Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all 2276 articles
Browse latest View live

Article 5

$
0
0

NYUMBA ZILIZOJENGWA KATIKATI YA MAKABURI YA MTWIVILA IRINGA ZAVUNJWA.

 

 Mgambo  wakivunja  nyumba  iliyojengwa  eneo la makaburi ya Mtwivila mjini Iringa

Mgambo  wa  Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa na  viongozi mbali mbali wakielekea  kuvunja nyumba zilizojengwa makaburi ya Mtwivila  leo

Mgambo  wa Manispaa ya  Iringa na mwanasheria  katikati Bw Innocent Kihaga  wakielekea  kuvunja nyumba  zilizojengwa makaburini Mtwivila

Mgambo  wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa  wakivunja  nyumba  iliyojengwa katikati ya makaburi ya Mtwivila
Kaburi  hili la Rashid M. Lukuvi likiwa  jirani kabisa na ukuta  wa nyumba  hiyo iliyovunjwa

Mgambo  wakivunja nyumba  iliyokuwa ikijengwa katika makaburi ya Mtwivila mjini Iringa  leo


Nyumba  iliyojengwa makaburini  yavunjwa  rasmi leo na mgambo wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
Makaburi  yaliyozunguka  nyumba  hiyo
Hii  ndio  nyumba ambayo ipo  jirani na kaburi la marehemu Idd Chonanga aliyekuwa  diwani wa kata ya Nduli kaburi  lenye mashada kushoto ,na hapo  waliposimama mgambo ndipo alipokaa waziri mkuu Mizengo Pinda  wakati wa mazishi na viongozi mbali mbali  wa mkoa wa Iringa
Uvunjaji wa  nyumba ambayo nje katika msalaba hapo ndipo  waziri mkuu Mizengo Pinda alikaa wakati wa mazishi ya diwani Chonanga ,nyumba  hii imevunjwa  sehemu ya ukuta na mmiliki wake amepewa  siku 30  kuanzia  leo  kuivunja

Wananchi ambao  wamezika  ndugu  zao katika makaburi hayo  wakishuhudia  zoezi hilo
HATIMAYE Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa imeivunja nyumba  iliyokuwa ikijengwa katikati ya makaburi  ya Mtwivila   ambayo  iliripotiwa na mtandao www.francisgodwin.blogspot.com  na  vyombo mbali mbali  vya  habari likiwemo gazeti la Jamboleo , radio Ebony Fm na  radio Cloud FM  pamoja na   nyumba nyingine mbili ambazo pia zilikuwa  zikianzwa  kujengwa eneo hilo .

Pamoja na  kuendesha  zoezi la  kuzivunjwa  nyumba  hizo ambazo  zilikuwa katika  hatua ya mwanzo  kabisa  pia Halmashauri hiyo  imetoa  muda wa  siku  30  kuanzia  leo  kwa mmiliki  wa  nyumba nyingine iliyokutwa  imekamilika ambayo pia  imejengwa karibu na makaburi ya Mtwivila eneo ambalo waziri Mkuu Mizengo Pinda alikaa wakati  wa mazishi  ya  aliyekuwa diwani wa kata ya Nduli marehemu Iddi Chonanga

Hatua ya  kuvunjwa kwa makaburi hayo  imekuja  ikiwa ni  siku  mbili zimepita  baada ya mtandao huu  wa matukio daima  kuibua suala  hilo  kuibua ujenzi huo holela  na  ni  siku  moja  baada ya mkurugenzi mtendaji  wa halmashauri ya  Manispaa Bi  Terresia  Mahongo  kutoa agizo kwa  maofisa mipango  miji , afisa ardhi na mwanasheria  wa Manispaa ya  Iringa  kufika  eneo hilo  ili  kuchukua hatua sitahiki.

Zoezi la  kuvunja nyumba  hizo  leo  majira ya  saa 3 asubuhi limeongozwa na maofisa mbali mbali  wa Manispaa ya  Iringa akiwemo mwanasheria  wa Halmashauri  hiyo Bw Innocent Kihaga pamoja na mgambo  zaidi ya  watano wa Halmashauri  hiyo.

Kuvunjwa  kwa  nyumba  hizo  kumeshuhudiwa na umati  mkubwa wa  wananchi  wa  maeneo mbali mbali ya mji  wa Iringa ambao  walifika  kushuhudia  utekelezaji  wa agizo la mkurugenzi baada ya  baadhi  yao  kudai  wamiliki wa nyumba  hizo  wamejenga katika makaburi ya ndugu  zao  hivyo  walikuwa  wakishindwa  kuchukua hatua  kutokana na kutojua  wahusika  wa  ujenzi huo wa nyumba makaburini.

Miongoni mwa makaburi yaliyokuwa hatarini  kuvunjwa na  wajenzi  wa nyumba  hizo ni pamoja na kaburi la Rashind  M. Lukuvi ambalo lilikuwa hatarini  kuvamimiwa na  wajenzi hao  iwapo ujenzi  huo ungefumbiwa macho.

Wakipongeza  hatua  iliyochukuliwa na uongozi  wa Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa  wananchi  waliofika  eneo  hilo kushuhudia  zoezi akiwemo Yustina Malinga , Yohana  Sanga na Juma  Ally   walisema  kuwa  mbali ya  kupongeza  uongozi  wa Manispaa chini ya mkurugenzi  wake  Bi Mahongo kwa  kuchukua hatua  ila  bado  waliwataka  wananchi  wenzao  wanaoendelea  kujenga makaburini  kuwa na huruma na  marehemu  waliozikwa katika maeneo  hayo kwani watambue kuwa hata  hao marehemu  walikuwa kama  wao .

Alisema  Bi Malinga  kuwa  wakati mwingine  wananchi  wamekuwa  wakiitafua  ugomvi  serikali kwani kitendo  cha  kujenga katika makaburi  ni  kinyume na tamaduni za  kitanzania  na  kuwa makaburini  ni eneo la kuishi wafu  sasa mtu  mzima  na familia  yako kujenga makaburini   utajiweka katika mazingira  ya  kuogopwa na  kila mtu.

Huku kwa  upande wake mzee  Sanga  akisema  kuwa  mbali ya  wananchi hao  awali kuonekana  wakilima maeneo  hayo ila bado baada ya  kuona hakuna mtu anayewafuatilia  waliamua  kujenga  kabisa.

"Tunawaomba  hawa  ndugu ambao inasemekana  si  wenyeji wa  eneo  kutumia utu  kabla ya  kuanza  kuvamia makaburi  yetu na kuanza  kujenga nyumba juu ya makaburi ya ndugu  zetu.....pia  tunaomba wahusika  wasakwe ili  wachukuliwe hatua kali za kisheria"
Mbali ya  kutaka  wahusika  hao kusakwa  bado  walielekeza  lawama  zao kwa  watendaji wa mitaa na kata  kwa  kushindwa  kuwawajibisha  wananchi wanaojenga  kiholela katika milima na maeneo ya makaburi kama  hayo.
Mwanasheria  wa Manispaa ya  Iringa Bw Kihaga  alisema  kuwa  wamelazimika  kuvunja nyumba  hizo baada ya  kuonekana zimejengwa maeneo ambayo si rasmi na  bila kibali  cha mipango miji .
Hata  hivyo  mwanasheria  huyo  alisema  wametoa  muda wa  siku 30 kwa mmiliki wa nyumba iliyopo  jirani na makaburi eneo  ambalo  waziri mkuu Mizengo  Pinda alikaa wakati wa mazishi ya diwani Chonanga  kuivunja  nyumba  hiyo ndani ya  siku 30  kuanzia leo kabla ya  kuvunjiwa nyumba hiyo na  kufikishwa mahakamani.
Pia  alisema  kuanzia  sasa msako mkali kwa  wote  waliojenga maeneo ambayo si rasmi na  wale  wanaojenga  bila  vibali  litaanza katika mji mzima  wa Iringa na  kuwataka wananchi  wanaotaka  kujenga  kufuata  sheria  ya ujenzi ikiwa ni pamoja na kutafuta ardhi halali  na kabla  ya  kujenga ramani  zao kupitisha ili  kupewa  kibali  cha ujenzi zaidi ya hapo  watachukua hatu.
Awali  mkurugenzi  wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa Bi Mahongo  aliwataka  wananchi kuheshimu  sheria na kuwa  hatakubali  kuona  ujenzi  holela unaendelea katika maeneo mbali mbali ya mji  wa Iringa na  kuwataka  wananchi  kutoa ushirikiano kwa  kufichua  watu  wanaojenga nyumba  kiholela na  kuvamia maeneo  ya  wazi .
Hata  hivyo  kutokana na uchunguzi wa kina uliofanywa na mtandao huu  wa  www.matukiodaima.com umebaini  kuwepo maeneo mengi zaidi ambayo  wananchi  wamejenga  kiholela yakiwemo maeneo ya Mtwivila ,Mwang'ingo , Zizi la Ng'ombe, Ipogolo  na  Semtema ambako wananchi  wameamua  kujenga hadi katika vilele  vya  milima .
 
Kwa Hisani ya FG Blog

Article 4

$
0
0
MAJINA YA MADIWANI NANE WALIOFUKUZWA CCM BUKOBA HAYA HAPACCM Kagera yawafukuza madiwani wake 8 Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Bw Avelin Mushi amemaliza Press Conf hivi punde na kufafanua kuwa kikao cha Halmasahuri Kuu ya mkoa wa Kagera imemaliza kikao chake hivi punde na kuamua madiwani 8 wa Manispaa ya Bukoba kufukuzwa katika chama na kufutiwa nyadhifa za udiwani kutoka na mgogoro uliokuwa ukiendelea.
Waliofukuzwa ni:
1. Richard Gaspar (Miembeni )

2. Murungi Kichwabuta (viti maalum)

3. Alexander Ngalinda ambaye pia ni Naibu Meya (Buhembe)

4. Yusuf Ngaiza ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa wilaya (Kashai)

5. Deusdedit Mutakyahwa (Nyanga)

6. Robert Katunzi (Hamugembe)

7. Samwel Ruhangisa (Kitendaguro) na

8. Dauda Kalumuna (Ijuganyondo).

Katibu huyo ameongeza kuwa madiwani hao wanaweza kukata rufaa kwa ngazi za juu za chama wakiona hawakutendea haki na kuwa ngazi ya mkoa ina mamlaka ya kufanya hivyo kwa madiwani wa ngazi hizo.

Aidha amesema kwa Bw Yusuph ngaiza amabye ni mwenyekiti wa CCM bukoba,nafasi yake hiyo inasubiriwa ngazi za juu amabazo ndizo zenye mamlaka juu yake(kwa cheo hicho)

Manispaa ya Bukoba ina kata 14 na kati ya hizo kata 4 zinaongozwa na CDM(2) na CUF(2) hivyo kwa Bukoba mjini CCM imebakiza madiwani 3 TU wa kuchaguliwa .kama ifuatavyo
1.Kashai-Amefukuzwa
2. Miembeni-Amefukuzwa
3.Miembe-Amefukuzwa
4.Nyanga-Amefukuzwa
5.Hamugembe-Amefukuzwa
6.Kitendaguro-Amefukuzwa
7.Ijuganyondo-Amefukuzwa
8.(1)Kagondo-Amebaki (CCM) (Meya Amani)
9.(2)Nshambya-Amebaki(CCM)
10.(3)Kahororo-Amebaki(CCM)
11.Bilele-Amebaki(CUF)
12.Kibeta-Amebaki(CHADEMA)
13.Bakoba-Amebaki(CUF)
14.Rwamishenye-Amebaki(CHADEMA).


Chanzo cha Mgogoro soma chini hapo
.
 
Kwa karibu miezi sita sasa, siasa za Jimbo la Bukoba mjini zimegeuzwa siasa za chuki, kutishana, fitina, kuchambana, kulaumiana, kuonesha umwambwa, uwezo wa kifedha, dharau, ubaguzi  na ujenzi wa matabaka yanayosigana katika jimbo hili.
Msuguano chanzo chake ni siasa za kutafuta ‘kula’  na ‘Uheshimiwa’ miongoni mwa wanasiasa hali inayodumaza maendeleo.

Wanasiasa wanaosuguana ndani ya CCM ni Mbunge wa Jimbo la Bukoba, Balozi Khamis Kagasheki na Meya wa Manispaa ya Bukoba, Dk. Anatory Aman. Kila mmoja ana kundi lake.
Dk. Kagasheki si ‘mzawa’ wa jimbo hili. Anatajwa kuwa ni mtu wa kutoka nchini Uganda aliyehamia Tanzania na kujichimbia wilayani Karagwe, wakati wa ujana wake ambapo taarifa zinaeleza kwamba alipewa heshima ya kukimbiza Mwenge wa Uhuru nchini Tanzania akiwa bado kijana na huo ndiyo uliokuwa mwanzo wa kuingia katika siasa za Tanzania.

Dk. Amani aliwahi kuwa Mwenyekiti Vijana wa CCM Mkoa wa Kagera na baadaye alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera. CCM walimfukuza, akanyang’anywa uraia na akajichimbia kwenye biashara kwa kuanzisha shule za masomo kwa mchepuo wa Kiigereza ziitwazo Amani. Alianzisha pia biashara ya usafiri wa baiskeli, akiita ASECDO.

Alikuwa na utitiri wa baiskeli ambapo aliwagawia vijana baiskeli wasafirishe abiria kwa malipo na kila jioni wawasilishe ujira kwake. Kampuni hiyo ilikufa baada ya vijana kujua siri na kuachana na baiskeli za Amani alizokuwa amewanunulia wakanunua baiskeli zao na kufanya shughuli hiyo wao.

Dk. Amani alirejea katika siasa mwaka 2010 kwa kugombea udiwani kata ya Kagondo ambako amejenga shule ya mchepuo wa Kiingereza.

Balozi ni mzaliwa wa Bukoba Mjini, lakini ametumia muda mwingi nje ya nchi. Alikuwa mwakilishi wa Tanzania nchini Uswizi na alirejea nchini mwaka 2004 akiwa  ‘ameitwa’ na wana-CCM kuanza maandalizi ya kumng’oa Lwakatare wa CUF.

Kabla ya kurejea nchini, Kagasheki alianza kufadhili miradi kadha wa kadha ikiwamo ujenzi wa vyumba vya madarasa, kulipia watoto ada, kufunga taa za barabarani na mingine kupitia kampuni ya Kananga Investment.

Kagasheki aliingia rasmi katika siasa za Bukoba mwaka 2005 wakati huo akiitwa ‘mkombozi’ na wana-CCM wenzake wakiongozwa na Mzee Pius Ngeze na Dk. Deodorus Kamala, aliyekuwa Mbunge wa Nkenge. Kagasheki alishinda ubunge kupitia CCM kwa kumwangusha Lwakatare wa CUF.

Akiwa mbunge kati ya 2005 na 2010, Kagasheki na wana-CCM wengine wakiwamo madiwani kutoka chama hicho, hawakuelewana vema na Meya wa Bukoba, Samuel Ntambala Luangisa, kwa jinsi alivyokuwa akitekeleza Ilani ya CCM, hivyo mipango ya kumwangusha ilianza.

Madiwani kwa kushirikiana na wana-CCM wengine waliamua kumtafuta Dk. Amani agombee udiwani kupitia Kata ya Kagondo hatimaye ‘wampitishe’ kuwa Mstahiki Meya. Nakumbuka madiwani wote walipelekwa Chato kupanga mbinu za kumng’oa Luangisa na kumwingiza Aman. Nyuma ya huu mchezo alikuwapo Kagasheki.

Hivyo, kauli ya Kagasheki ya kwamba ‘alimchonga’ Meya ni kweli kabisa wala hakuna ubishi katika hili labda kama mfumo wa uwasilishaji haukuwa sawa. Kwa nguvu ya Kagasheki, Dk. Amani alimwangusha Luangisa na kushinda umeya.
Kagasheki, Amani na mipango ya maendeleo
Kupitia kampeni za 2010 na ilani ya CCM wanasiasa hawa kwa pamoja walipanga kuifanya Bukoba kuwa Jiji kabla ya 2020 na pia kupitia vipaumbele vya halmashauri, ahadi za mbunge, ahadi za rais za 2010 na Ilani ya CCM walibuni miradi kadhaa ambayo waliamini ikitekelezwa, Bukoba ingepiga hatua kimaendeleo na ikaongeza mapato ya halmshauri.

Miradi waliyopanga kutekeleza ni ujenzi wa kitegauchumi, upimaji wa viwanja 5,000, ujenzi wa stendi ya mabasi Nyanga, mradi wa kuosha magari, ujenzi wa soko kuu, uendelezaji makazi Kashai na Miembeni, ujenzi wa chuo cha ualimu, ujenzi wa kituo cha maarifa na ujenzi wa bwawa la maji kwa ajili ya utalii.

Katika utekelezaji wa miradi hii, wanasiasa hawa walikuwa pamoja na kati yao hakuna asiyejua faida za kutekeleza miradi hiyo kwa maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo.

Halmashauri ilianza utekelezaji wa miradi hasa miradi ya ujenzi wa soko kwa kubomoa lililopo na upimaji wa viwanja 5,000 ambapo mpango huu ulipanuliwa kupima viwanja vya kutosheleza watu 40,000 yaani sawa na viwanja 8,000 katika kata saba.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba, Khamis Kaputa, anasema katika hatua hii halmshauri iliandaa andiko la mradi wa viwanja kwa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, kupata fedha kwa ajili hiyo lakini hawakupata, hali iliyowafanya kutafuta wabia.

“Tuliamua kuwapata Mfuko wa Dhamana Tanzania (UTT) ambao tuliingia makubaliano nao watoe fedha zipatazo bilioni 2.6 kwa ajili ya kutekeleza mradi huo na mkataba tulioingia Juni 20, 2011 upo katika mfumo wa ushirikiano (joint venture),” anasema Kaputa.

Kwa mujibu wa Kaputa, viwanja vingeendelea kuuzwa hadi Februari 2013 ambapo watafunga mradi na kugawana faida kwa uwiano wa  asilimia 60 kwa UTT na asilimia 40 kwa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba. Halmashauri inatarajia kupata gawio la sh bilioni 2.

Halmashauri ilizungumza na Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB) kuhusu kufadhili ujenzi wa soko ambapo Aprili 16, 2012 waliingia mkataba.

Kaputa kabla ya kubomoa soko la sasa ilikuwa ni lazima kuwatafutia maeneo mbadala wafanyabiashara walioko katika soko la sasa. Maeneo yaliyopendekezwa ni jengo la CCM Mkoa, soko la Nyakanyasi, machinjio ya zamani na eneo la CCM Miembeni. Hii ilikuwa itekelezwe kabla ya Agosti 2012.
Malalamiko juu ya miradi
Kabla ya malalamiko kuanza, tulishangaa kuona kila diwani wa Manispaa akiendesha gari na tulipouliza wakadai kwamba meya ‘amewafanyia’ mpango wa mkopo wa Sh milioni 10 kila mmoja ili wapate usafiri.

Baadaye madiwani wote wakapelekwa kutalii Dodoma kwa gharama za meya. Hapa tukasema mambo si ndiyo hayo! Wapiga kura wanasota, wapigiwa kura wanakula bata!

Lakini punde madiwani wakaanza kulalama kwamba meya sasa amekuwa ‘jabali’ kwamba ameanza kuwatambia kuwa  ‘Yeye ni halmashauri na halmashauri ni yeye’ na wengine wakaenda mbali zaidi kwamba ‘anakula’ peke yake.

Hazikupita siku meya akafanya mahojiano na Redio Kasibante ya mjini hapa, Mei 18, 2012 na kumdhalilisha mbunge kupitia Chadema, Conchester Lwamlaza, kwa kumwita malaya, baadaye katika kikao cha Julai 2011 akamdhalilisha Samuel Luangisa kwa kumwamuru kama mtoto akisema “kaa chini wewe”.

Kwa kuwa madiwani wote walikuwa kitu kimoja katika uibuaji, upangaji na utekelezaji wa miradi husika taratibu wakaanza kutengeneza makundi. Yakawapo makundi yanayofaidika na yasiyofaidika na utekelezaji wa miradi. Kundi linalodaiwa kufaidika ni lile lililomo katika Kamati ya Uchumi na Fedha. Hapa madiwani bila kujali vyama wanakotoka wengi wakasaliti kambi! Wakaasi!
Malalamiko ya wananchi juu ya miradi
Kwa kuwa madiwani hawa ndiyo waliokuwa ‘jikoni’, walijua kila kitu hivyo waliwandaa wapiga kura wao kulalamikia baadhi ya miradi na vipengele kadhaa ambavyo wao pasipo kuwa na shaka, walijua vilifanywa kinyume na taratibu za uendeshaji wa halmashauri kwani walishiriki kufanya hivyo lakini wakijua ikitokea tatizo wataruka.

Katika mradi wa soko, walijitokeza madiwani wanaolalamika kwamba hakuna zabuni iliyotangazwa kuipatia kandarasai kampuni ya OGM kuwa mkadarasi mshauri na kulipwa Sh milioni 522 iandae andiko la mradi. Kwamba OGM haikushindanishwa na kampuni nyingine kama taratibu zilivyo bali ililetwa na Meya.

Kumbuka wamiliki wa vibanda sokoni asilimia kubwa ni madiwani wale wale na taarifa za wafanyabiashara kufungua kesi mahakamani kupinga soko lao kuvunjwa bila kupewa sehemu mbadala nyuma yao kulikuwa na madiwani hawa. Mkurugenzi Kaputa amekiri kwamba watawajengea maeneo mbadala.
Madiwani wanamwomba Kagasheki amuonye meya
Baadhi ya madiwani kwa kutazama mwenendo wa meya na ‘kufifia’ kwa mazingira yao kufaidika na miradi waliamua ‘kumshtaki’ kwa ‘mkubwa’ wake Kagasheki na taarifa zilizopo ni kwamba meya aliwahi kwenda kwa Kagasheki kuungama. Taarifa zinasema meya baadaye aliona ni dharau sana kuungama kila wakati.

Akaona ni bora ajitoe mhanga kwa kufanya kazi bila kuingiliwa na ama madiwani au Kagasheki. Kwamba nani amweheshimu mwenzake katika lipi na wapi!  Wote si wanasiasa? Huu ndiyo uliokuwa mwanzo wa unamwaga mboga nami namwaga ugali!

Kagasheki anaongea wazi wazi kwenye mikutano, huku meya akiwasaka viongozi wa juu ya chama na mkoa kuomba msaada.

Kagasheki pia anatumia Redio yake ya Kasibante FM kuelezea mipango ya kuendeleza mji, meya anatumia Redio Vision FM kuelezea mipango hiyo hiyo na wakati mwingine wanatofautiana kwa lengo la kupata ‘wafuasi’. Katika hili redio hizi zinasaidia kukuza mgogoro.

Pia kupitia vijiwe zikajitokeza tetesi kuwa meya anataka kugombea ubunge 2015 ‘kumpora’ jimbo Kagasheki kwa sababu anatekeleza miradi ya maendeleo hasa ujenzi wa soko. Inadaiwa Dk. Amani hakuwahi kutamka popote maneno haya.
Mipango ya kumg’oa meya
Baada ya meya kuwa ‘ngangari’ kwa kukataa kuungama kila wakati kwa ‘aliyemchonga’ na kukataa kukubali baadhi ya matakwa ya madiwani anaowaongoza. Hapa inadaiwa kuna walioonekana kufaidi zaidi ya wenzao. Sasa wale wasiofaidika sana waliandaa mipango ya kummaliza kisiasa. Walimtumia Kagasheki kama kamanda mkuu wa ‘Operation Ondoa Meya’ (OOM).

Meya naye aliandaa majeshi yake kwa kuunda kikosi cha ‘Operation Bakisha Meya (OBM) kwa kusaidiana na Chief Kalumuna, Diwani wa kata ya Kahororo (CCM).

Awali walikuwa ni CCM pekee waliopanga kumng’oa lakini hawa wanawashawishi wengine wa upinzani kutoka CUF. Madiwani wa Chadema hawakusaini kwa sababu ambazo bado hazijulikani kwani hawakuwa upande wowote ingawa katika dakika za mwisho walishajiunga na kundi la OOM katika hatua ya mwisho ya kupiga kura za kumuondoa.
CCM Mkoa, Taifa inaingilia kati
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa kupitia Kamati ya Siasa ya Mkoa, imefanya vikao zaidi ya vitatu kujadili ‘siasa’ za watu hawa na mara zote wakidai kuwa mgogoro umalizwe ndani ya vikao vya wilaya na kuwa haina tija kwa chama.

Article 3

$
0
0

WANYARWANDA WALIOTIMULIWA TANZANIA WAKIMBILIA UGANDA AMBAKO NAKO WAMEKATALIWA.


Wengi wa wahamiaji haramu waliokuwa mkoani Kagera ambao wengi wao ni wanyarwanda wamekimbilia Uganda kama wakimbizi lakini makambi ya wakimbizi huko Uganda yamekataa kuwapokea.

Pamoja na serikali ya Rwanda kupitia ubalozi wake Uganda kufanya jitihada ya kutaka kuwarudisha Rwanda lakini wakimbizi  hao  wamegoma  kurudi  kwao  kwa  hofu  ya  kuuawa  wakirudi  Rwanda.
 Source:  jamii forum

Article 2

$
0
0

NAPE NNAUYE AAGIZA MADIWANI WALIOFUKUZWA HUKO BUKOBA WARUDISHWE KAZINI HARAKA.


Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kagera jana tarehe 13/08/2013 katika kikao chake cha siku moja kilichofanyika mjini Bukoba imetangaza uamuzi wake wa kuwafutia dhamana ya CCM hivyo kuwavua Udiwani Madiwani wanane wa Manispaa ya Bukoba waliotokana na CCM.
 
Kwa mujibu wa utaratibu wa kutoa adhabu kwa viongozi wa CCM walio kwenye vyombo vya dola hasa Wabunge na Madiwani uamuzi wa Halmashauri Kuu ya Mkoa sio wa mwisho.  Uamuzi huo unapaswa kupata Baraka za Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ndipo utekelezwe.
 
Hivyo basi, mpaka sasa Madiwani hao wanane waliosimamishwa wanapaswa kuendelea na kazi zao kama kawaida wakisubiri kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kitakachoketi tarehe 23 Agosti, 2013 mjini Dodoma ambacho pamoja na mambo mengine kitapitia uamuzi huo wa Halmashauri Kuu ya Mkoa wa Kagera.

Pamoja na hilo, tumepokea barua za Madiwani hao za kukata rufaa kupinga uamuzi huo wa Halmashauri Kuu ya Mkoa kwa msingi wa madai ya kukiukwa kwa utaratibu katika kufikia uamuzi huo.
 
Tunawasihi wananchi wa Bukoba na Kata husika, wanachama na viongozi wote kuwa watulivu katika kipindi hiki ambapo suala hili linashughulikiwa na vikao vya Kitaifa.
Imetolewa na:-
Nape M. Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
ITIKADI NA UENEZI

Article 1

$
0
0

HAYA NDO MAJINA 250 YA WAUZA UNGA NA BANGI NCHINI TANZANIA.


Majina ya watanzania 255 wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya   yamejulikana  na  JAMHURI  imeamua kuyachapisha...

Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa kwenye orodha hiyo wapo watu maarufu na baadhi wamekuwa wakitoa misaada ,huku wengine wakijifanya ni wazee  wa kanisa na kushiriki  shughuli mbalimbali za kijamii....

Uchunguzi wetu usio na chembe ya shaka  unaonesha kuwa orodha hii ya watu watakaoandikwa hapo chini kwa sasa wapo chini ya uangalizi wa mahakama na polisi..

  "Ni kweli kuna watu tumewapeleka mahakamani, huko wamewekwa chini ya uangalizi na wanatakiwa kuripoti  kwa  muda wanaopangiwa.Tunafanya hivyo baada ya uchunguzi wetu kubaini kwa ni kweli  wanahusika na biashara hii haramu."Alisema  Nzowa

Nzowa aligoma kuyataja majina hayo, lakini uchunguzi uliofanywa na JAMHURI  kutoka ndani ya jeshi la polisi na  mahakama  umefanikiwa  kuyapata  majina  hayo...

Katika orodha hii, yumo mchungaji aliwekwa chini ya uangalizi , na baada ya kumaliza muda huo, siku tatu baadaye alikamatwa na  dawa nchini Brazil.Pia yumo Sheikh anayetoa misaada mbalimbali,lakini baada ya kukamatwa na dawa kilo 211, eneo la Kunduchi Dar es salaam, kwa sasa  amekimbilia  Afrika kusini....

DAWA ZINAVYOINGIZWA NCHINI:
Hadi sasa kiwango kikubwa cha dawa za kulevya kinaingizwa nchini kwa njia ya meli katika bahari ya Hindi.

Baada ya meli kuwasili Tanzania, wasafirishaji hutumia boti ndogo ziendazo kasi kuchukua dawa hizo.Maeneo yanayotumiwa zaidi kuingiza dawa ni Bagamoyo, Zanzibar, Tanga na Mtwara....

Jijini Dar, boti hizo hutia nanga  katika eneo la  Bagamoyo ambako pia ndiko kwenye njia kuu ya uingizaji  wa bidhaa za magendo  zisizolipiwa kodi...

Biashara  hiyo  haramu  huwahusisha  baadhi  ya  polisi  ambao  mara  kadhaa  wamekuwa  wakiwapa  ulinzi   wahalifu  hao.

Viwanja  vya  ndege   vinavyotumiwa  kuingiza  madawa  ya  kulevya  ni  Julius  Nyerere ( DAR )  na  Abeid  Amani  Karume ( ZANZIBAR)

Taarifa  toka  kitengo  cha  kuzuia  dawa  za  kulevya   zinasema  kuwa  wasafirisha  wanaotumia  ndege  wamekuwa  wakibuni  mbinu  mbali  mbali  zikiwemo  za  kutumia  manukato  kwa  ajili  ya  kuwapumbaza mbwa  wenye  mafunzo  ya  kubaini  madawa  ya  kulevya....

Habari zaidi  zinasema  kuwa  kitengo  kimepata  vifaa  maalumu    vya  kubaini  kama  ndani  ya  mizigo  kuna  madawa  ya  kulevya. Vifaa  hivyo  ni  mfano  wa  sindano  ambayo  huchomwa  kwenye  mizigo  na  kuipitisha  kwenye  ngozi  ya  mwili.

Kama  kuna  dawa, ikigusishwa  kwenye  ngozi  unga  hupukutika  na  kama  mzigo  hauna  dawa  za  kulevya  basi  hakuna  kitakachotokea....

Tayari  vifaa  hivyo  vimeanza  kutumika  katika  uwanja  wa  kimataifa wa  Julius  Nyerere.

Ifuatayo  ni  orodha  ya  wauza  unga  ambao   mahakama  imewaweka  chini  ya  uangalizi:


Source: Gazeti la Jamhuri.

Article 0

$
0
0
Hii ni Taswira ya Mji wa Njombe na Makazi yake Ambako wafanyabiashara hao wanalalamikia Ukosefu wa Nishaiti ya Umeme Katika Soko la Samaki.

Na Gabriel Kilamlya 

Wafanyabiashara wa Soko Kuu Wilayani Njombe Wamelalamikia Ubovu wa Miundombinu Sokoni Hapo Pamoja na Ukosefu wa Huduma Muhimu Kama Vile Maji na Umeme Hali Ambayo Wamesema Imechangia Kuzorotesha Biashara Sokoni Hapo.

Wakizungumza na www.gabrielkilamlya.blogspot.com Baadhi ya Wafanyabiashara Sokoni Hapo Wamesema Kuwa Ukosefu wa Umeme Sokoni Hapo Umekuwa Ukikwamisha Shughuli Zao Hasa Nyakati za Usiku Kutokana na Kukosa Ulinzi wa Uhakika.

Wamedai Kuwa Kukosekana Kwa Huduma ya Maji Kumesababisha Kushuka Kwa Ubora wa Bidhaa Zinazouzwa Sokoni Hapo Hasa Samaki Ambao Wamekuwa Wakihitaji Sana Maji Ili

Kuweza Kuwa na Ubora  Kwa Kipindi Chote Cha Soko

Kutokana na Hali Hiyo Wafanyabiashara Hao Wameiomba Serikali Kuwaboreshea Soko Hilo Kwa Kuhakikisha Upatikanaji wa Huduma ya Nishati ya Umeme na Maji Ambayo Mara Kadhaa Ilikwisha ahidiwa Kuboreshwa Bila Utekelezaji.

Edward Mdemu ni Afisa  Biashara Halmashauri ya Mji wa Njombe Amekiri Kuwepo kwa Changamoto Hizo Katika Soko Hilo na Kwamba Awali wafanyabiashara Hao waliomba Kuongezewa Mwanga wa Mabati hali iliyopelekea zoezi hilo Kufanikiwa

Pamoja na Mambo Mengine Bwana Mdemu Amewataka Wafanyabiashara Hao Kuwa wavumilivu na Kwamba atazifikisha Taarifa hizo kwa Mhandisi ili Ashughulikie Tatizo Hilo.  

Article 10

$
0
0

"LEO NITAWAANIKA VIGOGO WOTE AMBAO NI WAUZA UNGA ".....MWAKYEMBE.


Siku moja baada ya kufanya ziara ya ghafla Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amesema leo ataweka hadharani majina ya watu wanaosafirisha dawa za kulevya nchini.


Dk Mwakyembe juzi alifanya ziara hiyo JNIA kukagua utendaji kazi kwenye uwanja huo ikiwa ni siku chache baada ya kutokea kashfa ya kupitishwa kwa dawa za kulevya na baadhi ya Watanzania wakiwamo wasanii kukamatwa sehemu mbalimbali duniani.



Aidha, hatua ya waziri huyo imekuja siku tatu baada ya ahadi aliyotoa akiwa Mwanza kwamba katika kipindi cha wiki mbili kuanzia juzi, atahakikisha anawakamata vigogo wote walio katika mtandao wa usafirishaji na uingizaji wa dawa za kulevya kupitia viwanja vyote vya ndege nchini.



Akihutubia katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Vijana iliyoandaliwa na Taasisi ya Jitambue Foundation, yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Nyamagana, Dk Mwakyembe alisema yuko tayari kufa katika vita hivyo.



Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake jana, Dk Mwakyembe alisema: “Kesho (leo) nitawataja wanaojihusisha na dawa za kulevya. Kwa sasa nakamilisha ushahidi wa kutosha ikiwa ni pamoja na picha za wahusika.”



Aliwaonyesha waandishi wa habari picha ya mtuhumiwa mmoja ambaye alisema alikamatwa saa nane baada ya waziri huyo kufanya ziara uwanjani hapo. “Ninataka watu wafahamu wanaoliingiza taifa hili katika aibu hii, ambayo inasababisha Watanzania wasiaminike katika viwanja vya ndege vya mataifa mengine.”


“Hatuwezi kuwa taifa la kuogopaogopa, hii ni vita ya kusafisha nchi yetu, kwani ni nani mwenye mkataba na Mungu kuwa ataishi milele?” alihoji Waziri huyo alipokuwa akijibu swali kuwa suala la kuwataja watu wanaowafichua wasafirisha unga linaweza likaweka rehani maisha yake.

“Kama hupendi joto usiingie jikoni”, alisema.



Akizungumzia watendaji wa JNIA kuhusiana na dawa za kulevya, alisema: “Mfanyakazi yeyote atakayebainika kuhusika kuwasaidia wasafirisha unga atafukuzwa kazi na ambaye atafanya juhudi ya kuwakamata wasafirishaji hao atapewa zawadi.”



“Kuna watu wanadhani tunafanya mzaha katika jambo hili. Jana baada ya mimi kuondoka usiku wa saa 2:30 huyu (kijana aliyekamatwa) akaingia na mzigo,” alisema Dk Mwakyembe na kuongeza kuwa alikamatwa na kete 86 za dawa aina ya heroini na misokoto 34 ya bangi aliyokuwa akiisafirisha kwenda Italia kupitia Zurich.



Aliiagiza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kuwatunuku wafanyakazi waliofanikisha kukamatwa kwa kijana huyo.



Akizungumzia hali ya Uwanja wa JNIA baada ya kufanya ziara juzi, Dk Mwakyembe alisema tatizo halipo kwenye vitendea kazi, bali wafanyakazi wasiokuwa waaminifu.

“Tulikagua ili kujiridhisha kwa vifaa vilivyopo na tumeridhika kuwa kiwanja ni kizuri, hata Shirika la Kimataifa linalokagua viwanja vya ndege limeukubali kuwa uko vizuri katika vifaa kwa hiyo tatizo lipo kwa sisi wenyewe wenye dhamana.


“Ukaguzi huu utaendelea katika viwanja vyote hapa nchini mpaka bandarini na kila tutakayemkamata tutachapisha picha yake,” alisema Dk Mwakyembe.


Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, Watanzania 240 walikamatwa katika nchi za Brazil, Pakistan na Afrika Kusini huku wengine wawili wakikamatwa Hong Kong wakiwa na dawa za kulevya zenye thamani ya mabilioni ya fedha.


Akizungumzia kijana aliyekamatwa, mmoja wa askari ambaye hakupenda jina lake litajwe alisema: “Tulipewa taarifa za kiitelijensia saa tisa alasiri na raia mwema kuwa kuna mtu anasafiri na atafika uwanjani hapo kuanzia saa moja usiku na anasafiri kwenda Italia.


“Baada ya kupewa taarifa hizo tulijipanga na ilipofika saa 1:49 usiku alifika kijana mmoja, kwa kuwa tulishaelezwa wajihi wake, hatukupata shida, tulimchukua, tukamhoji na tulipompekua tulimkuta na kete 84.”

Kamanda wa Vikosi vya Uwanja wa Ndege, Deusdedit Kato akizungumzia tukio hilo alisema: “Alikuwa kwenye ukaguzi wa kawaida akiwa kwenye mstari na ilipofika zamu yake aliamriwa akae pembeni akafanyiwa upekuzi.

Alisema Mtanzania anatumia muda mwingi kukaa Italia na kwamba polisi wanaendelea kumfanyia mahojiano ili kujua alikozitoa na mhusika anayempelekea huko.


Alisema dawa hizo zimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kupimwa ili zifahamike ni za aina gani na anatarajiwa kufikishwa Mahakama ya Kisutu kati ya leo na Jumatatu kutegemea kukamilika kwa upepelezi.

-Mwananchi

Article 9

$
0
0

SHEIKH PONDA AONDOLEWA HOSPITALI NA KUPELEKWA GEREZA LA SEGEREA.

WAKILI WAKE ALAANI TUKIO HILO.


Wakili Nassor Jumaa anayesimamia Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda (54) ambaye kwa sasa anakabiliwa na kesi mpya ya kufanya uchochezi katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amezungumzia kitendo cha kumhamisha mteja wake kutoka hositalini hadi Segerea.

Leo hii majira ya saa 7 mchana nje ya viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar  es Salaam amesema kuwa amesikitishwa na hatua  ya vyombo vya dola kumuondoa Sheikh Ponda aliyekuwa amelazwa katika wodi ya Kitengo  cha Taasisi ya Tiba  ya Mifupa  na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu (MOI) alikokuwa akipatiwa matibabu na kisha kumhamishia katika gereza la Segerea.

Wakili Jumaa amesema amesikitisha na kitendo hicho kwani muda mfupi baada ya wakili mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka kumaliza kumsomea Sheikh Ponda shitaka linalomkabili, Hakimu Hellen Riwa alitoa amri ya kukaa chini ya ulinzi Sheikh Ponda aendelee na matibabu.

Jumaa akaongeza  kuwa   ameshangazwa kuona leo, wanausalama wamemtoa Sheikh Ponda wodini na kumpeleka katika gereza la Segerea na kwamba atalazimika kurudishwa tena mahakamani siku kesi yake itakapojatwa Agosti 28 mwaka huu, ambapo upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

“Kwa kweli kitendo hicho kime nisikitisha na kunishitua sana… ila tunatafakari ni hatua gani za kisheria tutazichukua huko siku za usoni,”alisema Jumaa.
 Kwa upande wao familia ya Sheikh Ponda wamesema wanalaani kitendo kilichofanywa na serikali cha kumuondoa ndugu yao hospitalini huku akiwa anaendelea kupata matibabu.

Msemaji wa familia hiyo Is-haq Rashid, alisema kutokana na hali hiyo kama familia wanalirudisha suala la Sheikh Ponda kwa uongozi wa jumuiya na Taasisi za kiislamu kwa ajili ya hatua zaidi ya kuhakikisha kiongozi mwenzao anakuwa salama.

“Uporaji huu wa mgonjwa unazidi kutupa mashaka juu ya dhamira ya serikali hasa ikiwa tunalituhumu jeshi la polisi katika kumdhuru Sheikh,hatujui kwanini kila wakati wanafanya mambo yao kwa kuvizia kama mwanzoni tuliwaomba viongozi wenzie wawe na subira juu ya yaliyotokea sasa tunaachia hili walizungumzie wao.”alisema Is-haq.

Wakati huo huo taarifa zilizopatikana zinaeleza kuwa viongozi wa Jumuiya na Taasisi zaKiislamu  walikuwa katika kikao kizito cha kujadili hatua hiyo ya kuporwa kwa Sheikh Ponda akiwa katika matibabu 

-Via  wavuti
Mpekuzi blog

Article 8

$
0
0

WATU 2,200 WAMERIPOTIWA KUUAWA LEO NA JESHI LA MISRI.

Посмотреть изображение в Твиттере

Harakati ya Ikhwanul Muslimin nchini Misri imesema jeshi la nchi hiyo leo Jumatano limewaua watu 2,200 baada ya kutumia nguvu kuvunja mkusanyiko wa wafuasi wa rais aliyepinduliwa, Mohammad Mursi katika eneo la Rabaa al-Adawiya katika mji mkuu wa nchi hiyo, Cairo.
 
Aidha Ikhwanul Muslimin kupitia tovuti yake ya ikhwanonline imesema zaidi ya watu 10,000 wamejeruhiwa katika vurugu hizo za leo.
 
Baadhi ya duru za Ikwanul Muslimin zimesema idadi ya waliouawa ni zaidi ya 2,600. Wizara ya Afya Misri imedai kuwa ni watu 149 waliouawa katika machafuko ya leo.

Huku hayo yakijiri makamu wa Rais wa Misri Mohammad el Baradei amejiuzulu kulalamikia mauaji hayo ya umati yaliyotekelezwa na jeshi.

Katika upande mwingine rais Adli Mansour wa serikali ya mpito Misri ametangaza hali ya hatari nchini humo kwa muda wa mwezi moja ujao.
Katika kulalamikia jinai za jeshi, wananchi waliokuwa na hasira wanaendeleza maandamano katika mikoa na miji mbalimbali ya nchi hiyo kama vile Asyut ,Ismailia na Alexandria.

Baadhi ya ripoti zinasema watu 15 wameuawa katika machafuko mabaya yaliyoibuka Ismailia na wengine 10 wamepoteza maisha huko Alexandria. Waandamanaji waliokuwa na hasira wamelaani hatua ya vikosi vya usalama kuwafyatulia risasi waandamanaji mjini Cairo.

Hii ni katika hali ambayo Sheikh Mkuu wa Chuo Kikuu cha Al-Azhar nchini humo, Ahmad al-Tayyib amewataka Wamisri wote kwa ujumla kudhibiti nafsi zao sambamba na kutumia akili katika kuamiliana na hali ya mambo.

TAMKO LA VIONGOZI WA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAMU BAADA YA KUTOLEWA HOSPITALI SHEIKH PONDA.

$
0
0
Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Rajan Katimba (katikati) akiongea na wanahabari
Wanahabari wakiwa kazini wakati wa mkutano huo.
Polisi wakidumisha ulinzi nje ya msikiti wa Mtambani ambapo mkutano umefanyika.
Mjumbe kutoka Organization of Scholers in Tanzania, Ally Basalleh naye akiongea wakati wa mkutano huo.
Wanajumuiya hao wakinena mara baada ya mkutano huo.
Taarifa iliyotolewa na Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini.
Viongozi wa  Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, leo wamekutana na wanahabari katika msikiti wa Mtambani Kinondoni jijini Dar, kujadili juu ya kutolewa hospitali katibu mkuu wa jumuiya hiyo, Sheikh Ponda Issa Ponda. Sheikh Ponda alichukuliwa na polisi kutoka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya Mifupa (MOI) jana majira ya saa nne na nusu asubuhi. Katika taarifa yao waliyoitoa kwa wanahabari, viongozi hao wamelaani kitendo hicho alichofanyiwa Sheikh Ponda na kuitisha mkutano wa dharura utakaofanyika Jumapili ya Agosti 18 mwaka huu majira ya saa 9 alasiri katika Viwanja vya Nuruh Yakin Temeke jijini Dar es Salaam ili kutafakari kwa pamoja na kuchukua hatua.
(PICHA NA DENIS MTIMA / GPL)

Article 6

$
0
0
 Kushoto ni Diwani wa Viti Maalumu Wa Tarafa ya Njombe Mjini Bi.Anjela Mwangeni Akiwa na Diwani wa Kata ya Yakobi Bi.Ester Mgeni Wakisani Kitabu Katika Ofisi za Mradi wa Maji Limage Wakati wa Wiki ya Maji

 Eng.Tembo Ambaye ni Makandarasi wa Maji Katika Miradi ya Limage na Igominyi.

 Mzee Maarufu Katika Kijiji cha Limage Akiishukuru Serikali Kwa Kuzindua Mradi wa Maji Wiki ya Maji Ambao Hadi sasa Hauja kamilika
 Diwani wa Kata ya Yakobi Bi.Ester Mgeni Akiwa na Wananchi wake Katika Kijiji cha Limage Mara Baada ya Kuzinduliwa kwa Mradi wa Maji Uliotakiwa Kukamilika Mwezi Julai.

Na Gabriel Kilamlya Njombe.

Serikali Imekiri Kuwa Ukosefu wa Fedha Unaotokana na Mfumo wa Kimtandao[EPICA] Umeendelea Kuwa Kikwazo Katika Utekelezaji wa Miradi Mbalimbali ya Maendeleo Ikiwemo Mradi wa Maji wa Limage-Igominyi Uliozinduliwa Wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Maji Mwaka Huu.

Aidha Serikali Imesema Kuwa Inaendelea na Jitihada Mbalimbali Kuhakikisha Mradi Huo Unakamilika Kwa Wakati Ili Kuwawezesha Wananchi wa Vijiji Hivyo Kupata Huduma ya Maji Safi na Salama na Kuondokana na Kero Inayowakabili Kwasasa.

Mhandisi wa Maji Halmashauri ya Mji wa Njombe Bw Job Mwakasala Amesema Kuwa Awali Mradi Huo Ulitarajiwa Kukamilika Mwezi July Mwaka Huu Lakini Kutokana na

Matatizo ya Kifedha Yanayotokana na Mfumo wa Kimtandao[EPICA] Kwa Kushindwa Kufunguka Umeshindwa Kukamilika Kama Ilivyokusudiwa na Hivyo Kulazimika Kuongeza Muda wa Siku 45 Ili Kuweza Kukamilisha Mradi Huo.

Amesema Pamoja na Upungufu Huo wa Fedha Bado Wamefanikiwa Kumlipa Mkandarasi Kwa Malipo ya Awali na Hivyo Wamekusudia Kuhakikisha Wanakamilisha Malipo ya Awamu ya Pili Ili Kumuwezesha Kuendelea na Ujenzi na Kukamilisha Mradi Huo.

Ameongeza Kuwa Kwasasa Wanaendelea na Kazi ya Kupitia Vyanzo Vya Maji na Kusafisha Matanki Ili Yaweze Kutumika Katika Usambazaji wa Maji na Kuongeza Kuwa Huduma ya Maji Kwasasa Itaendelea Kupatikana Kupitia Mabomba Yaliopo Katika Vijiji Hivyo.

Hata Hivyo Amesema Mradi Huo Unatarajiwa Kukamilika Agost 20 Mwaka Huu na Hivyo Amewataka Wananchi Kuhakikisha Wanaitunza Miundombinu Yake na Kuchangia Mradi Huo Ili Uweze Kuwa Endelevu.

Article 5

$
0
0
MADAWA YA KULEVYA GUMZO TANZANIA

WATANZANIA ambao idadi yao inaweza kupita mamia, wameshanyongwa nchini China kutokana na kupatikana na hatia ya kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.
Mkuu wa Jeshi la Polisi, Kitengo cha Kuzuia na Kudhibiti Madawa ya Kulevya, Godfrey Nzowa.
Ripoti maalum ya madawa ya kulevya, iliyofanyiwa kazi na gazeti hili kwa kukusanya taarifa ndani ya nchi, Afrika Kusini na China kwenyewe, inaweka hadharani siri ya mamia ya Watanzania kunyongwa.

Katika ripoti hiyo, inaonesha kwamba mataifa ya Afrika Kusini na Uganda, yapo mstari wa mbele kuripoti taarifa za raia wao kunyongwa China lakini Tanzania imekuwa
ikisuasua.
Sharifa Mahmoud, yupo nchini Misri.
“Huu ukimya wa serikali yetu, unafanya wengi kukosa taarifa sahihi, matokeo yake wanajiingiza kwenye biashara hiyo haramu ambayo mtu akikamatwa tu China na akikutwa na hatia lazima anyongwe,” alisema Joel Mabruki, mfanyabiashara wa nguo na simu kati ya Tanzania na China.
Mabruki aliongeza: “Kama serikali yetu ingekuwa na utaratibu wa kutangaza kila Mtanzania anayenyongwa China, pengine vijana wengine wangeogopa na baadhi yao wangeacha kabisa. Hivi sasa idadi inaongezeka kwa sababu hawaambiwi ukweli.”

KITENGO CHA MADAWA YA KULEVYA KINAJUA
Kwa mujibu wa Mkuu wa Jeshi la Polisi, Kitengo cha Kuzuia na Kudhibiti Madawa ya Kulevya, Godfrey Nzowa, ofisi yake inazo taarifa kuhusu Watanzania kunyongwa China lakini akatupa mpira kwa Mkurugenzi wa Kuzuia na Kudhibiti Madawa ya Kulevya, Christopher Shekiondo.
“Kuhusu idadi na majina, hilo suala aulizwe mkurugenzi. Ila ukweli ni kwamba Watanzania wengi wanakamatwa China na wananyongwa,” alisema Nzowa.

MAAFA PAKISTAN
Kwa upande mwingine, Nzowa alisema kuwa watu wanaizungumzia sana China lakini ukweli ni kwamba nchi nyingine ambayo inanyonga Watanzania wengi ni Pakistan.
Nzowa alisema kuwa pengine taarifa za Pakistan hazipatikani sana kutokana na mwingiliano wa Tanzania na nchi hiyo, tofauti na China ambayo Watanzania wanakwenda na kurudi kila siku iendayo kwa Mungu.
“Tunaposema madawa ya kulevya ni janga kubwa inafaa ieleweke hivyo. Watanzania wanaonyongwa China na Pakistan ni wengi sana. Tuwe makini juu ya hili na tuzingatie kwelikweli,” alisema Nzowa.

Dawa za kulevya.
TAARIFA ZA MITANDAO YA KIJAMII
Tofauti na mataifa mengine ambayo ripoti za raia wao kukamatwa na kunyongwa China hutolewa rasmi na balozi zao, hapa Tanzania, habari huenezwa na mitandao ya kijamii.
Mfano; mitandao ya kijamii ndiyo pekee iliyoripoti kuhusu kunyongwa kwa mrembo mwanamitindo (jina tunalo) aliyeshiriki video ya wimbo Twende Zetu wa mwanamuziki Saidi Juma ‘Chegge’, aliyewashirikisha Amani James Temba ‘Mheshimiwa Temba’, Feruzi Mrisho Rehani ‘Ferouz’ na Yessaya Ambilikile ‘YP’.
Vilevile, alipokamatwa aliyewahi kushika nyadhifa za makamu mwenyekiti na katibu msaidizi kwenye Klabu ya Simba (jina tunalo), mitandao ya kijamii iliandika bila serikali kutoa tamko rasmi.
Hata hivyo, kutokana na kukosekana na taarifa rasmi kutoka serikalini, mitandao ya kijamii ilitoa habari zenye kushitua, nyingine ikidai mtu huyo aliyewahi kuwa kiongozi wa Simba alifungwa miaka 70 jela, nyingine ikieleza kwamba tayari alishanyongwa.

MWAKALEBELA ATOA USHUHUDA WAKE
Katibu Mkuu Mstaafu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Frederick Mwakalebela, alipozungumza na gazeti hili, alisema kuwa kati ya mwishoni mwa mwaka 2009 na mwanzoni mwa 2010, alikwenda China katika safari ya kikazi.
“Nikiwa kule, niliambiwa taarifa za Watanzania wengi ambao walinyongwa baada ya kukutwa na hatia ya kujishughulisha na biashara ya madawa ya kulevya,” alisema Mwakalebela.
Alipoulizwa kuhusu kiongozi huyo wa Simba, Mwakalebela alijibu: “Nikiwa China niliambiwa amenyongwa. Niliporudi hapa nchini ndiyo nikasikia amefungwa miaka 70.”
Mwakalebela aliongeza: “Ukweli ni kwamba kwa taarifa nilizopata nikiwa China, Watanzania wengi sana wananyongwa kwa sababu ya madawa ya kulevya. Naweza kusema ni mamia. Ikiwa kwa muda mfupi niliokuwepo pale nimeambiwa karibu watu 10, je mwaka mzima inakuwaje?”

WENGINE WANAPONZWA NA WANIGERIA
Mfanyabiashara Mtanzania, Hashim Rau, ambaye hufanya biashara zake kati ya Tanzania, Afrika Kusini na China, alisema kuwa kuna Watanzania walinyongwa baada ya kuponzwa na Wanigeria.
Rau alisema, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa O. R. Tambo, uliopo nje kidogo ya Jiji la Johannesburg, umewasababisha matatizo Watanzania wengi kutokana na tabia yao ya ukarimu.
Agnes Gerald 'Masogange' aliyekamatwa na madawa Afrika Kusini.
Alisema: “Mtanzania anaweza kutoka na biashara yake kuja kuuza Afrika Kusini, baada ya hapo anapanda ndege ya moja kwa moja kwenda China. Akiwa uwanja wa ndege anakutana na Mnigeria muuza madawa ya kulevya.
“Mtanzania anakuwa hana mizigo mingi, kwa hiyo yule Mnigeria anamwomba Mtanzania amsaidie kupitisha begi lake moja kwenye mzani, akidai kuwa yeye mizigo yake ni mingi, anaogopa atatozwa fedha nyingi.
“Kumbe lile begi linakuwa na unga. Sasa Mtanzania kwa kutojua, atakubali, baada ya hapo lile begi litaandikwa jina la Mtanzania. Mbele ya safari kama litavuka salama, Mnigeria atamshukuru Mtanzania na kuchukua begi lake lakini likikamatwa, Mnigeria atakimbia, Mtanzania atabaki na mashtaka ambayo mwisho wake ni kunyogwa China.”
Akisimulia ushuhuda wake, Rau alisema kuwa aliwahi kuombwa msaada wa aina hiyo na Mnigeria mmoja lakini alipotaka kukagua begi lina nini ndani alikataa.
Melisa Edward aliyekamatwa na Masogange Afrika Kusini wakiwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8.
“Alipokataa nikague ndani ya begi kuna nini nami nikamkatalia kumsaidia kwa sababu naujua mchezo wao. Sasa pale uwanjani alikuwepo Mtanzania mwingine mwenye asili ya Tanga (jina tunalo), alipoombwa na yule Mnigeria alikubali.
“Nilijitahidi kumwonesha ishara hakunielewa, mwisho nikamwambia asikubali lakini hakunielewa. Tulipofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Guangzhou Baiyun, China, yule Mtanga alikamatwa baada ya lile begi kukutwa na madawa ya kulevya mchanganyiko wa heroine, cocaine na methamphetamine.
“Kama kawaida, yule Mnigeria alitoweka. Mimi niliujua ule mchezo lakini nilijiweka pembeni kwa sababu ningejionesha najua chochote au namtambua yule Mtanga ningeshikiliwa. Tena pengine na mimi ningekuwa nimeshanyongwa siku nyingi zilizopita kwa sababu hiyo ni kesi ya mwaka 2008.
“Watanzania wajue kwamba China hakuna mchezo, hawana muda wa kufuatilia ushahidi, ukikutwa na unga, ikithibitika hivyo, kwao huo ni ushahidi tosha kwamba wewe ndiye mmiliki na unanyongwa,” alisema Rau.

PEMBE TATU HATARI
Uchunguzi wa gazeti hili kwa kufanyia kazi matukio ya Watanzania kukamatwa na madawa ya kulevya, umebaini kuwa pembe tatu hatari imetengenezwa na wauza unga katika nchi za Tanzania, Afrika Kusini na China.
Imebainika kwamba wafanyabiashara wa madawa ya kulevya, wamekuwa wakisafirisha idadi kubwa ya madawa hayo kwenda Afrika Kusini ambako husafirishwa kwa mafungu kwenda China.
Ripoti za hivi karibuni, zinaongeza nguvu katika madai kwamba Tanzania na Afrika Kusini, kuna udhaifu mkubwa wa udhibiti wa madawa ya kulevya ndiyo maana wafanyabiashara huingiza na kusafirisha mizigo mikubwa kwa urahisi.
Kutokana na hali hiyo, wafanyabiashara hao husafirisha madawa ya kulevya yenye uzani mkubwa tena kupitia katika viwanja vya ndege kisha kuziweka katika mafungu madogomadogo kwenda China na kwingineko ambako mahitaji ni makubwa na bei ni nzuri.
Uchunguzi umebaini kuwa sheria kali za China za kudhibiti madawa ya kulevya, zinasababisha uhaba mkubwa wa mihadarati ndani ya nchi hiyo, kwa hiyo anayefanikiwa kupitisha, huuza kwa bei kubwa sana.

WATUMWA WENGI NI WANAWAKE
Mwanamke, Janice Bronwyn Linden, 38, raia wa Afrika Kusini, alinyongwa China mwaka 2011, baada ya kukutwa na hatia ya kusafirisha madawa ya kulevya aina ya methamphetamine yenye uzito wa kilogramu tatu.
Nobanda Nolubabalo, 23, raia wa Afrika Kusini, alikamatwa Uwanja wa Ndege wa Suvarnabhumi, Bangkok, Thailand, akiwa ameficha cocaine zenye uzani wa kg 1.5.
Nobanda Nolubabalo raia wa Afrika Kusini, aliyekamatwa Uwanja wa Ndege wa Suvarnabhumi, Bangkok, Thailand, akiwa ameficha cocaine zenye uzani wa kg 1.5.
Watanzania, Agnes Gerald na Melisa Edward, hivi karibuni walikamatwa Afrika Kusini, wakiwa na mzigo wa madawa ya kulevya aina ya methamphetamine, yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8.
Mtanzania mwingine, Sharifa Mahmoud, yupo nchini Misri akisubiri adhabu ya kunyogwa, baada ya kukutwa na hatia ya kuingiza nchini humo, madawa ya kulevya aina ya heroine.
Saada Ally Kilongo, ni mwanamke mwingine wa Kitanzania ambaye hivi karibuni alikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam, akiwa na madawa ya kulevya aina ya methamphetamine yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 170.
Zahra Thomas, kutoka Visiwa vya Sao Tome, alikamatwa mwaka jana, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hong Kong, akiwa na mzigo wa heroine wenye uzito wa kilogramu 12.
Mnigeria, Helen Okechukwu, alinaswa Falme za Kiarabu akiwa na madawa ya kulevya aina ya cocaine, uzani wa kg 20.
Mifano hiyo, inatosha kuonesha jinsi wanawake wanavyotumiwa na wauza unga kusafirisha mizigo yao kwa imani kwamba mwanamke ni rahisi kupita sehemu za ukaguzi bila kushtukiwa, vilevile kukwepa dhuluma.

MSEMAJI WA POLISI
Msemaji wa polisi nchini, Advera Senso, aliliambia gazeti hili wiki iliyopita kuwa Watanzania wengi wananyongwa China kwa sababu ya hatia ya kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.
“Majina ya wahusika kwangu hayapo. Ila nafahamu kuwa wengi wananyongwa,” alisema Senso.

NI SIRI KUBWA
Habari zinasema kuwa mara nyingi utekelezaji wa adhabu ya kifo China ni siri lakini ubalozi wa Tanzania hujulishwa.
“Ila mara nyingi wauza madawa ya kulevya husababisha mkanganyiko wa uraia kutokana na kuwa na hati hata tatu, hii husababisha ubalozi wa Tanzania China ubaki na siri ya mtu aliyenyongwa bila kujulishwa ndugu zake,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:
“Ikitokea ndugu wanaulizia hapo hupewa taarifa kamili kuhusu taarifa za ndugu yao kama ameshanyongwa au bado anatumikia kifungo.”
Chanzo chetu kilibainisha kuwa mbali na kunyongwa, vilevile hutokea vifo vya kimafia, kwani wauza unga huuana wao kwa wao ili kudhulumiana.
“Ikitokea mtu ameuawa, taarifa zikifika ubalozini, zinafuatiliwa lakini kama hazieleweki hubaki siri,” kilisema chanzo.

STORI YA MKUMBUKWA
Aprili mwaka jana, kijana wa Kitanzania, Mkumbukwa John Shayo, aliuawa China na maiti yake ilikaa mochwari mwaka mzima, kabla ya kuletwa nchini mwaka huu na kuzikwa mkoani Mwanza.
Mkumbukwa, anasadikiwa kuuawa na mtandao wa wauza madawa ya kulevya, ingawa haijulikani sababu yake ni nini.
Marehemu Mkumbukwa John Shayo aliyeuawa China.
TUNACHUNGUZA
Gazeti hili linaahidi kupita kila panapotakiwa ili kukamilisha orodha kamili ya Watanzania walionyongwa China kisha ripoti hiyo, tutaichapisha katika matoleo yajayo.

CHINA YAONGOZA KWA KUNYONGA
Chati iliyopo ukurasa wa kwanza ni takwimu za Shirika la Kimataifa la Haki za Binadamu, Amnesty International mwaka jana ambayo inaonesha kwamba China ndiyo kinara wa kunyonga watu duniani ambapo inanyonga maelfu kila mwaka kwa makosa mbalimbali ikiwemo kusafirisha madawa ya kulevya, ikifuatiwa na Pakistan na Falme za Kiarabu

chanzo the global

KIVUKO CHA KIGAMBONI CHATEMBELEWA NA NAIBU WAZIRI WA UJENZI ENG.GERSON LWENGE LEO.

$
0
0

Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge(kushoto) akisikiliza taarifa kutoka kwa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya TAMESA ,Masel Magesa (kulia) wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea leo Kivuko cha Kigamboni kuangalia kuona mfumo mpya wa ukatishati tiketi. Kivuko hicho kinasafirisha zaidi ya watu 50 elfu kwa siku.


Mweka Hazina wa Kivuko cha Kigamboni Juliet Julius(kushoto) akimuonyesha Naibu Waziri wa Ujenzi ,Mhandisi Gerson Lwenge(mwenye suti) jinsi ya mfumo mpya wa ukatishaji wa tiketi katika Kivuko hicho leo jijini Dar es Salaam. Mfumo huo umeboresha ukataji wa tiketi naumesaidia kupunguza msongamano pamoja na kuongezeka kwa makusanyo kuliko awali .Pichani (alievaa gauni la kitenge) ni Mtendaji Mkuu waMamlaka ya TAMESA , Masel Magesa, (kulia) Mkuu wa Kivuko cha Kigamboni Charles Irege.

Mkuu wa Kivuko cha Kigamboni Charles Irege (mbele aliesimama kulia) akionyesha mfumo mzima mpya wa ukatishaji wa tiketi leo kwa Mh, Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge (kulia) pamoja na baadhi ya waandishi wa habari . Mfumo huo umepunguza msongamano kwa wanachi wanaotumia kivuko hicho na kufurahia huduma nzuri ziinazotolewa na serikali ya Tanzania.


Baadhi wa wananchi wakisubiri kivuko baada ya kukata tiketi zao. Leo jijini Dar es Salaam.Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO

Article 3

$
0
0

Tshs, MILIONI 100 Kutumika ktk UJENZI WA KITUO CHA AFYA IKUNA .

DIWANI WA KATA YA IKUNA AKIWA PAMOJA NA WAJUMBE WA BARAZA LA KATA KUKAGUA JENGO LA KITUO CHA AFYA KINACHOJENGWA KATIKA KIJIJI CHA IKUNA



HIKI NI KITUO CHA AFYA CHA IKUNA AMBACHO KINAENDELEA KUJENGWA










DIWANI KATA YA IKUNA VALENTINO HONGORI AKIZUNGUMZA NA WAJUMBE WA BARAZA LA KATA IKUNA



WAJUMBE WA BARAZA LA KATA HIYO WAKIWA KWENYE MSAFARA KURUDI OFISINI KWAO

AFISA MTENDAJI WA KATA YA IKUNA AKIWAKARIBISHA WAJUMBE  KUANZA KUJADILI  MAENDELEO YA KATA

WAJUMBE WA BARAZA LA KATA HIYO WAKIWA KATIKA OFISI YA KATA WAKIENDELEA KUJADILI MAENDELEO YA KATA IKUNA
WAJUMBE WA KIKAO CHA KAMATI YA MAENDELEO YA KATA KAMAKA


 AGENDA MBALIMBALI ZILIWEKWA UBAONI

Na Michael Ngilangwa


Wajumbe wa kikao cha baraza la Kata ya Ikuna KAMAKA jana wamekagua ujenzi wa mradi wa kituo cha afya kinachojengwa katika kijiji cha Ikuna ambapo pamoja na mambo mengine kituo hicho kinatarajia kugharimu takribani shilingi milioni mia nmoja hadi kukamilika kwake.

Akizungumza na wajumbe wa baraza la kata mwenyekiti wa kikao cha baraza hilo bwana Valentino Hongori amesema kuwa hadi sasa shingi milioni hamsini zimetolewa na halmashauri ya wilaya ya Njombe kupitia mfuko wa afya MAM ambapo ujenzi huo bado unaendelea.


Aidha bwana Hongori amesema kuwa fedha hiyo imetokana na bajeti ya mwaka wa fedha wa 2012/2013 na kwamba katika bajeti ya mwaka 2013/2014 wanategemea kupatiwa shilingi milioni 50 itakayokamilisha jumla ya shilingi milioni mia 100 ya ujenzi wa kituo hicho cha afya huku wananchi wakishiliki kujitolea nguvu katika uchimbaji wa mawe na kazi nyinene.


Akizungumza mbele ya wajumbe hao afisa mtendaji wa kata ya Ikuna bwana Jobu Fute amesema kuwa kila kiongozi wa serikali ya kijiji na vitongoji katika kata hiyo wanatakiwa kuhakikisha kila mwananchi anachangia mchango wa ujenzi wa miradi mbalimbali inayotekelezwa katika kata hiyo ikiwemo ujenzi wa madarasa na nyumba za walimu katika shule ya sekondari Ikuna.


Aidha bwana Fute amesema kila mwananchi anatakiwa kuhudhuria katika mikutano inayoitishwa na viongozi wao wa serikali za vijiji ili kuenda sawa na katika kutekeleza maazimo kwani kumekuwa na tabia ya baadhi ya wananchi kushindwa kuhudhuria mikutano hali inayopelekea kuhoji maswali ambayo yalikwisha kujibiwa pamoja na kusomewa hesabu za  mapato na matumizi.


WATANZANIA TUNAJIFUNZA NINI KATIKA PICHA HII?

$
0
0
 
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Rais Joyce Banda wa Malawi muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Lilongwe tayari kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi za SADC
 
 

Article 1

$
0
0

'WALIOBA'TUME YA KATIBA HAISHAWISHI WANANCHI KUKUBALIANA NA RASIMU.




Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akiwa na baadhi ya Wajumbe wa  Baraza la Katiba la Manispaa ya Morogoro leo (Jumamosi, Agosti 17. 2013). Mwisho kulia ni Mjumbe wa Tume hiyo Bw. Omar Sheha.

Mjumbe wa Baraza la Katiba la Manispaa ya Morogoro ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Dkt. Modesta Opiyo akitoa maoni katika mkutano wa Baraza hilo uliofanyika katika Chuo cha Ualimu Kigurunyembe leo (Jumamosi, Agosti 17, 2013).

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Katiba la Manispaa ya Morogoro wakifuatilia mkutano wa baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Kigurunyembe mjini Morogoro leo (JUmamosi, Agosti 17, 2013).

Mjumbe wa Baraza la Katiba la Manispaa ya Morogoro Bi. Mary Nzara akitoa maoni katika mkutano wa Baraza hilo uliofanyika katika Chuo cha Ualimu Kigurunyembe leo (Jumamosi, Agosti 17, 2013).

Mjumbe wa Baraza la Katiba la Manispaa ya Morogoro Bw. Dotto Rangimoto (27) akitoa maoni katika mkutano wa Baraza hilo uliofanyika katika Chuo cha Ualimu Kigurunyembe leo (Jumamosi, Agosti 17, 2013).
...............................................................................................................................



Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba Amesema Tume Yake Haishawishi Wananchi Kukubali Mapendekezo Yaliyomo Katika Rasimu ya Katiba Waliyoiandaa Kama Inavyodaiwa na Baadhi ya Watu Badala Yake Tume Hiyo Hulazimika Kutoa Ufafanuzi Pale Inapohitajika.

Jaji Mstaafu Warioba Ametoa Ufafanuzi Huo Hii Leo Mjini Morogoro Wakati Akijibu Swali la Mmoja wa Wajumbe wa Baraza la Katiba la Manispaa ya Morogoro Aliyeomba Ufafanuzi wa Tume Kuhusu Kauli za

Baadhi ya Wanasiasa Kuwa Tume Hiyo Inashawishi Wajumbe wa Mabaraza Kukubali Rasimu ya Katiba Iliyotolewa.

Akielezea Itikadi ya Ujamaa Ndani ya Katiba Sasa , Jaji Mstaafu Warioba Amesema Tume Yake Imependekeza Katika Rasimu ya Katiba Kuwepo Kwa Dira na Malengo ya Taifa Ambayo Yatapaswa Kkutekelezwa na Serikali ya Chama Chochote Kitakachokuwa Madarakani.

Aidha Mwenyekiti Huyo wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Amewapongeza Wananchi na Wajumbe wa Mabaraza Wanaohoji Juu ya Masuala Mablimbali Yaliyomo Ndani ya Rasimu Kwa Lengo la Kupata Ufafanuzi Zaidi.

Katika Hatua Nyingi Baraza la Katiba la Manispaa ya Morogoro Hii Leo Limemaliza Mkutano Wake wa Siku Tatu Uliohudhuriwa na Wajumbe 155 Kutoka Kata 29 za Manispaa Hiyo Huku Baraza la Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Likitarajiwa Kuanza Mkutano Kama Huo Agosti 19 Mwaka Huu


Kwa Hisani ya Francisgodwinblog
.............................................................................................................................................

MPIGA DEBE ASIYE NA SARE ATAKAMATWA KWA UZULULAJI NJOMBE

$
0
0
 
 Kwa Mara Nyingine Tena Uongozi wa Kituo cha Mabasi cha Njombe Mjini Kimewataka Wafanyakazi na Mawakala wa Mabasi Kituo Hapo Kuvaa Sare Maalum Zinazoonesha Ofisi za Kampuni Wanazofanyia Kazi.

Agizo Hilo Limetolewa na Mwenyekiti wa Kituo Hicho Bw. Agustino Mgeni Maarufu Kwa Jina la Guoguo Wakati Akiongea na Wafanyabiashara wa Kituo cha
Mabasi cha Njombe Mjini na Kwamba Sare Hizo Zitasaidia Kuwabaini Watu Wanojihusisha na Vitendo Vya Uhalifu Dhidi Wasafiri Katika Kituo Hicho.

Aidha Uongozi Huo Pia Umewataka Madereva wa Magari Yanayofanya Shughuli za Usafirishaji wa Abiria na Mizigo Kufuata Sheria na Taratibu za Kuengesha Magari Katika Kituo Hicho.

Kwa Upande Wake Kaimu Afisa Mkuu wa Kituo cha Polisi  cha Njombe Salum Mkalah Ambaye Pia ni Mkaguzi Katika Tarafa za Njombe na Igominyi Amesema Kumekuwepo na Tabia za Baadhi ya Madereva Hao Kuegesha Magari Yao Pasipo Kufuata Utaratibu na Kupelekea Vurugu Baina ya Wafanyabisha wa Kituoni Hapo na Madereva Hao

..........................................................................................................................................


WAUMINI WAKUBALI YAISHE UJENZI WA KANISA NJOMBE.

$
0
0












Kama Maandiko yanavyosema Mwenye Nacho Huongezewa na Ombeni Mtapewa Basi Maandiko Hayo Yamejidhilisha Pale Wakati wa Harambee ya Ujenzi wa Kanisa la Lutherani Katika Kitongoji cha Makungu Kijiji cha Igwachanya Wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe Ambapo Idadi ya watu na Kiasi Cha Fedha Kilichopo patikana Huwezi Kuamini Kwa Macho yako Kama Sio Tomaso.

Zaidi ya Shilingi Milioni Mbili Pamoja na Ahadi zimeweza Kupatikana Jana Katika Harambee ya Ujenzi wa Kanisa la KKKT Mtaa wa Nazareth Usharika wa Usuka Wilayani Wanging'ombe,Kiserikali ni Kitongoji cha Makungu Kijiji cha Igwachanya Kata ya Igwachanya Kufuatia Udogo wa Kanisa Lililopo na Kupelekea Waumini Hao Kutumia Hema Katika Kuendeshea Ibada zao siku Zote za Bwana Kwa Kipindi cha Miaka Mitatu Sasa.

Aidha Wananchi na Waumini wa Kitongoji Hicho Wameeleza Kutumia Hema Hilo wakati wa Jua na Mvua Katika Ibada zao Hali Iliyopelekea Kuchukua Uamuzi wa Kuanza Kujenga Kanisa Ambalo lipo katika Hatua za Awali za Msingi na Kisha Kuamua Kuitisha Harambee ya Kuchangia Ujenzi Huo.

Risala ya Ujenzi wa Kanisa Hilo Iliyosomwa na Mwanjilisti wa Igwachanya Bi.Lonika Yelemia Yombwi Imebainisha Malengo ya Dhati Katika Kujenga Kanisa Hilo Litakalo Gharimu zaidi ya Shilingi Milioni Kumi Hadi Kukamilika kwake na Kwamba Waumini wa Mtaa Huo Tayari wameshaanza Kwa Kuandaa Tofali Elfu Kumi,Mawe Pamoja na Kukamilisha Ujenzi wa Msingi

Kufuatia Taarifa Hiyo iliyoibua Hisia za Waumini na Wageni Mbalimbali walioshiriki Harambee Hiyo Ilimfanya Mgeni Rasmi Bwana Belshaza Muhanga Ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Igwachanya Kutoa Neno Lililomgusa Kila Mmoja Hadi Kupelekea Kufanikisha Zaidi ya Shilingi Milioni Mbili.

Miongoni Mwa Maneno yaliyosemwa na Bwana Belshaza Kutoka Kwenye Maandiko Matakatifu ni Pamoja na Kwamba Kushindwa Kutoa Sadaka Kubwa Wakati Unayo ni Kumuibia Mwenye Mungu Kwani Kila Kitu ni Mali yake,Maneno Ambayo yalitabiri Ukweli Katika shughuli Hiyo Muhimu na Kufanikisha Kiasi Hicho.

Mara Baada ya Kuzungumza na Kuchangia Mchango wake Huo Pamoja na Ahadi ya Shilingi Laki Mbili Kutoka Kwa Mbunge wa Jimbo la Njombe Magharibi Mhandisi Gerson Lwenge Ndipo Bwana Belshaza Akasimama na Kutangaza Mafaniko ya Harambee Hiyo.

Kwa Upande wake Mchungaji wa Usharika wa Usuka Ambaye Alishiriki Ibada Hiyo Bwana Gideon Mtagawa Amepongeza Jitihada Kubwa na Mafanikio yaliyopatikana Kupitia Mgeni Rasmi Aliyeweza Kuhamasisha Harambee Hiyo.

Ombeni Nanyi Mtapewa,Njooni Kwangu Msumbukao na Mnaolemewa Na Mizigo nami Nitawapumzisha.

Article 2

$
0
0

Mwanamke avunjwa nyonga na kunyolewa nywele kwa kisu na mume wake.


Tajiri ambaye ni mfanyabishara mkubwa katika maduka ya Kariakoo, Dar aliyetajwa kwa jina moja la Urio anadaiwa kumvunja nyonga na kumjeruhi mkewe Eva Pascal anayeuguza majeraha kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Akizungumza kwa uchungu akiwa wodini hospitalini hapo, Eva au mama Tina alisema kuwa tukio hilo lilitokea hivi karibuni nyumbani kwao Kimara-Temboni, Dar.


Mama Tina alisimulia kuwa siku ya tukio mumewe alikuwa ana siku kadhaa hajarudi nyumbani hivyo akamfuata katika Baa ya Temboni Resort kwa ajili ya kumuuliza sababu za kushindwa kurudi nyumbani.

Alisimulia huku akitokwa machozi: “Nilipofika tu nikamuuliza swali hilo, alinitandika kofi kisha akanipiga ngumi ya jicho hadi nikazimia.


“Nilishangaa nilipozinduka na kuwakuta manesi wamenizunguka. Nilipomuuliza mume wangu imekuwaje aliniambia eti nililewa na kuanguka ndiyo sababu nipo hapa.

“Kiukweli baba Tina ananinyanyasa sana, ananipiga hadi kufikia hatua ya kuniunguza na pasi. Kwa sasa naiona ndoa ni mateso makubwa na Mungu akinijalia nikapona, sitarudi tena katika mateso haya, nimechoka jamani.
 

“Ni baba Tina huyuhuyu aliwahi kuninyoa nywele na kisu eti kisa tu nilimcheleweshea supu ambayo ilikuwa bado haijaiva ikiwa jikoni. Alinichukua akaniingiza chumbani akaninyoa nywele na kisu kisha akaniingiza bafuni akaniosha na maji baridi eti akidai nywele hizo zilikuwa zinanipa kiburi.
 

“Yaani nikikorofishana naye kidogo tu ananitupia kila kitu nje na kufunga chumba chetu cha kulala.”


Baada ya kusikia upande wa mama Tina, Ijumaa ilimgeukia baba Tina ambaye alikanusha kumpiga mkewe lakini akakiri kuwa aliwahi kumpiga na kumchoma na pasi huko nyuma ingawa walishakaa na kuyamaliza mambo hayo.
 

“Safari hii sijampiga kabisa, alikuja baa akanifanyia fujo, alikuwa amelewa sana, baadaye alianguka na kuumia ndiyo nikampeleka hospitalini, hayo mengine watu wananisingizia tu,” alisema baba Tina.

Hata hivyo, mwandishi wetu hakuishia  hapo kwani alitinga eneo la Kimara-Temboni nyumbani kwa wanandoa hao na kuzungumza na baadhi ya majirani ambao walikiri kuwa mama Tina alipigwa na amekuwa akinyanyaswa na mumewe kiasi cha kufikishana polisi.

Wanahabari wetu walifika polisi katika kituo kidogo cha Kimara-Temboni ili kupata taarifa ya tukio hilo ambapo walisema kuwa Urio alifika kituoni hapo akiwa na mkewe mahututi na kuomba PF-3 ambapo walimpa na kumsihi mgonjwa akishapokelewa hospitalini airudishe lakini siku iliyofuata alikwenda pale na kusema kuwa mgonjwa anaendelea vizuri.

-GPL
Mpekuzi blog

Article 1

$
0
0

SHEIKH PONDA ALIVYOFIKISHWA MAHAKAMANI MOROGORO LEO



Sheikh Issa Ponda Akiondoka mahakamani mara baada ya kusomewa mashtaka matatu na kesi yake imehairishwa Hadi  tarehe 28.08.2013
Ulinzi Ukiwa umeimarishwa mahakamani leo 
Sheikh Issa Ponda Akiwa mahakamani mkoani Morogoro asubuhi ya leo Sheikh Ponda Amesomewa Mashtaka Matatu katika Mahakama ya mkoa wa Morogoro Likiwemo la uchochezi alilolitoa Kwenye  Mkutano wa Hadhara Tarehe 10 mwezi huu Ambapo Inadaiwa alisema kwamba ”Ndugu waislamu 
 
Msikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za Misikiti kwani kamati hizo zimeundwa na Bakwata ambao ni vibaraka wa Serikali ”katika viwanja vya shule ya kiwanja cha ndege Mkoani Morogoro.Baada ya kusomewa Mashitaka hayo Mahakama imesema Upelelezi Umekamilikaa Dhamana Imefungwa  na Amerudishwa Rumande Mpaka tarehe 28 mwezi huu ambapo kesi hiyo itaanza kusikilizwa katika Mahakama ya Mkoa wa Morogoro..Picha Na MATUKIO NA MICHAPO BLOG
Viewing all 2276 articles
Browse latest View live