Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Article 3

$
0
0
.Awarudhisha Igwachanya watumishi waliohamia Njombe.
 
 Baadhi ya Waandishi wa Habari Wakiendelea na Kazi Yao Kwenye Kikao Hicho


 Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Bwana Jackson SaitabauAliyehamia Hivi karibuni Akitokea Mkoani Arusha Ambako Alikuwa Katibu Tawala Msaidizi


Baadhi ya Wanahabari Akiwemo Mwandishi na Mmiliki wa Mtandao Huu Bwana  Gabriel Kilamlya wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Njombe.

Na Gabriel Kilamlya Njombe

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Captain Mstaafu Asseri Msangi  Ametengua Maamuzi ya Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe Lililoridhia Maombi Ya Wataalamu wa Halmashauri Hiyo Kuhamia Katika Majengo ya SIDO Yaliyopo Mjini Njombe Kutokana na Kutokamilika Kwa Ofisi Katika Halmashauri ya Wanging'ombe.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Ofisini Kwake Mkuu Huyo wa Mkoa Capteni Mstaafu Msangi Amesema Kuwa Kutokana na Baraza Hilo la Madiwani Kuridhia Maombi ya Watendaji Hao Pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri Hiyo Amelazimika Kutengua Maamuzi Hayo Kwani Serikali Iliagiza watendaji na wataalamu wote Kuhamia Igwachanya.

Amesema Kuwa Kitendo cha Mkurugenzi na Wataalamu Wake  Kuhama Igwachanya Ambako Ndiko Makao Makuu ya Wilaya Ya Wanging'ombe na Kuhamia Njombe ni Kukiuka Agizo la

Rais Pamoja na Waziri Mkuu Aliyeagiza Watumishi Wote Kuhamia Huko.

Amesema Katika Ziara Yake ya Hivi Karibuni Aliyoifanya Katika Wilaya za Ludewa,Makete na Wanging'ombe Amebaini Kuwepo Kwa Changamoto Mbalimbali na Kuwaagiza Viongozi wa Ngazi Mbalimbali Kushughulikia Changamoto Hizo Zikiwemo za Sekta ya Elimu,Maji na Umeme.

Katika Hatua Nyingine Keptein Mstaafu Msangi Ameagiza Kila Halmashauri Kuunda Kamati Itakayosimamia Suala la Mchakato wa Ufikishaji Nishati ya Umeme Vijijini Kupitia Wakala wa Nishati Vijijini REA Ili Kuendana na Ilani ya Uchaguzi Mkuu ya Mwaka 2010/2015.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles