mwa polisi.
ADAIWA KUNASWA UJAMBAZI, ATUPWA JELA MIAKA 30
Mtoa habari wetu aliendelea kumwanika trafiki feki huyo kuwa, mwaka 2002 mtuhumiwa huyo alidaiwa kupata msala wa tukio la ujambazi lililotokea Mpwapwa, Dodoma ambapo kesi yake iliunguruma hadi mwaka 2003 ambapo hukumu ilitolewa yeye na wenzake kwenda jela miaka 30.
 “Mwaka 2002 mpaka 2003, Kinanda alipata kesi ya ujambazi akiwa na wenzake, sikumbuki idadi yao. Kesi iliisha kwa hukumu ya miaka 30 jela kwenye Gereza la Isanga hapa Dodoma,” alisema mnyetishaji huyo.
“Akiwa gerezani, Kinanda alionekana mtiifu kiasi kwamba alipewa cheo cha kusimamia wenzake, yaani mnyapara wakiamini anaendelea vizuri na kifungo chake hicho.

                                                 Trafiki feki katika pozi baada ya kudakwa.
“Hakuna aliyejua kama jamaa anaweza kutoroka. Ama kweli moyo wa mtu anaujua mwenyewe. Hivi hapa (Gereza la Isanga) wafungwa wenzake wameshangaa kusikia jamaa amekuwa trafiki huko Dar es Salaam,” kilidai chanzo.
ADAIWA KUTOROKA JELA
Habari zaidi ziliendelea kudai kwamba, Desemba 10, 2012 akiwa gerezani, mfungwa huyo alitoroka katika mazingira ya kutatanisha akiwa chini ya uangalizi wa askari magereza aliyejulikana kwa jina moja la Shaibu.
Ilidaiwa kuwa, baada ya picha yake kuonekana kwenye gazeti, askari magereza wa Isanga waliutaarifu uongozi mara moja ambapo nao ulituma wachunguzi  jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuanza mchakato wa kumtia mikononi mfungwa huyo ili akamalizie kifungo chake cha miaka thelathini jela.
Inadaiwa kuwa, wachunguzi hao ambao ni askari magereza  wapo Dar wakisubiri siku ya kesi ya kujifanya trafiki itakapopelekwa kusikilizwa kwa hakimu.

 HABARI MPYA, ADAIWA KUFARIKI DUNIA SEGEREA, DAR
Wakati mnyetishaji wetu kutoka gerezani Isanga Dodoma akianika madai ya siri hiyo nzito, Agosti 26, mwaka huu jijini Dar es Salaam, Mwandishi Wetu, Makongoro Oging’  alipata taarifa kuwa, mtuhumiwa huyo wa kutenda kosa la kujifanya trafiki amefariki dunia ghafla akiwa gerezani Segerea.
Ilibidi mwandishi wetu amtafute Msemaji wa Jeshi la Magereza Tanzania, Meja Mtiga Omar na kumuuliza kuhusu madai hayo ya kifo ambapo alisema:

 “Si kweli kwamba amekufa, bali ana tuhuma nyingine ya kutoroka gerezani ambapo tutamfungulia mashitaka mengine  ya kutoroka akiwa gerezani anatumikia kifungo chake.”
Juhudi za kumpata Mkuu wa Gereza la Isanga, Dodoma zilishindikana baada ya simu yake ya mkononi kuita kwa muda mrefu bila kupokelewa.
James Hussein kama ndiye Ali Kinanda yupo Gereza la Segerea, hadi Septemba 5, 2013 kesi yake itakaporudi tena mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Joyce Minde kwa ajili ya kusikilizwa.

Article 0

$
0
0

ASKOFU KULOLA wa EAGT TANZANIA AFARIKI DUNIA.


IMG_0602Photo0086 
Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God hapa nchini Dk.Moses Kulola siku za hivi karibuni
 
Na salesi Malula
 
Askofu Mkuu wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God hapa nchini Dk.Moses Kulola amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Taarifa za kifo cha askofu huyu maarufu zimetolewa na mtoto wake Mwiinjilisti Daniel Kulola ambaye ameitoa kupitia mtandao wa face book ambapo ameueleza umma wa watanzania kuwa baba yake mzazi amefariki dunia katika hospitali ya Aga khani ambako alikuwa amelazwa.

Hajaeleza marehemu alikua anaumwa nini lakini taarifa zinasema amekuwa mgonjwa siku nyingi ambapo aliwahi kulazwa nje ya nchi na baadae akarudishwa nchini na hatimae kufariki Dunia.

Hadi hivi sasa haijajulikana askofu kulola atazikwa lini lakini pia taarifa zimethibitishwa rasmi kutoka kwa wachungaji mbalimbali ambao wako chini ya kanisa lake ambalo lina mtandao nchi nzima na lenye waumini zaidi ya milioni 5 nchini kote.

 Moses Kulola, alizaliwa mwezi Juni 1928, katika familia ya watoto kumi, na watano kati yao bado ni hai. alisajiliwa katika shule  ya kwanza mwaka 1939 iitwayo Ligsha Sukuma shule ya misheni baada ya Ligsha, alijiunga na taasisi ya usanifu mwaka 1949. Alibatizwa mwaka 1950 katika Kanisa la AIC Makongoro.

Alimwoa Elizabeth na wamezaa  watoto 10 ambapo saba bado hai.
Alianza kazi za kimisionari mwaka1950 japokuwa aliitwa mwaka 1949 mara tu baada ya kubatizwa. Mwaka 1959 alianza kufanya kazi serikalini, wakati huo huo akihubiri Injili katika miji na vijiji. 
Utumishi wake mkubwa kwa nchi ulifika mwisho mwaka 1962, ambapo aliamua kujitolea moja kwa moja nguvu zake zote, mwili na nafsi. Mwaka 1964 alijiunga na chuo cha kiteolojia na 1966 alitunukiwa stashahada.

Hakuacha elimu pale tu, aliendelea na masomo mbalimbali ambapo alitunukiwa vyeti mbalimbali katika mataifa mbalimbali.

Alihudumu kikazi kwa miaka miwili kama Mchungaji kabla ya kuwa mpentekoste mnamo 1961-1962, alifanya kazi katika kanisa la TAG 1966 mpaka 1991 ambapo aliamua kuanzishaa makanisa Evangelistic Assemblies God (EAGT), ambapo yalifanikiwa kukua kwa kasi kubwa katika nchi za Tanzania, Zambia , Malawi na kwa ujumla kuna makanisa yapatayo 4000 katika nchi mbalimbali yakiwemo makubwa na madogo.


Askofu Moses Kulola anayeongoza makanisa elfu nne, Askofu Msaidizi wake ni Mwaisabila.
 
  Mchakato wa kuongoza makanisa elfu nne si rahisi na kwamba kumefanyika mgawanyiko wa majimbo yasiyopungua 34 ya kazi na kanda tano kwa ajili ya kurahisisha kazi na kila kanda na jimbo lina mwangalizi wake.

 Nampenda sana Askofu Moses Kulola maana anafanya kazi ya MUNGU kwa moyo na kwa mujibu wa kitabu cha historia yake Askofu Kulola amezunguka Tanzania nzima tena wakati mwingine kwa kutembea kwa miguu na kwenye mazingira magumu sana kiasi kwamba ni wito mkuu wa MUNGU mkuu alionao Askofu Kulola na kwa miaka zaidi ya 60 amekuwa akihubiri neno la MUNGU na hadi sasa MUNGU anamtumia sana,

 katika mkutano uliopita wa askofu Kulola pale viwanja vya jangwani jijini Dar es salaam maelfu ya watu walihudhulia na wengi sana kufunguliwa na injili anayohubiri askofu Kulola na injili iliyonyooka na akiwataka wanadamu kumpa YESU KRISTO maisha yao ili wapate uzima wa milele bure.

MUNGU ambariki sana mtumishi wake huyu ni mfano hai kwa watumishi wa MUNGU wa sasa
Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina la Bwana libarikiwe( Na Fullshangwe Blog)
Viewing all 2276 articles
Browse latest View live