Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Dk.Rehema Nchimbi Amewataka Wataalamu Wa Mawasiliano TCRA Kuwasimamia Kikamilifu Wamili Na Wafanyakazi Wa Vyombo Vya Mawasiliano Hususani Simu Za Mkononi Ili Wasiwaibie Wateja Wa Mawasiliano Hayo.
Dokta Nchimbi Ametoa Wito Huo Wakati Akizungumza Na Baadhi Ya Akina Mama Wa CCM Wa UWT Wilaya Ya Njombe Wakati Wa Semina Ya Siku Moja Iliyotolewa Na Wataalamu Kutoka TCRA Kanda Ya Mbeya.
Aidha Dk Nchimbi Ameendelea Kusisitiza Wananchi Kujiandaa Kuupokea Ugeni Unaotarajiwa Kufika Mkoani Njombe Kwaajili Ya uwekezaji wa Rasilimali Madini Zilizopo Wilayani Ludewa Ambapo Zaidi ya Wawekezaji Elfu Sita Watafika Mkoani Hapa.
Amesema Wakazi Wa Njombe Wanapaswa Kutambua Fursa Mbalimbali Za Maendeleo Ikiwemo Kupata Masoko Ya
Mazao Kwa Kutumia Mawasiliano Huku Wakulima Wakitakiwa Kulima Kilimo Cha Kisasa Kufanikisha Sekta Ya Kilimo.
Awali Akimkaribisha Mkuu Wa Mkoa Wa Njombe Naibu Waziri Wa Maendeleo Ya Jamii,Wanawake,Jinsia Na Watoto Dk Pindi Chana Amepongeza Wataalamu Wa Mawasiliano TCRA Kufika Njombe Kutoa Elimu Ya Matumizi Ya Simu Za Mkononi Ambazo Zimechangia Kuharibu Ndoa Ndani ya Familia.