Wadau wa Nishati ya Umeme wa Maporomoko ya Maji Wakiwa Kwenye Picha ya Pamoja Kwenye Mitambo ya Mradi wa Umeme wa Mawengi Wilayani Ludewa
Hapa Ndipo Chanzo cha Maporomoko ya Umeme wa Maji Katika Mradi wa Mawengi Unaozalisha Kilowatt 300 na Kuhudumia Zaidi ya Wananchi Mia Nane.
Picha ya Pamoja ya Wadau wa Nishati Hiyo Wakiwa Jirani na Maporomoko ya Maji Yanayofua Umeme Huo.
Mmoja wa Wadau wa Umeme Akipiga Picha ya Vyanzo vya Maji na Wadau Wenzake Katika Mradi wa Umeme Huo Walikokwenda Kutembelea.
Na Gabriel Kilamlya Ludewa
Wadau wa Nishati ya Umeme wa Maporomoko Madogo ya Umeme Wanaoendelea na Mafunzo Yao ya Wiki Mbili Mjini Njombe Wamesema Tatizo la Fedha Ili Kuendleza Miradi Yao Imekuwa ni Kikwazo Kikubwa Kwao Ili Kusogeza Huduma Kwa Wananchi
Wakizungumza na www.gabrielkilamlya.blogspot.com Mara baada ya Kufanya Ziara ya Kwenda Kutembelea Vyanzo Vya Umeme wa Maporomoko ya Maji vya Mawengi na Chanzo cha Mkongobati Wilayani Ludewa Jana wadau hao wamesema kuwa kutokana na hali ya miradi yao imekuwa ikienda kwa kusuasua kutokana na kukosa namna ya kuomba ufadhili toka
maeneo tofauti.
Pamoja na mambo mengine wameeleza kuwa ili kurahisisha tatizo hilo wanatarajia Kuunda umoja wao utakaorahisisha upatikanaji wa fedha toka serikali kupitia vikundi vyao.
Kwa upande wake mwezeshaji wa mafunzo hayo katika kundi la pili litakalohitimu disemba 17 mwaka huu Mhandisi Emmanuel Michael amesema kuwa kutokana na elimu aliyoitoa kwa siku zote pamoja na mafunzo ya vitendo itawafanya wadau hao kupanua wigo wa kuongeza miradi hiyo pamoja na kuomba ufadhili toka kwa wahisani mbalimbali.
Mhandisi Emmanuel Amesema Miongoni mwa mambo Aliyofundisha ni pamoja na kujua namna ya kuandika maandiko mbalimbali ya kuomba ufadhili na mbinu za kuomba mikopo kwenye taasisi nyingine za kifedha kwani wengi wao hawakufahamu watapata wapi wafadhili
Mafunzo hayo yamewakutanisha wadau mbalimbali wa nishati ya umeme wa maporomoko ya maji kutoka katika Mikoa mbalimbali hapa Nchini Chini ya ufadhili wa Wakala wa nishati Vijijini REA watakao hitimu Disemba 15 na 17 mwaka huu.
Hapa Ndipo Chanzo cha Maporomoko ya Umeme wa Maji Katika Mradi wa Mawengi Unaozalisha Kilowatt 300 na Kuhudumia Zaidi ya Wananchi Mia Nane.
Wadau wa Nishati ya Umeme wakiongozwa na Mwalimu wao Mwenye T-shirt ya Bluu Mhandisi Emmanuel Michael wakielekea Kwenye Chanzo cha Umeme wa Maji Huko Ludewa.![]()
Hii ni Mitambo Iliyopo Power House Kwenye Mradi wa Umeme wa Maporomoko ya Maji Mawengi Huko LudewaPicha ya Pamoja ya Wadau wa Nishati Hiyo Wakiwa Jirani na Maporomoko ya Maji Yanayofua Umeme Huo.