Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mheshimiwa Deo Filikunjombe akiingia katika Ukumbi wa IDYDC Mjini Iringa kuzungumza na wakazi wa Ludewa waishio Mkoani Humo ambao ni Wanakikundi cha KIPAMAMBA Akiwa Mgeni Rasmi.
Viongozi wa Kikundi cha KIPAMAMBA Wananchi wa Ludewa waishio Mkoani Iringa wakieleza Changamoto mbalimbali mbele ya Mbunge wa Ludewa Mhe.Deo Filikunjombe Hivi karibuni.
Na Shedrack Mwansansu Iringa.
PAKIMAMBA juzi wamekutana katika ukumbi wa IDYDC na kujadili maswala mbalimbali yanayokihusu chama ,na mbunge wa jimbo la Ludewa mh, DEO FILIKUNJOMBE akiwa ni mgeni Rasmi katika kikao hicho.
Ikisomwa Risala mbele ya mgeni rasmi wana Ludewa hao waliemtaka mh, Filikunjombe kuweza kutolea ufafanuzi wa miundombinu pamoja na makaa ya mawe ya mchucuma na kuwasaidia wana ludewa kuwaboreshea miundo mbalimbali zikiwemo bara bara pamoja na mawasiliano kwa mitandao mbalimbali ya simu hususani maeneo ya mwambao mwa ziwa nyasa.
Akizungumza katika tafrija hiyo FILIKUNJOMBE amewahidi wana ludewa kuwaboreshea miundombinu wananchi wa Ludewa kupitia serikali ya tanzania zikiwa ni ahadi za chama cha mapinduzi (ccm) na kusema kuwa viwanda mbalimbali vitajengwa wilayani Ludewa kwa lengo la kuwapatia ajira vijana.
Ameahidi kuongeza huduma ya umeme katika maeneo mbalimbali wilayani ludewa.
Hivi karibuni Mbunge huyo aliwahakikishia wananchi wake juu ya Ujenzi wa Barabara ya Njombe-Ludewa kwa
Kiwango cha Lami pamoja na kuongeza Nishati ya Umeme kwenye baadhi ya Vijiji Wilayani Humo na Hivyo kuitaka Serikali kuweka bajeti ya Kutosha katika Jimbo la Ludewa.
Wakati wa Ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndg.Abdulrahman Kinana Hivi aliyoifanya Wilayani Humo na Mkoa wa
Njombe Kiujumla Hivi Karibuni Mbunge huyo alisema kuwa wananchi wake wamepongeza kwa hatua ya Serikali kugundua miradi Mikubwa ya Liganga na Makaa ya Mawe ya Mchuchuma huku wakisema hawako tayri kuona Viwanda vikijengwa Nje ya Wilaya hiyo.
Katika Hatua Nyingine bwana Filikunjombe alisema kuwa wananchi wake wameridhia madini hayo kutumika na
watanzania Wote hivyo kama Wilaya husika ya Ludewa inatakiwa kupewa Kipaumbele katika Kuboreshewa miundombinu ya Barabara,Umeme pamoja na Huduma nyingine Muhimu.