Diwani wa Kata ya Uwemba Mheshimiwa Edward Mwalongo Akitangaza Nia Yake ya Kugombea Ubunge Jimbo la Njombe Kusini Kupitia Tiketi ya CCM![]()

Na Gabriel Kilamlya Njombe
Diwani wa kata ya uwemba ambaye ni Mkurugenzi wa taasisi ya Elimu ya Hagafilo leo ametangaza
rasmi nia yake ya kutaka kugombea ubunge katika jimbo la Njombe kusini kupitia tiketi ya chama
cha mapinduzi Ccm.
Akitangaza Nia Yake Hiyo na Vyombo vya Habari bila Kuwahusisha wananchi Bwana Mwalongo Amesema
Licha ya Vipaumbele Vingi na Changamoto Nyingi Kuwepo katika jimbo hilo lakini lazima apiganie
suala la elimu kwa nguvu zote.
Amesema endapo chama kitampitisha na wananchi wakamchagua kuwa mbunge wa jimbo hilo basi
atapigania suala la miundombinu mbalimbali kama maji, barabara, umeme kwa
kuwa karibu zaidi
wakati wa uwekaji vipaumbele Katika bajeti.
Akizungumzia suala la wabunge wengi kuwa na Mazoea ya kutelekeza majimbo yao mara baada ya
kuchaguliwa amesema yeye hawezi kuwa mbunge wa Christmas, Pasaka na mwaka mpya kwani hana
makazi mengine yanayoweza kumuingizia pato Nje ya Njombe hivyo Hawezi kuwa kama wabunge hapo.
Akijibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari yaliyolenga juu ya kuboresha na kukuza
maendeleo katika Jimbo la Njombe kusini ikiwemo ufinyu wa bajeti kwa kila mwaka pamoja na
uchache wa fedha ya jimbo ambapo amesema ataendelea kupigania kadri atakavyoweza kwa kuvutia na
kuwekeza masuala ya kiutalii ndani ya Mkoa wa Njombe badala Ya kuhama jimboni humo.
Pamoja na mambo mengine amesema kinachopaswa ni kuwakaribisha kwa wingi wawekezaji katika mkoa
wa Njombe ikiwa ni pamoja na kuongeza fursa za kutosha za kiuwekezaji na kuzisimamia vizuri.
Hata hivyo amesema kwa kuwa mkoa wa njombe umekuwa na fursa nyingi za kujiingizia kipato hivyo
suala la elimu kwa wananchi linahitajika zaidi ili kukuza pato la mkoa na wananchi kwa ujumla.