

Rais
Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt
Jakaya Mrisho Kikwete aliyefika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi
rasmi Ofisi ya Rais leo Novemba 12, 2015
Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt
Jakaya Mrisho Kikwete aliyefika Ikulu jijini Dar es salaam kukabidhi
rasmi Ofisi ya Rais leo Novemba 12, 2015
TAARIFA YA MAKABIDHIANO RASMI YA OFISI IKULU.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, leo katika Ikulu ya Dar es Salaam amepokea taarifa rasmi ya makabidhiano yaOfisi kutoka kwa Rais Mstaafu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo mchana na kushuhudiwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na Maafisa wa Ofisi Binafsi ya Rais.
Utaratibu wa kukabidhiana Ofisi katika Ofisi Kuu hapa nchini ni jambo la kawaida na hivyo imebidi makabidhiano hayo kati ya
“Umeanza vizuri, baki na msimamo huo huo utasaidia sana wananchi” . Mhe. Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne amemueleza Mhe. Rais Magufuli wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano.
Mhe.
Rais Mstaafu amekabidhi taarifa rasmi yenye kurasa 53, ambayo kwa ujumla
inaelezea kazi zilizokwisha kufanyika, ambazo zinasubiri kukamilika na zile
ambazo zinasubiri maamuzi ya utekelezaji. Mengine ni hali halisi ya nchi katika nyanja zote za
kiuchumi, kisiasa na kijamii.
Mhe.
Rais Dkt. Magufuli amemshukuru Rais Mstaafu
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi kwa muongozo wake siku zote .“Nikushukuru
kwa kuiacha nchi salama na itaendelea kuwa salama, nikushukuru kwa muongozo
wako, na taarifa ya muelekeo
na ninaahidi kuwa Hapa ni Kazi Tu”.
Mhe. Rais amesema
na kumueleza Rais Mstaafu kuwa ametengeneza mazingira mazuri ambayo nchi nyingi
zimeshindwa kufanya na hivyo basi kuahidi kuendelea kuchota hekima na busara
kwa Marais wote wastaafu wakiwemo Mhe. Benjamin William Mkapa wa Awamu ya Tatu
na Mzee Ally Hassan Mwinyi wa Awamu ya pili.
Wakati
huo huo Mhe. Rais Magufuli ameendelea kupokea salamu za pongezi kutoka Kwa Msimamizi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP) Bibi Helen Clark.
“Chini
ya uongozi wako, tunatarajia kuzidi kuimarisha ushirikiano baina yetu,
demokrasia, kushughulikia masuala ya umaskini na ajira kwa vijana , kukuza
uchumi, na kulinda na kuhifadhi
mazingira, masuala ambayo Tanzania na UNDP tumekuwa tukishirikiana
kuyaendeleza
na
kuyatimiza”
amesema Bi Clark.
Salamu
zingine ni kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Uswiss, Mhe. Simonetta Sommaruga,
Rais wa Jamhuri ya Italia Mhe. Sergio Mattarella, Rais wa Jamhuri ya Shirikisho
la Ujerumani Mhe. Joachim Gauck na pia kutoka kwa Rais wa Finland Mhe. Sauli
Niinisto.
Pongezi
zingine zimetoka kwa Rais wa Jamhuri ya Urusi, Mhe. Vladimir Putin, Rais wa
Jamhuri ya Sudan Kusini, Mhe. Salva Kiir Mayardit, Rais wa Jamhuri ya Korea
Mhe. Park Geun-hye na kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. XI
Jinping.
Salamu pia zimemfikia Mhe. Rais Dkt. Magufuli kutoka
kwa Rais wa Taifa la Eritrea Mhe. Isaias
Afwerki na kutoka kwa Rais wa Ufaransa Mhe. Francois Hollande.Katika
ujumbe wao, viongozi hao mbali na kumpongeza Mhe. Rais Dkt. Magufuli kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, wamesisitiza
kuendeleza na kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na nchi zao.
Pia
wameipongeza Tanzania kwa kudumisha demokrasia imara na Watanzania kwa ujumla
kwa kuimarisha amani na utulivu wakati wa Uchaguzi Mkuu.
Imetolewa
na:Premi Kibanga,Mwandishi
wa Habari wa Rais, Msaidizi.
Ikulu,
DARES SALAAM.
DARES SALAAM.
12 Novemba, 2015