KWA MKOA WA NJOMBE TUKIO LITATOKEA KATIKA KIJIJI CHA LITUNDU WILAYANI WANGING'OMBE
Kupita kwa kivuli cha mwezi duniani wakati wa kupatwa kwa jua. Watu katike eneo kubwa la giza waliona kupatwa kwa jua kisehemu. Nukta nyeusi yaonyesha sehemu ambako jua lilipatwa kabisa.
"Central duration" inataja muda wa kupatwa kabisa kwenye kitovu cha kivuli; namba katika kona ya juu huonyesha saa za tar. 29 Machi kupatwa kulipotokea.
Misingi ya kupatwa kwa jua
Kupatwa kwa jua kunatokea kama dunia, mwezi na jua zinakaa kwenye mstari mmoja mnyoofu yaani wakati mwezi unapita kati ya dunia na jua. Katika hali hiyo kuna kivuli cha mwezi kwenye uso wa dunia. Kivuli hiki hakifuniki dunia yote. Kwa hiyo kupatwa kwa jua kunaonekana kwa watu wengi kama kupungua kwa mwanga wa jua.Aina za kupatwa kwa jua
Kuna aina mbalimbali za kupatwa kwa jua.- kupatwa kabisa: jua lapotea kabisa kwa dakika chache. Hali hii yaonekana kwenye kanda nyembamba duniani kinapopita kitovu cha kivuli.
- kupatwa kipete: mwezi huonekana mdogo kuloko jua. Kwa hiyo duara ya kung'aa ya jua ni kubwa kuliko duara ya mwezi na mwanga wa jua waonekana kama pete.
- kupatwa kwa jua kisehemu: Katika eneo kubwa la kivuli cha kando watu hona upungufu wa mwanga; kiasi chake hutegemea umbali na kitovu cha kivuli. Wakitazama jua kwa filta kwa mfano kioo kilichopakwa dohani katika moshi ya mshumaa huwa wanaona sehemu ya duara ya jua imefunikwa.