





Mtia nia Ubunge Jimbo la Njombe kusini Rose Mayemba
Na Gabriel Kilamlya Ludewa
Mtaalamu wa Madini Ambaye ni Mwananchi wa Wilaya ya Ludewa Bwana Batholomeo Mkinga[Msambichaka] ametangaza rasmi nia yake ya Kugombea Ubunge Jimbo la Ludewa kwa Deo Filikunjombe Mkoani Njombe Kupitia Tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA.
Akitangaza rasmi Nia yake Hiyo Akiwa Mlangali Wilayani Humo Wakati wa Ufunguzi wa Watangaza Nia Kupitia Chama Hicho Mkinga Amesema Kutokana na Utaalamu Wake wa Madini Ameona ni Lazima Arudi Wilayani Kwake Kuwasaidia Wananchi Kutokana na Rasilimali Madini Zilizopo.
Amesema Kutokana na Mikataba Mingi ya Madini Hayo Kuonekana Kutokuwa wazi huenda yakaenda kuwanufaisha wawekezaji wa Nje kwa Asilimia Kubwa Badala ya Watanzania Kwa Kushindwa Usimamizi Thabiti.
Ally Mhagama[Dokta Sagasaga] ambayeAnatarajia Kutangaza Nia ya Kugombea Ubunge jimbo la
Njombe Kusini[CHADEMA] aliyekuwa kwenye msafara huo amesema ifike wakati sasa wakazi wa Ludewa wapiganie haki zao kwa kuhakikisha Madini Hayatoki Wilayani Humo Bila Kujengewa Barabara Kwa Kiwango Cha Lami.
Katika Hatua Nyingine Naye Rose Mayemba Ambaye Naye anatarajiwa Kutangaza Nia ya Kugombea Ubunge Katika Jimbo Hilo la Njombe Kusini Akiwa Wilayani Ludewa Amesema Akina Mama Wengi Wamekuwa ni Watu wa Kuelekezwa Kwenda Kupiga Kura Kwa Shinikizo Kutokana na Kuhongwa Nguo na Baadhi ya Wanasiasa Ambapo Inatakiwa Ifike Wakati Sasa Suala Hilo Likome.
Kwa Upande Wake Edward Kazimoto Amesema Kuwa Suala la Wabunge Mbalimbali Kuwadanganya Wananchi Kuwa Umeme wa REA Wanaupeleka Wao Kwa Wananchi Halipaswi Kufumbiwa Macho Kwani ni Mradi ambao ni Mpango wa Serikali Toka Kwa Wafadhili.
Amesema Umeme wa REA Umekuwa Kipigio Cha Kupata Kura Katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka Huu jambo ambalo ni upotoshaji mkubwa na ni Wizi wa Kisiasa kuwalaghai wananchi.
Pamoja na Mambo Mengine Lakini Pia Hata Madiwani Mbalimbali Wamejitokeza Kutia Nia ya Kugombea Tena na Wengine Kutarajia Kupitia Mkutano Huo Ndani ya CHADEMA.