DIWANI MPYA WA KATA YA NJOMBE MJINI Agrey Mtambo AAPISHWA RASMI JANA KATIKA MAHAKAMA YA WILAYA YA NJOMBE.
Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Njombe Augustine Rwizile Hii Jana Amemuapisha Rasmi Diwani wa Kata ya Njombe Mjini Agrey Joseph Mtambo Kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.
Hakimu Rwezile Amemtaka Diwani Huyo Kufanyakazi Kwa Kufuata Misingi ya Uongozi Pamoja na Kutatua Changamoto Zinazowakabili Wananchi Anaowaongoza na Kuweka Maslahi ya Kata Mbele Badala Ya Maslahi Yake Binafsi.
Akizungumza Mara Baada ya Kuapishwa Diwani wa Kata ya Njombe Mjini Agrey Mtambo Amewashukuru Wakazi wa Kata ya Njombe Mjini Kwa Kumchagua Kuwa Diwani Wao Huku Akiwaomba Kuondoa Itikadi Zao za Vyama na Badala Yake Washirikiane Kuleta Maendeleo ya Kata Hiyo.
Awali Akiapa Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Njombe Augustine Rwizile, Diwani Agrey Mtambo Ameahidi Kuitumikia Halmashauri ya Mji wa Njombe na kufuata misingi bora ya uongozi.
Amesema kuwa kufuatia kuapishwa kwake rasmi tayari amekwisha kuweka mipango ya kuwatembelea wananchi wake wa kata hiyo kwa lengo la kuwashukuru kwa kumchagua pamoja na kujadili namna ya kutatua matatizo yanayowakabili na kuendeleza miradi ya maendeleo iliyopo katika kata hiyo.
Kwa Upande Wao Baadhi ya Wananchi Waliohudhuria Zoezi la Kuapishwa Kwa Diwani Huyo Wamempongeza Kwa Kuchaguliwa Kuiongoza Kata ya Njombe Mjini na Kumtaka Kushirikiana na Uongozi wa Halmashauri ya Mji Katika Kutatua Changamoto Zinazowakabili Wakazi wa Kata Hiyo.
Diwani Agrey Mtambo Ameapisha Rasmi Hii Leo Kuwa Diwani wa Kata ya Njombe Mjini Ikiwa ni Takribani Siku Kumi na Mbili Tangu Kumalizika Kwa Uchaguzi Mdogo wa Udiwani wa Kata Hiyo Uliofanyika Februari Tisa Mwaka Huu na Kuibuka Mshindi Kwa Kupata Kura 2222 na Kumshinda MPinzani Wake Kutoka CCM Aliyepata Kura 1094.