MTOTO ATELEKEZWA MKOANI IRINGA.
Mtoto aliyetelekezwa
Mtoto huyo wa kiume anayekadiliwa kuwa na mwaka mmoja alikutwa jana majira ya saa 2 usiku katika eneo hilo la Ndiuka 'A' huku akiwa na vifurushi viwili vya nguo pamoja na dawa za aina mbali mbali .
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo wa Ndiuka A Siwema Ally alisema kuwa mtoto huyo aliokotwa na wasamaria wema na kupelekwa kwake kabla ya kuchukuliwa na polisi na kupelekwa kituo cha yatima cha Daily Bread Life MInistries kinachomilikiwa na Neema Mpeli
Mwanamke huyo pia aliacha namba za simu ambazo ni 0766663281 inayomilikiwa na Kastori Mlyatage pamoja na namba ya Mahenge wa Mabadaga 0753493063 na namba ya mama Fatuma 0757 519270 pamoja na barua inayoonyesha alisaidia kituo cha polisi Makambako kwa ajili ya Kwenda Singida
kwa hisani ya Francisgodwin