Mchakato wa Upigaji Kura Kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Wilaya ya Ludewa Ili Kumpata Mbunge Atakayekwenda Kupeperusha Bendera ya Chama Hicho Kupambana na Vyama Vya Upinzani Umefanyika Jana Huku Baadhi ya Wagombea Wakielezwa Kujitoa Katika Mchakato Huo Kabla ya Zoezi Hilo.
Miongoni Mwa Wagombea Ambao Wanadaiwa Kujitoa Mapema Leo Dakika Chache Kabla ya Kupigwa Kura ni Pamoja na Bwana Johnson Mgimba,Saimon Ngatunga na Edgar Lugome Ambao Bado Hawajaweka Wazi Sababu za Kujiengua Katika Mchakato Huo Licha ya Taarifa za Ndani Zikieleza Ni Kutokana na Ukata wa Fedha Kwa Waliokuwa Wagombea Hao.
Pamoja na Mambo Mengine Lakini Pia Taarifa Toka Wilayani Humo Zimebainisha Kuwa Deogratias Ngalawa Ndiye Aliyefanikiwa Kuongoza Kwa Kura 537 Kati ya Kura Zote Zilizopigwa Huku Akiwashinda Washindani Wenzake Wote.
Akitangaza Matokeo Hayo Jioni Hii Msimamizi wa Uchaguzi Huo Bwana Lukas Nyanda Katibu wa Wazazi Wilaya ya Njombe Amesema Licha ya Ngalawa Kupata Ushindi Huo Lakini Kazi Kubwa Ipo Katika Kuelekea Mchakato wa Kampeni Hadi Kumpata Mbunge Halisi wa Jimbo Hilo.
Aidha Chama Hicho Kimesema Kuwa Mshindi Huyo wa Leo Atakwenda Kushindani na CHADEMA Katika Uchaguzi Mdogo Utakaofanyika Mwezi Disemba Mwaka Huu.