Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA umesema kuwa mgombea wao wa Urais watamtoa baada ya siku saba.
![]()
Akizungumza na Waandishi wa Habari usiku huu,Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi, Mhe. James Mbatia amesema kuwa kuchukua muda mrefu kwa kikao hicho imetokana na kuandaa utaratibu jinsi ya kumtoa mwali wao wa Urais kwa tiketi ya UKAWA aliye bora. Amesema kuwa mkutano huo pia umechukua muda mrefu kutokana na mambo mengi ikiwemo mgawanyo wa majimbo.
![]()
Afisa Habari wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Tumaini Makene akizungumza na waandishi habari hivi punde juu kinachoendelea katika mkutano wa kutafuta mgombea wa Urais kwa tiketi ya UKAWA, uliofanyika katika Hoteli ya Colesseum jijini Dar es Salaam,Makene amesema majadiliano hayo sio urais tu bali kuna mipaka ya majimbo mapya jinsi watavyojipanga katika kushiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 25 mwaka huu. Makene amezidi kuwataka waandishi wawe na subira kusubiri maamuzi yatakayotoka katika kikao hicho ambacho kimeanza tangu asubuhi ya leo.
![]()
Baada ya kusubiri kwa muda mrefu tangu mchana,Waandishi wa Habari waliopiga kambi wakisubiri kupata jina la mgombea Urais kwa tiketi ya UKAWA katika Hoteli ya Colosseum Masaki leo jijini Dar es Salaam,wakajikuta wanaacha stendi za Camera zao na kukaa pembeni wakisubiri lolote litakalojiri.
Waandishi wa Habari wakiwa wameweka kambi tangu saa saba mchana wakisubiri kupata jina la mgombea urais kwa tiketi ya UKAWA katika Hoteli ya Colosseum Masaki leo jijini Dar es Salaam, hiyo inatokana na taarifa zilizotolewa na
UKAWA kuwa leo ndio siku rasmi ya kutangaza jina hilo lakini masaa yanazidi kwenda huku kikao chao kikiwa kinaendelea.