Na Esther Macha,wa  matukio  daima  Mbeya
WATU wawili wamefariki dunia katika matukio tofauti Mkoani Mbeya likiwemo  la dereva wa boda boda aitwaye Osward Yohana (17)kuwawa kikatili kwa kukatwa mapanga na  kutobolewa macho kwa wivu wa kimapenzi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo  Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya ,Diwani Athuman alisema kuwa katika tukio la kwanza dereva boda boda  ambaye ni mkazi wa kijiji cha Muhela  wilaya ya Mbarali  alikutwa ameuwawa kikatili kasha mwili wake kutelekezwa  kwenye mashamba ya mpunga.
Kamanda  huyo alisema kuwa tukio hilo limetokea Agosti 9 mwaka huu majira ya saa 8:00 mchana huko katika kijiji cha muhela wilaya ya mbarali mkoa wa mbeya.
Alisema kuwa marehemu aliondoka nyumbani kwake tarehe Agosti 7 mwaka huu  majiora ya jioni  akiwa na  piki piki yake yenye namba t.770 byh aina ya  shinley ambayo nayo ilikutwa eneo la tukio.
Hata hivyo Kamanda Diwani alisema  mwili wa marehemu ulikutwa na majeraha ya  kukatwa mapanga ambapo vidole viwili vya mkono wa kushoto vilitolewa kwa kukatwa, jicho la upande wa kushoto kutobolewa  na majeraha makubwa manne kichwani.
Hata hivyo imeelezwa kuwa  chanzo cha tukio  hilo wivu wa kimapenzi baada ya marehemu kutuhumiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wa  mtu .
Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa ndugu kwa mazishi ,hata hivyo wahusika wakuu wa tukio hilo baada  ya kufanya tukio hilo walikimbia.
Katika tukio lingine Mkazi wa Kijiji cha Mwakaganga aitwaye Tegemeo Wilangali (29) alifariki dunia baada ya kukanyagwa na trekta lenye namba t.885 bpy baada ya marehemu kutaka kudandia wakati  tela likiwa kwenye mwendo kasi.
kwa Hisani ya Francisgodwinblog