Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

BREAKING NEWZZZZZZ

$
0
0
BARAZA LA MADIWANI  KATIKA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE  LAVUNJWA  RASMI  LEO
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba Akizungumza Katika Kikao Cha Kuvunja Baraza la Madiwani Hao Leo.

Na Gabriel Kilamlya Njombe

Wakati Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Likivunjwa Hii Leo,Halmashauri Hiyo Imesema Imefikia  Asilimia 91 ya Ukusanyaji Mapato Katika Kipindi Cha Miaka Mitano ya 2010/2015.

Akizungumza Wakati wa Kufungua Kikao Cha Kawaida Cha Baraza la Madiwani Kilichoambatana na Uvunjaji Baraza Hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Bwana Edwin Mwanzinga Amesema Kuwa Amesema Halmashauri Hiyo Katika Kipindi Cha Miaka ya Fedha ya 2010/2011 Hadi 2013/2014 .

Imefanikiwa Kukusanya Zaidi ya Shilingi Bilioni 4.1 Amesema Lengo Lilikuwa ni Kukusanya Kiasi Cha Shilingi Bilioni 4.5 Ambapo Kiasi Hicho Cha Shilingi Bilioni 4.1 Ambacho ni Sawa na Asilimia 91 Kimesaidia Kusogeza Mbele Shughuli Mbalimbali za
 Maendeleo.

Pamoja na Mambo Mengine Lakini Mwanzinga Amesema Katika 

Kipindi Hicho Chote Halmashauri Hiyo Imefanikiwa Kuandaa 

Hesabu na Kubuni Vyanzo Vipya Vya Mapato Jambo Lililoifanya 

Halmashauri Hiyo Kuendelea Kupata Hati Safi Katika Kipindi 

Chote.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba 

Wakati Akitoa Salaamu za Serikali Katika Baraza Hilo la 

Mwisho Ametumia Fursa Hiyo Kuwapongeza Madiwani kwa 

ushirikiano mkubwa walioutoa katika kutekeleza shughuli 

mbalimbali za maendeleo katika kata zao na hasa katika 

kutekeleza agizo la Rais la Ujenzi wa Maabara Tatu za 

Sayansi Katika Kila Shule ya Sekondari.

Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Njombe 

Limevunjwa Likiwa na Madiwani 19 Ambao 13 ni Wa Kata 

Husika,viti maalum 6 na mmoja kutoka chama cha CHADEMA  

kata ya njombe mjini Bwana Agrey Mtambo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles