Quantcast
Channel: GABRIEL KILAMLYA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

//kilamlya1.rssing.com/chan-14218227/article1125-live.html

$
0
0
AJALI YA MABASI KUGONGANA USO KWA USO WILAYANI SIKONGE TABORA IMEUWA 16 PAPO HAPO NA WENGINE 75 KUJERUHIWA
 
 
Watu  16  wanadaiwa kufariki dunia na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa  baada ya mabasi waliokuwa wakisafiria kugongana katka k ijiji  cha Mlogolo wilayani Sikonge mkoani Tabora.
 
Ajali hiyo imetokea Jana  jioni majira ya saa 11 jioni baada ya Basi la Kampuni ya Sabena lenye namba za usajiri T 110 ARV lililokuwa likitokea Mbeya kwenda  Mwanza kumegongana uso kwa uso na basi la AM Dreamline lenye namba za usajiri  T 803 ATN lililokuwa likitokea Mwanza kupitia Mpanda.

Ajali hiyo imetokea maeneo ya Mlogolo takribani kilometa 3 kutoka wilayani   Sikonge.Pia inadaiwa kuwa dereva wa basi la Sabena aliyefahamika kwa jina la James Kombe amepoteza maisha baada ya kukatika kiwiliwili na kufa papohapo a kuwa jitihada za kutafuta kiwiliwili chake zilikuwa zikifanyika baada ya kupondeka vibaya.
 
Mashuhuda wa ajali hiyo wamedai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni madereva hao kuwa ni wasaidizi ( Day-worker).Inakadiriwa kuwa karibu robo tatu ya basi la sabena imeharibiwa vibaya sana.Mabasi yaliyohusisha ajali hiyo ni basi la  Sabena lililokuokea  Mbeya kwenda -Mwanza na AM Dreamline lililokuokea  Mwanza kwenda Mpanda.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2276

Trending Articles