Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Article 6

$
0
0










Na Prosper Mfugale

 Shiriki Lisilo la Kiserikali la Upendo Nyombo Linalojihusisha na Utoaji wa Hudua Kwa Watoto Yatima na Wanaoishi Katika Mazingira Hatarishi Lililopo Kijijini Nyombo Limetoa Msaada wa Vifaa na Fedha Vyenye Thamani ya Shilingi Milioni Mbili Kwa Watoto Hao Waliko Katika Maeneo ya Wilaya ya
Njombe.

Misaada Iliyotolewa na Shirika Hilo ni Magodoro , Vifaa Vya Shule Pamoja na Fedha Taslim Kwa Wanafunzi 19 wa Shule za Sekondari na Vyuo Kwa Ajili ya Kulipa Karo .

Akizungumza Wakati wa Kukabidhi Misaada Hiyo Kwa Watoto Hao Kwaniaba ya Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa Kijiji Bwana Yohana Lisulile Amewataka Walezi na Watoto Hao Kuitumia Misaada Hiyo Kwa Malengo Yaliyokusudiwa.

Awali Akisoma Taarifa ya Shirika Hilo Mkurugenzi Mtendaji Joakimu Mwinami Amesema Misaada Hiyo Imetokana na Nguvu za Shirika Hilo Pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Huku Akitoa Wito Kwa Mashirika Mengi na Watu Wengine Kuendelea Kuwasaidia Watoto Hao.

Kwa Upande Wao Watoto na Walezi Hao Wamelirishukuru Shirika Hilo Kwa Msaada Walioutoa na Kuyaomba Mashirika Mengine Kuiga Jitihada Zinazofanywa na Shirika la Upendo Nyombo Hasa Katika Kuwalipia Karo Wanafunzi wa Shule za Sekondari na Vyuo.

Hadi  Sasa Shirika Hilo Lisilo la Kiserika la Upendo Nyombo Linahudumia Watoto Yatima na Wanaoishi Katika Mazingira Magumu Zaidi ya 170 Wilayani Njombe.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles