Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Article 12

$
0
0
MBUNGE LWENGE ATAKA KUFUTWA KWA NYUMBA ZA NYASI JIMBONI KWAKE.
 Mbunge Gerson Lwenge akisalimia na Wanachama wa CCM Kata ya Saja Leo.

 Kwaya ya Wananchi wa Kitongoji cha Makondo yaonesha Kipaji chake na Kutunukiwa amount Fulani toka kwa Mbunge wao Leo.
 Mbunge Lwenge akizungumza na Wananchi wake katika Kitongoji cha Makondo Kijijini Saja Leo alipofika kwa ziara ya
Wiki Moja Jimboni humo.






Mbunge Lwenge Pia ahamasisha Kupunguza Maambukizi ya Ukimwi Wilayani Wanging'ombe kwa Kugawa Mipira na Jezi kwa Michezo zaidi kwa Vijana.
..........................................................................................................................................................
Naibu Waziri wa Ujenzi ,Ambaye Pia ni Mbunge wa Jimbo la Njombe Magharibi Mhandisi Gerson Lwenge Amewataka Wananchi Kuchangia Miradi ya Maendeleo Kwenye Maeneo Yao na Kuacha Kuitegemea Serikali na Wafadhili Kwa Kiasi Kikubwa.

Akiongea Mara Baada ya Kupokea Taarifa za Utekelezaji wa Miradi Katika Vijiji Vya Itengelo na Saja Amesema Kwa Sasa Wananchi Wamesahau  Kuwa Jukumu la Kuleta Maendeleo Katika Maeneo Yao Linaanzia Kwa Wananchi Ndipo Serikali na Mashirika Nayo Yanachangia Kufanikisha Malengo ya Wananchi Hao.

Pamoja na Adha Kubwa ya Maji iliyopo katika Kata ya Saja na Vijiji Mbalimbali  Nchini Mbunge Lwenge amesema ni Lazima Miradi hiyo ijengwa kwani Hata Bunge la Bajeti lilipigania Kuongeza Fedha kwenye Bajeti ya Maji.
 

Aidha Naibu Waziri Lwenge Amechangia Kiasi cha Shilingi Milioni Mbili Kwa Vijiji Vya Itengelo na Saja Kwa Lengo la Kuendeleza Utekelezaji wa Miradi, Ukiwemo Ujenzi wa Shule ya Msingi Inayojengwa Kwa Nguvu za Wananchi wa Kitongoji cha Makondo Katika Kijiji cha Saja.
 

Akisoma Taarifa ya Ujenzi wa Madarasa Mawili na Ofisi Moja Unaotekelezwa na Wananchi wa Vitongoji Vya Makondo na Kagera Kijiji cha Saja, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Saja Baraka Willium

Amesema Ujenzi Huo Unatarajia Kugharimu Zaidi ya Shilingi
Milioni 30 Hadi Kukamilika Kwake Mwishoni Mwa Mwaka Huu.

Pamoja na Kiasi cha Shilingi Milioni Moja aliyoitoa Mbunge Lwenge lakini Pia Wananchi hao wameonekana kukabiliwa na Changamoto Mbalimbali na Hapa Wanabainisha.

Naibu Waziri Lwenge Ameanza Ziara ya Siku Sita ya Kutembelea Wananchi wa Jimbo la Njombe Magharibi jana ambapo Leo anatarajia Kutembelea Katika Vijiji vya Katenge,Utiga na Mayele Katika Kata ya Wanging'ombe Wilayani Wanginging'ombe.


Sanjali na Hayo Lakini Pia Amesema kuwa Kupitia Mpango wa Ondoa Nyasi Njombe[ONYAMBE] Ni lazima wananchi wake wajipange kuanza Kujenga Nyumba za Bati katika Kipindi cha Miaka Mitatu kuanzia Sasa kwani Kuishi kwenye Nyumba za Majani Miaka 50 ya Uhuru ni Fedha Kubwa.

Asema Kuwa Hata Kijana anayetaka Kuoa kwa Sasa Hastahili Kumuonesha Mpenzi wake Nyumba ya Nyasi kwani Hiyo ni Mwanzo wa Mifarakano katika Ndoa.

Na Gabriel Kilamlya.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles