Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe (katikati chini) akimsubiria Rais wa Zimbabwe Mhe. Robert Mugabe (katikati juu kwenye ngazi) alipokuwa akiteremka kwenye Ndege, Rais Mugabe amewasili nchini kwaajili ya kuhudhuria Sherehe za uapisho wa Rais Mteule Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli zitakazofanyika hapo kesho katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
![]()
Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini pia anayeiwakilisha Tanzania nchini Botswana Mhe. Radhia Msuya (kushoto) akisalimiana na Makamu wa Rais wa Botswana Mhe. Olale Eric Mothibi alipo wasili nchini kwaajili ya kushiriki Sherehe za Uapisho wa Rais Mteule Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Picha na Reginald Philip
================================
Mhe. Netumbo Nandi - Ndaitwah (wa pili kutoka kulia) akifurahia kikundi cha ngoma kilichopo mbele yao.