MWANAJESHI MARINO MBEYELA AZIKWA NJOMBE LEO
![]()
Wananchi wa mitaa ya Idundilanga Mjini Njombe wameshauliwa
kuimarisha ulinzi na usalaama katika maeneo yao ili kuhakikisha
uharifu wa mali unaofanyika kwa nyakati tofauti usiku na mchana
na baadhi ya watu wanaosadikika kuwa ni wezi unatokomezwa.
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa mtaa wa Idundilanga bwana
Augustino Mgeni wakati akitoa salaamu za serikali katika mazishi
ya aliyekuwa mwanajeshi Wa jesh la
wananchi Tanzania JWTZ Marino
Benedict Mbeyela yaliofanyika Jana kwenye makaburi ya Igominyi
Mjini Njombe.
Bwana Mgeni amesema kufuatia kukithili kwa uharifu unaofanywa na
baadhi ya watu, wananchi wanatakiwa kuonesha ushirikiano katika
kuwafichua wanaojihusisha na matendo hayo na kwamba uongozi wa
mtaa huo unatarajia kufanya msako muda wowote wa kuwabaini
waharifu.
Kwa upande wake Afisa mtendaji wa Mtaa wa Idundilanga Mashaka
Lulambo amehimiza wananchi kujitokeza kuchangia michango
kwaajili ya ujenzi mbalimbali ambao unaendelea katika mtaa huo
na kwamba wanafunzi wa shule ya sekondari Joseph Mbeyela
wamekosa vyumba vya madarasa vya kutosha jambo linalolazimu
kuhimiza ujenzi huo.
Amesema kuwa kwa watakaoshindwa kuwasilisha michango hiyo kwa
wakati hatua kali za kisheria zitaanza kuchukuliwa na kwamba
kila mwananchi anatakiwa kuchangia shilingi elfu sita ili
kukamilisha ujenzi unaoendelea katika mitaa ya kata ya Njombe
mjini.
Akisoma Ibada ya mazishi ya marehemu Marino Benedict Mbeyela
ambaye enzi za uhai wake ametumikia jeshi la Wananchi wa
Tanzania JWTZ Kwa kipindi cha miaka thelathini Na nne Katekista
wa kanisa Katholiki Kigango cha Njombe Mjini Kelvin Myamba
amesema kuwa wakristo wanapaswa kumtumikia Mungu siku zote ikiwa
ni pamoja na kuungama dhambi zao.
Muwakilishi wa jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ Akisoma
taarifa fupi ya marehemu akawambia wananchi waliohudhulia
mazishi hayo namna walivyokuwa wakifanya kazi na marehemu kwamba wameshirikiana vizuri hadi alipokuja kuchukuliwa na mwenyezi Mungu.
kwa hisani ya michaelngilangwa blog