Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all 2276 articles
Browse latest View live

Article 0

$
0
0
VURUGU MAANDAMANO YA CHADEMA JIJINI MWANZA.











MAANDAMANO ya amani yaliyokuwa yameandaliwa na chama cha demokrasia na maendeleo(chadema) yamegeuka shubiri kwa wakazi wa jiji la Mwanza baada ya kuibuka mapambano makali baina ya waandamanaji hao na jeshi la polisi mkoani Mwanza na kusababisha polisi kutumia nguvu kuwatawanya wafuasi wa chama hicho.

Maandamano hayo ya amani ambayo yalianzia katika eneo la Buzuruga nje kidogo ya jiji la Mwanza yalikuw ayakiongozwa na wabunge Highness Kiwia wa Ilemela  pamoja na Ezekiel Wenje kuelekea katika viwanja vya Furahisha yalilenga kumshinikiza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ernest Ndikilo kutoa barua zinazodaiwa kuandikwa na ofisi ya Waziri Mkuu Tamisemi kuwarejesha madiwani watatu waliotimuliwa katika Manispaa ya Ilemela kutokana na kushindwa kuhudhuria vikao vitatu mfululizo.

Polisi wenye silaha pamoja na askari kanzu walianza kutanda katika eneo hilo la Furahisha wakiongozwa na Mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Mkoa wa Mwanza RCO Konyo ambaye alikuwa akitumia gari lenye namba za usajili DK 068EXV aina ya Toyota Land Cruiser

Maandamano hayo ambayo awali yalionekana kana kwamba yangelimalizika salama yaliwasili katika viwanja vya Furahisha majira ya saa 5.38 huku yakiongozwa na gari la polisi lenye namba za usajili za nchi ya Uganda  779 UAG likiwa nimesheheni polisi wenye silaha nzito ikiwa ni pamoja na mabomu ya machozi na bunduki pamoja na askari kadhaa ambao walikuwa katikati ya maandamano hayo.

Baada ya maandamano hayo kuwasili katika viwanja vya Furahisha kwa amani,waandamani hao ambao walikuwa na mabango mbalimbali yaliyosomeka kuwa ‘Matata hatutaki uendelee kuwa Meya wa Ilemela rudia kazi yako ya awali, na jingine Jaji Sumari tumechoka kuahirisha mara kw amara kesi dhidi ya Matata na jingine  lililosomeka kuwa RD Ndikilo tunahitaji barua za kurejeshwa kwa madiwani wetu.

Hata hivyo tofauti na ilivyokuwa imetangazwa kuwa maandamano hayo ya amani yangelipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ernest Ndikilo,hakukuwa na kiongozi yoyote wa Serikali ambaye alikuwepo uwanjani hapo kupokea maandamano hayo.

Kufuatia kutoonekana kwa kiongozi yoyote wa Serikali,viongozi wa chadema pamoja na wabunge wao walikutana kwa faragha kwa dakika kadhaa kwa ajili ya kujua hatima ya maandamano hayo ambapo Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje alipanda jukwaani saa 6.45 na kuwaeleza maelfu ya waandamanaji kuwa wameamua kumtuma Mbunge wa Ilemela Highnes Kiwia kwenda ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kuchukua majibu kwa ajili ya kuwaletea wananchi walioandamana juu ya hatima ya madiwani hao.

Hata hivyo saa moja baadae Mbunge huyo alisimama jukwani na wakuwaeleza waandamani hao kuwa simu ya Mbunge Kiwia ilikuwa haipatikani hivyo kuwataka kuandamana kwenda kwa Mkuu wa mkoa wa Mwanza kujua kulikoni na hapo ndipo hali ya hewa ilipochafuka.

Jeshi la polisi baada ya kuona wandamanaji hao wameanza kuelekea katika ofisi za Mkuu wa mkoa liliwataka kutawanyika ambapo waandamanaji hao walikaidi ndipo jeshi la polisi lilipoamua kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi hao.

Vurugu hizo ambazo zilianza majira ya saa 7.30 zilisababisha kufungwa kwa baadhi ya barabara kutokana na waandamanji hao kuweka vizuizi vya mawe na kuchoma matairi,ambapo pia maduka na ofisi mbalimbali zililazimika kufungwa kwa muda kupisha vurugu hizo.

Baadhi ya wananchi ambao walikuwa wakitumia usafiri wa umma walionekana wakishuka kupitia katika madirisha ya magari hayo na kukimbia kwa hofu ya kujeruhiwa na mabomu pamoja na mawe ambayo yalikuwa yakirushwa na waandamanji hao kwa jeshi la polisi.

MKUU WA MKOA WA MWANZA ALONGA.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza akizungumza na Mbunge Kiwia pamoja na viongozi wa chadema ofisini kwake alisema kuwa ameshangazwa na uvumi huo kuwa ofisi yake imekalia barua  kurejeshwa kwa madiwani Abubakar Kapera(Nyamanoro),Dan Kahungu(Kirumba) pamoja na Marietha Chenyenge(Ilemela).

RC Ndikilo alisema kuwa Serikali imekuwa ikifanya kazi zake kwa maandishi na sio kwa kufuata maneno ya mtaani na kueleza kuwa hana barua yoyote toka ofisi ya Waziri Mkuu inayomualifu kuhusu kuwarejesha madiwani hao baada ya kukata rufaa.

“Hata Mbunge kuna siku ulinipigia simu ukiniuliza juu ya kuwepo kwa barua hizo name nilikujibu kuwa kwa kuwa uko hapo Bungeni Dodoma ambapo pia kuna ofisi ya Waziri Mkuu nilikujibu kuwa ni muhimu ukawaona viongozi wakuu wa Tamisemi ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu,pia nilikushauri kuwa wakupe japo nakala ya barua hiyo”,alisema RC Ndikilo.

“Lakini cha kushangaza nimekuwa nikisikia maneno ya ajabu kuwa nimeficha barua za madiwani hao,ikumbukwe kuwa madiwnai hao hawakukata rufaa kwangu bali walikata rufaa ngazi ya juu kabisa,ili kukata mzizi wa fitina naomba kati ya tarehe 26 hadi 27 wewe Mbunge pamoja na mimi twende TAMISEMI kukutana na viongozi ili kukata mzizi wa fitina na tuje tuwaeleze wananchi ukweli uliopo”,alisema RC Ndikilo.

Kuhusu suala la Meya Henry Matata kutoondolewa madarakani RC Ndikilo alisema kuwa hawezi kulizungumzia suala hilo kw akuheshimu mamlaka ya mahakama na kuwataka chadema kuvuta subira hadi pale mahakama itakapotoa maamuzi yake.

KAULI YA MBUNGE KIWIA.

Akizungumza katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Kiwia alisema kuwa waliamua kuitisha maandamano hayo kutokana na kuelezwa na Waziri Hawa Ghasia kuwa tayari barua hizo zimeishatumwa mkoani Mwanza.

“Mheshimiwa Mkuu wa mkoa hawa madiwani waliosimamishw ani wawakilishi wa wananchi,wamekaa nje kwa miezi saba sasa na uchaguzi wa Meya haukuwa halali ndio maana tuliamua kuitisha maandamano kwa ajili ya kuhakikisha madiwani hawa wanarejeshwa.

RPC MANGU.

Akizungumza kwa simu juu ya kutokea kwa vurugu zilizosababisha kupigw akwa mabomu ya machozi,Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Ernest Mangu alisema kuwa polisi walifanikiwa kudhibiti vurugu hizo na hadi sasa hawezi kusema ni wananchi wangapi ambao walikamatwa kuhusu vurugu hizo.

WANANCHI WAWALAUMU VIONGOZI NA WANASIASA NA KUWAPONGEZA POLISI.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na Mtanzania juu ya vurugu zilizotokea waliwaonyoshea kidole wanasiasa pamoja na viongozi wa mkoa wa Mwanza kutokana na kushindwa kusema ukweli juu ya tukio hilo.

Baadhi walisikika wakisema kuwa kama barua zipo kweli madiwani hao wanapaswa kupewa na kama azipo basi walioeneza maneno hayo wachukuliwe hatua kali kutokana na uchochezi.

Wananchi hao pia walilipongeza jeshi la polisi kutokana na kutumia busara badala ya nguvu kuhakikisha maandamano hayo yanakuwa ya amani. http://peruzibongo.blogspot.com


Article 4

$
0
0
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Acp Fulgency Ngonyan Akithibitisha Kutokea kwa Vifo Hivyo.

Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limethibitisha Kutokea kwa Vifo vya  Watu Wanne Katika Matukio Matatu Tofauti Likiwemo la  Ajali ya Gari  Aina ya Mitsubishi Fuso Lililowagonga waendesha Pikipiki wawili na Kusababisha Vifo  Papo Hapo.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Njombe ACP Fulgency Ngonyani Amesema Tukio la Kwanza Limetokea Agosti 19 Mwaka Huu Majira ya Saa Tatu na Dakika Kumi Usiku Katika Mtaa wa Melinze Mjini Njombe Ambapo Gari Lenye Namba za usajili T 862 AAD   Mali ya Zakaria Mbilinyi ILiyokuwa  Ikiendeshwa na Henry Ngimbudzi Mwenye Umri wa Miaka 35 Mkazi wa Makambako  LilimgongaMwendesha  Pikipiki  Aina ya T Better Yenye Namba za Usajiri T. 420 BNW  Iliyokuwa Ikiendeshwa na Michael Kiombo  Mwenye Umri wa Miaka 21 na  Mkazi wa Mji Mwema na  Abiria Aliyefahamiki kwa Jina la  Deogratias Mwenye Umri wa Miaka 20  Mkazi wa  Mjimwema Ambao wote walifariki Dunia.

Aidha Kamanda Ngonyani Amesema Ajali Hiyo Pia Imesababisha Majeruhi kwa Watu  Watano Ambao wamelazwa Katika Hospitali ya Kibena Huku Dereva Aliyesababisha Ajali Hiyo Akitokomea Kusiko Julikana na Chanzo cha Ajali Hiyo Kinaendelea Kuchunguzwa.

Kamanda Ngonyani Pia  Amewataja Majeruhi Watano wa Ajali Hiyo waliokuwemo kwenye Gari  Aina ya Toyota Mark ii Lenye Namba za Usajiri T.771 AWC Lililokuwa Likiendeshwa na Keneth Mng'ong'o Mwenye Umri wa Miaka 23 na Abiria Wengine Waliofahamika kwa Majina Sostenes Magembo Mwenye 

Umri wa Mwaka 1 na Miezi 7 MKazi wa Kijiji cha Lwangu,  Elasto Mayemba Mwenye Umri wa Miaka 30 Mkazi wa Gongo la Mboto DSM ,Henry Kiwale Mwenye Umri wa Miaka 41 Mkazi wa Njombe, Cresencia Kihindo Mwenye Umri wa Miaka 64 Mkazi wa Lwangu , Deus Mwinami,Richard Mwalongo Mwenye Umri wa Miaka 24 Mkazi wa Makambako  na Samweli Mkombo  mwenye Umri wa Miaka  30 Mkazi wa Luponde.

Katika Tukio Jingine Kamanda wa Polisi Amemtaja Danford Mkongwa   Mwenye Umri wa Miaka 46 Mkazi wa Kijiji cha Malombwe Ambaye Alikutwa Amekufa Chumbani kwake Mara Baada ya  Kukatwa katwa na Kitu chenye Ncha Kali baada ya Kuvamiwa na Watu Wasiofahamika na  Kufariki Papo Hapo na Chanzo cha Mauaji Hayo Bado Hakijafahamika.

Aidha Kamanda wa Polisi Amesema Kuwa Katika Kijiji cha Lupanga  Kata ya Lupanga  Wilayani Ludewa Mkoani Njombe MtotoVaileth Sambala Mwenye Umri wa Miezi 7  Alikutwa Amefariki Dunia Mara Baada ya Kutumbukia Kwenye Ndoo ya Maji na Chanzo cha Tukio Hilo Bado Hakijafahamika.

Kutokana na Matukio Hayo Kamanda wa Polisi Amewaasa Madereva Kuendesha Vyombo vya Moto kwa Uangalifu na Kwa Kuzingatia  Sheria za Usalama Barabarani Ili Kupunguza Ajali Hizo.

Article 3

$
0
0

MBUNGE Wenje atiwa mbaroni kwa kuongoza maandano ya CHADEMA jijini mwanza

Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza linamshikilia kwa mahojiano Mbunge wa Nyamagana jijini humo,Mh Ezekiel Wenje kwa madai ya kuongoza maandamano yaliyosambaratishwa na polisi  hapo jana kwa kutumia mabomu ya kutoa machozi.

Article 2

$
0
0
MWANAMKE AJILIPUA NA PETROL BAADA YA MUMEWE KUOA MKE WA PILI.

MWANAMKE mmoja ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Nyankumbu, Kata ya Kalangalala mkoani  Geita amenusurika kifo baada ya kujimwagia mwilini mafuta ya petroli kisha kujilipua baada ya mumewe kuoa mke wa pili.  

Imeelezwa kuwa mwanamke huyo, Anastazia Kubezya (28) Agosti 8 mwaka huu aliamua kujimiminia petroli mwili mzima kabla ya kuchukua kiberiti na kujilipua, hali iliyosababisha  akimbizwe katika Hospitali ya Geita alikolazwa katika wodi namba saba kwa matibabu.

Akizungumza na mwandishi wetu, Consolata Raphael ambaye ni dada wa majeruhi huyo alidai kuwa chanzo cha mdogo wake huyo kufikia hatua ya kutaka kutumia njia hiyo ya mkato kwa lengo la kujiua ni wivu wa mapenzi.

Consolata alisema: “Siku ya tukio shemeji yangu George Kubezya (mume wa majeruhi), alifika nyumbani kwa mdogo wangu wa kiume akidai kuwa mkewe huyo anatishia kujiua baada ya kuoa mke wa pili.
 

“Tukiwa tunaendelea kujadiliana mara alitokea mkewe Kubezya akiwa na viatu vya mwanaye mdogo akamkabidhi mdogo wetu mwingine aitwaye Rozalia akamwambia mpatie mwanaye kwa kuwa anaondoka na hajui atarudi lini.
 

“Baada ya kutamka maneno hayo aliondoka na niliwasiliana na ndugu yetu mwingine aitwaye Elizabeth aliyesema Anastanzia alipita kwake akiwa na chupa ikiwa na petroli na walipojaribu kumkimbiza alipotelea gizani.


“Kati ya saa 4 na saa 5 usiku Eliza na wenzake walisikia mtu akilia nje ya nyuma yao na baada ya kutoka nje walikuta Anastanzia akiwa tayari amekwisha jilipua moto, walipomhoji alidai amefanya hivyo ili afe kutokana na mumewe kumuolea mke mwenza na kumleta kwenye nyumba waliyoijenga yeye na mumewe,”alisema Consolata. 

Hata hivyo juhudi za kumpata mumewe kuzungumzia sakata hilo hazikuzaa matunda baada ya kile kilichoelezwa kuwa alitoroka muda mfupi baada ya kumfikisha mkewe hospitalini.
 
Mwandishi wetu alifika hospitalini hapo na kukuta mwanamke huyo aliyelazwa wodi namba nane akiwa anauguzwa chini ya ulinzi wa polisi ili akipona afikishwe mahakamani kwa kosa la kujaribu kujiua.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Geita, Dk. Adam Sijaona akizungumzia hali ya majeruhi huyo alisema bado si nzuri na wanafanya mpango wa kumhamishia katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando iliyopo jijini Mwanza.

Kwa Hisani ya Mpekuziblog

Article 1

$
0
0
Mpiga Debe asiye na Sare Atakamatwa kwa Uzululaji
 Mwenyekiti wa Chama cha Usafirishaji Mkoa wa Njombe Bwana Donatus Mwamanga[DOSMEZA] Aeleza Hali Hilisi ya Usajiri


Tabia ya Kunyang'anya Mizigo kwa Abiria Imepigwa Marufuku na Hivyo Kuagizwa Kuwa na Sare Kila Kondakta na
Wapiga Madebe.


Katibu wa Kituo cha Mabasi Mjini Njombe Bwana Kelvin Mwarwanda naye Aeleza hatua Hiyo

Na Gabriel Kilamlya Njombe.
Baadhi ya Wamiliki wa Magari Yanayofanya Shughuli za Usafirishaji Abiria  Mikoani na Wilayani Katika Kituo Kikuu cha Mabasi Mjini Njombe Wameanza  Kutekeleza Agizo la Uongozi wa Kituo Hicho la Kuwasajili Wafanyakazi Wao Ikiwa ni Pamoja na Uvaaji wa Sare na Vitambulisho Hali Ambayo Itasaidia Kupunguza Vitendo Vya Uhalifu Dhidi Abiria na Kuwabaini Watu Wanaojihusisha na Vitendo Hivyo.

Akiongea na Kituo Hiki Mwenyekiti wa Chama cha Usafirishaji Mkoa wa Njombe Donatus Mwamanga Amesema Licha ya Kuanza Kwa Zoezi Hilo Lakini Bado Kuna Changamoto Kadhaa Ikiwemo Baadhi ya Wafanyakazi Kufika Ofisini Kwake Kwa Lengo la Kujisili Bila ya Kuwa na Wajiri Wake Jambo Ambalo ni Kinyume cha Sheria.

Aidha Mwenyekiti Huyo Amewataka Waajiri Kufika Katika Ofisi Yake Akiwa na Wafanyakazi Wake Kwa Ajili ya Kufanya Usajili na Kwamba Kila Gari la Abiria Linatakiwa Kuwa na Wafanyakazi Watatu Tu na Si Vinginevyo.

Kwa Upande wake Katibu wa Kituo Hicho cha Mabasi Kelvin Mwarwanda Amesema  Zoezi Hilo Litasaidia Kuwabaini Watu Wanaofika Kituoni Hapo Kwa Lengo la Kufanya Uhalifu na Kuliomba Jeshi la Polosi Kuendelea Kushirikiana na Uongozi wa Kituo Hicho Ili Kukomesha Viendo Vya Uhalifu Dhidi ya Mali za Abiri.

Hivi Karibuni Uongozi wa Kituo Kikuu cha Mabasi Mjini Njombe Kwa Kushirikiana na Jeshi la Polisi Ulitoa Agizo Kwa Wafanyakazi Wote wa Kituo Hicho Kuvaa Sare na Vitambulisho Vinavyoonesha Ofisi Wanazofanyika Kazi Ifikapo Agosti 19 Mwaka Huu na Kwa Yeyote Atakaekaidi Hatua za Kisheria Zitachukuliwa Dhidi Yake

Article 0

$
0
0
SPIKA WA BUNGE Bi.Anne Makinda Kuongoza Mazishi ya NEEMA MANGULA Kijijini KinenuloWanging'ombe.
Marehemu Neema Mangula Enzi za Uhai Wake.

Neema Mangula Akiwa na Wazazi Wake Enzi za Uhai wake
Kushoto ni Marehemu Neema Mangula akiwa Kwenye Picha ya Pamoja na Wageni Mbalimbali Pamoja na Familia Yao.

Na Gabriel Kilamlya Njombe 
 
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi.Anne Makinda Leo Anaongoza Mazishi ya Msiba wa Mtoto wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Mzee Philip Mangula Katika Kijiji cha Kinenulo Imalinyi Wilayani Wanging'ombe.

Akizungumza na Kituo Hiki leo Katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Bwana Hosea Mpagike Amesema Kuwa Marehemu anayefahamika kwa Jina La Neema Mangula anazikwa Katika Kijiji cha Kinenulo Ambapo Spika wa Bunge Anaongoza Msiba Huo Pamoja na Viongozi Mbalimbali wa Kitaifa Akiwemo Waziri wa Ofisi ya Rais Sera na Uratibu Stephen Wasira wakiwemo Viongozi Kutoka Vyama Mbalimbali vya Kisiasa.

Taarifa za Awali zinaeleza Kuwa Neema Mangula (25) amefariki dunia juzi usiku kwa ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Aga Khan Wilayani Ilala wakati akitokea kwenye sherehe ya harusi iliyokuwa ikifanyika katika Ukumbi wa

Waterfront uliopo Gerezani.

 Neema alipoteza maisha muda mfupi baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Aga Khan ambako aligundulika kuwa alikuwa amepata majeraha ya ndani.

Aidha Imedaiwa Kuwa Marehemu alikuwa anatoka kwenye harusi na alipofika maeneo ya Aga Khan, alipunguza mwendo kupisha gari lingine lililokuwa mwendokasi, lakini alimfuata upande wake, wakagongana uso kwa uso.

PICHA ZOTE NA MICHUZIblog

MSAFARA WA MBIO ZA MWENGE WAPATA AJALI DODOMA.

$
0
0

Mnamo tarehe 20/08/2013 majira ya 08.45 hrs. huko katika kijiji cha Fufu, Kata ya Fufu, Wilaya ya Chamwino, takribani magari matano (5) yaliyokuwa kwenye msafara wa Mwenge wa Uhuru, yakitokea Wilaya ya Dodoma kuelekea kwenye makabidhiano Wilaya ya Mpwapwa, moja ya magari yaliyokua kwenye msafara huo lilikutana na tuta huku dereva wake akishika ‘brake’ ghafla na kusababisha magari yaliyokuwa nyuma yake kugonga gari la mbele kwa kila moja lililokuwa likitimka kutokana na vumbi kubwa lililokuwa likifuka wakati wa msafara huo kufuatia matengenezo ya barabara Dodoma – Iringa yanayoendelea.

Baadhi ya washiriki walikuwa katika msafara wa kwenda kukabidhi mwenge kutoka wilaya ya Dodoma mjini na kuukabidhi katika wilaya ya Mpwapwa wakiangalia moja ya magari yaliyoharibika baada ya kutokea ajali hiyo Gari namba DFP.7178 TOYOTA LAND CRUISER (AMBULANCE) ambayo ni mali ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Dodoma, Mrakibu wa Jeshi la Polisi Bw. Bonventure Nsokolo Akikagua moja ya gari iliyoharibika katika ajali iliyotokea katika kijiji cha Fufu, Kata ya Fufu, Wilaya ya Chamwino, ambapo takribani magari matano (5) yaliyokuwa kwenye msafara wa Mwenge wa Uhuru, yakitokea Wilaya ya Dodoma kuelekea kwenye makabidhiano Wilaya ya Mpwapwa.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Bi. Suzzan Kaganda Akiongea na waandishi wa Habari hawapo pichani, Katika ukumbi wa Mikutano wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma Kuhusia na ajali iliyotokea katika kijiji cha Fufu, Kata ya Fufu, Wilaya ya Chamwino, ambapo takribani magari matano (5) yaliyokuwa kwenye msafara wa Mwenge wa Uhuru, yakitokea Wilaya ya Dodoma kuelekea kwenye makabidhiano Wilaya ya Mpwapwa, ambapo Watu wapatao tisa (9) walijeruhiwa katika ajali hiyo.


Katika ajali hiyo magari yaliyoathirika ni kama ifatavyo:-
1. STK 3007 TOYOTA LAND CRUISER
2. STK 3357 TOYOTA LAND CURISER yote ni mali ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa Katibu Tawala [M] Dodoma.
3. SM 5835 TOYOTA LAND CRUISER mali ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma
4. DFP.7178 TOYOTA LAND CRUISER (AMBULANCE) nayo ikiwa ni mali ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma.
5. T.627 BFJ TOYOTA LAND CRUISER mali ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma
6. STK 4983 TOYOTA LAND CRUISER HARD TOP Mali ya Wizara ya Kilimo. Watu wapatao tisa (9) walijeruhiwa katika ajali hiyo, kati yao wanne (4) wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa Dodoma na watano (5) walipatiwa matibabu na kuruhusuiwa kurudi nyumbani.

Majeruhi waliolazwa ni kama ifuatavyo:-
1. JUMA S/O ALLY @ SIMAI, Miaka 32, Mpemba, Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Mkazi wa Kusini Unguja.
2. CHARLES S/O MAMBA, Mgogo, Miaka 50, Mkazi wa Ipagala, Diwani wa Kata ya Ipagala
3. DATIVA D/O KIMOLO, Miaka 46, Mrangi, Afisa Mifugo, Manispaa ya Dodoma, Mkazi wa Mailimbili.
4. AMINA D/O MGENI, Miaka 36, Muuguzi Kituo cha Afya Makole, Mkazi wa Area ‘C’ Manispaa ya Dodoma.

Majeruhi waliotibiwa na kuruhusiwa kurudi makwao ni kama ifuatavyo:-
1. JACKLINE D/O MAGOTI, Miaka 39, Mjita, Muuguzi Kituo cha Afya Makole, Mkazi wa Area C Manispaa ya Dodoma
2. RICHARD S/O MAHELELA, Miaka 51, Mgogo, Mwenyekiti wa Mtaa wa Ipagala, Mkazi wa Ipagala Manispaa ya Dodoma
3. JUMANNE S/O NGEDE, Miaka 58, Mrangi, Diwani Kata ya Chamwino/ Naibu Meya wa Manispaa ya Dodoma, Mkazi wa Chamwino Manispaa ya Dodoma.
4. ZAITUNI D/O VARINOI, Miaka 43, Mkazi wa Mbwanga, Manispaa ya Dodoma.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linatoa wito kwa madereva na watumiaji wa barabara hususan zilizopo kwenye matengenezo wanapokuwa katika misafara, wanapaswa kuwa makini na wapeane nafasi kati ya gari moja hadi jingine ili kuepusha madhara yanayoweza kuepukika.
 
kwa hisani ya talkbongo.blogspot.com

Article 5

$
0
0
Deo sanga Awa Mgeni Rasmi.
 
 Mbunge Deo Sanga Kutoka Jimbo la Njombe Kaskazini Afanikisha Kupata zaidi ya Shilingi Milioni Kumi Harambee.


Mbunge Deo Sanga Ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe

Na Gabriel kilamlya Wanging'ombe

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Njombe Bwana Deo Sanga Ameweka Jiwe la Msingi Kwenye Ujenzi wa Madarasa Katika Shule ya Msingi Mambegu Wilayani  Wanging'ombe Huku Zaidi ya Shilingi Milioni Kumi Zikipatikana Katika Harambee Iliyoendeshwa  Kwa Ajili ya
Kuchangia Ujenzi  Shule Hiyo

Akiongea Mara Baada ya Kuweka Jiwe la Msingi Katika Shule Hiyo Kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe, Katibu wa Chama Hicho Mkoani Njombe Hosea Mpagike Amesema Fedha Hizo Zitatumika Katika Ujenzi na Ukarabati wa Madarasa Katika Shule ya Msingi Mambegu .

Aidha Mpagike Amewataka Wananchi Kushirikiana na Serikali Katika Shughuli Mablimbali za Maendeleo Ikiwemo Kuchangia Michango Miradi Inayotekelezawa na Kuanzishwa Katika Maeneo Yao.

Akielezea Hali ya Shule Hiyo Mratibu Elimu Kata wa Luduga Gibson Sauga Amesema Inakabiliwa na Chanagamoto Mbalimbali Ikiwemo Uhaba wa Walimu, Nyumba za Walimu Pamoja na Uchakavu wa Majengo.




Mbunge Deo Sanga  Wa Jimbo la Njombe Kaskazini Achangia Shilingi Laki Nane na Mbunge Gerson Lwenge Kutoka Jimbo la Njombe Magharibi Akichangia Shilingi Laki Tano
...........................................................................................................................................

Article 4

$
0
0
KESI YA WIZI WA KUTUMIA SILAHA YAENDELEA KUSIKILIZWA NJOMBE.

Na Gabriel Kilamlya Njombe

Mahakama ya Wilaya ya Njombe Hii Leo Imeendelea Kusikiliza Kesi ya Wizi wa Kutumia Silaha Inayowakabili  Stanley Kaduma Mwenye  Umri wa Miaka 30 na Shem Mgiliche Mwenye Umri wa Miaka 35 Wote Wakazi wa Ilunda Mkaoni Njombe.

Akisoma Hati ya Mashtaka  Mbele ya Hakimu wa Mahakama Hiyo Augustino Rwezile ,Mwendesha Mashtaka Atupakisye Mwakasitu Ameiambia Mahakama Kuwa   Washtakiwa Walitenda Kosa Hilo Oktoba Tatu Mwaka 201o Katika Kituo cha Kituo cha Kulelea Watoto Yatima Kilichopo Ilunda  Mkoani Njombe .

Imedaiwa Mahakamani Hapo na Mwendesha Mashtaka Mwakasitu Kuwa Washitakiwa Wakiwa na Bunduki Aina ya Shotgun Pomoja na Mapanga Walivamia Kituo cha Kulelea WatotoYatima na Kuiba Fedha Taslimu Shilingi Milioni Tisa Laki Tisa na
35 Elfu.

Washtakiwa Walipohojiwa Kutenda Kosa Hilo , Wamekana Kutenda Kosa Hilo Mbele ya Mahakama .

Hakimu wa Mahakama  Hiyo  Augustino Rwezile Ameahirisha Kesi Hiyo Hadi Septemba 18 Mwaka Huu Itakapo Sikilizwa Tena Huku Akiuagiza Upande wa Mashtaka Kuleta Mashahidi na Washtakiwa Wamerudishwa Lumande. 

Kwa Mara ya Kwanza Washtakiwa Hao Walifikishwa Katika Mahakama Hiyo Oktoba 27 Mwaka 2012 na Kusomewa Hati ya Mashtaka

Article 3

$
0
0
Freeman Mbowe,Tundu Lisu na Wanasheria Wengine wa CHADEMA KUTUA NJOMBE AGOST 24.
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe Akiendeleza Mchakato wa Rasimu ya Katiba.
Tundu Lissu.
 Kaimu Mwenyekiti  wa CHADEMA Mkoa wa Njombe bwana Alatanga Nyagawa aeleza Ujio wa Viongozi Hao Mjini Njombe Agosti 24 Mwaka Huu.

Agosti 24 Mwaka Huu Viongozi wa CHADEMA Taifa wakiongozwa na Kiongozi wao wa Anga Freeman Mbowe wanatarajia Kutua Mjini Njombe Katika Kuendeleza Mapambano ya Rasimu ya Katiba Mpya.

Kaimu Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Njombe Bwana Alatanga Nyagawa amesema Kuwa Msafara Huo Utatua Mkoani Njombe Ukitokea Mkoani Mbeya Kwa Lengo Kuu la Kuendelea Kukusanya na Kuchambua Rasimu ya Katiba Mpya.

Bwana Alatanga Amesema Kuwa Mkutano Huo Utafanyika Katika Uwanja wa National Housing  Mjini Njombe Ukiongozwa na Bwana Mbowe,Tundu Lissu na wanasheria Mbalimbali wa Chadema .

Article 2

$
0
0
TANESCO NJOMBE WAELEZA HATUA ZA KUKABILIANA NA FOLENI KWA WATEJA
 Hapa ni nje ya ofisi za TANESCO Wilaya ya Njombe huku wateja wakiendelea kumiminika kwenda kulipa ankra za Umeme.

 Baadhi ya watumishi wa shirika la Umeme Tanesco wilaya ya Njombe wakijiandaa kwenda site kuendelea na majukumu ya kiserikali kuhakikisha jamii inapata nishati ya umeme.
 Tazama Foleni ya wateja wa Umeme Tanesco wilaya ya Njombe wakiwa wanalipa Bili zao.
 Hapa ni wateja wanaoendelea kuomba kuunganishiwa Huduma za umeme kwenye majumba yao na hivyo kuongeza Idadi ya wateja katika Shirika hilo.

Foleni yaendelea kuongezeka kulipia Ankra za Umeme katika ofisi za Tanesco Njombe.
 Kaimu meneja wa shirika la Umeme Tanesco wilaya ya Njombe bwana Omary Ally Akieleza Malengo ya Kuongeza Dirisha Jingine.

Shirika la Ugavi Umeme Nchini TANESCO Wilayani Njombe Limesema Lipo Katika Hatua za Mwisho za Kuboresha Huduma Zake Hasa  Sehemu za Ulipiaji Ankara na Kuwaomba Wateja Wake Kuwa na Subira Wakati Shirika Hilo Likiendelea na Kuboresha Huduma Zake.

Kauli Hiyo ya TANESCO Imekuja Kufuatia Ombi la Wananchi Wanaofika Katika Ofisi za Shirika Hilo Kwa Lengo la Kupata Huduma na Kujikuta Wanasubiri Kwa  Muda Mrefu Kutokana na Kuwepo Kwa Dirisha Moja Linalotoa Huduma Zote za Ulipaji Ankra na
Huduma Nyingine.

Omary Ally ni Kaimu Meneja wa Tanesco Wilaya ya Njombe Ambea Amekiri Kuwepo Kwa Tatizo la Msongamano wa Wateja Wanaofika Katika Ofisi Hiyo Kwa Lengo la Kupata Huduma Mbalimbali, Huku Akiwataka Wanachi Kujijengea Tabia ya Kulipia Ankara Zao Kwa Hiyari na Kuacha Kusubiri Oparesheni Kata Umeme Kwa Wadaiwa Ili Kuepusha Msongamano.
 
Uplands Redio Imeshuhudia Msongamano wa Wateja Katika Ofisi za Tanesco Kwa Siku Mbili Mfululizo za Agosti 19 na 20 Mwaka Huu Wakilipia Ankara Zao Huku Wakilalamikia Ucheleweshewa Huduma Kufuatia Kuwepo Mhudumu Mmoja Anaehudumia Wateja Zaidi ya Wateja 40
........................................................................................

Article 1

$
0
0

UTPC WAANZA MKUTANO MKUU DODOMA.


 Mtendaji  mkuu  wa  UTPC  Bw  Karsan akitoa  neno la ufunguzi  kabla ya  kumkaribisha  Rais  wa UTPC  kufungua mkutano huo

 Viongozi  wa  UTPC  wakiwa katika  ukumbi  wa  mkutano  ukumbi  wa Golden Grown Hotel
 Wanachama  wa  UTPC wakiwa katika mkutano  hyuo


 Rais  wa  UTPC Keneth Simbaya kulia akiwa na mtendaji mkuu  wa UTPC Bw Karsan











 Mwenhyekiti  wa IPC Bw  Frank Leonard  akiwa katika ukumbi  wa  mkutano  huo
 Mwenyekiti  wa  Lindi Abdulaziz Video akiwajibika

katibu  wa Tanga  Press Club Bi  Lulu  George  akiwa  katika mkutano  huo

source Francis Godwin blog

Article 0

$
0
0

POLISI FEKI 7 WANASWA TENA


SIKU chache baada ya kukamatwa kwa askari feki wa usalama barabarani, Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imewakamata watuhumiwa saba wa ujambazi, wakiwa na sare za Polisi, huku mwingine akijifanya ofisa Usalama wa Taifa.
 
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaa, Suleiman Kova alisema watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na sare za Polisi jozi mbili.

Watuhumiwa hao ni Khamis Mkalikwa (40), Magila Werema (31), Nurdin Bakari (46), Materu Marko (32), Louis Magoda (34), Amos Enock (23) na Amiri Mohammed (45), wote wakazi wa jijini Dar es Salaam.
 
Sare hizo, kwa mujibu wa Kamanda Kova, ni zenye cheo cha Sajenti wa Kituo, huku jozi moja ikiwa na jina linalosomeka SSGT A.M Mduvike.
 
Watuhumiwa hao walikamatwa jana katika eneo la Kiluvya, baada ya askari kuweka mtego, ambao ulifanikiwa kuwanasa. 


Alisema watu hao walikuwa wakitumia silaha, sare za jeshi la Polisi na redio ya mawasiliano katika uhalifu wao na hivyo kuwafanya baadhi ya watu kutupia lawama Jeshi la Polisi kwa kujihusisha na uhalifu.
 
Alisema watuhumiwa hao, wanahusishwa na uhalifu katika maeneo ya Boko, Tegeta, Mbweni, Bahari Beach, na maeneo mengine ya jiji. Alisema watu hao ni hatari zaidi.
 
Watuhumiwa hao walikuwa wakitumia gari aina ya Cresta GX, 100 yenye namba T 546 BWR na baada ya kuona wamezingirwa na askari maeneo hayo, walifyatua risasi moja hewani, lakini askari walipambana nao na kufanikiwa kuwakamata.
 
“Mbali na vitu hivyo pia wamekamatwa na bastola moja aina ya Brown yenye namba B.3901, ambayo ilikuwa na risasi nne na ganda moja, tunawashikilia kwa upelelezi na baada ya kukamilika watafikishwa mahakamani,” alisema Kova.
 
Katika hatua nyingine, Kamanda Kova alisema wanamshikilia mtuhumiwa Alquine Masubo (42) maarufu kama Claud, kwa kosa la kujifanya ofisa wa Usalama wa Taifa.
 
Claud ambaye ni mkazi wa Yombo Buza, alikamatwa akiwa na vielelezo mbalimbali pamoja na nyaraka za idara hiyo, ambapo baada ya kuhojiwa alikiri kuwa yeye si mfanyakazi wa idara hiyo.
 
Kova alisema mtuhumiwa huyo alipopekuliwa zaidi, alikutwa na bastola aina ya Browing yenye namba A. 956188-CZ83 ikiwa na risasi 12 ndani ya kasha lake.
 
“Alipopekuliwa nyumbani kwake alikutwa na bastola nyingine aina ya Maknov yenye namba BA4799 ikiwa na risasi 19 na kitabu cha mmiliki chenye namba CAR 00071678, ikiwa na jina la P.1827 LT COL Mohammed Ambari, jambo ambalo haliwezekani kwa mtu mmoja kumiliki silaha mbili,” alisema Kova.
 
Mtuhumiwa huyo pia alikutwa na kitambulisho cha Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) chenye namba 7001- E. 1075 na kompyuta mpakato aina ya Toshiba.

“Huyu ni tapeli wa siku nyingi na taarifa zake tulikuwa nazo, anatumia kivuli cha idara ya usalama wa taifa kufanya utapeli, lakini sasa ndiyo mwisho wake na wananchi wamjue” alisema.

-Habari leo

Article 2

$
0
0

BIG RESULTS NOW IMEANZA KWA KUWAPANGUA MAKATIBU NA MANAIBU WAKE.


Imeandikwa na Na Magreth  Kinabo  na Eleuteri  Mangi — RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya uongozi katika ngazi za juu za utendaji wa Serikalini kwenye nafasi za Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu katika Wizara mbalimbali, ambapo  wapo waliohamishwa, wataopangiwa kazi nyingine na yumo anayestaafu.

Kauli hiyo ilitolewa leo jioni na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

“Rais amefanya mbadiliko haya kwa lengo kuu la kuimarisha utendaji wa kazi za Serikali katika ngazi hizo za juu,” alisema Balozi Sefue.

Mabadiliko yaliyofanywa kwa upande wa Makatibu Wakuu ni kama ifuatavyo:
  • Dk Florens Turuka amekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, awali alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

  • Joyce Mapunjo amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, awali alikuwa Katibu Mkuu Wizara  ya Viwanda, Biashara na Masoko.

  • Jumanne Sagini amekuwa Katibu  Mkuu  Ofisi ya Waziri Mkuu - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) awali alikuwa Naibu Katibu  Ofisi wa Waziri Mkuu - TAMISEMI.

  • Dk Servacius Likwalile amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, awali alikuwa Naibu Katibu Wizara ya
Fedha.
  • Dk Patrick Makungu amekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, awali alikuwa  Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo.

  • Alphayo Kitanda amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, awali alikuwa Naibu Katibu Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI.

  • Dk Shaaban Mwinjaka amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara  ya Viwanda, Biashara na Masoko.

  • Dk Uledi Mussa amekuwa Katibu Mkuu Wizara  ya Viwanda, Biashara na Masoko, awali alikuwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki. 

  • Profesa Sifuni Mchome amekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya  Elimu na Mafunzo ya Ufundi, awali alikuwa Katibu Mtendaji Mkuu wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania.

  • Charles Pallangyo amekuwa Katibu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri.

  • Anna Maembe amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, awali  alikuwa Naibu Katibu Mkuu wizara hiyo.

  • Sihaba Nkinga amekuwa Katibu  Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo.

  • Sophia Kaduma amekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, awali alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.

Balozi Sefue aliongeza kwamba:
  • Katibu Mkuu aliyepewa uhamisho ni  Peniel  Lyimo ambaye anahamia Ofisi ya Rais - Ikulu  kwenye “Presidential’s Delivery Bureau” kama Naibu Mtendaji Mkuu mwenye jukumu la kuanzisha na kuongoza Idara ya Mageuzi ya Kilimo mwanzoni alikuwa  Katibu Mkuu  Ofisi ya Waziri Mkuu.

Makatibu wakuu watakaopangiwa kazi nyingine ni:-
  • Sethi Kamuhanda aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo 
  • Kijakazi Mtengwa aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto 
  • Injinia Omari  Chambo aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi

Katibu anayestaafu ni Patrick Rutabanzibwa ambaye alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ambaye sasa amestaafu kwa hiari.

Aidha, Balozi Sefue alisema Rais Kikwete pia amefanya uteuzi wa Naibu Makatibu Wakuu wapya na kuwapa uhamisho baadhi yao.  Aliiwataja Naibu Makatibu Wakuu wapya walioteuliwa kuwa ni:-
  • Angelina  Madete amekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais  Mazingira

  • Regina Kikuli amekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu

  • Zuberi Sumataba amekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, anayeshughulikia  suala la elimu katika ngazi za Serikali za Mitaa

  • Edwin Kiliba amekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI

  • Deodatus Mtasiwa amekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI ambaye atashughulikia saula la afya  upande wa  Serikali za Mitaa.

  • Dk Yamungu Kayandabila amekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika

  • Profesa Adolf Mkenda amekuwa Naibu Katibu Mkuu ya Fedha anayeshughulikia sera

  • Dorothy Mwanyika amekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya  Fedha anayeshughulikia Fedha za Nje na Madeni

  • Rose Shelukindo amekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

  • Dk Selassie Mayunga amekuwa Naibu Katibu Mkuu  Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi

  • Monica Mwamunyange amekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi

  • Consolata Mgimba amekuwa  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya  Elimu na Mafunzo ya Ufundi

  • Profesa Elisante ole Gabriel Laizer amekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

  • Armantius Msole amekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Balozi Sefue aliwataja Naibu Makatibu Wakuu waliopewa uhamisho kuwa ni:-
  • John Mngondo ambaye amehamishiwa Wizara ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia ametoka Wizara ya Uchukuzi katika nafasi hiyo

  • Selestine Gesimba amehamishiwa Wizara ya Maliasili na Utalii, anatoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi

  • Injinia Ngosi Mwihava anahamia Wizara ya Nishati na Madini kutokea Ofisi ya Makamu wa Rais

  • Maria Bilia amehamia Wizara ya Viwanda na Biashara kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi 

  • Nuru Milao anahamia  Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.
-Via Wavuti

Article 1

$
0
0

 Mhandisi wa Ujenzi Katika Halmashauri ya Mji wa Njombe Bwana Peter Kawogo Aliyeagizwa Kushughulikia Tatizo Hilo Lakini Hadi Dakika Hii hakuna Mafanikio,Taarifa zaidi Juu ya Majibu ya Mkurugenzi Zatakujia.

 Mhandisi Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Eng.Ibrahim Mkangallah Alipotoa Agizo La Kushughulikia Daraja Hilo Agosti 21 Mwaka Huuu lakini Hakuna Utekelezaji.
Mkazi wa Mtaa wa Kihesa Akiondoa Ubao ulioharibika Kwenye Daraja Hilo Ambalo Limekuwa Tishio Kwa Wapita Njia Hiyo.
 Haya ni Magogo yanayotajwa Kutakiwa Kutumika Katika Ukarabati wa Daraja Hilo Ambalo Limebomoka.
 Hilo ndilo Daraja Lenyewe Linalolalamikiwa.
 Mwandishi na Mmiliki wa Mtandao Huu Bwana Gabriel Kilamlya akihojiana na Wakazi wa Mtaa huo wanaolalamikia Ubovu wa Daraja Hilo.
 Namna Magogo yalivyo haribika Kwenye Daraja Hilo.


Huu ndio Muonekana wa Daraja Hilo Jinsi Linavyotiririsha Maji.

Pamoja na Agizo la Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Kuagiza na Kuahidi Kushughulikia Daraja Linaounganisha Mtaa wa Kihesa na Njombe Ambalo Lilitajwa Kujengwa Agosti 21 Mwaka Huu Lakini Hadi sasa Hakuna Kilichofanyika.

Mtandao huu wa www.gabrielkilamlya.blogspot.com umefika Kufuatilia Daraja Hilo leo Asubuhi na Kukuta Kama Lilivyokuwa Awali huku Likiendelea Kubomoka Siku hadi siku hali inayoendelea Kuhatarisha Usalama wa Maisha ya Wakazi wa Maeneo hayo hususani Nyakati za Usiku.

Agosti 2o Mwaka Huu Mtandao Huu Ulizungumza na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Bwana Ibrahim Mkangallah Alikiri Kuwepo kwa Adha Hiyo Huku Akisema suala Hilo Lipo kwenye Mchakato wa Kulishughulikia Ambapo Aliahidi Kulifanyia Kazi Agosti 21 Kitu Ambacho Hadi sasa Hakijatekelezwa.

Pamoja na Mambo Mengine Mtandao Huu umezungumza na Mwenyekiti wa Mtaa wa Kihesa Bi.Merry Mng'ong'o Kwa Njia ya Simu Alijibu Kuwa Yupo Njiani Kuelekea Msibani Lakini Hata HIVYO Juu ya Daraja Hilo Ameshaandika Barua tatu hadi sasa ambazo hazijapata Majibu yoyote toka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe.

Amesema Barua Hizo Alianza Kuziandika Tangu Mwezi February Mwaka Huu Lakini Kimya na Kutokana na Daraja Hilo Kuingizwa kwenye Mipango ya Halmashauri Wao kama Viongozi wa Mtaa hawana la Kulifanya kwa Sasa.

Bi.Mng'ong'o Ameongeza kuwa Daraja Hilo Lilitajwa Kujengwa kwa Kumiminwa na si Kwa Magogo Kama Lililovyo namna walivyojenga wananchi hao Hivyo kwa sasa kama wananchi hawana Fedha za Kufanyia Shughuli Hiyo Tena.

Jitihada za Kumtafuta Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Kujibia sakata Hilo zinaendelea Baada ya mtandao huu Kufika Ofisini Kwake Leo Asubuhi na Kuambiwa Yupo kwenye Kikao.

Edelea Kufuatilia Mtandao Huu kwa
majibu zaidi Toka kwa Mkurugenzi.

Article 0

$
0
0

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe ACP Fulgency Ngonyani Amethibitisha Kutokea Kwa Tukio Hilo.

Na Gabriel Kilamlya Njombe.

Mkazi Mmoja wa Ikang'asi Wilayani Njombe Isaka Kaberege Mwenye Umri wa Miaka 35  Amekutwa Amefariki Baada ya Kunywa Sumu ya Mahindi Aina Actelik Super.

Kamanda wa Polisi Mkoani Njombe ACP Fulgency Ngonyani Amesema Mwili wa Marehemu Umeoneka Ukiwa Kwenye Nyasi Ndefu  Agosti 21 Mwaka Huu Majira ya Saa Nne Asubuhi na Kwamba  Marehemu Hakuacha Ujumbe Wowote.

ACP Ngonyani Amesema Hadi Sasa Hakuna Mtu Yeyote Anayeshikiliwa Kuhusiana na Tukio Hilo na Kwamba Jeshi la Polisi Linaendelea na Uchunguzi Juu ya Tukio Hilo Huku Akitoa Wito Kwa Wananchi Kuacha Kujichukulia Maamuzi Yasiyofaa Ikiwemo Kujinyonga.

Article 6

$
0
0

MKUU WA FFU - ARUSHA NA POLISI WENGINE WATATU WAFUKUZWA KAZI

Imeandikwa na Lydia Churi— Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewavua madaraka Maafisa wanne wa Jeshi la Polisi nchini na kumsimamisha kazi mmoja ambaye atafunguliwa mashtaka ya kijeshi kutokana na kukiuka maadili na taratibu za jeshi hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Waziri Nchimbi amesema hatua hiyo ni katika kuendeleza vita ya kuhakikisha kuwa jeshi la polisi linakuwa na nidhamu, linatekeleza wajibu wake wa kutenda haki na kuwalinda raia na mali zao.

Alisema amewachukulia hatua Maafisa hao baada ya kuridhia maoni ya kamati aliyoiunda kufanya uchunguzi wa matukio yaliyolalamikiwa dhidi ya askari polisi katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro na Kigoma kati ya Desemba 2012 na Mei, 2013.

Waziri Nchimbi aliwataja waliovuliwa madaraka kuwa ni Mkuu wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoani Arusha Mrakibu wa Polisi Ramadhan Giro, Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro Inspekta Jamal Ramadhan, Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Dumila Inspekta Juma Mpamba na mkuu wa upelelezi wa wilaya ya 


Kasulu ASP Daniel Bendarugaho na kumsimamisha kazi Inspekta Isaack Manoni.

Alifafanua kuwa  Mrakibu wa Polisi Ramadhan Giro alivuliwa madaraka kwa kushindwa kusimamia kikamilifu askari na maafisa walio chini yake ambao walikamatwa wakisafirisha bangi yenye uzito wa kilogramu 540 kwa kutumia gari la polisi.

Alisema askari hao wawili waliokamatwa wakisafirisha bangi, walikuwa wakifanya kazi kwenye kituo cha Ngarananyuki na baada ya kukiri kosa walifukuzwa kazi mwezi Mei mwaka huu.

Alisema kwa upande wa Inspekta Jamal Ramadhan amevuliwa madaraka yake kwa kutochukua hatua stahiki baada ya kupata taarifa za mfanyabiashara wa Mvomero Samson Mwita kubambikiwa fuvu la kichwa cha binadamu na askari polisi watatu wakishirikiana na matapeli wawili.

“Katika tukio hilo Inspekta Isaack Manoni amesimamishwa kazi na atashtakiwa kijeshi kutokana na tuhuma za kumtorosha mtuhumiwa, Cpl. Edward aliyekuwa dereva wa gari la Polisi lililokamatwa na bangi kitendo ambacho kimelifedhehesha jeshi la polisi” alisema Waziri Nchimbi.

Alibainisha kuwa Inspekta Juma Mpamba amevuliwa madaraka hayo kwa kuonesha udhaifu katika utendaji wake wa kazi kwa kutosimamia kikamilifu askari walio chini yake kitendo kilichosababisha askari kujipangia kazi nje ya utaratibu na kumbambikiza mfanyabiasha huyo kesi kwa lengo la kujinufaisha kinyume na maadili ya kazi. Aliongeza kuwa askari waliohusika na tukio hilo wamefukuzwa kazi na kushtakiwa.

Waziri Nchimbi alisema ASP Daniel Bendarugaho amevuliwa madaraka kwa kutokuwa makini katika kufanya na kusimamia upelelezi wa kesi ya mauaji ya marehemu Gasper Mussa Sigwavumba aliyeuawa baada ya kupigwa na askari polisi wawili Desemba mwaka jana.

Alisema upelelezi mbovu uliofanywa chini ya usimamizi wa Mkuu huyo wa upelelezi ulisababisha kesi hiyo kuondolewa mahakamani. Aliongeza kuwa upelelezi wa kesi hiyo utaanza upya ili haki itendeke.
 
kwa hisani ya Mpekuziblog

Article 5

$
0
0
WANANCHI KIHESA NJOMBE WATUPIWA MZIGO WA KUJENGA DARAJA. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Bwana Edwin Mwanzinga akizungumza na www.gabrielkilamlya.blogspot.com juu yaUjenzi wa Daraja Hilo leo 

Kauli ya Mwenyekiti Edwin Mwanzinga Imekuja Ikiwa ni Siku Mbili tu Tangu Mtandao Huu kuripoti Kuwa Halmashauri ya Mji Njombe Kupitia Kaimu Mkurugenzi Ambaye ni Mhandisi Mkuu wa Halmashauri hiyo Bwana Ibrahim Mkangallah Kuahidi Kwenda Kujenga kwa mAGOGO daraja hilo Agosti 21 bila Mafanikio.

Mwenyekiti Bwana Mwanzinga Amesema Kuwa Hadi sasa hAKUNA  Bajeti ya Ujenzi wa Daraja hilo hivyo kama Wananchi wanawajibu wa kujenga Tena Kwa Mbao na Kuendelea Kulilinda kwa kuzuia mAGARI YENYE Zaidi ya Tani 10 kupita hupo.

 Namna Magogo yalivyo haribika Kwenye Daraja Hilo.


Huu ndio Muonekana wa Daraja Hilo Jinsi Linavyotiririsha Maji.

Article 4

$
0
0
APOTEZAMAISHAAKIFYATUA TOFALI MAHEVE NJOMBE 
Aangukiwa na kifusi
 Mwili wa Marehemu Ukiwa Umefunikwa mara baada ya Kufukuliwa kwenye Kifusi

Na Gabriel Kilamlya Njombe

Mtu Mmoja Juma Liduke Mkazi wa Makambako Mwenye Umri Kati ya Miaka 30-35  Amefariki Dunia Baada ya Kufukiwa na Kifusi Alicho kuwa Anafyatulia Tofali Leo Asubuhi.

Tukio Hilo Limetokea Katika Mtaa wa Maheve Eneo la Howadi Mjini Njombe Ambako Alikuwa Akifanya Shughuli za Kufyatua Tofali kama Kibarua Kwa Bwana Chesco Mwogofi.

Mashuhuda wa Tukio Hilo Ambao walikuwa wakifanya Kazi naye Wamesema Kuwa Walisikia Kelele mara Moja walipogeuka wakakuta Mwenzao Amefukiwa na Kifusi Kutokana na Bonde Kubwa Alilochimba kwa Shughuli ya Ufyatuaji Tofali.

Katika Hatua Nyingine Mmiliki wa Tofali Hizo Bwana Chesco Mwogofi Mkazi wa Mtaa wa Maheve Amesema Kuwa ni Kweli Kwamba Kijana Huyo ni Mfanyakazi wake Hivyo hadi sasa
Wanaendelea na Jitihada za Kuangalia namna ya Kusafirisha Mwili wa Marehemu baada ya Jeshi la Polisi Kufika na Kuthibitisha Tukio Hilo.

Christopher Mligo ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Maheve Ambaye amethibitisha Kutokea Kwa Tukio Hilo Ambapo Amesema Kuwa Kama Uongozi wa Serikali umefika Kutoa Taarifa Polisi Ambao Tayari wamefika Katika Eneo Hilo.



 samahani kwa picha hizi za kusikitisha

 Hizi ndizo Tofali zilizokuwa Zikifyatuliwa na Marehemu Pamoja na Vijana Wenzake

 hapa ndipo Mauti Yalipo Mkuta Marehemu Juma Liduke baada ya udongo kumuangukia.
 hawa ndio Vijana waliokuwa wakifanya kazi Pamoja na Marehemu.
 Miongoni mwa Waliokuwa wakifanya Kazi na marehemu Bwana Willy Ndunduru Amesema Marehemu alikuwa Akifanya kazi Karibu na bonde hilo.
 Mmiliki wa Tofali Hizo Ambaye ni Mwajiri wa Vibarua Hao Bwana Chesco Mwogofi Amesema hadi sasa Wanasubiri Kusafirisha Maiti Kwenda Makambako.

 Dokta Omar Kutoka Hospitali ya Mji Njombe Kibena Baada ya Kufika na Maafisa wa Polisi Katika Eneo la Tukio Hilo.

Mwenyekiti wa  Mtaa wa MAHEVE Bwana Christopher Mligo Amethibitisha Kutokea Kwa Tukio Hilo.


Article 3

$
0
0

WATANZANIA 3 WAUAWA KWA KUPIGWA RISASI HUKO SOUTH AFRICA KISA DAWA ZA KULEVYA.

Watanzania watatu wameuawa hivi karibuni jijini Cape Town, Afrika ya Kusini kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya. Watanzania hao walipigwa risasi na kundi la watu waliokuwa wameficha nyuso zao nje ya duka lijulikano kama Maisha Tuck Shop jumanne iliyopita katika barabara ya Veld, Athlone, Cape Town.


Watanzania wawili walifariki papo hapo na mmoja kufia hosipitali. Mtu mwingine, raia wa Afrika Kusini, alijeruhiwa vibaya katika shambulio hilo. Mmiliki wa duka la Maisha Tuck, Ashim Nassoro, alisema kuwa aliona kundi la watu wakiwa na bunduki za aina ya AK-47 na pistols wakipiga risasi nje ya duka lake.

Bw. Nassoro alidai waliouawa walikuwa marafiki zake, alisema yeye alikuwa nyumbani na mke wake na mtoto wake, ambapo ni karibu na duka hilo aliposikia milio ya risasi.

 
 “Nilikuwa ndani na nilimwambia mke na mtoto wangu walale chini mpaka milio ya risasi iishe” alisema Nassoro na kuongeza “waliwapiga risasi watu waliokuwa ndani ya nyumba halafu wakaenda kwenye duka. Walipiga risasi watu wawili dukani, mmoja aliyekuwa kwenye geti na mwanamke mmoja aliyekuwa kwenye nyumba.”

Nasroro aliongeza kuwa alikuwa anawajuwa Watanzania hao kwa sababu wote wanatoka Tanzania na wamekuwa wakiishi pamoja tokea walipowasili Cape Town miaka mitano iliyopita. Mtu mwingine aliyeshughudia tukio hilo alisema kuwa waliowauwa Watanzania hao walikuwa hawana wasiwasi na walirudi kwenye gari yao taratibu na kuondoka eneo la tukio.



Kufuatia tukio hilo, polisi ilimkamata Abdus Salaam Ebrahim ambaye ni kiongozi wa kikundi kinachopiga vita dhidi ya uhalifu na madawa ya kulevya nchini humo kinachojulikana kama People Against Gangsterism and Drugs (Pagad). Abdus Salaam Ebrahim amefikishwa mahakami leo kwa mashtaka ya mauaji.

Hata hivyo, mahakama imeyaondoa mashtaka hayo kwa muda kufuatia ombi la mwendesha mashtaka ili kuruhusu uchunguzi zaidi kufanyika. Wakati hakimu akiyandoa mashtaka hayo, wafuasi wa kikundi hicho cha Pagad waliokuwa wamejazana mahakamani hapo walishangilia huku wakisema “Allahu Akbar”. Majina ya Watanzania waliouawa hayakuwekwa kwenye charge sheet.

Pagad ni kikundi kilichoanziswa mwaka 1995 kupambana na uhalifu na madawa ya kulevya kwenye jiji la Cape Town baada baada ya juhudi za serikali kulegalega. Kampeni ya kikundi hiki ilianza mwaka 1996 baada kumkamata, kumpiga na kumchoma moto hadi kufa Rashaad Staggie ambaye alikuwa kiongozi wa kikundi cha uhalifu jijini Cape Town. Serikali ya Afrika Kusini ilishawahi kudai huko nyuma kuwa Pagad ni kikundi cha kigaidi baada ya kudaiwa kulipua kwa bomu hoteli ya Planet Hollywood mwaka 1998. Hata hivyo, Pagad ilipinga kuhusika kwenye shambulio hilo.

Kikundi hiki kilipotea lakini kikaja kuibuka tena kuanzia mwaka 2011 na kampeni yake ya kuchukua mitaa inayotawaliwa na uhalifu na biashara ya madawa ya kulevya. Wadadisi wa mambo wanadai kuwa kurudi tena kwa Pagad kwa gia ya kupambana na uhalifu, hasa madawa ya kulevya, itafanya hali kuwa mbaya hasa kwenye jimbo la Western Cape.

Hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la milipuko ya mabomu kwenye sehemu zinazouza magari na pia kwenye nyumba za makazi ya watu zilizopo Athlone na maeneo mengine jijini Cape Town. Matukio haya yamekuwa yakitokea zaidi kwenye nyuma za makazi zinazotuhumiwa kutumika kufanyia biashara ya madawa ya kulevya. Kikundi cha Pagad kimekanusha kujihusisha na matukio hayo.
 
kwa hisan ya the choiceblog.
Viewing all 2276 articles
Browse latest View live