WATU WANNE WANASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA UVAMIZI WA KITUO CHA MAFUTA CHA ORYX MAKAMBAKO PAMOJA NA KUWAUA WALINZI WAWILI.
Focas Malengo Afisa Mnadhimu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe azungumza na www.gabrielkilamlya.blogspot.com
.....................................................................................................................
Siku Moja Baada ya Watu Wanaodaiwa Kuwa Majambazi Kuvamia Kituo Cha Mafuta Cha ORYX Makambako na Kuwaua Walinzi Wawili wa Kituo Hicho na Kumjeruhi Meneja wa Kituo Hicho,Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Linawashikilia Watu Wanne Kwa Madai ya Kuhusika na Tukio Hilo.Hata Hivyo Jeshi la Polisi Halikuweza Kuweka Wazi Majina ya Watu Hao Kutokana na Sababu za Kiuepelelezi na Hivyo Kuwaomba Wananchi Kutoa Ushirikiano Kwa Jeshi Hilo Ili Kuweza Kuwabaini Watu Waliotenda Tukio Hilo.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Njombe Focas Malengo Amesema Katika Tukio Hilo Pia Jeshi la Polisi Walifanikiwa Kuokota Silaha Moja Inayodaiwa Kuporwa na
Majambazi Hao.
Amesema Kutokana na Tukio Hilo Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limeanzisha Msako Mkali Katika Miji ya Jirani Kwa Kushirikiana na Mikoa Hiyo.
Mnamo June 24 Mwaka Huu Majira ya Saa Kumi na Mbili na Nusu Asubuhi Watu Wanaodaiwa Kuwa Majambazi Walivamia Kituo Cha Mafuta ORYX Makambako na Kuwaua Kwa Risasi Walinzi wawili wa Kituo Hicho na Kupora Kiasi Cha Fedha zinazokisiwa kuwa ni kati ya shilingi Milioni tano au sita.
Mashuhuda wa Tukio Hilo walisema kuwa majambazi hao wawili wakiwa na usafiri wa piki piki ambapo walifika katika kituo hicho kwa ajili ya kununua mafuta ya Tsh 5000 na wakati wakiendelea kuhudumiwa ghafla walianza kuwashambulia walinzi kwa risasi na kuwaua walinzi wawili na kumjeruhi meneja wa kituo hicho.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Focas Malengo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataja waliouwawa kuwa ni Jonas Mpogole na Chesco Sanga ambao ni walinzi wa kampuni ya ulinzi ya Makambako .
Mbali ya kuwaua walinzi hao wawili pia majambazi hayo yalimjeruhi kwa risasi meneja wa kituo hicho Jonas Msenyi na kupora fedha zaidi ya Tsh milioni 5
Alisema kuwa jeshi la polisi linaendelea na msako wa kuwasaka majambazi hayo ikiwa ni pamoja na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo la polisi Licha ya kuwashikilia watu wanne wanaosadikiwa kuhusika katika Tukio Hilo.