Mabaki ya ndege ya Urusi ililyoanguka Misri
Uingereza imetoa angalizo kwamba huenda mlipuko ndio uliosababisha ndege ya shirika la ndege la Urusi kuangukia nchini Misri na kuua abiria wote mia mbili na ishirini na wanne waliokuwa kwenye ndege hiyo.
Halikadhalika safari za kutoka na kuingia katika rasi hiyo zimesitishwa na Ireland.
Mamlaka ya safari za anga nchini Urusi hivi karibuni walitoa tahadhari kuwa ni mapema mno kuhisi nini chanzo cha
ajali hiyo.
Mabaki ya ndege hiyo na kisanduku cheusi chenye kurekodi mwenendo wa ndege hiyo bado vinafanyiwa uchunguzi.
Mpaka sasa kundi la wanamgambo wa kiislamu, la Islamic State limereudia kukiri kuwa linahusika na ajali hiyo.