Baadhi ya Wanachama wa CHADEMA Mjini Njombe Wakiweka Ishara ya Kujenga UKUTA
Mkuu wa Idara ya Uenezi CHADEMA Bwana Hemed Ally azungumza na Vyombo Vya Habari Baada ya Kikao Cha Ndani Njombe
Edward Lowasa Akiondoka Katika Kituo Cha Watoto Yatima Cha COF Mjini Njombe Kuelekea Mkoani Iringa
Baadhi ya Wanachama wa CHADEMA Wakiondoka katika kituo cha COF Baada ya kikao cha Ndani Cha LOWASA na Viongozi wa Chama Mkoa wa Njombe Jioni ya Leo.
Na Gabriel Kilamlya NJOMBE
Wakati Jeshi la Polisi Likipiga Marufuku Maandamano na Mikutano ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Kupitia Kampeni Waliyoipa Jina la Kupambana na Udikta Nchini UKUTA Baadhi ya Viongozi na Wanachama wa CHADEMA Mkoani Njombe Wamesema Kampeni Hiyo ni Lazima Ifanyike Kama Ilivyopangwa.
Kauli Hiyo Wameitoa Muda Mfupi Baada ya Kumalizika Kwa Kikao Cha Ndani Cha Mkakati Huo wa UKUTA Kilichofanyika Mjini Njombe Kikiongozwa na Mjumbe wa Halmashauri ya Mkutano Mkuu wa CHADEMA Taifa na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa Alipowasili Mkoani Njombe Akitokea Mbeya.
Obadia Choga ni Katibu wa CHADEMA Jimbo la Njombe Mjini Ambaye Amesema Jeshi la Polisi Linapaswa Kwenda Kuimarisha Ulinzi Katika Maandamano na Mikutano Yao ya UKUTA ya Septemba Mosi Mwaka Huu Badala Ya Kuwazuia .
Akizungumza Kwa Niaba ya Edward Lowasa Mkuu wa Idara ya Uenezi CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Bwana Hemed Ally Licha ya Kuendelea na Ziara Yao Kupitia Vikao Vya Ndani Lakini Jeshi la Polisi Limeendelea Kuwadhibiti Ilihali Wanafanya Vikao Hivyo Kisheria.
Bwana Hemed Ally Amesema Walipaswa Kuelekea Mkoani Rukwa Kabla ya Kufika Njombe Lakini Ziara ya Waziri Mkuu Mkoani Humo Imetajwa Kumzuia Lowasa Kufanya Ziara Yake
Huko.