Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi Sarah Dumba akiongea na vyombo vya Habari kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Bi. Rehema Nchimbi kabla ya kuanza kwa maandamano kuelekea uwanja wa sabasaba mjini Njombe kwa ajili ya Uzinduzi wa Maadhimisho ya siku ya Ukimwi.
Wa kwanza kutoka kushoto ni Mwandishi wa Habari wa TBC, Fredrick Siwale mwandishi wa Habari Kutoka Star TV, na mwisho ni Afisa Habari wa TACAIDS.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Joseph Mbeyela wakiwa wamepumzika kabla ya kuanza maandamano.
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule za msingi na sekondari Mjini Njombe wakiwa wanajiaandaa kwa maandamano
Moja kati ya mahema yaliyosambazwa Mjini Njombe kwa ajili ya kila mwananchi kupima afya.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Akiongoza maandamano hayo na hapa ni mtaa wa masasi.
KWA HISANI YA Festo James
Wananchi Mkoani Njombe Wametakiwa Kujitokeza Kupata Elimu ya Ukimwi,Uzazi wa Mpango na Magonjwa Mbalimbali Ikiwemo Saratani ya Shingo ya Uzazi Kwa Akinamama.
Kauli Hiyo Imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi.Sarah Dumba Kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dokta Rehema Nchimbi Kwenye Kikao Maalumu na Waandishi wa Habari Juu ya Taarifa ya Uzinduzi wa Maazimisho ya Ukimwi.
Bi.Dumba Amesema Kuwa Kutokana na Taifa Kutambua Hali Mbaya ya Maambukizi ya UKIMWI Yanayofikia Asilimia 14.8 na Kushika Nafasi ya
Kwanza Kitaifa Serikali Imeona ni Vyema Maazimisho Hayo Yakafanyika Mkoani Njombe Kitaifa Ambayo Yamezinduliwa Rasmi Leo.
Jackson Saitabau ni Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Ambaye Amesema Kuwa
Katika Kipindi Cha Wiki Nzima Wakati wa Maazimisho Hayo Huduma za
Magonjwa Sugu na Upimaji wa Hiari.
Kaulimbiu ya Maazimisho Hayo Kwa Mwaka Huu ni “Tanzania Bila Maambukizi Mapya Ya Vvu,Vifo Vitokanavyo Na Ukimwi Na Ubaguzi Wa Unyanyapaa Inawezekana”.