Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Article 0

$
0
0
 Msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Capteni Mstaafu Asseri Msangi Ukitoka Kukagua Mizinga ya Wanakikundi cha Mshikamano Katika Kijiji cha Iyayi.
 Mwenyekiti wa Kikundi cha Ufugaji Nyuki cha Mshikamano Kijiji cha Iyayi Wilayani Wanging'ombe

 Mkuu wa Mkoa wa Njombe Capteni Mstaafu Asseri Msangi Akiwa na Kaimu Afisa Tarafa ya Wanging'ombe Akivuka Barabara Kuelekea Eneo lenye Mizinga ya Nyuki.
 Baadhi ya Mizinga ya Nyuki katika Kikundi cha Mshikamano Katika Kijiji cha Iyayi Wilayani Wanging'ombe
Taarifa ya Kikundi hicho

Na Gabriel Kilamlya Wanging'ombe

Wanachama wa Kikundi cha Ufugaji Nyuki cha Mshikamano Kilichopo Katika Kijiji cha Iyayi Wilayani Wanging'ombe Mkoani Njombe  Kimetajwa Kukabiliwa na Uhaba wa Mtaji wa Kuongeza Mizinga Ya Nyuki Ili Iweze Kufikia Mizinga Mia Tano.

Hadi Sasa Kikundi Hicho Kimefanikiwa Kumiliki Mizinga 225  Ya Nyuki Ambayo Imetolewa na Wafadhili Katika Kuwakwamua Wananchi Kiuchumi.

Akizungumzia Hali ya Kikundi Hicho Mwenyekiti wa Kikundi Bwana S-----Sungura Amesema Kuwa  Kikundi Hicho Tangu Kianze Mwezi April 17 Mwaka 2013 Kimefanikiwa Kupa Fedha Kiasi Cha Zaidi ya Shilingi Milioni Mbili Kutokana na Mavuno Ya Asali.

Akizungumzia Suala la Ufugaji Nyuki Katika Kikundi Hicho Mkuu wa Mkoa wa Njombe Capteni Mstaafu Asseri Msangi Amewataka Wataalamu wa Nyuki Kuhakikisha Wanasaidiana na

Wananchi Katika Kuhakikisha Wanafuga Kitaalamu Ili Waweze Kupata Asali Nyingi Zaidi.

Aidha Msangi Amewashauri Wananchi Hao Kuboresha Maeneo Ya Ufugaji wa Nyuki Hao Kutokana na Hali Ya Mvua Zinazoendelea Kunyesha Ili Kuongeza Kiwango cha Uzalishaji wa Asali.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles