Abiria Wanaotumia Kituo Kikuu Cha Mabasi Mjini Njombe Wameiomba Serikali Kuongeza Askari wa Ukaguzi wa Magari na Kuhimiza Matumizi ya Sare Miongoni Mwa Maafisa Wanaotoa Huduma ya Usafiri Kituoni Hapo.
Aidha Madereva na Makondakta Hao Pia Wameombwa Kuacha Tabia ya Kufanya Kazi Kwa Mazoea na Badala Yake Wanapaswa Kutii Maagizo Yanayotolewa na Serikali Ikiwemo Uvaaji wa Sare.
Wakizungumza na www.gabrielkilamlya.blogspot.com Baadhi ya Abiria Wamesema Kuwa Uamuzi wa Makondakta Hao Kuvaa Sare Utasaidia Kupunguza Usumbufu na Kuwawezesha Abiria na Watu Wengine Kuwatambua Kwa Haraka Watoa Huduma Kituoni Hapo.
Wamesema Serikali Inatakiwa Kutoa Elimu Kwa Madereva na Makondakta Pamoja na Maafisa Wengine Wanaotoa Huduma ya Usafiri Kuhusu Umuhimu wa Kuvaa Sare na
Kuongeza Kuwa Hali Hiyo Itasaidia Kuongeza Usalama Kituoni Hapo.
Mussa Mapunda ni Afisa Usafirishaji Katika Mabasi Yaendayo Mikoa ya Mbeya na Ludewa Anasema Serikali Inatakiwa Kuwachukulia Hatua Kali za Kisheria Wale Wote Wanaoshindwa Kuvaa Sare na Kukiuka Maagizo ya Serikali.
Kwa Mujibu wa Taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Maafisa Wote Wanaotoa Huduma ya Usafiri Katika Kituo Kikuu Cha Mabasi na Mabasi Yaendayo Mikoani na Vijijini Wametakiwa Kuvaa Sare Maalum na Kuboresha Huduma Zao.