ZAIDI YA WATU 35 WAdaiwa KUFARIKI KATIKA AJALI YA MABASI ILIYOTOKEA MCHANA MJINI MUSOMA ANEO MAARUFU LA SABA SABA

Watu zaidi ya 35 wamepoteza maisha papo hapo na wengika kujeruhiwa vibaya sana.
kwa mujibu wa Taarifa Kutoka eneo la Tukio Imeelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo Basi la J4 ambalo lilikuwa likijaribu kuipita gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye nambari za usajili T 332 AKK katika sehemu ambayo mbele kuna daraja linaloweza kupitisha gari moja kwa wakati huo,kutokana na kuwa basi hilo lilikuwa kwenye mwendo kasi liliweza kuisukuma kwa ubavuni gari hiyo ndogo ambayo haikuweza kuhimili nguvu ya Basi hilo na kutoka kwenye njia na kwenda kuingia mtoni.hali iliyoipelekea basi hiyo kuamini kuwa itawahi kupita katika daraja hilo bila kufahamu kuwa Basi lingine
linalokuja mbele nalo liko kwenye mwendo kasi huku nalo likitaka kuwahi kupita kwenye daraja hilo.
Ndani ya gari hiyo ndoho kulikuwa na watu watatu,ambapo wawili wamefariki na mmoja amejeruhiwa.Picha na Ahmad Michuzi,Musoma.












kwa Hisani ya Michuzi Blog