Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

KUBOMOKA KWA TUTA LA KIJIJI CHA JOMBWE MKOA WA KUSINI PEMBA KUNATOKANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI

$
0
0
Na Mwanaisha  Moh’d  Na Kijakazi Abdallah -Madownload (7)elezo Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema sababu ya kubomoka kwa tuta Kijiji cha Jombwe Mkoa wa Kusini Pemba ni kupanda kwa kina cha maji kinachotokana na athari za mabadiliko ya tabia ya Nchi na baadhi ya  Wananachi walivunja mawe yaliyokuweko kwenye tuta hilo.
Hayo yameelezwa huko Baraza la Wawakilishi Chukwani Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabibu Fereji wakati alipokuwa akijibu suala  la Mh. Saleh Nasouro Juma (Jimbo la Wawi).
Alisema kuwa tuta hilo lipo Mkoa wa Kusini Pemba  Kijiji cha Jombwe na Sipwese Wananchi waliweza kulitumia tuta hilo ni kama njia ya kwenda Muambe pia wanafunzi walilitumia kwa ajili ya kwendea Skuli hiyo  mnamo mwaka 2010 tuta hilo lilianza kubomoka na kurahisisha njia ya maji ya chumvi  kupita na kuelekea
  Kijiji  cha Sipwese hadi Chuo cha Mafunzo Kengeja.
Alifahamisha kuwa tuta hilo zaidi ya urefu wa mita 100  mbali ya kuwani kizuizi cha maji ya chumvi yanayoingia katika maeneo hayo  kwani  tuta hilo limetumika zaidi kama kivuko katika maeneo hayo.
Aidha alisema uingiaji wa maji ulianza mwaka 2002 wakati tuta hilo lilijengwa mwaka 2004  kutokana na kutumiwa vibaya halikuweza kuchukuwa muda mrecu likabomoka.
 Hata hivyo Serikali kwa sasa haijasaidia kujenga tuta hilo bali Mpango huo ndio utakao toa dira ya kushughulikia maeneo yalioingia maji ya chumvi ambayo yapo (145) Uguja na Pemba.
Sambamba na hayo Waziri huyo amesema juhudi za kupunguza maji ya chumvi kuelekea maeneo hayo Serikali ikishirikiana na wananchi kupitia Ushirika wa (Green Peace and Enveronmetal Conservation- GPEC) imeweza kupanda miti ikiwemo Mikoko,Mikandaa yenye urefu wa heka tatu za miti hiyo zimepandwa eneo hilo na imeweza kuendelea kustawi vizuuri kuhifadhi mazingira .

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles