NG'O YA ILAWA NJOMBE YAADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA LUDEWA LEO.
Siku ya Mazingira yaadhimishwa kwa kukata kuni wakiharibu mazingira kwa wanafunzi wilayani Ludewa.
Mwenyekiti wa Shirika la ILAWA Bwana Nathanael Mgani akipanda mti Wilayani Ludewa katika kijiji cha Lusitu ndani ya chanzo cha maji cha Mto Ligomelo leo
Hapa mwenyekiti wa Shirika la ILAWA AKIKAGUA Chanzo cha Maji wilayni Ludewa kwa ajili kupanda miti siku ya
mazingira Duniani.Mwenyekiti wa Shirika Lisilo la Kiserika Linalojihusisha na Uhamasishaji wa Utunzaji Mazingira la Mkoani Njombe la Ilawa Iprovement Organization, Bwana Nathanael Mgani mwenye suti ya Kijani.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Luvuyo wakipumzika wakiwa wameshika Mzigo wa Nyasi na Fito walizoagizwa na walimu wao kwa ajili ya Ujenzi wa Choo shuleni hapo walipokutwa na kamera ya Mtandao huu.
Baadhi ya Viongozi wa Serikali na wa Shirika la ILAWA Wakipanda miti katika kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani Leo Wilayani Ludewa.
Wanafunzi wanavyoishi hadi karne hii.
Aliyevalia Barakashia ni Afisa mtendaji wa kata ya Idope Wilayani Ludewa ambako siku ya mazingira imefanyika kupitia shirika la ILAWA na Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Shirika la ILAWA Linalojishughulisha na Utunzaji wa Mazingira lililoko Mjini Njombe
Na Prosper Mfugale Ludewa.
Akizungumza na Wananchi wa Kata ya Idope Kwa Lengo la Kuwahamasisha Wananchi Hao Kutunza Mazingira na Vyanzo Vya Maji Mwenyekiti wa Shirika Lisilo la Kiserika Linalojihusisha na Uhamasishaji wa Utunzaji Mazingira la Mkoani Njombe la Ilawa Iprovement Organization, Bwana Nathanael Mgani Amesema Kwa Kiwango Kikubwa Vyanzo Vya Maji na Mazingira Yanaharibiwa Kutokana na Shughuli Mbalimbali za Kiuchumi Ikiwemo Kilimo.
Kwa Upande Wake Afisa Mtendaji wa Kata Hiyo Bwana Atanasio Mtulo Amesema Atashirikiana na Maafisa wa Vijiji Kuendelea Kutoa Elimu Kwa Wananchi Juu ya Utunzaji wa Mazingira Huku Akiwataka Wananchi Wanaoendesha Shughuli za Kiuchumi Karibu na Vyanzo Vya Maji Kuacha Mara Moja Kabla Serikali Haijawachukulia Hatua za Kisheria.