WAFANYABIASHARA WADOGO WANAOUZA PEMBEZONI MWA BARABARA KUU MJINI NJOMBE WATAKIWA KUHAMIA ENEO JINGINE
DIWANI WA KATA YA NJOMBE MJINI AGRY MTAMBO KUPITIA CHADEMA AKIZUNGUMZA NA WAFANYABIASHARA HAO AKIWA OFISI YA MKURUGENZI
WAFANYABIASHARA HAO WAMEDAI WAKIWA NYUMBANI WANADAIWA MICHANGO WAKIFANYA BIASHARA KANDO YA BARABARA KUU ILI WAKAPATE FEDHA YA MICHANGO WANAONDOLEWA SASA TUFANYAJE TUKAIBE ? KIBAYA ZAIDI LEO WAMEKUJA NA POLISI MBONA MICHANGO WANAKUJA WENYEWE TU BILA ASKALI POLISI
WAFANYABIASHARA HAO HAPA WANARUDI KWENYE MAENEO WALIOAINISHIWA KUFANYA BIASHARA BAADA YA DIWANI KUKUTANA NA UONGOZI WA HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE NA KUOMBA WAFANYIE BIASHARA HIZO KANDO YA BARABARA ZA PEMBENI NA SIYO BARABARA KUU
Picha na Michael Ngilangwa
Sakata la Wafanyabiashara Wadogowadogo Wanaofanya Biashara Zao Pembezoni Mwa Barabara Kuu Mjini Njombe Limeendelea Kutikisa Katika Mji wa Njombe Kufuatia Wafanyabiashara Hao Kuandamana Hadi Kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Leo Kufuatia Oparesheni ya Kuwaondoa Inayoendelea.
Wafanyabiashara Hao Wamelazimika Kwenda Kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Baada ya Viongozi Ngazi ya Mtaa na Kata ya Njombe Mjini Kuendesha Oparesheni ya Kuwahamisha Katika Maeneo Hayo Kwa Madai Sio Maeneo Sahihi Kwa Biashara Kwa Mujibu wa Sheria ya Barabara.
Akizungumza na Wafanyabiashara Hao Baada ya Kupokea Maelekezo ya Kisheria Kwa Mkurugenzi wa Halmashauri Hiyo,Diwani wa Kata ya Njombe Mjini Bwana Agrey Mtambo
Amesema Kuwa Licha ya Mazungumzo ya Muda Mrefu Baina Yake na Serikali Lakini Bado Mwafaka Haujapatikana Ambapo Majibu Zaidi Yatatolewa Wiki Lijalo Siku ya Juma Nne.
Bwana Mtambo Amesema Kuwa Katika Mazungumzo na Mkurugenzi wa Halmashauri Hiyo Wamekubaliana Wafanyabiashara Hao Kwa Sasa Wafanyie Katika Eneo Lolote Ndani ya Mji wa Njombe Isipokuwa Kwenye Barabara Kuu ya Njombe Songea.
Pamoja na Kukubaliana Kwa Maagizo Hayo ya Kufanyabiashara Kwenye Maeneo Tofauti na Barabara Kuu Lakini Bado Wafanyabiashara Hao Wameonekana Kuendelea Kuitupia Lawama Serikali Kwa Kuwanyanyasa Katika Biashara Zao.
Wamesema Awali Walifukuzwa Katika Eneo Hilo na Kuambiwa Warudi Nyuma Lakini Bado Tena Wanaendelea Kufukuzwa na Kuharibiwa Mali Zao.
Kwa Upande Wake Ispekta Martinus Mirumbe Amewataka Wafanyabiashara Hao Kuzingatia Maagizo Yanayotolewa na Viongozi Wao Ikiwa ni Pamoja na Kutii Amri Bila Shuruti.
Na Gabriel Kilamlya