Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

AJIRA MPYA ZA WALIMU NJOMBE BADO WALIMU HAWATOSHI.

$
0
0
 Zoezi la Usajiri kwa walimu wapya katika Halmashauri ya mji wa Njombe laandelea.
 Baadhi ya Walimu Wapya Wakisajiriwa Leo na Maafisa Toka Halmashauri ya Mji wa Njombe baada ya Kuripoti.


 Mwalimu Agrey Ragweni  ambaye amepangwa katika Halmashauri ya Mji wa Njombe kupitia ajira mpya za mwaka huu.
afisa elimu wa Shule za msingi katika Halmashauri ya mji wa Njombe Mwalimu Zegeli Shengelo Akizungumza na www.gabrielkilamlya.blogspot.com juu ya ikama ya walimu waliopangwa katika Halmashauri ya mji wa njombe 
Jamila Nachenga mmoja wa Walimu aliyekutwa na kamera za mtandao huu akifanya usajiri leo.

Na Gabriel Kilamlya Njombe

Licha ya Serikali Kutoa Ajira Kwa Walimu Wapya Ili Kupunguza Uhaba wa Walimu Katika Shule Mbalimbali Hapa Nchini,Halmashauri ya Mji wa Njombe Bado Inaupungufu wa Walimu 241 Kwa Shule za Msingi Licha ya Kuletwa Walimu 44.

Idadi Hiyo ni Ile Ambayo Imekuja Baada ya Kupangwa Kwa Walimu 44 Katika Ajira Hizo Mpya Ambao Tayari Wameanza Kuwasili Katika Halmashauri Hiyo na Kupangwa Katika Vituo Vyao Baada ya Kusaini Mkataba wa Ajira na Serikali.

Akizungumza Wakati Zoezi la Usajiri Likiendelea Katika Halmashauri Hiyo,Afisa Elimu wa Shule za Msingi Zegeli Shengelo Amesema Kwa Upande wa Shule za Msingi ni Walimu Watatu Pekee Ambao Washaripoti Hadi Sasa Kati ya 44 Waliopangwa Katika Halmashauri Hiyo Huku Kwa
Shule za Sekondari Wakiwa Wamewasili Walimu 87 Kati ya 152 Waliopangwa Katika Halmashauri Hiyo.

Bwana Shengelo Amesema Kuwa Serikali Inaendelea Kushughulikia Fedha zao za Kujikimu Huku Walimu Wakuu Wakiagizwa Kuwaandalia Mazingira Mazuri ya Kufikia Walimu Hao Baada ya Kupangiwa Vituo Vyao Vya Kazi.

Agrey Ragweni na Jamila Nachenga ni Miongoni Mwa Walimu Wapya Ambao Wamekutwa Wakiendelea na Usajiri Katika Halmashauri Hiyo Ambao Licha ya Kupongeza Hatua ya Serikali Kutoa Ajira Kwao Lakini Wameiomba Serikali Kuwasaidia Kupata Fedha Zao Haraka Ili Waweze Kujikimu Katika Kipindi Hiki Kigumu Kwao.

Wamesema Endapo Serikali Itawacheleweshea Fedha Zao Huenda Wakijikuta Wanaishi Katika Mazingira Magumu na Hatarishi Katika Maisha Yao Kutokana na Ugeni wa Mazingira na Ugeni Katika Ajira Zao.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles